LATEST POSTS

Wednesday, November 20, 2013

KESI YA KAJALA KUANZA UPYA


AMA kweli hujafa hujaumbika! Bado bundi anamnyemelea staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja baada ya kurejeshwa kortini kwa mara nyingine huku kesi ikimjia upya, Risasi Mchanganyiko limesheheni.
                                                            Kajala Masanja.
MUME AKATA RUFAA
Pamoja na kutoa faini ya Sh. milioni 13 alizolipiwa na staa mwenzake wa filamu, Wema Isaac Sepetu, Kajala anatarajiwa kuhukumiwa tena Novemba 25, mwaka huu baada ya mumewe, Faraji Agustino Chambo kukata rufaa katika mahakama kuu.
Kwa mujibu wa jaji aliyezungumza na gazeti hili, kuna kila dalili wawili hao wakaachiwa huru au wakafungwa tena kwa adhabu kubwa zaidi ya ile ya awali, hivyo huu ni msala mpya kwa Kajala ambaye tayari alikuwa uraiani.
Kajala na mumewe, Faraja Chambo wakisubiri siku ya  hukumu yao.
Kesi iliyokuwa ikiwakabili wanandoa hao ilihusiana na utakatishaji wa fedha haramu uliofanywa na mume wa Kajala wakati akifanya kazi kwenye Benki ya NBC, Dar.
Mume wa staa huyo ndiye anadaiwa kukata rufaa wakati akitumikia kifungo cha miaka saba jela baada ya kukutwa na hatia.
Habari za ndani zilieleza kwamba, Kajala alisharidhika na hukumu iliyotolewa Machi 25, mwaka huu ambapo yeye  alitakiwa kufungwa mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni 13.
                                                               Wema na Kajala.
Katika hukumu hiyo, mume wa Kajala alifungwa miaka saba na ndipo alipoamua  kukata rufaa na akamuingiza Kajala kwa maelezo kuwa wote hawakuridhishwa na hukumu iliyotolewa mwanzoni.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Kajala, staa huyo amekuwa katika wakati mgumu na mara nyingine na kujikuta akiangua kilio hasa anapokumbuka maisha ya gerezani.
Baba Kajala (kushoto) akishauriana jambo na wasanii wa filamu na maswahiba wa mwanaye siku ya hukumu ya mwanae.
KAJALA KORTINI
Ili kuthibitisha habari hizo, juzi (Jumatatu) Kajala akiwa na shosti wake, Wema anayehaha kumnasua, alipigwa chabo na mashushushu wetu wakitinga tena katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Habari zilieleza kuwa jaji ambaye alikuwa akipitia ya hukumu ya awali ya wanandoa hao, alidai kwamba  Jaji Temba aliyetakiwa kutoa hukumu ya kesi hiyo upya alikuwa anaumwa.
HUKUMU NOVEMBA 25
Kufuatia kuumwa kwa hakimu huyo, kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 25, mwaka huu, ambayo itakuwa siku ya hukumu huku ikielezwa kuwa kila kitu kipo tayari.
Akiwa katika viunga vya mahakama hiyo, Kajala alionekana mwenye wasiwasi na woga kwa sababu hakuwa anajua kama anaweza kuburuzwa kortini kwa mara nyingine kuhusiana na suala hilo kwa kuwa aliamini alishamaliza kwa kulipa faini ya Sh. milioni 13 kisha kurejea uraiani huku mumewe akienda jela.
Kajala alisema anaomba Mungu ili kikombe hicho kimuepuke kwani alishasahau kama anaweza kurudi kortini.
“Sikudhani kwa kweli kama ninaweza kurudi mahakamani, Mungu anisaidie kwa kweli…” alisema Kajala.
Naye Wema alipigwa na mshangao baada  ya kuona kesi hiyo imeibuka tena.
“Siku ile niliuliza kilikuwa kinahitajika nini ili Kajala awe huru, nikaambiwa milioni 13, nikatoa, sasa iweje tena arudishwe mahakamani?” alihoji na kuonesha wasiwasi mkubwa baada ya kuambiwa  kuwa Kajala anaweza kufungwa kwa kuwa hukumu inapitiwa upya.
Wakili wa Kajala, Peter Kibatala alisema anapambana kunyoosha sheria kuhakikisha mteja wake anakuwa huru.
 
SOURCE: GLOBAL PUBLISHERS

UGONJWA WA HEPATITIS B UPO NA UNAUA, NENDA KAPIME SASA

Mgonjwa mwenye Hepatitis B ngozi na macho yake vikiwa vya njano
 
Mgonjwa mwenye Hepatitis B ngozi na macho yake vikiwa vya njano.
HEPATITIS B NI NINI?
Hepatitis B ni ugonjwa wa manjano ambao hushambulia ini.
Ugonjwa huu kama haujatibiwa hutengeneza uvimbe katika ini na kusababisha kansa ya ini na baadaye KIFO.
Inakadiriwa watu milioni 350 duniani wameathirika na ugonjwa huu ambapo watu 620,000 hupoteza maisha kila mwaka kwa ugonjwa huu.
HEPATITIS B UNASABABISHWA NA NINI?
Ugonjwa huu husababishwa na virusi waitwao Hepatitis B (HBV) ambao hukaa katika ini, damu na baadhi ya majimaji mwilini.
             Virusi vya Hepatitis baada ya kulishambulia ini.
UNAAMBUKIZWAJE?
Ugonjwa huu huambukizwa kwa njia zifuatazo:
-Kujamiana bila kinga
-Kunyonyana ndimi
-Mama mwenye ugonjwa kumwambukiza mtoto wakati wa kujifungua
-Kuchangia damu isiyo salama
-Kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k
-Kuchangia miswaki
Mojawapo ya njia zinazoambukiza ugonjwa wa Hepatitis B.
NB: Ugonjwa huu hauambukizwi kupitia chakula, maji au kushikana mikono na waathirika.
DALILI ZAKE
Dalili za ugonjwa huu huchukua muda mrefu kuonekana, zikionekana mgonjwa anakuwa tayari ameathirika sana na ni kama ifuatavyo:
-Uchovu
-Kichefuchefu
-Mwili kuwa dhaifu
-Homa kali
-Kupoteza hamu ya kula
-Kupungua uzito
-Maumivu makali ya tumbo upande wa ini
-Macho na ngozi kuwa vya njano
-Mkojo mweusi
           Daktari akifavya vipimo vya ugonjwa wa Hepatitis B.
KINGA
-Chanjo
-Kutumia kinga wakati wa kujamiana
-Kuacha kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k
-Kutochangia miswaki
-Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu
-Kutochangia damu isiyo salama
          Mgonjwa wa Hepatitis B akipandikizwa ini na madaktari.
TIBA
-UGONJWA HUU HAUNA TIBA, japo mgonjwa akiwahi hospitali atapatiwa dawa za kupambana na virusi kuvipunguza nguvu za kushambulia ini.
-Kupandikiza ini ambapo ini lililoathirika huondolewa na kuwekwa ini lingine japo ni vigumu kupata ini salama.
-Mgonjwa anashauriwa kuacha kutumia pombe, madawa ya kulevya na vitu vingine vinavyochosha ini.
SOURCES: GLOBAL PUBLISHERS

Monday, November 18, 2013

ISSUE YA DENTI ANAYEDAIWA KUBAKWA NA KAPUYA UTATA MTUPU.


ANGALIA VIDEO YA DENTI ANAYEDAI KUBAKWA NA KAPUYA WAKATI WA MAHOJIANO NA GPL.
Stori: Waandishi Wetu
MNYONGE mnyongeni haki yake mpeni, skandali ya kumbaka na kumwambukiza Ukimwi mwanafunzi, inamtafuna na kumuumiza Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Juma Athuman Kapuya.
Denti anayedai kubakwa na Prof Kapuya akiongea na GPL.
Kuhusu ukweli wa skendo hiyo, vyombo vya sheria vitazungumza lakini gazeti hili limejiridhisha pasipo shaka yoyote kuwa denti husika ni tapeli na anacheza rafu ili kumharibia Kapuya kwa maslahi yake.
Gazeti hili, liliamua kumchunguza denti husika ili kumjua kiundani katika kutimiza ahadi ambayo Global Publishers Ltd, ilishaitoa kwenye Gazeti la Risasi, nakala ya Jumamosi iliyopita kuwa waandishi wake watafuatilia kinagaubaga na kuanika kila kitu kupitia magazeti yake, utekelezaji unaendelea.
Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Profesa Juma Athuman Kapuya.
HUU NDIYO WASIFU WA DENTI MWENYEWE
Baada ya jana kupitia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuzungumza na Kapuya ambaye alifunguka kila kitu, gazeti hili linaendelea kwa kumchambua denti husika, wasifu wake na maisha yake yote ya kitapeli.
ANA MAJINA MENGI
Denti huyo amekuwa akijulikana kama Felista, ila anatambulika pia kama Halima Hamad, hivi karibuni aliamua kujiita Leylat na wakati mwingine Leila.
Jina ambalo alimuingia nalo Kapuya ili kumtapeli ni Halima Hamad, upande mwingine hujitambulisha kama Halima Humudi, yaani huchezea ubini.
Denti akiwa busy na simu yake wakati wa mahojiano na GPL.
MSHANGAO KUHUSU DENTI HUYO
Mwezi mmoja kabla ya sakata la Kapuya halijapamba moto, Felista alizungumza na waandishi wetu wawili kwa nyakati tofauti, akielezea uhusiano wake na mheshimiwa huyo ambaye kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Miundombinu.
Felista alimweleza mwandishi wa kwanza ambaye ni mwanamke: “Nina stori kuhusu Kapuya, yule ni mtu wangu, ila subiri kidogo nitakupa stori kamili.”
Siku mbili baadaye, Felista alimfuata mwandishi wa pili ambaye ni wa kiume, akamwambia: “Kapuya ananitongoza, ngoja mambo yakae sawa nitakwambia.”
Hata hivyo, waandishi wetu hawakuingia kwenye mtego huo kwa sababu mbili. Mosi; si kawaida ya Global Publishers kuandika habari zenye sura ya upande mmoja kwa maslahi ya mtu, isipokuwa husimamia zaidi weledi na mizani.
Pili; Felista siyo mgeni kwa waandishi wetu kwa sababu ana rekodi nyingi za matukio yenye sura ya utapeli, kwa hiyo hakuweza kufua dafu kuiingiza mkenge Global Publishers.
Denti akiwasikiliza wana GPL wakati wa mahojiano.
ENDELEA KUMSHANGAA DENTI HUYO
Baada ya sakata hilo kuibuka kwa nguvu, kasi na ari, waandishi wetu walimpigia simu Felista kumuuliza ilikuwaje akalifikisha suala mbali zaidi, huku akijisema yeye ni mwanafunzi wakati siyo kweli?
Felista alimjibu mwandishi wa kwanza: “Huyo aliyepeleka hizo habari ni Leylat. Mimi Kapuya nafahamiana naye kwa sababu nilishiriki vikao vya usuluhishi kati ya Leylat na Kapuya. Walimalizana vizuri. Mimi kama shahidi nilipata shilingi 3,000,000.
“Siku ya kwanza nilipewa shilingi 2,300,000, baadaye alinimalizia shilingi 700,000, tukawa tumemalizana.”
Mwandishi wa pili alipomuuliza, alijibu: “Jamani siyo mimi, yule ni Leila. Yule mtoto sijui kafikishaje hayo mambo huko, ila mimi najua kila kitu.”
Baadaye Felista alimpigia simu yule mwandishi wa kiume, akamwambia: “Kama utanihakikishia pesa ya usafiri nakuja, nitaeleza kila kitu kwa sababu mimi ndiye shahidi muhimu.”
Denti huyo akiondoka katika ofisi za GPL baada ya mahojiano.
Mwandishi wetu akambana Felista: “Mimi bado nahisi huyo Leylat unayemtaja ndiye wewe mwenyewe ila unaficha.”
Felista akajibu: “Siyo mimi, halafu sasa hivi sijui mahali alipo ila najua yote kuhusu Leylat na Kapuya.”
Mazungumzo hayo yalifika mwisho, huku Felista akiahidi kufika ofisi za Global Publishers Ltd, Bamaga, Mwenge lakini baada ya kukata simu, dakika tatu baadaye alimpigia simu mwandishi wetu, safari hii akiwa na maelezo haya:
“Nimeongea na Leylat. Amefichwa Maili Moja, Kibaha, Pwani, hakuna watu wanaoruhusiwa kumuona zaidi ya wanaharakati ambao wamejitolea kumsaidia kisheria.”
Felista alipotakiwa na mwandishi wetu atoe namba ya Leylat, alijibu: “Namba hapana ila mkitaka nitawapeleka mkamuone. Yule mtoto anasikitisha sana, unajua sasa hivi anatumia dawa.”
AKAZUA SEKESEKE OFISINI GLOBAL PUBLISHERS
Jumamosi iliyopita, Gazeti la Risasi likiwa lina uhakika wa asilimia zaidi ya 95 kwamba Felista ndiye anayecheza sinema yote ya Kapuya, akibadilisha majina na kujiita mwanafunzi, lilitoa picha yake kisha likaiziba ili kumtega kisha likamtambulisha kama shahidi muhimu kama alivyojiita.
...Akiwa nje ya ofisi za Global.
Asubuhi mapema siku hiyo, Felista alimpigia simu mwandishi wetu akilalamika: “Mmeniharibia, Kapuya amenipigia simu anatishia kuniua kwa sababu anasema mimi nimejifanya kiherehere kwamba najua kila kitu.”
MWANDISHI: Wewe ungekuja ofisini tuongee vizuri.
FELISTA: Sawa nakuja ila lazima muangalie jinsi ya kunilinda, maisha yangu yapo hatarini.
Baada ya takriban saa moja, Felista alifika Global Publishers na kusema: “Yaani hatari kweli, Kapuya amekuja nyumbani kwangu, akiwa ameongozana na Leylat. Amesema ataniua kwa sababu mimi ndiye kiherehere nataka kumharibia.”
MWANDISHI: Kapuya amekuja nyumbani kwako kivipi? Tena akiwa ameongozana na Leylat, mbona unatuchanganya.
FELISTA: Amekuja ndiyo, tena inavyoonekana Leylat mwenyewe sasa hivi yupo pamoja na Kapuya. Ugomvi wao umeisha.
Kapuya anafungua kesi kwa magazeti na mitandao iliyomchafua, Leylat yupo upande wake, mimi nikipingana na Kapuya si nitakufa?
MWANDISHI: Hebu Felista usiongee sana, wewe asubuhi uliniambia Kapuya alikupigia simu, sasa hivi unasema alikuja kwako, tukueleweje?
FELISTA: Kapuya hakupiga simu, alikuja na Leylat.
MWANDISHI: Inawezekana Kapuya akawa mtoto kiasi hicho? Na kwako alipajuaje?
FELISTA: Mimi sijui, ila pale nyumbani aliletwa na Leylat.
MWANDISHI: Haya tuambie wewe unatakaje?
FELISTA: Nataka pesa ya kodi, nikapange nyumba sehemu nyingine, pale hapanifai tena, nitauawa. Leoleo nataka kuhama.
UWAZI LIKAENDA MBELE ZAIDI
Gazeti hili, lilimuweka ‘pending’ Felista na madai yake kisha likaingia kazini kumtafuta Kapuya, aweze kueleza wasifu wa denti husika.
“Ni mfupi, mwembamba, mweusi, ana macho makubwa, pua kama ya Kitutsi, kichwa kirefu,” alisema Kapuya baada ya kukiri kumtambua msichana huyo anayejiita mwanafunzi.
Kwa kuchambua maelezo hayo, jawabu moja kwa moja lilikwenda kwa Felista kwa sababu sifa ambazo zimetajwa zinashabihiana naye kwa asilimia 100.
MWANDISHI: Anaitwa nani?
KAPUYA: Halima Hamad.
MWANDISHI: Mmejuana kwa muda gani?
KAPUYA: Tangu mwaka 2011.
MWANDISHI: Katika kipindi hicho, ulikutana naye mara ngapi?
KAPUYA: Kama mara nne, alikuja kuomba msaada akalipe ada Tumaini University. Nilimpa shilingi 3,000,000. Awamu ya kwanza nilimpa shilingi 2,300,000, mara ya pili shilingi 700,000. Nilimsaidia akasome, sikujua kama ni tapeli.
(Rejea maelezo ya Felista kwamba alipewa shilingi 3,000,000 kwa awamu mbili. Zilianza shilingi 2,300,000, baadaye zikafuata shilingi 700,000).
MWANDISHI: Ulijuaje kama ni tapeli?
KAPUYA: Kwanza niligundua hasomi na kuna watu alikuwa anashirikiana nao kunizunguka ili wanitapeli. Nikagundua pia kumbe hata Mkurugenzi wa CRDB, Dk. Charles Kimei, alimtapeli kwa njia hizohizo.
 MWANDISHI: Alikwambia anaishi wapi?
KAPUYA: Yule mtoto muongomuongo, kuna kipindi aliniambia anaishi Mbagala, baadaye akasema Gongo la Mboto, hapa juzujuzi, alisema amehamia jirani na Shoppers Plaza.
(Felista aliwaeleza waandishi wetu kuwa anaishi Gongo la Mboto).
MWANDISHI: Namba yake ya simu ni ipi?
KAPUYA: 0713 7...20…0 (tarakimu mbili zimefichwa).
Lengo la kuuliza namba ni kutaka kujua namba aliyonayo Kapuya ili kuifananisha na ile ya Felista ambayo ipo kwa waandishi wetu.
Namba hiyo ndiyo hasa ya Felista, hivyo kuzidi kujidhihirisha kuwa ndiye anayecheza sinema yote.
MWANDISHI: Pamoja na utapeli wake, vipi kuhusu tuhuma za kumbaka na kumuambukiza Ukimwi?
KAPUYA: Jamani sijawahi kubaka katika maisha yangu yote. Sina Ukimwi. Huyo mtoto anatumiwa na watu kunichafua, maana kuna SMS alinitumia akaniambia atahakikisha sipati cheo chochote.
TUKARUDI KWA FELISTA
MWANDISHI: Kapuya ameshatufungua na tunajua wewe ndiye mhusika,
FELISTA: Siyo kweli, Kapuya anataka tu kutengeneza mambo ili ajisafishe.
MWANDISHI: Kapuya ametaja namba yako kuwa wewe ndiye mhusika. Na kwa nini ataje namba yako?
FELISTA: Labda kapata namba yangu kupitia kwa Leylat.
MWANDISHI: Kapuya amesema wewe unaitwa Halima Hamad na ndivyo ulivyojitambulisha kwake.
FELISTA: Siyo kweli, mimi naitwa Felista. Hilo jina la Halima silitambui.
(Papo hapo, mwandishi wetu aliiangalia namba hiyo usajili wake wa laini na Tigopesa na kubaini kwamba jina lililosajiliwa ni Halima Hamad).
MWANDISHI: Mbona simu yako, laini na Tigopesa, imesajiliwa kwa jina la Halima Hamad ambalo limetajwa na mheshimiwa? Halima ni nani sasa?
FELISTA: Turudi kwenye madai ya msingi, msitake kunibadilishia mada?
MWANDISHI: Wewe ndiye Halima, ndiye Felista, ndiye Leylat na Leila. Wewe ndiye unamchezea Kapuya, siyo mwanafunzi, ni tapeli.
FELISTA: Najua mnataka kunichezea mchezo. Mimi siyo Halima.
MWANDISHI: Mbona namba yako umesajili Halima?
FELISTA: Nimesema mimi siyo Halima.
KAMA HUMJUI FELISTA
Felista wa Kapuya ndiye yule binti aliyewahi kumtapeli mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma kupitia Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama).
Msichana huyo, alidai yeye ni yatima, akiishi kwa tabu sana, Mama Salma akaingia mkenge na kumpa kiwanja Mbagala. Baadaye ilipokuja kujulikana, alishtakiwa kwa utapeli, akapelekwa mahabusu kwenye Gereza la Segerea, Dar es Salaam.
Felista alikiri kuwekwa Segerea kisha akajitetea: “Kuna watu walitaka kunigombanisha na Mama Salma lakini mbona nilitoka?”
Felista, alishawahi kumuibia marehemu Steven Kanumba kamera, alipokwenda ofisini kwake, akijidai ni yatima na ana kipaji cha kuigiza, alipopata mwanya tu, alimliza supastaa huyo ambaye alifariki dunia, Aprili 7, mwaka jana.
Ukiachana na hilo la Kimei ambalo limetajwa na Kapuya, yapo matukio mengine ambayo Felista alishayafanya, ikiwemo kudanganya anasoma alipiwe ada, vitabu, madaftari na sare za shule, kumbe ni ‘gia’ yake ya kupata fedha kwa njia ya udanganyifu.
SIYO MTOTO KABISA
Uchunguzi wa gazeti hili unalo jawabu kuwa kama kuna uongo ambao jamii haipaswi kubisa kukubaliana nao ni huu kwamba Felista ana umri wa miaka 16 na anasoma sekondari.
Gazeti hili limebaini kuwa Felista ni mama wa mtoto mmoja na lilipombana alikiri: “Ni kweli nina mtoto mmoja, nina umri wa miaka 21.”
Waandishi wetu walifika mpaka Shule ya Sekondari Turiani, Magomeni ambako alidai anasoma, huko kila mwalimu aliyeulizwa alisema: “Hakuna mwanafunzi kama huyo anayesoma hapa labda kama mmechanganya shule.”

GLOBAL PUBLISHER

LOLA OMOTAYO OFFICIALLY MRS PETER OKOYE.

 TAZAMA PICHA ZAO ZA HARUSI YA KIMILA WALIYOFUNGA

























SOURCE: LOLADEVILLE BLOG

Sunday, November 17, 2013

KAPUYA KULISHTAKI GAZETI LINALOMTUHUMU KUBAKA

 
Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya
 
Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya, amefunguka na kusema tuhuma zinazomhusisha na kumbaka na kumuambukiza virusi vya Ukimwi msichana mwenye umri wa miaka 14, zimeasisiwa na baadhi ya wapinzani wake wa ndani na nje ya chama chake (CCM) wenye uwezo mdogo kisiasa.
Amesema nia ya wapinzani wake hao, ambao hakuwataja, ni kumchafua na kudhoofisha juhudi na utendaji wake wa kila siku, ili aonekane hafai katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Profesa Kapuya, ambaye amewahi kushika wadhifa wa uwaziri katika wizara mbalimbali katika utawala wa serikali za awamu ya tatu na nne, alisema hayo kupitia tamko alilolisambaza kwa umma jana juu ya kile alichokiita uzushi unaoenezwa dhidi yake kuhusiana na tuhuma hizo.
Alitoa tamko hilo siku moja baada ya wakili wake, Yasin Memba, kumtetea, ikiwa ni pamoja na kutishia kulishtaki mahakamani gazeti moja la Kiswahili litolewalo kila siku (siyo NIPASHE) endapo halitamwomba radhi mteja wake huyo, kwa kuchapisha tuhuma hizo bila kumpa nafasi ya kujitetea.
Profesa Kapuya alisema tuhuma hizo zilizuka wakati akiwa jimboni akiendelea na shughuli za utekelezaji wa ilani ya CCM, zikiwa hazina kichwa wala miguu kutokana na kutokuwa na ukweli wowote.
“…Tuhuma kadhaa zilizoelekezwa dhidi yangu zimeasisiwa na wanasiasa wenzangu wa ndani na nje ya chama changu ili kudhoofisha juhudi na utendaji wangu wa kila siku,” alisema Profesa Kapuya.
Profesa Kapuya alisema amekuwa akiitumikia nchi kwa kipindi kirefu katika nyanja na sekta mbalimbali, kuanzia darasani mpaka kwenye siasa.
“Kwa tamko hili, ninapenda kuwaambia kuwa nimefedheheshwa sana na uwezo mdogo wa kisiasa unaofanywa na hawa watu kwa kuwa dhamira yao haitatimia,” alisema Profesa Kapuya.
Alisema taarifa hizo ni za kutungwa zenye lengo la kumdhalilisha na kumuondolea heshima yake aliyojijengea kwenye jamii kwa kipindi kirefu.
“Waswahili wanasema dawa ya mjinga ni kumpuuza. Na hili linajidhihirisha zaidi kwa habari hii kuandikwa na chombo kimoja tu cha habari kinachotumiwa na chama kimoja cha siasa na baadhi ya wanasiasa wa chama changu wasiokitakia heri chama chetu,” alisema Profesa Kapuya.
“Chombo hiki cha habari kiliwahi kuripoti mwaka jana kuwa kuna mitambo imeingizwa nchini inayoweza kuandika ujumbe na kisha kuufanya uonekane umetoka kwenye namba fulani. Kwa kipindi kile sikuwaelewa.”
“Lakini sasa ninawaelewa na nimewaona kuwa wako sahihi na wao ndiyo waliouingiza mtambo huu na sasa wameamua kuutumia dhidi yangu kwa kutengeneza meseji na kuzihusianisha na mimi. Ninaamini ukweli utawaumbua muda si mrefu.”
Alisema ameijenga heshima na familia yake kwa jamii kwa kipindi kirefu, hivyo hawezi kuruhusu kuharibiwa na kupotezwa na watu wachache tena kwa muda mfupi.
“Hivyo, basi nimechukua hatua za kisheria kuhakikisha heshima yangu inaendelea kulindwa na utu wangu unaheshimiwa,” alisema Profesa Kapuya na kuongeza:
“Nimemwagiza mwanasheria wangu afungue kesi na tayari amewashitaki watu wote wanaohusika kwenye mpango huu na tayari wameshapokea taarifa ya kuitwa mahakamani. Nitaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote watakaoendelea kutaka kujipatia umaarufu ama wa kisiasa au wowote ule kwa kutumia jina langu.”
Alishauri yeyote mwenye kuona jambo hilo lina ukweli alipeleke kwenye vyombo husika ili lishughulikiwe kwa mujibu wa sheria na siyo kutumia vyombo vya habari kuchafuana.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

SITTA AFYATUA BOMU

 
 
  Awapa `vidonge` mahasimu wanaofukuzia urais
  Atoboa walivyoandaa bajeti bil.10/- za rushwa
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta
 Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amefyatuka na kuwananga mahasimu wake wanaowania urais wa 2015 kwa kuandaa bajeti ya zaidi ya Sh. bilioni 10 ili waingie madarakani kwa njia ya rushwa.
Amedai kuwa watu hao wamekula yamini ya nchi kuongozwa na mtu tajiri kupitia njia ya mkato.
Aidha, akasema kuna hatari wakati taifa likielekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani, na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, kuzuka kwa kundi la matajiri, ambao wengi wao ni wakwepa kodi mashuhuri, watoroshaji wa madini ya nchi na watoroshaji wa nyara na maliasili za nchi.
Akizungumza jana katika mahafali ya 17 ya Shule ya Sekondari ndogo ya Agape inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Sitta alisema walafi hao wa madaraka ni pamoja na baadhi ya viongozi waliojitajirisha kupitia fursa za serikali kwa njia ya rushwa, mikataba mibovu, wauza madawa ya kulevya na mawakala wa maovu.
Alisema kutokana na mwelekeo huo potofu, amewataka wananchi wamruhusu kutumia hadhara hiyo kuzungumzia hatari kubwa inayoikabili nchi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
“Katika mazingira haya inasikitisha kwamba viongozi wengi hususani wenye uroho wa madaraka na mali wamejigeuza kuwa wachekeshaji wa mfalme kwa kumuunga mkono, kujipendekeza na kumsifia kiongozi wanayejua maovu yake kwa mategemeo ya kupewa fedha na vyeo. Watu hao katika miaka miwili wamejipambanua kwa njia ya harambee mbalimbali zinazotangazwa kwa mbwembwe na kelele katika baadhi ya makanisa, misikiti na makundi mengine ya jamii,” alisisitiza.
Alisema kuwa hadi sasa, watu hao wamechangia fedha zinazokadiriwa kufikia Shilingi bilioni saba huku wakiwa wameshaandaa bajeti ya bilioni 10 kwa ajili ya rushwa ya uchaguzi ambayo hawataki iitwe rushwa kwa sababu macho yao yamepofuka.
Alisema kuwa Watanzania hawahitaji shahada ya siasa kubaini watu hao wakifanikiwa katika malengo yao. Alisema uongozi utakaotokana na genge hilo hautaweza kuleta neema kwa Tanzania kwa kuwa ngazi zote za uongozi katika himaya ya aina hiyo, zitajazwa na watu wanaofanana katika maadili potofu.
“Masikini na wanyonge watabanwa mbavu zaidi, matabaka ya wenye utajiri na masikini yatapanuka kiwango ambacho hakitavumilika. Lakini pia ukusanyaji wa kodi na mapato mengine ya serikali utadorora na kudidimiza huduma zote za jamii na kipato cha kila Mtanzania… hatimaye misingi yetu ya umoja na usawa itabomoka na kulitumbukiza taifa katika machafuko,” alisema.
Kuhusu hatma ya taifa kabla na baada ya uchaguzi mkuu, Sitta alisema Watanzania wasipokuwa na mtazamo wa kizalendo na wakasimama kwa dhati ya mioyo yao kupambana na kulikataa jambo hilo, watawaachia watoto wao urithi ambao utatafuna vizazi hata vizazi.
“Dhambi kubwa katika taifa lolote ni pale mbele ya maovu, watu wema wanaamua kukaa kimya. Mimi na wewe tukiamua hali hii ikome sasa, inawezekana na cha msingi ni kurudi nyuma na kujipanga upya kupambana na hali hii kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho,” alisema.
Kuhusu suala la maamuzi magumu, Sitta alisema tatizo jingine linalodhihirisha mgawanyiko wa kitabaka ni kiburi cha baadhi ya viongozi ambao wanatamba kwamba hawawajibiki kwa vyombo vya sheria kama wafanyavyo watu wa kawaida.
Sitta ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliyoambatana na harambee ya kuchangia ujenzi wa chepo ya Seminari hiyo, alichangia Sh. 5,750,000.
Awali akisoma risala ya wahitimu wa seminari hiyo, Shaine Mapunda, alisema inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ukosefu wa zahanati ya shule ambayo husababisha wanafunzi kukosa masomo kwa ajili ya kufuata matibabu hospitali ya Marangu.
“Tunaomba kuongezewa vitabu vya michepuo ya sanaa ili kuongeza ufaulu na ubora kwa wanafunzi wa michepuo ya sanaa, uboreshaji wa viwanja vya michezo ufanyike kwa awamu ili kuzidi kukuza na kuinua vipaji vya michezo mbalimbali,” alisema Shaine.
Mkuu wa Shule hiyo, Sista Elistaha Mlay, alisema shule hiyo yenye mikondo ya kidato cha tano na cha sita yenye jumla ya wanafunzi 548, inakabiliwa na tatizo la uhaba wa maji na umeme hali inayosababisha kero kwa wanafunzi kujisomea. Jumla ya wanafunzi 108 wa kidato cha nne wamehitimu.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Friday, November 15, 2013

MTOTO HUYU ANA MATESO MAKUBWA

MATESO kila kukicha. Kijana Shaggy Sadick mwenye umri wa miaka 18, mkazi wa Musoma mjini, Mkoa wa Mara yuko katika mateso makubwa baada ya tumbo lake kuvimba na kuongezeka ukubwa hali inayomfanya ashindwe kutembea.
 

                                     Shaggy Sadick mwenye umri wa miaka 18, mkazi wa Musoma mjini.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa, dada wa Shaggy, Mariam Sadick, alisema mdogo wake alianza kuumwa ugonjwa huo tokea akiwa na umri wa miaka 12 na kwa muda wote huo, wamehangaika katika hospitali mbalimbali nchini bila mafanikio.
Alisema awali walianza kumpeleka katika Hospitali ya Musoma na baadaye Bugando jijini Mwanza ambako baada ya vipimo, iligundulika kwamba alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo ambao umejaa maji, ugonjwa ambao anapaswa kutibiwa nje ya nchi ili kuumaliza.
“Kwa kweli tumehangaika naye sana kumsaidia apone, lakini imeshindikana kwani ili apone, wanapaswa kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu, kitu kinachotishia uhai wake kwani familia ni duni,” alisema dada huyo.
Dada huyo alizidi kulia kwa kusema kwamba kingine kinachomsikitisha ni kwamba mdogo wake amekosa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu kwani kwa matatizo aliyonayo, hawezi kutembea tumbo limefika hadi magotini.
Alisema wakati wa kulala ukifika, mdogo wake hupata wakati mgumu kwani wanalazimika kumuwekea mito mingi ya kulalia nyuma yake, vinginevyo anaweza kupoteza maisha kwa sababu ya kushindwa kupumua vizuri.
“Kwa kweli kitu ambacho kinatusikitisha wote ni kukosa kufanya mtihani wa kidato cha nne, maana hawezi kutembea tena  wakati wa kulala ndiyo kama hivyo,” alisema.
 Mtoto Shaggy yupo katika mateso makali sana, anahitaji msaada wa hali na mali ili aweze kuyaokoa maisha yake ili apate matibabu, endapo utaguswa na habari yake, wasiliana na chumba cha habari kwa namba  0713 612 533.
 
SOURCE: GLOBAL PUBLISHERS

WACHEKI MABILIONEA WANNE VINARA TANZANIA

Dar es Salaam.
Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz (49), ametajwa kuwa ndiye tajiri namba moja Tanzania kwa sasa.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Jarida la Marekani la Forbes na kutoa taarifa yake juzi, Rostam amekamata nafasi hiyo na ya 27 katika Afrika akiwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni moja (Sh1.6 trilioni).
Mbunge huyo wa zamani wa Igunga, ameingia kwa mara ya kwanza katika orodha ya matajiri 50 wa Afrika ya jarida hilo, pamoja na wafanyabiashara wengine wa Tanzania, Reginald Mengi na Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohamed Dewji ‘Mo’. Katika orodha hiyo pia yumo Said Bakhresa ambaye aliwahi kutajwa siku za nyuma.
Rostam, ambaye aliachana na siasa mwaka 2011, amempiku Bakhresa, ambaye mwaka jana Jarida la Ventures Africa la Nigeria lilimtaja kuwa ndiye aliyekuwa tajiri namba moja wa Tanzania. Bakhressa katika kipindi hicho alikadiriwa kuwa na utajiri wa Dola 620 milioni (Sh971 bilioni).
Katika orodha hiyo ya Ventures Africa, Bakhresa alifuatiwa na Rostam, Mengi na mfanyabiashara mwingine maarufu, Ali Mufuruki.
Mengi anashika nafasi ya pili kwa Tanzania na ya 34 Afrika akiwa na utajiri wa Dola 550 milioni (Sh861 bilioni).
Forbes linaonyesha kuwa Bakhresa amefungana na Mo katika nafasi ya tatu ya orodha ya matajiri wa Tanzania na ya 38 kwa Afrika, wote wakiwa na utajiri wa Dola 500 milioni (Sh783 bilioni).
Rostam, Mengi na Bakhresa hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo huku Mo akisema kwamba asingeweza kuzungumzia suala hilo kwa kuwa jana alikuwa katika mapumziko ya Sikukuu ya Ashura.
Tajiri wa Nigeria, Aliko Dangote, ambaye anajenga Kiwanda cha Saruji huko Mtwara ndiye anayeshika nafasi ya kwanza katika orodha ya Afrika, akiwa na utajiri wa Dola20 bilioni (Sh31.7 trilioni), akifuatiwa na familia ya Johanny Rupert ya Afrika Kusini yenye utajiri wa Dola7 bilioni (Sh10.7 trilioni) na Nick Oppenheimer, pia wa Afrika Kusini mwenye utajiri wa Dola 6.6 bilioni (Sh10.3 trilioni).
 
1)Rostam Aziz
Jarida la Forbes limeripoti kuwa utajiri wa Rostam unachangiwa zaidi na biashara ya mawasiliano ya simu za mkononi, ujenzi na uchimbaji wa madini.
Anamiliki asilimia 35 ya hisa katika Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom. Ni kampuni inayoongoza kwa biashara ya simu za mikononi nchini Tanzania ikiwa na wateja zaidi ya milioni 9.5.
 
Pia anamiliki Kampuni ya Caspian, ambayo inafanya kazi za kuchimba madini katika migodi inayomilikiwa na Kampuni za BHP Billiton na Barrick Gold.
Pia ana hisa katika Kampuni ya Hutchison Wampoa inayofanya kazi za kupakua mizigo bandarini na anamiliki majumba nchini na katika nchi za Mashariki ya Kati.
2) Mengi
Ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP.
Utajiri wake unatokana na kumiliki vyombo vya habari, kiwanda cha vinywaji baridi na madini.
Mengi anamiliki magazeti kumi na moja, vituo vitatu vya televisheni na takriban vituo 10 vya redio.
Pia ana mgodi wa madini ya dhahabu na viwanda vya CocaCola.
Kwa mujibu jarida hilo, Mengi alizaliwa katika familia maskini na baadaye kusomea uhasibu huko Uingereza na kufanya kazi huko.
Alijiunga na Chama cha Wahasibu cha Uingereza kabla ya kurejea Tanzania mwaka 1971 na kuajiriwa na Kampuni ya Ukaguzi ya Coopers & Lybrand Tanzania (sasa Price Water House Coopers) hadi mwaka 1989, alipoacha kazi na kujikita zaidi katika biashara.
3) Bakhresa
Said Salim Bakhresa ni mwasisi na Mwenyekiti wa Kampuni ya Bakhresa Group na ana utajiri wa Dola500 milioni (Sh783 bilioni).
Ni kampuni kubwa inayoajiri zaidi ya watu 2,000 ikijishughulisha zaidi katika kusaga nafaka, kusindika matunda, usafiri wa meli na biashara ya mafuta. Pia kwa kutengeneza pipi na ice cream.
  
Bakhresa aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuanza biashara ya kuuza viazi mbatata. Baada ya hapo alifungua mgahawa na baadaye kuingia katika biashara ya kusaga nafaka.

4) Mo
Mafanikio yake yamechangiwa zaidi baada ya kuendeleza mali ya wazazi wake. Anafanya biashara ya nyumba, kuuza mazao na viwanda vya mafuta.

Mo alirejea Tanzania baada ya kumaliza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Georgetown, Marekani na kuendeleza biashara ya maduka ambayo yalianzishwa na baba yake.

Alinufaika baada ya kununua viwanda vilivyobinafsishwa na Serikali.

Alivifanya viwanda hivyo kutengeneza faida na kuinyanyua Kampuni ya Mohamed Enterprises (MeTL) kuwa miongoni mwa kampuni zenye mafanikio makubwa Tanzania.

Mo pia anajihusisha na biashara ya usambazaji bidhaa, viwanda vya nguo na kilimo.

Jarida hilo lilipiga hesabu za utajiri wa wafanyabiashara hao kwa kuangalia thamani ya bidhaa zinazouzwa na kampuni zao, mikataba yao na hasa wale walio kwenye sekta ya mafuta na ukubwa wa kampuni zao.

SORCE: MWANANCHI

Thursday, November 14, 2013

WAZIRI MSTAAFU ADAIWA KUBAKA MTOTOTO WA SHULE
























MBUNGE wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), ameingia katika matata. Katika kujaribu kudhibiti mtoto wa shule ambaye anadai alibakwa naye na kuambukiwa virusi vya ukimwi, mbunge huyo ametoa vitisho vya kuua mtoto huyo na kujiua kama njia ya kuepuka dhahama inayoelekea kumkabili. 
Siku moja baada ya gazeti hili kuripoti habari za mbunge mmoja (bila kumtaja jina), jana asubuhi Profesa Kapuya ameibuka na kumtisha mwanafunzi huyo mwenye miaka 16 anayesoma Shule ya Sekondari Turiani iliyoko Magomeni jijini Dar es Salaam.

Baada ya kujua kuwa mtoto huyo ndiye alitoa habari za masahibu hayo, ambayo mbunge hakutaka yajulikane, alimpigia simu mtoto huyo, na baadaye kutuma meseji kadhaa za vitisho.

Jana Tanzania Daima ilishuhudia baadhi ya meseji za simu zilizotumwa na Mbunge huyo kwenda kwa mtoto huyo.

Alfajiri saa 11:21 kupitia simu yake ya mkononi yenye namba 0784993930, Mbunge huyo alituma ujumbe ufuatao kwa mtoto huyo: “chagueni kunisubiri tuje tuongee au mnataka kufa?”

Baadaye saa 1:07 asubuhi, alituma ujumbe mwingine kutoka simu hiyo hiyo kwenda kwa mtoto huyo, ukisema: “Mkiuawa, itakuwa nzuri, itawapunguzia gharama za kuishi. Usitake kugombana na serikali, mtoto mdogo kama wewe. Sisi ndo wenye nchi yetu.
“Mwambieni Mbowe mwenye hilo gazeti awape nyumba ya kuishi. Si mmemuingizia hela leo? Mnatumika bure watu wanaingiza hela nyingi, mmenitibua lazima niwauwe wiki hiii haitaisha, nitapanga kambi popote.

“Jana si wamekuficha? Tuone kama utalindwa milele. Kazi ya kulindwa imeisha, maana wameshatengeneza hela. Lazima mvae sanda. Hilo sio ombi, ni wajibu wenu. Mnajitia mafia watoto sio? Watoto wetu wanauza unga, nani anawakamata? Nani atapigana nasi?”

Hata hivyo, baada ya kuhisi kuwa watoto hao wamedhamiria kumchukulia hatua, na wamewasiliana na taasisi mbalimbali za kiraia na serikali zenye uwezo wa kumtia adabu, mbunge huyo alimtumia mtoto huyo ujumbe wa kuonyesha alikuwa anafikiria kunywa sumu.

Ujumbe huo uliotumwa kwa mtoto huyo saa 11:2 3 ulisema: “nimwakosea sana, acha nife mie nakunywa sumu nijiue, na nyie mje mnizike.”

Hasira za Mbunge huyo dhidi ya mtoto hao zilitokana na hatua ya mtoto huyo na dada yake kufichua unyama wanaodai kutendewa na mbunge huyo, ambaye amewahi kushika nyadhifa kadhaa za uwaziri katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Tangu alipogundua kuwa mtoto huyo alizungumza na gazeti hili juzi, saa 5:17 usiku wa kuamkia jana alituma ujumbe usemao: “Si mpo Bilz? Sasa tupo pamoja na nyie mpaka usiku.”

Baadaye saa 5:31 alituma ujumbe  huu: “Hivi hamkubali kushindwa? Leo ulifuata nini ofisi ya CCM?”

Ujumbe huo ulitokana na ukweli kwamba dada wa mtoto anayedaiwa kubakwa alifika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) juzi asubuhi kuonana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, ili kuomba chama kimsaidie kumbana Profesa Kapuya, ambaye alikuwa ameanza kuwatisha yeye na mdogo wake.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mtoto huyo, Kinana alisema suala hilo si la chama bali la Profesa Kapuya binafsi.

Mtoto huyo alikataa ushauri wa kupeleka shauri hilo mbele ya vyombo vya sheria, akidai kuwa jitihada zake zimekuwa zinazimwa na mbunge huyo anayedai serikali haiwezi kumfanya lolote.

Alisisitiza kuwa hana imani na serikali, lakini akasema yupo tayari kuchukua hatua kali dhidi ya Profesa Kapuya iwapo atasimamiwa na watetezi wa haki za binadamu.

Baadhi ya mashirika yanayotetea makundi kadhaa yakiwamo Kituo cha Sheria na Haki za BInadamu (LHRC) na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) yalijitokeza kumsaidia watoto hao, ambao ni yatima.

Mtoto huyo na dada yake, wakizungumza na gazeti hili kwa hofu mafichoni, walisema kwa sasa hawana imani tena kama kuna serikali nchini Tanzania kwa kuwa wamedhalilishwa, wametembezwa hadi Bungeni na wabunge bila hatua kuchukuliwa, licha ya kutoa taarifa katika kituo cha polisi Oysterbay tangu mwaka jana.

Hata hivyo, kabla ya tukio la watoto hao kuripoti, ofisi za gazeti hili juzi usiku kulikuwa na watu waliokuja wakiwatafuta watoto hao, huku wakiwatisha kwa simu na kuwatolea maneno ya kejeli, wakidai watawamwagia tindikali.

Mmoja wa watoto hao, alidai kuwa miongoni mwa vijana waliokuwa wanawatisha juzi walikuwa katika gari T170 BGY, Benz, Cream Metalic, ambayo inamilikiwa na mbaya wao.

Jana gazeti  hili lilichapisha habari kuwa  mwanafunzi huyo aliyesema kuwa waziri huyo  alimbaka kwenye hoteli moja ya kitalii iliyoko jijini Dar es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012 alipoitwa kwenda kuchua ada kwa mara ya pili. 

Akizungumza kwa uchungu, alisema mbunge huyo alifanya kitendo hicho kwenye Hoteli ya Giraffe, Jijini Dar es Salaam mwaka 2011.

Alisema kuwa yeye alikuwa na urafiki na mwanafunzi mwenzake Zuhura Mwaking’inda. Mwaking’inda amewahi kuwa Diwani wa Kata ya Sinza Jimbo la Ubungo, Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo, rafiki yake (mtoto wa Mwaking’ida) alikuwa amepooza hivyo alikuwa analazimika kumhudumia hali iliyowaunganisha hadi huyo mtoto alipochukua jukumu la kumtambulisha kwa baba yake ambaye naye alimtambulisha kwa Kapuya ili aweze kumsaidia fedha kwa jili ada.

Mwanafunzi huyo alisema baada ya kutambulishwa aliitwa katika hoteli moja jijini Dar ambapo baada ya kufika mapokezi wafanyakazi wa  hoteli hiyo walimkataza kuingia chumbani katika maana kwamba umri wake alikuwa mdogo (mwaka 2011 alikuwa na miaka 14), lakini Kapuya aliamrisha aje chumbani pamoja na dereva na kumwingiza kwa nguvu.

Akiwa chumbani alimlazimisha kulala naye kisha kumpa sh laki saba, badala ya sh elfu sitini na saba kiasi ambacho kilikuwa ndio mahitaji halisi ya ada.

Mwanafunzi huyo amesema baada ya muhula mmoja aliitwa tena na mbunge huyo katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala tarehe 3 June 2012, ambapo pia alimlazimisha kulala naye kwenye zulia la ofisi yake, kisha kumpa sh 350,000/.

Alisimulia kwamba wakati anatoka kwa huzuni ofisini kwa mbunge huyo, mmoja wa wahudumu wa hapo alimuuliza kwanini anatoka kwa huzuni, alimweleza kisa hicho, na huyo mama aliangua kilio kwa kumwambia “mwanangu umekufa pole tu, huyu baba ni muathirika wa ukimwi”.

Aliongeza kuwa baada ya kuambiwa vile alilia na kufanya fujo hapo mapokezi hadi alipokamatwa na walinzi wa kisha kupelekwa kituo cha polisi kufunguliwa mashtaka, lakini akiwa polisi alipoeleza mkasa wote, Polisi walilazimika kumwita Kapuya na wakawasuluhisha kwa makubaliano kwamba Kapuya atakuwa anamlipia ada, na kumpa pesa za matumizi sh. laki tatu kila mwezi, jambo ambalo amekuwa akilitekeleza kupitia simu yake ya mkononi 0755993930.

Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo, 24 Januari 2013, alifika mtu nyumbani kwao mtu mmoja (jina tunalihifadhi) na kujitambulisha kuwa yeye ni jambazi na kuwa alitumwa kwenda kuwaua kwa malipo ya sh. milioni 50, lakini alipokuta ni watoto wadogo aliwasamehe, na kusema yeye ni jambazi sugu hawezi kupoteza nguvu zake kuua vitoto.

Alienda akiwa na bastola, maji kwenye chupa yanayodhaniwa kuwa ni tindikali na bomba la sindano. Kwa mujibu wa mtoto huyo, jambazi huyo anasema kuwa tayari alilipwa milioni 15 za awali.

Mtoto huyo alisema jambazi huyo aliwambia kuwa yeye ni rafiki wa mtoto wa Kapuya na wanamfahamu vizuri, lakini hataweza kuaua baada ya kubaini kuwa wao ni yatima tu.

Hata hivyo kufikia mwezi Februari mwaka huu, mtu asiyefahamika alienda nyumbani na kutelekeza gari aina ya T.199 BGY Mercedes Benzi ya Blue wakati wanafunzi hao wakiwa shuleni, kisha kuacha ufunguo kwa jirani yao kwa maelekezo kuwa wakifika awapatie.

Na Kapuya aliwapigia simu kuwaarifu kuwa amempa zawadi ya gari kwa ajili ya matumizi ila yeye na dada yake wanaruhusiwa kuuza ili wapate pesa kwa ajili ya mahitaji yake siku zilizosalia, kwani muda sio mrefu baada ya uchguzi mkuu 2015, Kapuya atakuwa Waziri Mkuu, hivyo itakuwa ngumu yeye kumtumia huyo binti pesa kama alivyoelekezwa na jeshi la polisi kituo cha Oysterbay.

Baada ya mwanafunzi huyo na dada yake ambaye ana umri wa miaka 20, kupewa gari walishindwa kulitumia hivyo kutoa taarifa polisi kwani kwa kupokea gari hilo  ilikuwa ni kuwatelekeza kwani yeye hana hata hela ya kuweka mafuta ya gari, hivyo walienda polisi ili kesi ipelekwe mahakamani kumshtaki kapuya.

Polisi wa Oysterbay walikubali kulipeleka tatizo hilo kwa Katibu wa Bunge, ambaye alimwita mwanafunzi huyo na mdogo wake waende Dodoma kukutana na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ingawa walipofika Dodoma walikaa na kamati ya hiyo kwa maelezo kuwa Kapuya hakuwepo hadi Bunge lilipoisha walirejeshwa Dar es Salaam.

Mtoto huyo na dada yake alitoka ofisi za CCM lakini akiwa anaelekea kituo cha basi alithadharishwa na mwanafunzi mwingine kwa haraka kuwa akimbie kwa kuwa atamwagiwa tindikali na watu waliokuwa wanamfuata nyuma, alikimbilia katika mtaa wa Hoteli ya Star light kisha aliomba msaada baada ya kupotea njia na hivyo alisaidiwa na mama mmoja kufikishwa chumba cha habari cha Channel Ten.

Ni katika chumba hicho ndio mwandishi wa habari hizi alienda na kuwakuta watu wawili hao waliokuwa wanamhitaji binti huyo lakini walikatazwa kumchukua.

SOURCE: TANZANIA DAIMA