LATEST POSTS

Friday, January 3, 2014

KIGOGO WA WEMA ATANGAZA VITA NA DIAMOND

Stori: Shakoor Jongo
Yule kigogo au taita aliyekuwa akimpa jeuri ya fedha Wema Isaac Sepetu ajulikanaye kwa jina moja la Clement anadaiwa kutangaza vita na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.
Habari ‘hoti’ zinadai kuwa Clement anataka Diamond arudishe gharama alizomgharamia Wema ndipo waendeleze mapenzi yao.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa kigogo huo, Clement anadai kwamba gharama alizotumia kwa Wema ni kubwa mno lakini bidada hakujali chochote na kuukabidhi moyo wake kwa ‘Mtoto wa Tandale’ ambaye ndiye barafu wa moyo wake.

Stori: Shakoor Jongo
Yule kigogo au taita aliyekuwa akimpa jeuri ya fedha Wema Isaac Sepetu ajulikanaye kwa jina moja la Clement anadaiwa kutangaza vita na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.
Habari ‘hoti’ zinadai kuwa Clement anataka Diamond arudishe gharama alizomgharamia Wema ndipo waendeleze mapenzi yao.

“CK (Clement) anaumia sana kuona kuwa ameteketeza fedha nyingi kwa Wema lakini bila hiyana, mrembo huyo akabwaga manyanga kisha akarudisha mpira kwa kipa na kuanza moja huku kaka mkubwa akiachwa kwenye mataa,” alitonya mnyetishaji huyo bila kufafanua kama Clement aliachwa mataa ya eneo gani.

Akiendelea kutiririka bila kuweka nukta au ya mkato, mtu huyo alisema kuwa kiasi ambacho kinadaiwa kuteketea kwa Wema kinakaribia Sh. milioni 279.6 ambazo gharama hizo zinahusisha vitu kadhaa alivyowekeza kwa Wema.
“Kuna gharama za utengenezaji wa Filamu ya The Super Star ambayo haijulikani kilichotokea kwani hadi leo haionekani sokoni.

“Kama hiyo haitoshi kwenye uzinduzi wa filamu hiyo akamleta staa wa filamu wa Nollywood, Nigeria, Omotola Jalade Ekeinde na sherehe mbili za uzinduzi zilifanyika katika hoteli kubwa mbili tofauti, ikasemekana milioni arobaini na nane ziliteketea.
“Kuna kodi ya pango la ofisi ya Wema ya Endless Fame iliyopo Mwananyamala Koma-koma, Dar, jamaa alilipa milioni nane na laki nne kodi ya miaka miwili ambayo kwa mwezi ni laki tatu na nusu.

“Ukiachana na gharama za nyumba na ofisi, kuna gari aina ya Audi Q7, inadaiwa kanunua Clement kwa Sh. milioni 98, Toyota  Harrier Lexusya Sh. milioni 48 na Toyota Mark X iliyomtoa Sh. milioni 25.
“Usisahau hata lile Toyota Noah ‘kitimoto’ la ofisi alinunua Clement kwa Sh. milioni 10, faini aliyolipiwa

Kajala Masanja mahakamani Sh. milioni 13, gharama za kuirekebisha ngozi yake alipoenda nchini China iligharimu Sh. milioni 14, yaani jumla ni kama Sh. milioni 279 na ushee. Na hiyo ni kwa vitu vinavyojulikana ukiachia mbali shopping za Dubai,” alitiririka kikulacho huyo.

Baada ya kujazwa data, Risasi Jumamosi lilijaribu kumtafuta kigogo huyo lakini licha ya juhudi zote hizo hakuweza kupatikana ndipo alipogeukiwa Diamond:
 “Sitishiki kwa lolote lile kwani huko nyuma kabla sijawa maarufu kivile enzi ya Nenda Kamwambie (wimbo) niliwahi kukaa mahabusu kwa siku kadhaa na sababu ilikuwa mapenzi kwa hiyo kwa hili siogopi kitu kwanza mimi ndiyo alinichukulia na mwana mpotevu amerudi kundini,” alisema Diamond anayekimbiza na Ngoma ya Number One.

Chadema ngoma nzito,wafuasi watwangana makonde mahakamani


Wanachama wa Chadema, wakitwangana nje ya Mahakama Kuu, jijini Dar es Salaam.
 
Vurugu za aina yake zimezuka katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam, baada ya watu wanaodhaniwa kuwa wanachama wa Chadema  kumzomea aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho,  Zitto Kabwe.
Vurugu hizo zilihusisha wafuasi wa chama hicho wanaomuunga mkono Zitto na wale wanaompinga, ambao walikuwa wamebeba mabango ya kumsifia na wengine wakiwa wamebeba ya kumkashifu.
Katika vurugu hizo, baadhi ya wanachama hao waliamua kufanya doria isiyo rasmi ndani ya mahakama hiyo ya kuwasaka watu waliodai kuwa ni mamluki,  huku wakimkamata askari kanzu, kabla ya kumpiga ngumi na kumchania shati mtu mmoja wakidai kuwa alikuwa akiwarekodi kwa kutumia simu yake ya mkononi.


Tukio hilo la aina yake lilitokea jana asubuhi ambapo kundi la wanachama hao, huku baadhi wakiwa wamevaa nguo za kaki zinazotumiwa na chama hicho kufika katika mahakama hiyo kwa lengo la kusikiliza  kesi ya pingamizi iliyofunguliwa na Zitto. 
Mara baada ya kuwasili kwa Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, huku akiwa ameongozana watu kadhaa wakiwamo wanasheria wake na mabaunsa, wanachama hao walianza kumzomea huku baadhi wakimwita fisadi.
Hali hiyo iliibua zogo katika eneo la mahakama hiyo, hali iliyowalazimu maofisa kadhaa wa polisi kuingilia kati kwa kuamua kumchukua Zitto na kumhifadhi kwenye chumba maalumu na kumtoa saa 6 mchana kesi yake ilipoanza kusikilizwa.  Baadhi ya mabango ya kumkashifu  yalisomeka; Zitto tulimpenda, CCM imempenda zaidi, Zitto rudisha fedha za CCM.
Yale yaliyomsifia yalisomeka; Zitto kama Mandela na Zitto ni Mkombozi.Baada ya kumalizika kusikilizwa kwa kesi hiyo, saa 12 jioni wanachama hao walianza kurushiana ngumi, hasa baada ya kuibuliwa kwa mabango yaliyosomeka ‘Zitto kwanza Chadema baadaye’.
Awali hali hiyo ilimfanya Zitto kutaharuki, huku mabaunsa wake wakijihami na kuanza kumlinda.
Baada ya Zitto kuhifadhiwa baadhi ya wanachama hao ambao waliingia kwa kuandikishwa majina yao getini, walianza kuwasaka watu waliowahisi  kuwa mamluki, ambapo walimnasa askari kanzu na kuanza kumzonga wakimuhoji anapeleleza nini katika eneo hilo.
“Hapa tunataka kujua wewe ni nani na unataka nini hapa, maana hatukuelewi kabisa kwa nini unakuja kusikiliza mazungumzo yetu, jitambulishe,” alisisika mmoja wa wanachama hao akimhoji askari huyo huku akiwa amemkandamiza ukutani,
“Tunajua wewe ni askari kwa nini hujavaa sare leo? Kisha unajichanganya kwenye kundi letu.”
Kesi hiyo ilimalizika saa 12 jioni ambapo Zitto alitolewa chini ya ulinzi mkali wa polisi kwa kupitia mlango wa nyuma wa mahakama hiyo na kuwaacha wafuasi hao wakionyeshana ubabe kwa mabango na kauli za kejeli.
 
MWANANCHI

Ray C asema hamhurumii Jackie Cliff

 
Jackie Cliff na madawa aliyokamatwa nayo
 Jackie akiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya huko China
Jackie cliff kabla hajapatwa na matatizo akiwa katika pozi

ray c

 RAY C

MWANADADA aliyetikisa miaka ya nyuma katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesema hana hata chembe ya huruma kwa mwanamitindo Jackie Cliff anayedaiwa kukamatwa na dawa za kulevya huko Macau nchini China, hivi karibuni.
Ray C kupitia akaunti yake ya Instagram, aliandika kuwa, ana hasira sana na watu wanaouza dawa za kulevya kutokana na yeye alipokuwa katika janga hilo alikuwa anakubali kuwapa kila kitu wauzaji ili apate ‘unga’ maana tayari alikuwa ameathirika.
“Omba sana isiwahi kutokea kwa ndugu yako wa karibu, maana mimi nikifikiria mama yangu alivyopata shida wakati mimi naumwa mpaka naambiwa teja, yaani nyie acheni tu, hawa wauzaji wanyongwe kabisa, yaani wao wanafurahia kuona watoto wa wenzao wanaharibika,” aliandika Ray C.
Ray C aliokolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa kumpeleka katika kliniki ya dawa za kulevya Hospitali ya Mwananyamala na kupatiwa matibabu.
Mwanadada huyo alishawahi kutamba na nyimbo zake mbalimbali ikiwemo ‘Chochote Utapata’ ambayo ilifanya vizuri zaidi katika tasnia ya muziki huo.

Wananchi wa Kaliua wagoma kuhamia Katavi

UONGOZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora na wananchi wa kata mbalimbali wilayani humo wamesisitiza kupinga mpango wa wilaya hiyo kutaka kuhamishiwa Mkoa mpya wa Katavi
Wamesema mpango huo wa kutaka kuwahamishia wananchi wa wilaya hiyo katika mkoa mwingine wa Katavi hauna tija katika suala zima la mustakabali wa maendeleo yao na taifa kwa ujumla, hivyo hawapo tayari kuhamia Katavi.
Wakizungumza hivi karibuni katika ziara ya kikazi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kaliua, Mhe. John Kadutu, wananchi wengi wakiwemo viongozi wa chama tawala (CCM) walisema mpango huo utarudisha nyuma maendeleo ya wananchi.
“Sisi hatutahama kutoka Tabora kwenda Katavi. Haiwezekani serikali itutoe karibu na makao makuu ya Mkoa wetu wa Tabora halafu watupeleke Katavi, umbali wa zaidi ya kilometa 70. Tunasema hatuondoki Tabora ng’o,” alisema mzee mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Musa Samuel, kauli ambayo iliungwa mkono na wananchi wengi wa kata 16 kati ya kata 18 za wilaya hiyo.
Akisisitiza hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kaliua, John Kadutu, alisema halmashauri yake haipo tayari kuondoka Mkoa wa Tabora na kuhamia Mkoa mpya wa Katavi.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, Ibrahim Kifoka, ambaye pia ni Diwani wa Silambo, alieleza kusikitishwa na mpango huo na kusema wananchi wake hawakubaliani na mpango huo.
Chanzo: Tanzania Daima

CHADEMA YATOA MAELEZO KUHUSU PINGAMIZI ALILOWEKA ZITTO KABWE MAHAKAMANI

Mmoja wa wanachama watatu wa CHADEMA waliovuliwa nafasi zao za uongozi ndani ya chama, Zitto Kabwe kupitia kwa Wakili wake, Alberto Msando, leo ameanza kufanya ‘FORUM SHOPPING’ kwa kupeleka maombi Mahakama Kuu ya Tanzania, akiomba Kamati Kuu isijadili na kuamua jambo lolote kuhusu uanachama wake, kwenye kikao maalum kinachofanyika kesho.


Awali muombaji kwa namna ambayo inaweza kuitwa kuwa ni kuvizia, alitaka Mahakama Kuu hiyo itoe amri kutokana na ombi lake hilo, bila upande wa chama kuwepo mahakamani, lakini kwa bahati nzuri mawakili wa chama, Mwanasheria Mkuu wa chama, Tundu Lissu na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu, Peter Kibatala; wakafanikiwa kuwepo kortini, hivyo wakawa-served maombi hayo kisha mahakama ikalazimika kusikiliza Preliminary Objections (PO) kutoka kwa mawakili wa CHADEMA dhidi ya waleta maombi.

Maombi hayo ya wakili Msando kwa niaba ya Zitto yamefunguliwa mahakamani dhidi ya Baraza la Wadhamini CHADEMA na Katibu Mkuu wa Chama.

Hoja za mawakili wa CHADEMA katika PO zilikuwa ni katika maeneo matatu ambayo ni vifungu vya kisheria ambavyo waombaji walikosea;

1. Vifungu vya sheria walivyotumia waombaji kuomba court injunction, haviipatii Mahakama Kuu mamlaka ya kufanya maamuzi hayo wanayoomba ifanye. Kwa sababu kwa ujumla ukikosea vifungu hasa vinavyohusu msingi wa kesi, ni sawa na kwamba hakuna kesi.

2. Hati ya kiapo ya waleta maombi haikuwa na facts kama inavyotakiwa badala yake ilikuwa imejaa maneno ya ubishi ubishi.

3. Mahakama haiwezi ku-entertain kusikiliza migogoro ya ndani katika vyama vya hiari mf; vyama vya siasa, dini na michezo (ambavyo uanachama wake ni wa hiari), kwa sababu mojawapo ya principle ni kwamba ili mtu awe mwanachama anakuwa amekubaliana na katiba, kanuni, taratibu na makatazo ya chama husika.

Aidha katika maombi yake kuna vitu vingine ‘muhimu’ ambavyo mleta maombi amejikuta akivionesha kuwa anakubaliana na taratibu za chama lakini wakati huo huo tena anataka mahakama imsikilize;

· Amekiri kuwa amevuliwa nafasi za uongozi na amekata rufaa

· Amekiri kuwa ameandikiwa mashtaka kwa maandishi na yeye amejibu

· Amekiri kuwa ameandikiwa kuitwa mbele ya kikao cha Kamati Kuu ili asikilizwe utetezi wake kwa mdomo.

Kwa maneno yake hayo ni kwamba anakubaliana na na process ya chama na kwamba anajua atasikilizwa lakini tena wakati huo huo anataka mahakama imsikilize. Huo ndiyo msingi wa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA kusema kuwa kuhangaika huko ni sawa na kufanya ‘FORUM SHOPPING’.

Mleta maombi angeweza kuwa na hoja katika maombi yake iwapo angeona kuna breach of natural justice kwenye suala lake. Kitu ambacho hakijatokea na hata yeye kwenye maelezo yake anakiri hivyo.

Uamuzi wa Mahakama Kuu

Katika uamuzi wake, Jaji Utamwa amesema chama kitaendelea na shughuli zake kama kawaida.

Hivyo kikao maalum cha Kamati Kuu kilichopangwa kufanyika kesho Januari 3, 2014, kitafanyika na kitajadili agenda zote (kama zilivyotolewa awali) na masuala yote yanayohusu uendeshaji wa chama, isipokuwa hakitajadili na kuamua kuhusu uanachama wa Zitto pekee, hadi Mahakama Kuu itakaposikiliza ombi lake kesho saa 3 asubuhi.
Chanzo: Chadema Blog

Thursday, January 2, 2014

Sitta: Hatuwezi kuwa na marais watatu

     http://freemedia.co.tz/daima/wp-content/uploads/2014/01/sitta.jpg
 Mhe. Samwel Sitta

WAKATI Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amewasilisha rasimu ya pili ya mabadiliko ya Katiba kwa Rais Jakaya Kikwete, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta, amesema Tanzania haiwezi kuongozwa na marais watatu.
Sitta alisema anakubaliana na mawazo ya tume ya Warioba ya kuwa na serikali tatu, lakini hakubali Rais wa Zanzibar na Tanganyika nao waitwe marais kama yule wa Muungano.

Akizungumza na gazeti hili jana, Sitta alisema kuwa ili serikali tatu zifanye kazi kwa kuheshimiana, kuwekeana mipaka, rais wa Tanganyika na wa Zanzibar, wapewe majina na hadhi nyingine ili Tanzania iwe na rais mmoja tu wa Muungano.
“Niliposikia maoni na ufafanuzi wa kina jinsi serikali tatu zitakavyokuwa, nimekubaliana na mawazo ya tume kwamba tuwe na serikali tatu. Lakini kwa maoni yangu tuwe na amiri jeshi mkuu mmoja tu ambaye ni Rais wa Muungano, maana hatuwezi kuwa na marais watatu kwenye nchi mmoja,” alisisitiza.
Waziri huyo mwandamizi wa Serikali ya Rais Kikwete, alitolea mfano wa Shirikisho la Afrika Mashariki (EAC) kwamba rasimu yake imependekeza kuwa na rais mmoja tu na si marais sita wanaounda shirikisho hilo.
Pia alipendekeza jina la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania libadilishwe na badala yake liitwe Shirikisho la nchi za Tanzania.
Akizungumzia msimamo wa Chama chake Cha Mapinduzi (CCM), kupinga serikali tatu na kutaka muundo wa serikali mbili uendelee, Sitta alisema kuwa CCM isibaki kuwa kichwa ngumu kupinga serikali tatu.
Alisema CCM inakosea kung’ang’ania serikali mbili wakati Katiba ya Zanzibar ndiyo iliamua serikali mbili, hivyo serikali ya tatu kwa sasa haiepukiki.
Akitolea mfano, alisema Katiba ya Zanzibar inataka miswaada yote inayopitishwa na Bunge la Jamhuri iridhiwe kwanza na Baraza la Wawakilishi, jambo ambalo alisema si sahihi.
Alisema Katiba ya Zanzibar imefanya mambo mengi kuihalalisha Zanzibar kuwa nchi kamili na imefanya mambo hayo bila ridhaa ya Tanzania Bara.
Alisema ili kubaki na serikali mbili, lazima Zanzibar ikubali kuifumua Katiba yake inayotoa mamlaka kamili kwa rais wa visiwa hivyo, jambo ambalo alisema Wazanzibari hawawezi kulikubali.
“Mimi nilipomsikiliza Jaji Warioba safari hii, jinsi alivyojenga hoja ya serikali tatu, nimeona kuna hoja za msingi sana zipo kwa sababu kuna mambo makubwa na ya msingi yameshafanyika. Huwezi kupitisha Katiba inayosema miswada inayopitishwa bungeni isifanye kazi Zanzibar hadi Baraza la Wawakilishi likae na kuridhia, ukishafika hapo, basi serikali tatu haziepukiki,” alisisitiza Sitta.
Sitta alisema tume ya Warioba imefanya kazi kubwa na nzuri kwani rasimu ya pili imekwenda mbali kuangalia vitu kama zawadi za viongozi, jambo ambalo zamani viongozi waliona ni haki yao kupata zawadi za aina hiyo bila kujali kwamba hiyo ni rushwa.
Kwa mujibu wa Sitta, kuna mambo ya msingi ya kuendelea kujadili nje na ndani ya CCM nayo ni namna ya kuiendesha Serikali ya Muungano kwani kwa maoni ya tume, serikali hiyo itakuwa ikichangiwa zaidi na Tanganyika, jambo ambalo linaweza kuibua manung’uniko ya upande mmoja wa Muungano.
Aliwataka Wana CCM na wadau wengine kuifanyia kazi kauli ya Rais Kikwete aliyokaririwa mara kuwa vyama visipojali masilahi ya taifa katika mchakato wa Katiba, Katiba mpya itakwama na Watanzania watalazimika kuendelea kutumia katiba ya sasa.
 Chanzo: Tanzania Daima

ISSUE YA JACK PATRICK KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA, KUMBE DADA YAKE ALIMUONYA LAKINI AKAKAIDI

http://api.ning.com/files/FqkiRUfegCil-FNuBwqz6vuDXySmdvnC413Gp1Ih5g3OItLRd1NGSKUHlWnQznfa5wOXr6lQlygXPSIs*LKBa0ZiRpVuwSn8/3JACK1.jpg
 Jack akiwa kwenye pozi

Habari kutoka kwa mtu wa karibu na dada wa Jack zinasema kuwa, wakati akitaka kusafiri akitokea Bongo, alimweleza dada yake juu ya mpango wake huo, akamuonya lakini modo huyo alikataa.
“Alimfuata dada yake na kumweleza mchongo mzima kuwa alitaka kwenda na mzigo China, dada yake akamwambia aachane na hizo biashara, akakataa. Jack alifikia hatua akamwambia dada yake kuwa hana mtoto, hana mume wala ndugu anayemtegea kwa hiyo yupo tayari kwa lolote kwani hakuwa na cha kupoteza.
“Kama angemsikiliza dada yake (jina linahifadhiwa) haya yote yasingemkuta na asingeingia kwenye mateso ya namna hii,” alisema mtoa habari wetu huku akiendelea kusisitiza jina lake lisionekane mahali popote kwenye ukurasa huu.

ABEBESHWA MZIGO, ALIPWA MALIPO YA AWALI
Ilizidi kusemekana kuwa, alipokaribia kuondoka Bongo, Jack alimwambia dada yake kwamba anakwenda kambini (kituo cha kuingiza mzigo tumboni) ambapo aliporejea kwa dada’ake alimuonesha dola za Kimarekani 21,000 (zaidi ya shilingi milioni 33) ambazo ni malipo ya awali huku akimwambia alishabebeshwa nusu ya mzigo.
Hata hivyo, habari zinasema Jack alimwambia dada yake huyo kuwa hakuwa akijisikia kusafiri lakini kwa kuwa anatafuta maisha aliamua kuondoka baada ya mzigo kukamilika wote siku iliyofuata.

INA MAANISHA NINI?
Kwa mujibu wa maelezo hayo, Jack aliondoka na unga hapahapa Bongo kwenda Thailand kupitia Nairobi, Kenya na baadaye Macau, China ambako alinaswa.
Chanzo: GPL

Sunday, December 29, 2013

Jaji Ramadhani awa mchungaji Anglikana



Zanzibar. Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani ametawazwa kuwa Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar na kusema ameshangazwa na mashambulizi ya tindikali dhidi ya viongozi wa dini Visiwani humo.
Akizungumza na waaandishi wa habari mara baada ya kutawazwa ndani ya Kanisa la Anglikana la Minara Miwili Mjini Unguja, Jaji Ramadhan amesema vitendo vya hujuma vinavyofanywa dhidi ya viongozi wa dini na Serikali ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar.
Alisema Wakristo na Waislamu Zanzibar kwa miaka mingi wamekuwa wakiishi kama ndugu bila ya kubaguana kwa sababu za itikadi ya dini licha ya Waislamu kuwa asilimia 95.
Hata hivyo, alikumbusha kuwa wakristo wana mchango katika harakati za ukombozi wa Zanzibar, ambapo idadi kubwa ya waumini wake walianzisha Chama cha African Association mwaka 1935, ambapo rais wake wa kwanza alikuwa hayati, Mzee Augustino Ramadhan na baadaye akafuata hayati  Mzee Abeid Amani Karume.
“Vitendo vya watu kumwagiwa tindikali vinanishangaza, sababu halisi siifahamu, najiuliza haya yametokea wapi, siyo jambo jema wala siyo sifa ya Zanzibar tokea enzi na enzi,” alisema.
Alisema wakati umefika na kuwataka viongozi kuwa mstari wa mbele kukemea matukio ya hujuma za tindikali na uhalifu mwingine ikiwemo mashambulizi ya kutumia silaha za moto na watu kupotezewa maisha.
Jaji Augustino amewahi kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar na Tanzania, Brigedia Jenerali wa JWTZ pia amewahi kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mahakama ya Afrika Mashariki, ambapo amesema kazi ya sheria hazitofautiani na kazi za kiroho kwa vile zote zinahitaji utende haki na kutimiza wajibu upasavyo. Kwa upande wake Askofu Philip Baji wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John cha Dodoma, alisema huu ni wakati mwafaka kwa Serikali kuwalinda viongozi wa dini bila ya kujali tofauti ya madhehebu yao kutokana na kukithiri kwa vitendo vya hujuma.
Chanzo: Mwananchi

Kwa nini wanawake wabakwe Operesheni Tokomeza Majangili?

Matukio ya baadhi ya wanawake kukamatwa, kudhalilishwa mbele ya familia kwa kushikwa sehemu za siri bila ya ridhaa yao, na kubakwa wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Majangili nchini, ni muendelezo wa madhila mbalimbali yanayoendelea kuwakumba wanawake nchini.

Hayo yamebainishwa katika Ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyoongozwa na mwenyekiti wake James Lembeli iliyosomwa bungeni hivi karibuni.
 
Operesheni hiyo ilifanyika katika maeneo mbalimbali ya nchi iliyoongozwa na wizara tatu za Maliasili na Utalii, Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Wizara ya Mambo ya Ndani.
 
Lengo la operesheni hiyo ni kuwatafuta, kuwakamata na ikibidi ‘kuwaua’ kama si kuwachukulia sheria majangili wanaoua tembo kwa ajili ya kupata meno yake na vifaru kwa ajili ya vipusa, badala yake baadhi ya waliopewa dhamana hiyo wakaacha lengo la msingi na kujikuta wakiwakamata wanawake, kuwachomea nyumba, kuwadhalilisha kwa kiwango cha kutisha na kuwabaka.
 
Mwanamke mmoja (jina linahifadhiwa) wilayani Babati  alivuliwa nguo na kulazimishwa kufanya mapenzi na wakwe zake kisha kuingizwa chupa sehemu zake za siri.
 
Mama mwingine mkazi wa Kata ya Matongo wilayani Bariadi, alibakwa na askari watatu huku akiwa ameshikiwa mtutu wa bunduki. 
 
Tukio la kuuawa kinyama kwa Emiliana Gasper Maro lilipotolewa na vyombo vya habari, Serikali kupitia Mkurugenzi wa Wanyama Pori ilitoa taarifa kwa umma ikipinga taarifa iliyorushwa kwenye vyombo vya habari Oktoba 19, mwaka huu kuhusu mauaji ya kutisha yaliyofanywa na askari wa kupambana na ujangili.
 
Serikali iliwatetea askari wa Operesheni Tokomeza Ujangili kuwa hawahusiki na kifo cha Emiliana. 
 
Hata hivyo, taarifa ya utetezi ilizungumzia majina mawili tofauti ya Evelyn Gasper na Mariana Gasper Mallo wa  eneo la Olongadiola wakati muathirika halisi ni Emiliana Gasper Maaro mkazi wa kijiji cha Omgadida, Gallapo. 
 
Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa) kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP), Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA),Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (Zafela) na Kituo cha Usuluhishi cha Tamwa (CRC), inatekeleza mpango wa kutokomeza ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (Gewe II) katika wilaya 10 za Tanzania Bara na Zanzibar.
 
Ili kufanikisha mpango huo wa miaka miwili (2012-2014) Tamwa iliongoza uundaji wa kamati katika wilaya 10 kwenye vijiji 60 vya Tanzania Bara na Zanzibar zenye jumla ya wajumbe 720. 
 
Kazi kubwa ya kamati hizo ni kufuatilia masuala ya ukatili unaofanywa dhidi ya wanawake na watoto wa kike kwenye maeneo yao.
 
Taarifa ya Ripoti ya Kamati ya Bunge iliyochunguza sakata hilo, yawezekana imepita sehemu ndogo ya hali halisi ya matukio yalivyokuwa nchini kutokana na muda iliopewa, uchache wa wajumbe ambao siyo rahisi kupita kila kijiji na kila sehemu, hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa baadhi ya matukio haya kubainishwa wazi licha ya kuathiri wanawake na watoto.
 
Hivyo ni muhimu kwa wanaharakati popote walipo ikiwa ni pamoja na Kamati zilizoundwa na Tamwa katika maeneo mbalimbali ya nchi kuendelea kufichua madhila mbalimbali yaliyowapata watu kutokana na operesheni hii ambayo baadhi ya watu wamepata vilema vya kudumu na vifo wakiwamo baadhi ya wanaume na watoto.
 
Baadhi ya wananchi waliopoteza maisha katika operesheni hiyo na vijiji vyao kwenye mabano ni Wegesa Kirigiti (Remagwe), Peter Masea (Mrito-Tarime), Mohamed Buto, Massi na Gervas Nzoya (Kasulu-Kigoma).
 
Utekelezaji wa Operesheni hiyo ni dhahiri umekiuka sheria hasa ibara ya 14 ya Katiba isemayo “Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake  kutoka kwa jamii kwa mujibu wa sheria” na ibara namba 15 (1) isemayo “ kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kama mtu huru”.
 
Inatisha kuona askari wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi walioiva kimafunzo kuthamini ustaarabu, kujali utu, kuheshimu na kuzingatia haki za binadamu wanageuka na kufanya unyama kama huo dhidi ya maisha ya raia na mali zao ambao walipaswa kutumia mafunzo yao kuwalinda.
 
Tayari mawaziri wanne wamejiuzulu kutokana na kadhia hiyo ambao ni Mawaziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki, Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchi,  Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha na  wa Maendeleo ya  Mifugo na Uvuvi Dk. Mathayo David.
 
Sasa inasubiriwa kuundwa Tume  ya Kimahakama ili matokeo ya kina zaidi yapatikane na hatua zaidi zichukuliwe kwa wahusika wote.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Saturday, December 28, 2013

KUFANIKISHA MAKUZI YA WATOTO KWA MZAZI MMOJA

 
 
Katika nyakati hizi, familia zilizochini ya uangalizi wa mzazi mmoja, hususani mama, zimeongezeka sana hata kufikia idadi sawa au zaidi ya familia zenye baba na mama katika jamii nyingi.
Kuna sababu nyingi zinazopelekea hali hii kama; kifo, utelekezwaji wa familia, kuhamishwa kikazi, masomo hususani elimu ya juu n.k

Changamoto zinazoambatana na malezi ya mzazi mmoja ni nyingi, ikiwamo; ufinyu wa kipato, kukosa ushirikiano kutoka kwa mzazi wa kufikia, upweke unaopelekea msongo mawazo n.k

Kukabili Jukumu.

Jukumu gumu katika malezi ni kelea mtoto/ watoto wachanga. Watoto wadogo wanahitaji uangalizi wa karibu. Hata hivyo jukumu hilo kubwa la malezi linaweza kupunguzwa kwa:

a) Kutafuta msaada.
Kutafuta msaada ni muhimu sana, hata kama mzazi husika anahisi ataweza kulea akiwa peke yake. Ni vigumu sana kulea mtoto bila msaada. Msaada unaweza kuombwa kutoka kwa ndugu, jirani, rafiki au mashirika yanayohusika na kulea watoto. Ikiwa kipato cha mzazi kinaruhusu mzazi anaweza kumwajiri yaya.

b) Kuweka mipango.
Mzazi anapaswa kupanga ratiba na kuhakikisha anaitekeleza. Watoto huwa na amani ikiwa wanajua saa ambayo baba/ mama atakayorudi. Pia ikiwa wanaona juhudi za mzazi katika kuwalea.

c) Kujibu maswali ya watoto.
Watoto huuliza maswali magumu sana, kwa kuwa watoto hupenda kudadisi juu ya yale wanayoyasikia. Watoto huuliza maswali juu ya baba/ mama ambaye hayupo. Mzazi husika hapaswi hata kidogo kupuuza maswali kutoka kwa watoto, bali atoe majibu sahihi na yenye ufafanuzi katika hali ya upole na unyenyekevu.

d) Kuzingatia maadili.
Mzazi anapaswa kuweka sheria na kanuni chache na zinazotekelezeka. Hii itawasaidia watoto kujiwekea mipaka maishani. Watoto wafundishwe kufanya kazi kwa ushirikiano tangu wakiwa wadogo. Mzazi awe na kiasi katika kutoa kazi na adhabu. Pia mzazi awaambie wasaidizi wake, juu ya matarajio yake kwa watoto wake.

e) Kuweka vipaumbele.
Ufinyu wa bajeti ni kikwazo kikubwa kwa familia ya mzazi mmoja. Mzazi anapaswa kuweka bajeti kadiri ya kipato chake. Ili kuepuka mzigo wa madeni, mzazi anapaswa kuepuka anasa. Pia mzazi awaambie watoto sababu za mapendekezo yao kutotekelezeka.

f) Kukaa na watoto.
Watoto huwa na furaha na amani ikiwa watakuwa na mahusiano mazuri na ya karibu baina yao na mzazi wao. Mzazi ahakikishe anapata muda kwa ajili ya kuongea, kusoma, kutembea, kuimba n.k na watoto. Mzazi asiruhusu watoto kuangalia TV kwa muda mwigi, hususani vipindi visivyo na umuhimu kwa watoto. Kufanya hivyo huimarisha familia.

g) Kujijali.
Mzazi ahakikishe anajali afya yake, kazi yake, jamii yake n.k. Kufanya hivyo kutasaidia kukuza ustawi wa roho na mwili. Mzazi atenge muda wa kupumzika na kuwasiliana na wadau wanaomsaidia katika malezi. Mzazi husika anapaswa kuchunga afya yake kwani, kama ikiwa ataugua hali ya familia itakuwa matatani. 
Source: Wilguy

Friday, December 27, 2013

Viongozi wa ukoo wakerwa Graca kunyanyaswa

Johannesburg, Afrika Kusini. Baada ya mjane wa aliyekuwa Rais wa Kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, Graca Machel kutakiwa kuondoka katika familia hiyo na kurudi kwao Msumbiji, viongozi wa ukoo wamewajia juu watoto wa Mandela.

Viongozi hao wa ukoo wa Aba Thembu, wamekasirishwa na kitendo hicho wakisema ni unyama wa kupitiliza wa kumuondoa mjane huyo aliyekuwa akiishi na marehemu Mandela mpaka alipofariki dunia.
Graca alianza kuishi na Mandela baada ya shujaa huyo wa Afrika kuachana mkewe Winnie kutokana na kashfa ya kutokuwa mwaminifu.
Msemaji ukoo huo wa Aba Thembu, Daludumo Mtirara alisema kumwondoa Graca katika ukoo huo ni kosa kubwa kwani bado anastahili heshima kubwa.
“Machel siyo mtu wa kumtukana wala kutumia lugha ambayo si nzuri kwake wala lugha ya vitisho,” alisema kiongozi huyo.
Taarifa za Graca (68), kutakiwa kuondoka nyumbani kwa Mandela zilitolewa na vyombo mbalimbali vya habari vya Afrika Kusini vikiwakariri watoto wa Mandela.
Awali, taarifa zilisema kwamba watoto hao walimtaka mjane huyo aachie mali zote za baba yao na arudi kwao Msumbiji.
“Nkosikazi Nosizwe anatakiwa kuwa ni kiongozi wa familia lakini yeye ndiye anayeongoza kutomheshimu mama yake. Huo ni utovu wa nidhamu,” alisema Mtirara.
Mandela alimuoa Graca ambaye alikuwa mke wa Rais wa Msumbuji marehemu Samora Machel katika sherehe ya kutimiza miaka 80 ya kuzaliwa kwake, Julai 18, 1998.
Rais huyo wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini alifariki dunia Desemba 5 mwaka huu.

Chanzo: Mwananchi


JACK PATRICK ADAIWA KUNASWA NA PIPI 66 ZA DAWA ZA KULEVYA ZENYE THAMANI YA MIL 215.5 CHINA


Mrembo anayedaiwa kuwa Jack Patrick (akiwa amefunikwa uso) mikononi mwa polisi nchini China baada ya kukutwa na pipi 66 za heroin tumboni.
Mwanamitindo Jack Patrick.…
Mrembo anayedaiwa kuwa Jack Patrick (akiwa amefunikwa uso) mikononi mwa polisi nchini China baada ya kukutwa na pipi 66 za heroin tumboni.
Mwanamitindo Jack Patrick.
 
Mrembo anayedaiwa kuwa Jack Patrick akipelekwa katika chumba maalum kwa ajili ya mkutano na wanahabari Jumanne Desemba 19, 2013 huko Macao China.
Polisi wakichunguza pipi zenye dawa za kulevya alizokutwa nazo mrembo anayedaiwa kuwa Jack Patrick.
Wanahabari nchini China wakichukua picha za dawa hizo za kulevya anazodaiwa kukutwa nazo Jack.
MODO maarufu Bongo, Jacqueline Patrick Cliff, anadaiwa kukamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao nchini China. Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya pipi 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720 sawa na shilingi milioni 215.5 za Kitanzania.
Inadaiwa kuwa Jack alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne ya Desemba 19, 2013. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko China.
Jack alipata jina aliposhika namba tatu kwenye Miss Ilala na kushiriki Miss Tanzania mwaka 2005/06. Pia uliuza nyago kwenye video ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marehemu Albert Magwea ‘Ngwair’ iliyokwenda kwa jina la She Got A Gwain. Kuanzia hapo jina likawa kubwa na akawa mwanamitindo maarufu Bongo.
Ni katika kipindi hicho cha umaarufu akaolewa na mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa mkongwe, Abdallah Fundikira, Abdulatif kabla ya jamaa huyo kutupwa nyuma ya nondo za mahabusu ya Keko, Dar akikabiliwa na msala wa kusafirisha mihadarati.

Kutoka Urambonews
Eeh!Mwenyezi Mungu hebu waokoe mabinti zetu maana shetani amewakamata sawasawa kupitia biashara ya madawa ya kulevya. Maana kwa utafiti wangu mdogo, idadi kubwa ya wanaokamatwa na madawa ni mabinti zetu wadogo tena warembo. Hivi kwanini hatujifunzi kupitia kwa wenzetu yarabi. Yaani mi hata sielewi. Kwanza naona hivi ninavyoandika, kuna watu wapo wanavusha madawa airport, bila hata woga.  Haya, mtu anakamatwa na madawa ya kulevya China ambapo sheria yao ni kunyongwa. Jamani hii si hasara kwa Familia na Taifa kwa ujumla. Hebu tujibiidishe kila mmoja kwa shughuli ambayo mwenyezi Mungu amemjalia. Kwa kweli inauma sana jamani.

Thursday, December 26, 2013

Maiti yabambwa na dawa za kulevya

Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro,Faustine Shilogile akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Hizi ndio baadhi ya Pipi zilitolewa tumboni mwa Marehemu Khalid Kitala. …
Baadhi ya Makachero wa Polisi wakijadiliana jambo baada ya kuona Mwili huo.
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limefanikiwa kukamata gari dogo aina ya Toyota Spacio likiwa limebeba mwili wa mtu aliefari ambaye alitambulikwa kwa Jila la Khalid Kitala (47) na kukutwa na kete kadhaa za Madawa ya Kulevywa tumboni.
 

 JESHI la Polisi mkoani Morogoro limenasa kete 24 za dawa za kulevya kwenye mwili wa marehemu Khalid Abdul Kitala (47) mkazi jijini Dar es Salaam.
Mwili wa marehemu Kitala aliyekuwa akiishi Kariakoo, Mtaa wa Kongo, ulikuwa ukisafirishwa kutoka Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustin Shilogile, tukio hilo lilitokea juzi usiku katika mizani ya magari makubwa iliyopo Mikumi wilayani Kilosa.
“Baada ya taarifa za siri kutoka kwa wasamaria wema kuwa kuna gari dogo kutoka wilayani Mbozi baadae lilitambulika kuwa ni aina ya Spacio T 887 BSW limebeba mwili wa marehemu wenye dawa za kulevya, tukaweka mitego sehemu mbalimali na kulinasa Mikumi,” alisema Shilogile.
Alisema gari hilo lilikuwa likiendeshwa kwa kupokezana na Teddy Esco (27), mkazi wa Mtaa wa Mwaka, Tuduma, Wilaya ya Momba mkoani Mbeya na Lucas Atubonekisye Swila (32) wa Mtaa wa Songea wilayani Momba, lilikuwa na abiria aliyetambulika kwa jina la Jumbe Hamad Mbano (36), mfanyabiashara wa Kariakoo, Mtaa wa Jangwani jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Shilogile, taarifa za uchunguzi za awali baada ya kukamatwa kwa gari hilo zilikutwa kete saba ndani ya gari zilizofanya jumla ya kete 24 katika tukio hilo na marehemu alikuwa mfanyabiashara katika soko la Kariakoo-Kongo jijini Dar es Salaam.
Naye Mganga Mkuu wa hospitali ya Rufaa Morogoro, Ritha Lyamuya alisema baada ya marehemu kufanyiwa uchunguzi zilitolewa kete 17 zinazohisiwa kuwa za dawa za kulevya.
Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali hiyo kwa taratibu nyingine za kisheria kabla haujaruhusiwa kuzikwa.
Chanzo: Tanzania Daima and GPL

Wednesday, December 25, 2013

ZITTO AWALIPUA DK SLAA, MBOWE


                                                    Mheshimiwa zitto Kabwe


Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe, amejibu mashambulizi kwa viongozi wa Chadema, kutokana na kile alichosema wanazunguka na kusema maneno yasiyo ya ukweli.
Akihutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika Uwanja wa Mwanga Centre, Kigoma mjini, alisema alichukua kadi ya uanachama wa Chadema mwaka 1993 wakati huo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa akiwa bado yuko CCM.
“Wakati hao wenye midomo mikubwa wanaoongea sasa, walipokuwa wamekumbatia watawala, nyinyi mlikuwa mnapigwa mabomu kutaka mageuzi, eti leo wao wapinzani zaidi kuliko sisi na ndiyo maana hatuwezi kuwaachia.
Hatuwezi kukubali, hatutoki, demokrasia ni mchakato na mwenzenu nimekuwa kwenye mchakato huu. Kadi yangu ya Chadema nimeichukulia kwenye uwanja huu, tarehe moja mwezi wa nne mwaka 1993, nikiwa na miaka 16, wakati nachukua kadi yangu, Katibu Mkuu wa chama changu alikuwa yuko CCM.
Akizungumza kile alichosema ni uongo unaosambazwa na viongozi wa juu wa chama hicho, Katibu Mkuu Dk Slaa na Mwenyekiti wake Mbowe waligawana maeneo Mbowe akaenda Kanda ya Ziwa na Dk Slaa Kanda ya Magharibi.
Alisema kwenye mikutano hiyo, Mbowe anasema kuwa endapo mbunge huyo atarudi yeye Mbowe atajiuzulu, suala alilosema linaonyesha kuwa tayari ameshafukuzwa bila hata utetezi wake kusikilizwa.
Alisema baada ya viongozi hao kuzungumza na kusema mambo hayo na yeye aliamua kurudi nyumbani Kigoma na baada ya kuona hilo Dk Slaa akahoji mbunge huyo anafanya vikao hivyo kama nani.
“Mimi nimekata rufaa, wajumbe wa baraza kuu wa Mtwara, Ruvuma wanaandika barua wanataka mkutano mkuu, Katibu Mkuu akiwa Igunga anasema hiyo ni haramu na hao wafuasi wa Zitto watafanya Zitto afukuzwe, si __wamwamesha nifukuza? takachokuja kunijadili, hivyo si wameshanifukuza ?
CHANZO: MWANANCHI

MERRY CHRISTMASS WADAU. NAWAPENDENI NYOOTE

Urambonews inawatakia wadau wote heri ya Christmass. Mungu awe nanyi katika mapumziko haya na yaishe kwa usalama. Msherehekee kwa amani.

Free Christmas Cards Download HD Wallpapers