LATEST POSTS

Thursday, June 25, 2015

Familia yasema maisha ya Bobbi Kristina wamemuachia Mungu

Maisha ya Bobbi Kristina Brown sasa yapo mikononi mwa Mungu na jamaa zake wanasubiri lolote lile kutokea.
Kauli hiyo imetolewa na mama yake mkubwa Pat Houston wakati wakimhamishia binti huyo katika hospitali ya wagonjwa mahututi.
 “Pamoja na kupewa huduma  bingwa za kitabibu katika hospitali mbalimbali hali ya Bobbi Kristina Brown imeendelea kuzorota.Kuanzia leo tumemuhamishia katika uangalizi wa wagonjwa mahututi.Tunamshukuru kila mmoja kwa sapoti mliyotupa na sala.sasa yuko katika mikono ya Mungu.”
Mtoto wa pekee wa Bobby Brown na Whitney Houston  amekuwa hospitalini toka Januari 31 baada ya kukutwa bafuni akiwa hajitambui.
Bibi yake Bobbi Kristina, Cissy Houston  amekuwa akitoa taarifa zinazokatisha tama akisema wazi kwamba hakuna matumaini ya uzima kwa mjukuu wake.

MJAMAICA KUTOA MAHALI YA HEKA 10 ZA BANGI ILI KIJANA WAKE AMUOE MTOTO WA OBAMA.

WANAUME WANAOMTAMANI KUMUOA BINTIYE RAIS OBAMA, MALIA OBAMA WANAZIDI KUONGEZEKA.

BAADA YA FELIX KIPRONOH WA KENYA NA MWENZAKE KUTOKA HUKO HUKO KENYA KUJITOKEZA NA NG’OMBE KADHAA KAMA MAHARI YA KUTAKA KUMUOA MALIA, JANA MZAZI MMOJA KUTOKA JAMAICA AMEJITOKEZA PIA NA MAHARI KWA AJILI YA KUMNASA MALIA OBAMA AWE MKE WA KIJANA WAKE.

MAHARI ILIYOTOLEWA MARA HII KUTOKA JAMAICA, SIO YA KAWAIDA MZAZI HUYO KWA JINA ROY CHAMBERS, AMEISHANGAZA DUNIA KWA KUTOA EKARI 10 ZA BANGI KAMA MAHARI KWA FAMILIA YA WHITE HOUSE KWA AJILI YA KUMPOSA MREMBO MALIA OBAMA KAMA MKE WA KIJANA WAKE.
MALIA OBAMA

“ NILIJARIBU KUMPATA OBAMA AKIWA HAPA JAMAICA WIKI CHACHE ZILIZOPITA LAKINI WALINZI WAKE WALINIZUIA, NIMEMTUMIA BARUA PEPE  NA NADHANI ATANIPA MREJESHO HIVI KARIBUNI”, CHAMBERS AMESEMA KATIKA MTANDAO WAKE.

“ SHAMBA LANGU LINA THAMANI KUBWA SANA KWANGU NA JAMAICA KWA JUMLA LAKINI KWA KUWA KIJANA WANGU ANAMPENDA MALIA OBAMA, NIKO RADHI KULITOA SHAMBA HILO KWA OBAMA ILI KIJANA WAKE AMUOE MREMBO HUYO” AMESEMA CHAMBERS.

ALI KIBA AWA KIVUTIO KWENYE DALADALA DAR



Ali Kiba akifurahia jambo na abiria.
 
Kondakta wa daladala akiwa na Ali Kiba.
 
Ali Kiba akiongea na baadhi ya abiria.
...akiwa ameshuka ndani ya daladala.
Ali Kiba akielekea kupanda daladala ya Kariakoo Makumbusho eneo la kituo cha daladala cha Usalama-Magomeni.
Abiria wakihitaji kila mmoja kumwona ndani ya daladala aliyopanda.
...akishuka ndani ya daladala.
Kushoto ni abiria akimuuliza swali msanii huyo (kulia).
Ali Kiba akizungumza na abiria ndani ya daladala ya Ubungo Makumbusho.
MSANII wa muziki wa Bongo fleva hapa nchini ambaye pia ni mshindi wa tuzo za KTM 2015, Ali Kiba ameendelea kuzunguka kwenye daladala zinazofanya safari zake hapa jijini Dar es Salaam kama njia ya kuwashukuru mashabiki wake.
Mwimbaji huyo wa Chekecha cheketua alianza ziara yake hapo jana kwa kutumia usafiri wa daladala kuzunguka viunga vya jiji la Dar es Salaam akianzia kituo cha Kariakoo hadi Mbagala huku akiwalipia nauli abiria aliowakuta.
Pia alitembea na daladala kutoka Kariakoo akipitia vituo vya Magomeni, Manzese, Ubungo Simu 2000, Mwenge, Makumbusho kabla ya kumalizia Kinondoni Mkwajuni.
Akizungumza na mashabiki kwenye daladala hizo, Ali Kiba alisema aliamua kupanda daladala kwa kuamini ataweza kukutana na mashabiki wake ambao hawezi kumuona na kutoa madukuduku yao.
“Ninawashukuru kwa mapenzi yenu kwangu, bila nyinyi nisingeweza kupata tuzo hizi, nisingeweza kuwakusanya wote pamoja na kuwashukuru, nimeona kwa kutumia usafiri huu wa daladala nitaweza kuonana na baadhi ya mashabiki wa muziki wangu,” alisema.
Aliwataka mashabiki hao kumuuliza maswali au kumshauri, na alipoulizwa kama ana uhusiano wa kimapenzi na muigizaji Wema Sepetu, alikana akidai wanafanya kazi tu pamoja.

Sunday, June 21, 2015

SUGU AMFIKISHA MZAZI MWENZIYE MAHAKAMANI KISA KUVAA NUSU UTUPU NA KUPIGA PICHA ZA AIBU

 

Deogratius Mongela na Chande Abdallah
KINDUMBWENDUMBWE! Mbunge wa Mbeya Mjini kwa ‘leseni’ ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’ amemfikisha kortini aliyekuwa mkewe,  Faiza Ally akitaka apewe mtoto wao, Shaa (2) ili amlee kwa vile mama yake huyo si mwadilifu.
Aliyekuwa mkewe na mbunge wa mbeya mjini Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’,  Faiza Ally akiwa katika pozi.
Ijumaa iliyopita, saa 2:00 asubuhi, Faiza alipanda kwenye kizimba cha Mahakama ya Mwanzo, Manzese/ Sinza iliyopo Sinza-Makaburini jijini Dar kwa ajili ya kukabiliana na madai hayo.
 Alieyekuwa mke wa mbunge wa mbeya mjini Joseph Mbilinyi "Sugu" akiingia mahakamani.
ZILIPO HASIRA ZA SUGU
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichomwaga ‘ubuyu’ huo, Mheshimiwa Sugu alifikia hatua hiyo baada ya kuchukizwa na tabia mbaya za mwanamke huyo hasa ya kuvaa nguo zinazomuacha nusu utupu na kupiga picha za aibu, akiamini kuwa, tabia hizo zinaweza kuathiri makuzi ya mtoto huyo.
Mnyetishaji huyo aliendelea kusema kuwa, kwa kipindi kirefu, Sugu amekuwa akimvumilia Faiza, lakini hivi karibuni uzalendo ulimshinda baada ya picha zake akiwa amevaa kigauni kifupi na makalio nje kusambaa mitandaoni.
 Joseph Mbilinyi 'Sugu' akiwa na katika picha na aliyekuwa mke wake Faiza Ally na mtoto wao.
PALIPOKOLEZEA HASIRA
Faiza alivaa kivazi hicho hivi karibuni kwenye hafla ya ugawaji wa Tuzo za Kili Music iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City, Dar.
 SUGU MBELE YA HAKIMU
Akizungumza mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Patrick Vaginga, Mheshimiwa Sugu alidai kuwa mbali na mzazi mwenzake huyo kuwa na tabia ya kuvaa nusu utupu pia ana mtindo wa kupiga picha zisizo na maadili na kuziweka mtandaoni yeye mwenyewe.
 Joseph Mbilinyi akionekana kwa mbali katika maeneo ya mahakama.
KUHUSU MTOTO
Sugu alikwenda mbele zaidi kwa kudai kwamba, pia mwanamke huyo amekuwa na tabia ya kumpiga picha mbaya mtoto wao na kuzimimina humohumo mitandaoni jambo ambalo alisema linamharibu mtoto huyo.
 FAIZA HANA PESA
Mbali na sababu hizo, pia Sugu aliongeza kuwa, Faiza hana kipato kizuri cha kuweza kumlea mtoto na mara kwa mara amekuwa akisafiri jambo ambalo husababisha mtoto huyo kutopata malezi ya mama kwa muda mrefu hivyo kuiomba mahakama impe haki yeye ya kuishi na mwanaye.
 FAIZA AJIBU MAPIGO
Naye Faiza akijibu mapigo katika utetezi wake alisema kuwa, Sugu hafai kumlea mtoto huyo kwa sababu naye ana tabia ya kusafiri kwa muda mrefu hivyo kuishi mbali na mtoto ambapo aliiomba mahakama hiyo isimruhusu baba mzazi huyo kuishi na mtoto kwa kuwa atamharibu.
KESI YAPIGWA KALENDA
Mheshimiwa Hakimu Vaginga akasema kwa vile kesi hiyo ndiyo imeanza kusikilizwa kwa mara ya kwanza aliiahirisha hadi baadaye mwezi huu ambapo hukumu itatolewa.
 SUGU NJIA YAKE, FAIZA NJIA YAKE
Ijumaa Wikienda lililokuwa mahakamani hapo, liliwashuhudia wazazi hao, kila mmoja akiondoka na njia yake.
KWA NINI FAIZA NI MKE WA SUGU?
Kwa sheria za Kitanzania, mwanamke na mwanaume wakiishi pamoja kwa zaidi ya miezi sita, hao tayari ni mke na mume kama ilivyokuwa kwa Faiza na Sugu ambao waliishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili.

GPL

KUANZIA JULAI MOJA AJIRA ZA SERIKALI ZITAOMBWA KWA NJIA YA MTANDAO KUEPUKA MALALAMIKO YA BARUA KUPOTEA


Serikali imesema kuanzia Julai mosi mwaka huu, ajira za utumishi wa umma zitakuwa zikiombwa kwa njia ya mtandao, ili kuongeza ufanisi wa mchakato wa kuwapata watumishi wenye sifa na kupunguza malalamiko ya kupotea kwa barua za maombi.
Akizindua baraza la kwanza la wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Sektretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani alisema mtandao huo umezinduliwa na waombaji watapaswa kuingia katika tovuti maalumu ya ajira na kutuma maombi yaliyoambatanishwa na vyeti vya taaluma walizosomea.
“Maombi kwa njia ya mtandao yatapunguza kazi ya kuchambua maelfu ya barua za maombi ya kazi zilizokuwa zinatumwa, itapunguza pia manung’uniko kwamba barua zimetumwa kisha zimekaliwa tu,” alisema Kombani.
Waziri huyo, alisema kwa kutumia utaratibu huo mpya, wananchi wanaotaka ajira serikalini watakuwa na uhakika kuwa barua zao zimefika na kupokewa na wahusika. Pia, wanaweza kupata mrejesho kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu zao za mkononi.
Kwa upande wake Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Xavier Daudi alisema baada ya kuona mchakato wa kuajiri unachangamoto nyingi, waliamua kubuni mfumo wa kuomba ajira kupitia mtandaoni.
“Utaratibu huu utatupunguzia gharama, wanafunzi wanaohitimu kila mwaka vyuoni ni maelfu kwa maelfu na nafasi tunazopata serikalini kupitia sekretarieti ya ajira hazizidi 12,000 kila mwaka,” alisema Daudi.
Hata hivyo, katibu huyo alisema wamekuwa wakipata changamoto kubwa kutokana na baadhi ya waombaji kutumia vyeti vya kughushi na hivyo kulazimika kwenda kwenye vyuo husika kuvithibitisha.