LATEST POSTS

Wednesday, December 18, 2013

YADAIWA JEURI YA FEDHA YA WEMA IMEKWISHA

Wema Isaac Sepetu.
Stori: Oscar Ndauka na Richard Manyota
NI kweli hakuna marefu yasiyokuwa na ncha? Kama ni kweli, basi ile jeuri ya fedha ya Miss Tanzania mwaka 2006 ambaye pia hufanya vyema kwenye gemu la sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu inadaiwa imefikia nchani, Risasi Mchanganyiko limepashwa ‘ei tu zedi’.

Baadhi ya magari anayomiliki Wema.
Kwa mujibu wa chanzo makini, hali ya kifedha ya staa huyo si nzuri kiasi kwamba kwa sasa amekuwa mtu wa kushinda ndani kwa kuwa hana mpunga unaomuwezesha kwenda kujirusha kama zamani.
SABABU NI NINI HASA?
Chanzo kilidai kwamba, binadamu aliyekuwa akimmwagia manoti staa huyo aliyetajwa kwa jina moja la Clement ambaye ni mwajiriwa wa Ikulu jijini Dar, yu hoi kwa kipato baada ya kunyofolewa kwenye kitengo kilichokuwa na uwezeshaji mwingi wa fedha.

Wema akiwa ofisini kwake.
Inadaiwa kuwa, baada ya Clement ambaye ni mume wa mtu, kuondolewa kwenye kitengo hicho amepelekwa sehemu nyingine ambayo mchana kutwa ni kupiga miayo mpaka muda wa kutoka kazini.

MKONO WA MKEWE WATAJWA
Katika madai hayo, inasemekana mke wa Clement (jina tunalo) ana mkono wa kile kilichompata mumewe, kuondolewa kwenye kitengo chenye ulaji na pia amekuwa akiwawinda wawili hao ili awafanyie fumanizi kwa sababu Clement ni mumewe wa ndoa.
Wema akiwa ndani ya nyumba aliyodai yake.
KILICHOTOKEA SASA
Chanzo kikaendelea: “Baada ya kuondolewa kwenye sehemu yenye fedha na kutupwa kwenye ukame, jamaa akaanza kupata tabu kwani fedha alizokuwa akimpa Wema zamani zikawa hazipo.
“Hilo likamwathiri na Wema mwenyewe kwani ile jeuri mliyokuwa mnamuona nayo akiifanya kwa rungu la fedha, mara sherehe, mara kumlipia Kajala (Masanja) makahamani (Kisutu), mara kwenda baa na wapambe imekatika ghafla.
“Siku hizi Wema ndani na yeye, yeye na ndani. Naamini hata mkienda kwake muda huu (juzi Jumatatu saa 5 asubuhi) mtamkuta.”

INADAIWA AMEUZA MAGARI MAWILI
Habari zaidi kutoka chanzo hicho, hali ilipozidi kubana sana, Wema aliamua kuuza magari mawili kati ya matatu anayomiliki ili apate fedha za kuendelea kujikimu katika maisha ya kila siku.
Magari hayo mawili yanasemekana ni Toyota Mark II GX 110 na Toyota Harrier na kubakiwa na Audi Q7.

YALIYOMPATA CLEMENT
Habari zinazidi kudai kwamba hali ikazidi kuwa mbaya kwa Clement kiasi kwamba alijikuta akikabwa koo na benki moja ya jijini Dar es Salaam ambayo aliiomba mkopo wa Shilingi mil. 120 akitumia hati ya nyumba ambayo pia si yake.

Benki hiyo ilipozidi kumbana, mkewe (sasa wametengana) ambaye naye anadaiwa kuwa ‘mzuri’ kwenye fedha alikwenda kulipa fedha hizo benki ili nyumba ya watu isinadiwe na benki hiyo iliyokuwa haitaki mambo ya utani kwenye marejesho.
Madai mengine ambayo hayajathibitishwa yanasema kuwa, mtikisiko huo wa kifedha kwa Clement umesababisha awe ‘choka mbaya’ kiasi cha sasa kuanza kupiga mizinga kwa rafiki zake.

WEMA ASAKWA ASEME UKWELI WAKE
Baada ya kupokea ishu hiyo, Risasi Mchanganyiko liliamua kumsaka Wema ili aseme lolote kuhusiana na tuhuma hizo.
Saa 4:32 Wema alipigiwa simu yake ya mkononi ambayo iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa hata pale iliporudiwa tena na tena.
Baada ya jitihada hizo kugonga mwamba, gazeti hili liliamua kumwendea hewani meneja wake Martin Kadinda ambaye naye hakupokea simu licha ya kupigiwa zaidi ya mara tatu.

Risasi Mchanganyiko halikukata tamaa, kwani ni haki ya msingi kwa Wema kuongelea suala hilo. Likampigia msaidizi wake wa karibu anayeitwa Pat Man, yeye alipokea, akaulizwa kuhusu bosi wake huyo, akasema:
“Wema anaumwa (hakutaja ugonjwa), ametoka hospitali sasa hivi  (hakusema hospitali gani) yuko nyumbani.”
Mapaparazi wetu wakafunga safari kutoka Bamaga – Mwenge, Dar yalipo Makao Makuu ya Nyumba ya Magazeti Pendwa Bongo, Global Publishers hadi nyumbani kwa Wema - Makumbusho (lakini ni Kijitonyama).

Getini alikutwa mlinzi mahiri kwa mwonekano ambapo alipoombwa kumwita Wema au kumwambia kuna waandishi wa Global wapo nje, alisema:
“Mh! Kwa kweli si rahisi kutoka, amelala anaumwa... alikwenda hospitali amerudi muda si mrefu.”
Alipochombezwa kwa maneno ya ‘kisiasa’ kwamba awaambie wasaidizi wake wa ndani wakamwamshe, alikataa akisema litazuka timbwili ambalo yeye hakuwa tayari kuliona.
“Bosi akilala huwa hapendi kuamshwa, hasa kama hayuko sawa. Watu wanaomwamsha ni wale wenye ahadi naye,” alisema mlinzi huyo.

WEMA ATUMIWA MESEJI
Baada ya kuondoka nyumbani kwa Wema, Risasi Mchanganyiko lilimtumia ujumbe mfupi (SMS) ‘mreeefu’ wenye madai yote na ikaonesha ‘delivered’ kwenye simu ya Wema, lakini pia haikujibiwa.

TUNARUDI KWA CLEMENT  
Simu yake haikuwa ikipatikana hewani alipopigiwa ili na yeye apewe nafasi ya kusema lolote kuhusu sakata hilo.

MKE WA CLEMENT AVUNJA UKIMYA
Risasi Mchanganyiko liliamua kumsaka kwa simu ya mkononi mke wa Clement ambapo alipopokea na kusomewa mashitaka ya mumewe na nafasi yake kama shahidi muhimu alikiri hali ya jamaa kuwa tete kimfuko.
“Kuhusu hilo la nyumba ni kweli ilikuwa inadaiwa na benki (aliitaja jina) na walitaka kuinadi ili wapate fedha zao, lakini nikaingilia kati ili kulinda heshima ya familia.

“Unajua ile nyumba kuna mtu alituuzia, kwa hiyo Clement alitoa kiasi cha fedha lakini hakumalizia na akatumia hati ya nyumba kwenda kuombea huo mkopo. Kwa sababu benki walikuja juu nilitafuta mtu akainunua, kiasi cha fedha nikammalizia aliyetuuzia na kulipa benki,” alisema mwanamke huyo.
KUHUSU KUMFANYIA FITINA MUME AKAHAMISHWA KITENGO
Huyu hapa mke wa Clement: “Hilo si kweli bwana. Kwanza mimi ndiyo nilimfikisha pale alipofika. Sasa mtu nimuinue mwenyewe nitamfanyiaje fitina?
“Kwanza mimi siko naye siku hizi. Nilipoona anachukua magari ya nyumbani na kuyapeleka huko kwa nani sijui (Wema) nikaamua kukaa pembeni na kunyamaza kimya.
“Kama ni mabalaa anayapata hukohuko aliko, nisisingiziwe mimi kwa lolote lile.”

KUHUSU KUMWANDALIA FUMANIZI WEMA
“Aaa wapi! Nimwandalie fumanizi la nini? Yeye ana maisha yake mengine mimi niko na mambo yangu, muda huo sina kabisa, yaani niko bize sana,” alisema mwanamke huyo huku akidai muda huo alikuwa akidraivu.

PRODYUZA WA WEMA ALIJUA HILI?
Wiki mbili zilizopita, gazeti damu moja na hili, Ijumaa Wikienda liliandika katika ukurasa wake wa mbele habari yenye kichwa; MAGARI YA WEMA YAGEUZWA GESTI.
Katika habari hiyo, Wema alidaiwa kumtimua kazi prodyuza wake katika Kampuni ya Endless Fame, Rashid Mohammed ‘Chid Classic’ kwa sababu ya kumtuhumu kufanya ufuska kwenye magari yake maeneo ya Ufukwe wa Coco, Dar.

Siku chache mbele, prodyuza huyo alifunguka katika gazeti lingine pendwa ndani ya mjengo, Amani kuwa, Wema ‘amechoka’ siku hizi, halipi mishahara wafanyakazi wake na alitaka yeye awe kuwadi ndiyo wangeendana jambo ambalo yeye hakuwa tayari.

Baadhi ya habari zilizowahi kuandikwa na magazeti ya GPL kuhusu jeuri ya fedha ya Wema.

HABARI NYINGINE YA MJINI Yapo madai kuwa, kutokana na maswahibu hayo ya kuwa kwenye wakati mgumu kifedha, kampuni yake imeanza kudoda na mbaya zaidi, marafiki zake anaokuwa nao kwenye raha, wamemkacha na kumwacha akihangaika mwenyewe.
“Msiniandike gazetini lakini ukweli ni kuwa, huu ndiyo wakati wake wa kujifunza kuchagua marafiki. Ona sasa, wale wote aliokuwa akila nao raha, wamekaa pembeni. Ni tatizo sawa, lakini pia ni funzo kwa upande mwingine,” alisema mpambe mmoja anayefanya naye kazi kwa karibu sana.
Chanzo: GPL

WOSIA WA LADY JAY DEE IKITOKEA AMETANGULIA MBELE ZA HAKI KABLA YA RUGE NA JOSE KUSAGA

Katika pitapita zangu nimekutana na wosia huu wa lady jay dee katika mapambano ya kupigania haki yake. Nami nimeona ni vyema nanyi muuone ikiwa hamkubahatika kuona.

Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.

Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.

Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.

Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.

Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.
Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.

Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.
Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.

Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.

Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.

Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame
Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.

Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai
Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.

Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.

Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..

Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.

Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani??
Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??

Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.

Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma??
Roho gani hiyo??

Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu

JIDE

Tuesday, December 17, 2013

WATU SABA WATIWA MBARONI KWA MAUAJI YA MWENYEKITI WA ZAMANI WA CCM MKOA WA MWANZA

Kilima cha Kanyama lilicho sababisha mauti, kilichokuwa kinamilikiwa na marehemu Mabina kwa kuridhiwa na serikali ya kijiji iliyotoa hati ya umiliki.
Kutoka barabara kuu ya Mwanza - Musoma kona ya kuelekea kijiji na kilima cha Kanyama, kwa kawaida eneo hili huwa lina changamka sana likiwa na watu na pilika pilika za biashara lakini limepwaya kana ndiyo kunakucha vile kumbe laa! 
Njia yenyewe ndiyo hii ambayo pia marehemu aliitumia kupita wakati akikimbia kujiokoa baada ya kundi la watu waliokuwa wakishambulia.
Ni kona ambayo ndipo shambulizi lilianzia huku marehemu akijivuta taratibu kuelekea eneo la msaada.         
Marehemu alifika eneo hili akijaribu kukimbilia katika moja ya nyumba zinazo onekana mbele ili kupata msaada wa kujiokoa.
Lakini kabla hajafika katika nyumba hizo eneo lililo zungushiwa duara ndipo alipo anguka baada ya kupigwa jiwe kichwani na kuanguka chini nakuanza kushambuliwa kwa mawe hadi mauti yalipomkuta. 
Kwa ukaribu zaidi na pembeni ni baadhi ya mawe yaliyo tumika kumshambulia.
Ndivyo alivyokutwa na mauti mwenyekiti huyo wa zamani CCM.
Nyumbani kwa marehemu na sehemu ya waombolezaji.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo (kulia) pamoja na Mkuu wa Usalama mkoa (kushoto) wakimfariji mjane wa marehemu Clement Mabina.
Meya wa Manispaa ya Ilemela Henry Matata (mwenye tai) ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa marehemu Mabina ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mazishi na hapa akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo.
Baadhi ya waombolezaji.
Huzuni kubwa imetawala kwa wafanyakati wa Mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Mwanza (MWAUWASA) nyumbani kwa marehemu.
WATU saba wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza wakituhumiwa kuhusika na mauaji ya kinyama ya aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Clement Mabina.

Watu hao wamekamatwa wakati hofu ikiwa imewakumba wakazi wa maeneo ya Kisesa na Kanyama, eneo ambalo marehemu Mabina aliuawa na watu wenye hasira katika kile kilichoelezwa kuwa mgogoro wa mashamba.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, SACP,Valentino Mulowola, akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya simu, alisema hadi sasa watu saba wanashikiliwa na jeshi hilo.

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti jana,ambapo jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine wanaodaiwa kuhusika katika mauaji ya Mwenyekiti huyo wa zamani wa CM Mkoa wa Mwanza.

“Tunaendelea na upelelezi wa tukio hili la mauaji ya kinyama  ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika na kuna maendeleo mazuri.Tuna washikilia watu saba wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji hayo,” SACP Mulowola

Katika tukio hilo la mauaji, Mabina aliuawa kwa kukatwa mapanga na kupigwa mawe ambapo alikutwa na majereha makubwa kichwani kichogoni.

Kabla ya kuawa na wananchi  hao,marehemu alimpiga risasi mtoto Temeli Malemi kwa (11) bahati mbaya wakati akijihami na mashambulizi ya wananchi hao.

Ilielezwa jana na Kamanda wa Polisi SACP Mulowola kuwa marehemu alikutwa na silaha mbili aina ya Short-gun na bastola moja.

Hata hivyo ndugu wa marehemu walishindwa kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari kuhusiana na habari zilizoandikwa na mitandao ya kijamii ikihusisha kifo cha Ndugu yao (Mabina) na masuala ya kisiasa.

Aidha habari kutoka eneo la tukio mmoja wa watuhumiwa waliokamatwa alikutwa na simu ya mkononi ya marehemu,hata hivyo kamanda hakutaka kutaja jina lake na watuhumiwa wengine kwa madai ya kuwa kutaja majina kungeweza kuvuruga upelelezi.  
  
taarifa za baadhi ya watu waliokuwa wakinong’ono kuwa kundi linalosadikiwa kuhusika na mauaji hayo lilijiandaa kufanya kitendo hicho cha kinyama.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa tayari hofu kubwa na taharuki imewakumba wakazi wa kijiji cha Kanyama na baadhi wameyakimbia makazi yao wakihofia kukamatwa.

Kwa upande wa familia , mdogo wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Timoth Grigory Mabina alisema kwamba tangu kutokea kifo cha Kaka yake kumekuwa na upotoshwaji wa taarifa za tukio hilo unaofanywa na mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kwa kuripoti kwa utashi wa kisiasa zaidi kuliko ukweli.

Akizungumza nyumbani kwa marehemu alisema kuwa taratibu za mazishi bado zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuwasubili watoto wawili wa marehemu walioko nje ya nchi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama alisema baada ya kupata taarifa za tukio hilo akiwa nje ya Mkoa huo alipokea kwa maskitiko makubwa na kushangazwa na watu ambao walitekeleza unyama huo baada ya kuamua kujichukulia sheria mkononi.

Mhandisi Ndikilo alisema kwamba serikali inaendelea kufanya uchunguzi wake kupitia vyuombo vya dola na kutoa wito kwa wananchi wa Kisesa na eneo la Kanyama kuwa watulivu na hakuna haja ya kukimbia nyumba zao kwa hofu ya kukamatwa na Polisi.

"Napenda kuwaeleza wananchi kuwa vyombo vya dola havitawakamata hovyo wananchi hao na wanaokimbia ni wale wanaodhaniwa ni waliotekeleza unyama na kutaka kuwa watulivu na kuisaidia serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kuwakamata watu waliohusika na si vinginevyo.

Kwa mujibu wa taarifa za hivi punde baada ya kuwasili kwa kijana mkubwa wa marehemu kutoka nchini Uingereza zimeeleza kuwa huenda mazishi ya mwenyekiti huyo wa zamani wa CCM mkoa wa Mwanza, Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Magu, Mjumbe wa Bodi ya NCU 1984 Ltd, Mjumbe wa Bodi ya MWAUWASA, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Mdau wa sekta ya Kilimo cha Pamba na mazao mengine ya chakula, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kisesa hadi mauti yanamkuta yanatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi juma hili.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwasili kesho na kuhudhuria mazishi ya mama yake Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Melick Sadiki aliyefariki leo sanjari na msiba huo wa mwenyekiti wa zamani ambaye alimuongoza kuomba kura kwa wananchi wa Mkoa huu katika Wilaya 7 katika Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 akiwa Mwenyekiti wa CCM kabla ya kushindwa uchaguzi wa CCM mwaka jana (2012) na mwenyekiti wa sasa Dkt. Anthony Dialo.
Chanzo: GSENGO BLOG

HALMASHAURI YA MANISPAA YA TABORA YATENGA HEKTA 14 KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI

HALMASHAURI ya Manispaa Tabora inatarajia kutenga jumla ya hekta 14 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa hiyo, Alfred Luanda kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya hiyo (DCC) kilichoketi kwenye ukumbi wa manispaa hiyo.
Luanda alisema awali manispaa ilitenga eneo la ujenzi wa hospitali hiyo karibu na kambi ya Wachina, lakini kiwanja hicho kilikuwa hekta 6.2 huku ramani iliyotoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) inahitaji kuwa na hekta 12.
Alisema waliamua kukaa kama menejimenti ili kuomba eneo la Shule ya Sekondari Wasichana Tabora kwa kuwa kuna eneo lenye ukubwa wa hekta 97.
Luanda alisema baada ya kutembelea na kuliona eneo hilo, waliomba hekta 14 hasa kwa kuzingatia baadhi ya wavamizi wameanza kuingia katika eneo hilo.
“Kutokana na mchakato huo, hakuna ofisi yoyote waliyokwenda kupata ushauri wa maamuzi hayo na ndipo kwenye kikao cha kamati ya ulinzi na usalama wilaya waliafikiana suala hilo,” alisema.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa kikao cha Baraza la Madiwani pamoja na cha Bodi ya Shule ya Sekondari wasichana Tabora waliunga mkono hatua ya kumega eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo.
Chanzo:Tanzania Daima

FAMILIA 30 ZAKOSA MAKAZI



mafuriko

ZAIDI ya familia 30 za wakazi wa kijiji cha Kasense nje kidogo ya Manispaa ya Sumbawanga, wamekosa pahala kuishi baada ya nyumba zao kubomolewa na nyingine kuezuliwa mapaa kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha.
Mvua hiyo iliyonyesha juzi kuanzia saa 9 alasiri na ilidumu kwa saa mbili huku upepo huo ukiangusha miti na kuwatia hofu wakazi wa kijiji hicho.
Diwani wa Kasense, Cretus Jumbe, alisema mvua hiyo pia iliharibu madarasa matatu na nyumba mbili za walimu katika shule ya Msingi Kasense ambazo nazo ziliangukiwa na miti kwenye mapaa yake.
Jumbe alisema hadi sasa kuna takriban nyumba 32 zilizopata madhara hayo ambapo familia zote zimehifadhiwa kwa ndugu na jamaa zao wakisubiri msaada zaidi toka serikalini.
Mkururugezni wa Manispaa ya Sumbawanga, William Shimwela, ambaye alifika eneo hilo muda mfupi baada ya maafa hayo, alisema timu ya wataalamu inatarajiwa kufika leo kufanya tathmini ya maafa na kuangalia ni msaada upi wa haraka unatakiwa.
“Tutakaa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ambaye ni Mkuu wa wilaya ili kuona hatua zingine zinazofuata kwani tayari tumejionea hali halisi ya wananchi walivyoathirika kutokana na tukio hilo na wanahitaji msaada wa haraka kwa sababu hawana sehemu za kuishi,” alisema Shimwela.
Alisema madarasa yaliyoharibika yanahitaji ukarabati kabla ya Januari mwakani, ili wanafunzi waweze kuendelea na masomo.
Chanzo: Tanzania Daima

DK. SLAA AIBUA UFISADI CHC




Dk. Willibrod Slaa
 
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amedai kupata nyaraka za siri zinazobainisha ufisadi ulioko nyuma ya mashirika yaliyobinafsishwa chini ya Shirika Hodhi la Serikali (CHC).
Amesema nyaraka alizonazo ambazo serikali ya CCM inakusudia kuzifanya kuwa za siri zimechambua namna Tanzania inavyopata hasara kutokana na ubinafsishaji holela uliofanywa kwa mali za Umma.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana mjini Urambo wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Urambo Square.
Alisema mengi ya mashirika hayo ni yale yaliyoanzishwa wakati wa utawala wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kuwasaidia wananchi.
Alitaja baadhi ya mashirika hayo kuwea ni pamoja na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), ambayo alisema serikali inamiliki asilimia 30 ya hisa pasipo wananchi kuambiwa.
Aliongeza kuwa NBC ni moja ya mashirika ya umma yaliyobinafsishwa kiholela kwa kwa thamani ya sh bilioni 15 zilizokuwa mali kauli.
Alisema nyaraka hiyo amewatumia wabunge wa chama chake na kuwaagiza waihoji serikali bungeni ili iwajibike kwa wananchi kueleza kwa nini rasilimali zao zinafujwa na viongozi wanaotakiwa kubeba dhamana ya kuongoza nchi.
“Mikononi mwangu hapa ninazo nyaraka ambazo wao wanataka ziwe za siri, wakati inahusisha ufisadi mkubwa wa rasilimali za Watanzania.
“Wananchi wenzangu mtakumbuka kuwa Mwalimu Nyerere, alianzisha mashirika ya umma yapatayo 435, ambayo moja ya madhumuni ilikuwa ni kuzalisha ajira kwa vijana wetu,” alisema Dk. Slaa.
Aliongeza kuwa madhumuni ya Mwalimu katika mashirika hayo ilikuwa fedha zinazopatikana kutokana na uendeshwaji wa mashirika hayo zitumike katika kuboresha huduma muhimu kama afya na elimu kwa kujenga zahanati, hospitali na shule za ngazi mbalimbali katika ubora unaostahili.
Dk . Slaa anaendelea na ziara mkoani Tabora kwa kufanya mikutano mbali mbali na leo atakuwa jimbo la Tabora mjini.
CHANZO: Tanzania Daima

Thursday, December 12, 2013

MWONEKANO MPYA WA MWANADADA AGNESS MASOGANGE



Pichani juu ni taswira za mpya za Video Queen wa Bongo, Agness Gerald 'Masogange' alizotupia kupitia ukurasa wake wa Instagram.

CHANZO: GPL

Wednesday, December 11, 2013

PICHA ZA MAANDAMANO YA WAFUASI WA ZITTO KABWE.. WALIOPINGA UJIO WA DK.SLAA KATIKA JIMBO LA ZITTO KIGOMA KASKAZINI

HIZI NI BAADHI YA PICHA YA WAANDAMANAJI WALIOPINGA UJIO WA DK.SLAA KUFIKA JIMBO LA ZITTO LA KABWE HUKO KIGOMA KASKAZINI NA MABANGO 








HAYO NI BAADHI YA MANENO YA WAZEE WA KIGOMA NA UBANI ULIOCHOMWA KUFIKISHA UJUMBE KWA DK.SLAAA



HUO NDO UBANI ULIOCHOMWA NA WAZEE WA KIGOMA KUMUONYA DK.SLAA ASIPOSIKIA NA KUU ATAVUNJIKA MGUU USICHEZEE NA WAZEE WA KIGOMA UNAAMBIWA KIGOMA MWISHO WA RELI....

HUO CHINI NDO UBANI ULIOCHOMWA NA WAZEE WA KIGOMA ..AKA MWISHO WA     RELI USICHEZEE NA                                               KIGOMAA