LATEST POSTS

Tuesday, July 28, 2015

Lowassa, mkewe watua Chadema, wakabidhiwa kadi

http://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2015/07/229.jpg 

Hatimaye ameingia Chadema. Ilianza kama uvumi lakini jana ilikuwa dhahiri baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kutangaza rasmi kukihama chama tawala, CCM na kujiunga na Ukawa kupitia Chadema, huku akisisitiza; “Sasa basi, imetosha.”
Baada ya kukabidhiwa kadi ya Chadema na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Lowassa alisema amejiunga na chama hicho kikuu cha upinzani ili kutekeleza azma yake ya kuwakomboa Watanzania na kuendeleza safari ya matumaini kupitia Ukawa.
“CCM kimepotoka, kimepoteza mwelekeo na sifa za kuendelea kuiongoza Tanzania,” alisema Lowassa katika mkutano wa kumkaribisha Chadema uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Ledger Bahari Beach na kurushwa moja kwa moja na vituo kadhaa vya televisheni na redio.
Dakika chache baada ya mkutano huo, CCM kupitia mitandao yake ya kijamii ilitangaza kuitisha mkutano wa wanahabari leo mchana kutoa taarifa muhimu, ikiaminika kuwa utakuwa wa kumjibu kiongozi huyo.
Katika mkutano huo, Lowassa alitumia dakika 13 kueleza sababu za kujiunga Chadema, mbele ya wenyeviti wenza wa vyama vinavyounda Ukawa; Mbowe, Dk Emmanuel Makaidi (NLD), James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Profesa Ibrahim Lipumba (CUF).
Katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, Naibu wake (Bara), John Mnyika, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu hawakuonekana na hawakupatikana kuzungumzia sababu za kutokuwapo katika tukio hilo muhimu.
Lowassa ambaye aliingia katika ukumbi huo saa 10.20 jioni akiwa ameambatana na mkewe, Regina, watoto wake, ndugu na jamaa, pia aligusia sakata la kampuni ya kufua umeme ya Richmond lililosababisha ajiuzulu wadhifa wa waziri mkuu mwaka 2008, kwamba alifanya hivyo kwa manufaa ya nchi na alishindwa kuvunja mkataba huo kutokana na amri kutoka mamlaka ya juu.
Ahama na wimbo wake
Wakati Lowassa akizungumza, wanachama wa Chadema walikuwa wakiitikia ‘peoples power’, na alipomaliza hotuba yake wanachama wao waliimba wimbo maalumu kuwa wana imani naye, “Tuna imani na Lowaasaa, oya oya oyaa.”
Wimbo huo pia uliimbwa na wanachama wa CCM katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho mjini Dodoma, baada ya jina mbunge huyo wa Monduli kutokuwamo kati ya wagombea watano waliopitishwa na Kamati Kuu kuwania nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu ambayo ilikwenda kwa Dk John Magufuli.
Mchakato CCM
Katika hotuba yake, Lowassa aligusia jinsi mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM ulivyogubikwa na mizengwe na kusisitiza: “Nimetumia muda huu kutafakari kwa kina yaliyotokea Dodoma na hatima yangu katika siasa nchini. Pamoja na yaliyotokea Dodoma azma yangu iko palepale ya kuanza mchakamchaka wa maendeleo ya kuiondoa nchi katika umaskini.
“Najua sote tumevunjika moyo kwa yaliyotokea Dodoma na mazingira yaliyopelekea matokeo yale. Mchakato uligubikwa na mizengwe, ukiukwaji wa maadili, uvunjaji wa katiba na taratibu za uchaguzi za CCM.”
Alisema mchakato huo ulisimamiwa kwa upendeleo wa dhahiri na chuki iliyokithiri dhidi yake... “Kikatiba Kamati ya Maadili si chombo rasmi na haina madaraka ya kuchuja na kupendekeza majina miongoni mwa wale wanaoomba kugombea urais kupitia CCM. Kilichotokea Dodoma ni kupora madaraka ya Kamati Kuu na kukiuka katiba ya CCM.”
Alisema vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu viliitishwa na kuburuzwa ili vitekeleze azma ya watu binafsi bila kujali demokrasia, katiba, kanuni na taratibu za uchaguzi ndani ya CCM.
“Kibaya zaidi ni kile kitendo cha kuwanyima wagombea wote 38 haki ya kujieleza mbele ya Kamati Kuu,” alisema.
Alisema Watanzania walitarajia chama kinachoongoza nchi kiwe mfano wa utawala wa sheria na kinara katika kutetea misingi ya haki na demokrasia na siyo kuihujumu, lakini yaliyotokea Dodoma yameitia dosari nchi.
Msimamo
“Sikutendewa haki. Kwa mantiki hii nitakuwa mnafiki kama nitaendelea kujidanganya mimi mwenyewe na umma wa Watanzania kwa kusema kuwa bado nina imani na CCM…,
CCM niliyoiona Dodoma siyo tena kile chama nilichokulia na kilichonipa malezi na maadili ya siasa yaliyojengwa kwenye misingi ya haki, usawa na uadilifu,” alisema.
Lowassa alisema hata Mwalimu Julius Nyerere alisema CCM siyo baba yake wala mama yake na kama Watanzania hawapati mabadiliko ndani ya CCM watayatafuta nje ya chama hicho.
“Baada ya kutafakari kwa kina nimeamua kuwa kuanzia leo ninaondoka CCM na kuitikia wito wa Ukawa kupitia Chadema kuungana nao katika kuleta mabadiliko ya kweli ya nchi yetu,” alisema.
Richmond
Akijibu maswali ya waandishi wa habari, Lowassa alizungumzia sakata la Richmond akisema anashangazwa jinsi anavyohusishwa nalo licha ya kuwa ameshalitolea ufafanuzi na kuwataka wenye ushahidi waupeleke mahakamani.
Alisema alijiuzulu uwaziri mkuu kwa niaba ya Serikali huku akisisitiza kuwa wakati huo waliingia mkataba na kampuni hiyo kutokana na shida ya umeme wakati huo, lakini baadaye waligundua kuwa ilikuwa na matatizo mengi na alipotaka kuvunja mkataba huo alizuiwa na mamlaka za juu.
Alisema walikaa kikao na makatibu wakuu kujadili suala hilo na kwamba mmoja wa makatibu hao alitoka nje na kuzungumza na simu kwa zaidi ya saa moja, baada ya kurudi katika kikao alimueleza kuwa mkataba huo usivunjwe na kwamba ni amri kutoka mamlaka ya juu.
Mbowe aweka msimamo
Katika hotuba yake ya kumkaribisha Lowassa, Mbowe alisema wakati jina la waziri mkuu huyo wa zamani likikatwa CCM, alifurahi na kuamini kuwa atajiunga na upinzani.
Alisema baada ya kuibuka kwa minong’ono juu ya Lowassa kuhamia Chadema, alipigiwa simu na viongozi wengi wa CCM wakimtahadharisha kuwa wasikubali ajiunge katika chama hicho.
“Hata mimi niliwajibu kuwa hatuwezi kumpokea Lowassa, tena niliwajibu kwa Kiingereza, “over my dead body (sitampokea mpaka kufa)”. Lakini kumbukeni kuwa Chadema ni chama cha kujenga mshikamano na hakiwezi kuhukumu bila ushahidi,” alisema Mbowe.
Akifafanua kauli ya ‘kula matapishi yake’, inayotokana na viongozi wa chama hicho kuwahi kumtuhumu Lowassa katika masuala mbalimbali ya ufisadi miaka ya nyuma alisema: “Hatuwezi kufikiri mambo mema mapya kwa kutafakari mambo mabaya ya zamani. Ni nani aliye mtakatifu mpaka awe na uwezo wa kushika jiwe na kumpiga mwenzake, hii si CCM tu hata Chadema au Lowassa.”
Alisema Ukawa ikichukua dola haitaongoza nchi kwa kulipa visasi, bali kuwaletea Watanzania maendeleo huku akisisitiza kuwa kumleta Lowassa Ukawa haikuwa kazi rahisi kwani vilifanyika vikao vingi.
“Lowassa ni waziri mkuu wa kwanza mstaafu kusema CCM si mama yake. CCM kimejenga hofu kwa wanachama wake. sisi Ukawa tunaamini nchi yetu inahitaji fikra na mtazamo mpya, tumevutana sana lakini tumeendelea kuwa kitu kimoja kwa masilahi ya Watanzania,” alisema.
Mbowe alisema angekuwa mwendawazimu kumkataa Lowassa ambaye ana nguvu kubwa ya kisiasa kujiunga na Chadema wakati atakiletea chama hicho wanachama zaidi ya milioni moja na kusisitiza kuwa mtaji wa chama cha siasa ni watu.
“Lowassa hujui tu minyororo uliyoifungua baada ya kuondoka CCM, umefungua minyororo ya watu wengine akiwamo Ole Medeye yule pale (akimwonyesha, Naibu waziri wa zamani, Goodluck). Siasa ni mchezo unaobadilika kulingana na wakati,” alisema.
Alisema chama ambacho hakiamini katika mabadiliko si chama na kwamba Chadema hakiongozwi kwa kauli yake (Mbowe), bali katiba, kanuni, maadili na miiko.
“Chadema hatupo kugombea vyeo, bali kulikomboa Taifa na kazi iliyopo mbele yetu ni kubwa, hivyo viongozi na wanachama wa Chadema na Ukawa msihofu. Aliyeingia Chadema 1992 na mwaka huu wote wana haki sawa. Wapo watu tuliowatukana sana huko nyuma lakini hiyo haizuii kuwapokea,” alisema na kuongeza:
“Watanzania ondoeni hofu maana tunapambana na mfumo si mtu, Lowassa na wenzake watatupa mbinu za kupambana na mfumo. Leo hii hata ukimchukua malaika na kumpeleka CCM baada ya mwezi mmoja atageuka ibilisi.”
‘Ampongeza’ Kikwete
Mbowe alimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kitendo cha kuliondoa jina la Lowassa kuwa mgombea urais wa CCM, kwa maelezo kuwa wakati wakimuondoa wapinzani walikuwa wakifurahia.
Mbali na Mbowe, Dk Makaidi, Mbatia na Makamu Mwenyekiti wa CUF, Juma Duni Haji walipongeza kitendo cha Lowassa kujiunga na Ukawa, huku Mbatia akisema Tanzania bila CCM inawezekana.
“Sasa ni Tanzania kwanza na vyama baadaye. Hakuna machafuko yatakayotokea nchini lakini walioko madarakani wasituchokoze maana hoja za kupambana nao tunazo,” alisema Mbatia
Ulinzi mkali
Watu waliofika katika ukumbi huo, wakiwamo waandishi wa habari walikuwa wakikaguliwa kwa vifaa maalumu kabla ya kuingia ndani. Ukaguzi huo ulifanywa na walinzi wa Chadema (Red Brigade) na walinzi wa kampuni binafsi.
Waandishi walioingia ndani ya mkutano huo waliitwa kwa majina yaliyokuwa yameorodheshwa mapema, hata walipokuwa ndani ya ukumbi walikaa maeneo waliyopangiwa na kutakiwa kutosimama hovyo.

Lowassa ajiunga rasmi na Ukawa, akabidhiwa kadi ya uanachama Chadema

Edward Lowassa (Kushoto) akiteta jambo na
Edward Lowassa (Kushoto) akiteta jambo na Profesa ibrahim Lipumba (Kulia) katika Mkutano uliofanyika katika hoteli ya Bahari Beach Jijini Dar es Salaam  

Aliyekuwa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametangaza rasmi kuhama CCM na kujiunga na Ukawa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.
Lowassa ametangaza uamuzi huo jana katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar na kusema amekubali mwaliko wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Amesema kuwa CCM haikumtendea haki katika kupitisha majina ya wagombea urais hivyo hawezi kuendelea kubaki kwenye chama hicho ‘’ Niliwekewa mizengwe kuhakikisha Jina langu halifiki Kamati Kuu na Halmashauri Kuu’’.
Waziri Mkuu huyo wa zamani ameeleza kuwa nia yake ni kuleta mabadiliko hivyo kujiunga na Chadema ni kuendeleza nia yake ya kuwatumikia Watanzania ‘’ CCM Si baba yangu wala Mama yangu, Watanzania kama wameyakosa mabadiliko ndani ya CCM, basi watayapata nje ya CCM’’
Aidha ameongeza kuwa hajakurupuka kufanya uamuzi huo na kuendelea  kubaki ndani ya CCM itakuwa ni unafiki ‘’ Sijakurupuka kwa uamuzi huu hivyo basi kuanzia leo natangaza rasmi kuondoka CCM na kujiunga na UKAWA kupitia Chadema’’ alisema Lowassa.
Hata hivyo muda mfupi baada ya kutangaza uamuzi huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alimkabidhi Lowassa kadi ya uwanachama.

Monday, July 27, 2015

Diamond amliza Wema


Inasikitisha! Mrembo Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amejikuta akiangua kilio baada ya kupewa maneno ya kejeli na aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kufuatia kupigwa chini kwenye kura za kuwania Ubunge wa Viti Maalum mkoani Singida kupitia Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
wemasepetuMrembo kunako Bongo movie aliyekuwa akiwania ubunge wa viti maalum Ikungi Singida, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.

TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini kililiambia Ijumaa Wikienda kwamba, Julai 24, mwaka huu Wema alijikuta akiangua kilio cha aina yake kufuatia maneno ya kumshambulia kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo Diamond muda mfupi baada ya kuangushwa katika kinyang’anyiro hicho cha ubunge kilichofanyika katika Wilaya ya Ikugi, Singida.
Kiliendelea kunyetisha kwa sauti ya upole kwamba, miongoni mwa vitu vilivyosababisha Wema kudondosha chozi ni pamoja na maneno ya Diamond aliyoandika muda mfupi tu katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram huku akijua wazi kwamba mwanadada huyo alishapoteza fedha nyingi ili apate nafasi ya kuingia mjengoni, Dodoma.
“Ujue watu wengi hawakujua kilichomuuma zaidi Wema ila mimi kaniambia kwamba, kilichomuuma si kukosa nafasi hiyo ila ni maneno ya Diamond aliyoandika kwenye ukurasa wake wa Instagram maana yamemchoma na hakutarajia kama ‘ex’ wake huyo angefikia hatua ya kuonesha chuki zake wazi kiasi hicho.
“Wema alikuwa na matumaini makubwa ya kuibuka mshindi kwenye mchakato huo kutokana na kujulikana kwake na namna wajumbe walivyokuwa wanampa matumaini ila hali imekuwa ndivyo sivyo.
“Baada ya matokeo, sisi tulimuona akiwa kawaida tu lakini baadaye alibadilika na kuwa mnyonge hali iliyonifanya nimuulize kisa cha kuwa vile ndipo akaniambia maneno ya kwenye mitandao yanamchoma.

KUMBE ALITUMIA FEDHA NYINGI
“Unajua amekuwa wa mwisho kwa kupata kura 90 hivyo ni wazi kuwa hana chake tena katika kuwania nafasi hiyo na alitumia fedha nyingi kwenye kuomba kura kwa wanachama (haikufafanuliwa kivipi kwa madai kwamba alitoa hongo), hawezi tena kuingia mjengoni kwani nafasi tatu zimechukuliwa na wenzake hao, hivyo anachotakiwa kuanzia sasa ni kujipanga ili kama itawezekana baada ya miaka mitano ijayo agombee tena,” kilisema chanzo hicho.

WEMA ANASEMAJE?
Ijumaa Wikienda, kama kawaida yake, baada ya kupata ‘unyunyuzi’ huo lilimtafuta Wema ili aweze kuanika hisia zake baada ya matumaini yake kuishia njiani ambapo alisema kwamba  anaamini kila jambo limepangwa na Mungu hivyo haikuwa bahati yake zaidi ataendelea kujipanga kwa kipindi kingine.
“Namuachia Mungu maana kila jambo hupangwa na yeye, hakuna mtu anayeshindana akashindwa halafu awe ‘happy’ tu, nimeumia isipokuwa Mungu ndiye jibu la kila kitu,” alisema Wema na kuongeza:
“Nilipoamua kugombea nilijua kuna kupata na kukosa. Awamu hii nimekosa lakini dunia inazunguka.
“Nawashukuru wote walionipinga kwa sababu waliniongezea ujasiri.”
Kwa upande wa Meneja wa Wema, Martin Kadinda aliweka ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Haikuwa vile tulivyotarajia….hongera Aysharose Mattembe.”
Maneno ambayo aliyaposti Diamond yaliyomchoma Wema hadi kufikia hatua ya kumwaga chozi yalisomeka: “Sitaacha kuwashukuru Wanasinginda kwa mapenzi yenu ya dhati mliyonioneshea, Moshi tukutane Kili Home.”
Wema alikuwa ni miongoni mwa wagombea wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), katika Wilaya ya Ikungi, Singida ambapo mchakato wa kura za maoni ulifanyika Julai 24, ambapo aliambulia kura 90 akishika nafasi ya nne huku mtu wa kwanza Aysharose Mattembe alikipata kura 311, nafasi ya pili ikichukuliwa na Martha Mlata aliyezoa kura 235 na ya tatu akichukua Diana Chilolo kwa kura 182.

SABABU ZA KUSHINDWA
Wikiendi iliyopita mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii ilikuwa ni ishu ya Wema kukosa ubunge ambapo miongoni mwa sababu hizo ni skendo mfululizo na picha zisizokuwa na maadili zilizojaa mitandaoni na kwamba CCM kwa sasa ipo kwenye mkakati mkali wa kusimamia maadili ya chama.

Dokta amfungia baba’ke ndani miaka 4!

Haya ni madai mazito! Pamoja na kukanusha kwa nguvu zote, bado dokta wa  upasuaji wa Hospitali ya Wilaya ya Temeke, Dar aliyetajwa kwa jina moja la Twalib, anadaiwa kumfungia ndani baba yake mzazi, Harub Fitina akimuweka pamoja na kuku na sungura huku akipata mateso ya kunyimwa chakula na huduma nyingine za kibinadamu kwa miaka minne sasa, Ijumaa Wikienda limeibua mazito.

Dokta (3) ….Akipewa chakula.

Akizungumza na gazeti hili huku akirekodiwa, shangazi wa daktari huyo anayeishi Tegeta Masaiti, Kulwa Pazi alisema kuwa, Twalib alimchukua baba yake kutoka nyumbani kwake, Bagamoyo mkoani Pwani mwaka 2011 kwa ajili ya matibabu baada ya kuanguka ghafla na kupooza upande mmoja.
Alidai kwamba, siku chache baada ya kuhamia nyumbani hapo walishangaa kuwa kila wakienda kutaka kumuona mgonjwa waliishia nje kwa kisingizio kuwa mgonjwa anapaswa atulie na asisumbuliwe.

Dokta (2)…Nyumba alimofungiwa.

Alidai kwamba, kama hiyo haitoshi, mke wa mgonjwa ambaye walitengana siku chache baada ya mumewe kuugua, Siasa Mloli aliyebaki Bagamoyo alidai kuwa alikosa mawasiliano na huduma ya watoto kutoka kwa mumewe kwa kipindi hicho cha miaka minne.
Akizungumza na gazeti hili, mke wa Harub alisema kuwa, mapema mwaka jana, mtoto wake ambaye ni mwanafunzi aliyetajwa kwa jina la Jafar alikwenda nyumbani kwa Twalib kuomba fedha za matumizi lakini jamaa huyo alimfukuza, kisa aligonga mlango kwa kutumia jiwe.

IMG_0047-001…Akiwa na wanafamilia

Mbali na shangazi na mke wa jamaa huyo, ndugu wengine walidai kwamba, mapema mwaka huu walisikia kutoka kwa majirani kuwa Twalib anamtesa Harub na kumfungia kwenye banda la sungura na kuku, lakini walipofika nyumbani hapo dokta aliwafukuza.

_MG_0009-001…Akiwa amelala kitandani.

“Baada ya hapo tulikwenda kwa mjumbe wa mtaa na kuripoti kuhusu hali hiyo. Tukampelekea Twalib barua ya wito lakini siku ya kikao hakutokea,” alisema Siasa.

Ijumaa Wikienda lilipofika eneo la tukio liliwashuhudia ndugu hao wakizuiwa kuingia na mlinzi wa nyumba hiyo licha ya kuwa na mjumbe wa serikali ya mtaa kwa madai kuwa Twalib hakuwepo na hataki mtu yeyote aingie ndani kwake.
Ndugu hao na mjumbe walilazimika kuingia ndani kwa nguvu ambapo walijikuta wakitokwa na machozi kwa hali waliyomkuta nayo Harub akiwa amedhoofu.
Waandishi wetu walimshuhudia mgonjwa huyo akiwa amelala kwenye chumba kichafu ambacho upande mmoja kilikuwa kimetengwa kwa waya na chumba chenye kuku na sungura.
Hata hivyo, mgonjwa huyo aliangua kilio na kutoa sauti kwa tabu huku akitumia lugha ya ishara na kusababisha mkewe na mama yake mzazi aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwamvua naye aangue kilio.
Mwishowe ndugu hao walimchukua Harub hadi Kituo cha Polisi cha Wazo Hill ili kutoa taarifa na kupewa jalada WH/RB/6116/2015, TAARIFA kisha waliondoka naye kumpeleka nyumbani kwao Kunduchi.
Waandishi wetu walipokutana na daktari huyo na  kumbwagia tuhuma hizo, alikanusha vikali ambapo alisema shangazi zake wanamzushia mambo mengi kwa kuwa wanataka mali za baba yake.

Saturday, July 25, 2015

Fomu za urais Chadema kaa la moto

Viongozi wa Chadema  kutoka kulia ni Freeman
Viongozi wa Chadema  kutoka kulia ni Freeman Mbowe akifuatiwa na Tundu Lissu na Katibu Mkuu wa Chadema Dk.Wilbroad Slaa 

Wakati leo saa 10 jioni ndiyo muda wa mwisho uliopangwa kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais ndani ya Chadema, hadi sasa hakuna mwanachama hata mmoja aliyejitokeza kuzichukua.
Badala yake zimetolewa kauli tofauti kuhusu kusuasua kwa mchakato wa kumpata mgombea urais hadi chama hicho kulazimika kusogeza mbele tarehe ya mwisho ya kuchukua na kurejesha fomu.
Hali hiyo inazidisha sintofahamu iliyougubika mchakato wa urais ndani ya chama hicho na ndani ya Ukawa, kuwa huenda kuna ‘mtu wa nne’ anayesubiriwa kutoka nje ya chama hicho, kama ilivyoripotiwa na gazeti hili, wiki iliyopita.
Likikariri chanzo cha kuaminika ndani ya Ukawa, gazeti liliandika kuwa huenda umoja huo na hasa Chadema, wanasubiri mgombea kutoka nje ya chama kwa kuwa hata baada ya wajumbe wa vikao vya mashauriano kukubaliana kuwa mgombea wa Ukawa awe Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, baadhi ya wajumbe kutoka katika chama hicho wanadaiwa kukataa kutangazwa kwake.
Hata baadaye walipoulizwa nini msimamo wao kuhusu tetesi za mpango wa kumkaribisha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kutoka CCM, viongozi na wabunge wa chama hicho walisema anakaribishwa mradi tu afuate kanuni na taratibu.
Suala la mgombea urais wa Chadema na Ukawa limeendelea kuteka mjadala wa kisiasa nchini huku Watanzania wakisubiri kufahamu nani atateuliwa kupambana na yule wa CCM, Dk John Magufuli, hali inayosababisha baadhi ya watu kudai mchakato huo una mizengwe.
Hata hivyo, Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha mkoani Iringa, Gaudence Mpangala alisema anadhani hakuna mizengwe inayowazuia baadhi ya wanachama wasiwanie nafasi hiyo kwa kuwa kanuni na taratibu za vyama ziko wazi. Alisema anachokiona ni kwamba wanachama hawajajipanga kuwania nafasi hiyo ya juu.
Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Alexander Makulilo alisema wako watu ambao hawawezi kugombea nafasi ya urais kuwakilisha vyama vyao kwa sababu wanawaogopa viongozi wa juu wa vyama hivyo.
“Jambo la msingi la kuangalia ni haki kutendeka katika kila mchakato katika uteuzi lakini watu wanawania nafasi kulingana na walivyojipanga,” alisema.
Alisema wingi wa wagombea urais katika vyama si kigezo pekee cha kukua kwa demokrasia bali mchakato wa kuwapata wagombea hao ukiendeshwa kwa haki ndiyo demokrasia.
Alisema kuwa hakuna ubaya hata kama kuna mgombea mmoja anayewania urais bali kinachotakiwa kuangaliwa ni ubora wa mchakato.
Hakijaeleweka
Katika mkutano wake uliofanyika mjini Mwanza Jumatano ambao ulipangwa kutumika kumtangaza mgombea urais wa chama hicho, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe aliwaomba Watanzania wavumilie wakati wanakamilisha taratibu za kumpata mgombea huyo.
Pia, ilielezwa kuwa chama hicho kilikuwa kinasubiri mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi wa CUF unaofanyika leo, huku taarifa nyingine zikisema chama hicho kilikuwa hakijampata mgombea mwenza kutoka Zanzibar.
Wakati hayo yakiendelea, bado ratiba ya kuchukua fomu za urais na kurudisha ilikuwa inaonyesha ni leo na hakukuwa na dalili zinazoonyesha watu kujitokeza kuwania nafasi hiyo ya juu, ambayo mara kadhaa viongozi wa chama hicho wametamka kuwa tayari wamempata mgombea anayefahamika ndani na nje ya nchi.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Slaa aliliambia Mwananchi jana kuwa asingeweza kusema lolote kuhusiana na suala hilo kwa sababu alikuwa nje ya ofisi.
“Wasiliana na watu walioko ofisini, wao wataweza kujibu vizuri swali lako,” alisema Dk Slaa.
Katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Dk Slaa aligombea urais na kutoa upinzani mkali kwa mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
Gazeti hili lilipotaka kufahamu iwapo safari hii Dk Slaa amechukua fomu, alikataa kusema lolote akidai taarifa hizo zitapatikana kwa walioko ofisini.
Wabadili ratiba
Akizungumzia hali hiyo jana, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu alisema kuna marekebisho yamefanyika katika tarehe hiyo ya mwisho kurejesha fomu ambayo yatatangazwa ndani ya simu mbili au tatu ambayo yalilenga kupisha mchakato wa kura za maoni.
“Unajua viongozi wanatakiwa kusimamia kura za maoni majimboni, kwa hiyo tuliona kwanza tumalize hili, suala la mgombea urais lisubiri kwanza. Tunatarajia kutangaza tarehe mpya ya kurejesha fomu ndani ya siku mbili,” alisema Mwalimu na kuthibitisha kuwa hadi wanasimamisha shughuli hiyo hakukuwa na mwanachama yeyote aliyechukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea urais.
Baadaye jioni jana, chama hicho kilitoa taarifa ya kusogeza mbele tarehe ya kurudisha fomu hadi Julai 31, 2015 saa 10 jioni.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, watiania wote watapaswa kurejesha fomu hizo katika Ofisi ya Katibu Mkuu, Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni, Dar es Salaam.
Taarifa hiyo ilifafanua kuwa ratiba ya awali iliathiriwa na kitendo cha kusogeza mbele tarehe za uchukuaji na urejeshaji wa fomu za ubunge baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutangaza majimbo mapya 26.
“Hatua hiyo iliathiri ratiba ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania uteuzi wa kugombea urais kupitia Chadema ambapo awali wanachama wenye sifa walipaswa kuanza kuchukua fomu 20-25 Julai, mwaka huu,” ilisema taarifa hiyo.
Mkutano Mbeya waahirishwa
Katika hatua nyingine, ziara ya Dk Slaa aliyetarajiwa kuwasili na kuhutubia mkutano jijini Mbeya leo imefutwa hadi itakapotangazwa tena.
Mratibu wa chama hicho Kanda ya Nyasa (Chadema), Frank Mwaisumbe alisema sababu ya kufutwa ni viongozi wa kitaifa kuendelea na vikao vya ngazi ya juu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chadema mkoani hapa, Joseph China alisema ziara hiyo imefutwa kutokana na viongozi wakuu wa kitaifa kutingwa na vikao vya Ukawa.
Viongozi wa kitaifa wa Chadema wakiwa Mwanza walitangaza kwamba wangefanya mikutano mingine, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam.

Friday, July 24, 2015

ZIARA YA OBAMA NCHINI KENYA NI GUMZO SASA HADI KITAA



If Obama was Kenyan.
Calls Uhunye...
Obama: Man, I need to tell you something
Uhunye: Niaje mzito, Ehe sema...
Obama: And please don't be mad
Uhunye: Weee niambie aki
Obama: I just remembered I have a meeting on Friday
Uhunye: Hauko serious...
Obama: I will still come
Uhunye: Aaaah weee maaani.
Obama: I promise I will pass by.
Uhunye: Utapitia ama Utakam?
Obama: Will Ruto be there?
Uhunye: Ziiiii Ziiii hatakuwa.
Obama: Are you sure?
Uhunye: Eeeeh hatakuwa, double sure, ata nimempea leave saa hii like 5 minutes ago.
Obama: Ok, I really wanted to talk to him
Uhunye: Ako apa mtaongea na yeye?
Obama: On friday, not now
Uhunye: Atakuwa. Utakam saa ngapi?
Obama: 1PM i will be there
Uhunye: Atakuwa from 6AM
Obama: Hopefully i will be there
Uhunye: Weee niambie ama unakuja ama hukuji
Obama: Hey stop the altitude
Uhunye: Ok, ok, Am very sorry, are you coming yes or no
Obama: I will tell you
Uhunye: Sawa, lakini utakam?
Obama: Let me call you back
Uhunye: After how long?
Obama: Evening
Uhunye: Ngai
Obama: I will call you
Uhunye: Ok niseme upikiwe ama usipikiwe friday
Obama: I will tell you
Uhunye: So Wapike?
Obama: I will tell you.
Uhunye: Ok, ama wasipike, ndio tusijiwaste
Obama: Ok, tell them to hold on first
Uhunye: So haukuji?
Obama: I might be late
Uhunye: Meeting itakuwa wapi nikupick?
Obama: Moscow
Uhunye: Uko ni far, Uko sure huezi kam alafu uende meeting?
Obama: Putin says its urgent
Uhunye: Bado mnaongeanga na huyo jamaa, yani. Wee kuja, huyo jamaa hakuwangi mpoa
Obama: I will call you. [Hangs up.]
Uhunye Calls Putin
Uhunye: Sema Bro
Putin: Am Good man
Uhunye: Nikuulize mnameet na Obama Friday ama ananienjoy...
Putin: Zi, kwani amekushow?
Uhunye: Poa. Thanks [Hangs up.]
Uhunye Calls Obama
Obama: Hello
Uhunye: Putin ameniambia hamuna meeting Friday...

Mbowe: Watanzania Mtuvumilie

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akihutubia Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika Magomeni, jijini Mwanza jana.  

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema chama chake kimeshindwa kumtangaza mgombea wake wa urais kama ilivyotarajiwa jana, badala yake kikawaomba Watanzania kutokuwa na haraka, wasiwasi wala mihemko na kuwa muda ukifika kitamtangaza.
Akihutubia mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Magomeni jijini hapa, Mbowe aliwaomba wananchi kuuvumilia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa sababu viongozi wake wanaendelea na majadiliano na watakapokubaliana watamtangaza mgombea wao.
Awali, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu alisema ilikuwa wamtangaze mgombea urais kama ilivyoripotiwa na gazeti hili, lakini wenzao wa CUF wamewaomba kuwa wanaendelea na vikao vyao vya chama.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika alisema: “Wengi wana hamu ya kutaka kujua mgombea urais wa Chadema, naomba niseme kwamba tumekuja Mwanza kwa mambo mawili, kuja kuwapokea makamanda hawa wawili na kuitokomeza CCM.
“Ukawa itamsimamisha mgombea urais ambaye Oktoba lazima aiondoe CCM madarakani, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Magdalena Sakaya) ametuomba tena tusubiri hadi tarehe 25 (Jumamosi), kwani watakuwa na kikao cha Baraza Kuu la chama hicho, hivyo tunawasubiri wenzetu.”
Mbowe aliyetumia mkutano huo kuwakabidhi kadi wanachama wapya waliotoka CCM na kujiunga Chadema, Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya, aliweka msisitizo:
“Muungano wetu wa Ukawa ni wa msingi sana, kuna changamoto, tunaomba wananchi muwe wavumilivu, tuache mihemko ili tufikie uamuzi sahihi.
“Tunaomba mtuvumilie, hatuwezi kumtangaza mgombea wetu kwa sababu tu CCM wametangaza wa kwao, hapana! Tutamtangaza mgombea wetu na nyote mtafurahi,” alisema Mbowe huku akishangaliwa na maelfu ya wananchi.
Alisema, Mwenyekiti wa NLD, Dk Emmanuel Makaidi alikuwa ahudhurie mkutano huo lakini kutokana na foleni za Dar es Salaam alishindwa kuwahi ndege na kwamba, viongozi wengine wa CUF na NCCR Mageuzi walialikwa lakini walikuwa na vikao vya vyama vyao.
Mbowe alisema Ukawa ni mpango wa wananchi, siyo wa viongozi na kwamba ulianzishwa Dodoma na viongozi wote wa upinzani na Kundi la Wabunge 201 wa Bunge Maalumu la Katiba walihudhuria, lakini baadhi yao walipenyezewa ‘kitu kidogo’ wakaondoka hivyo kubaki vyama vinne vya siasa.
Udini, ukabila wamkera
Mbowe alionyesha kusikitishwa na kauli alizodai kutolewa na viongozi wa CCM, kumnadi mgombea wao kwa ukabila na kuwataka wananchi kuwakataa wanaotumia mbinu hizo kwani hali hiyo inaweza kusababisha machafuko.
“Nafurahishwa sana na kauli zinazotolewa na viongozi wa CCM, tunampata kiongozi kwa ukabila! Ukawa hatutamchagua mgombea wetu kwa misingi ya ukabila wala udini, huo ni upumbavu,” alisema Mbowe na kuongeza:
“Msikubali kurudisha ukabila wala udini, hapa uwanjani tupo makabila mengi, Wasukuma mpo! Wahaya, Wachaga, (Ezekiel) Wenje (Mbunge wa Nyamagana) ni Mjaluo yupo hapa.”
Alisema Watanzania wanataka mabadiliko na kwamba hali hiyo imeshuhudiwa wakati wa uandikishaji wa daftari la wapigakura.
Aonya wizi wa kura
Mbowe alisema hawatakuwa na tatizo iwapo ushindi utapatikana kwa njia za haki, lakini hawatakuwa na suluhu iwapo utatumika wizi wa kura kumuingiza mgombea madarakani.
“Hatutapiga magoti na kuomba, kama ushindi utapatikana kwa njia halali hatuna tatizo, lakini tukiona mambo yanakwenda ndivyo sivyo tunasema polisi mtatusamehe, mabomu hayatatosha,” alisema Mbowe.
Lembeli, Bulaya waombewa msamaha
Mbowe alisema Chadema kina maadili yake na kwamba Lembeli na Bulaya waliokuwa CCM wametenda mengi lakini anawaombea msamaha.
“Naomba muwasamehe. Wangapi wanasema tuwasamehe?” alihoji Mbowe huku akiitikiwa kwa sauti, “Woteee”.
Alisema viongozi hao ni miongoni mwa wengi wanaokaribia kutimka CCM na kuwapongeza kwa ujasiri wao makini walioonyesha.
Aahidi kutaifisha viwanja vya CCM
Baada ya kueleza jinsi alivyompigia simu bila mafanikio Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo kuomba kutumia Uwanja wa CCM Kirumba kwa ajili ya mkutano huo, Mbowe alisema Serikali ya Ukawa ikiingia madarakani itahakikisha viwanja vyote vilivyojengwa na wananchi vinavyohodhiwa na CCM vinarejeshwa kwenye halmashauri.
“Chadema kwa kushirikiana na Ukawa, viwanja vyote vilivyojengwa na wananchi vitarejeshwa kwenye halmashauri ili vitumiwe na wananchi wote,” alisema baada ya baadhi ya wanawake kuzidiwa na kuanguka kutokana na wingi wa watu na ufinyu wa uwanja wa Magomeni.
Wagombea kulishwa yamini
Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa aliwata wagombea ubunge waliopitishwa ambao wana mawazo ya kuuza nafasi zao kwa CCM kujiengua mapema kabla chama hakijawachukulia hatua.
Pia, Dk Slaa alisema chama hicho kitatoa fomu maalumu ambazo zitasainiwa na wagombea ubunge mahakamani ili kiweze kuwachukulia hatua za kinidhamu watakaokwenda kinyume na taratibu za chama hicho.
“Majimbo 157 yamekamilisha leo (jana), sisi Chadema hakuna jimbo ambalo mgombea atapita bila kupingwa kama wanavyofikiri CCM,” alisema Dk Slaa na kuongeza:
“Tutatoa fomu za uteuzi ambazo wote waliopitishwa kugombea ubunge watasainishwa mahakamani, naomba niseme atakayeuza jimbo atashughulikiwa, kama mtu anataka kujitoa ajitoe mapema.”
Dk Slaa alisema miaka 10 iliyopita wananchi waliahidiwa maisha bora kwa kila Mtanzania, lakini yamegeuka na kuwa kinyume, sasa ni maisha magumu kwa kila Mtanzania.
“Waswahili wanasema ukiumwa na nyoka hata jani likikugusa unakimbia, miaka 10 mliahidiwa maisha bora kwa kila Mtanzania, leo ni maisha magumu kwa kila Mtanzania. Cha kwanza tunachokisimamia Chadema ni kurudisha nchi kwa wananchi, CCM wamepoka madaraka ya wananchi na kuyaweka mikononi mwa wachache, tunawaambia mwisho wao ni Oktoba,” alisema Dk Slaa.
Lembeli afunguka
Akizungumza kwenye mkutano huo, Lembeli alisema: “Nakumbuka tarehe 16 nilisali nikiwa kijijini kwetu na mama yangu mzazi, nikamwomba Mungu anitoe nchi ya laana anipeleke nchi ya matumaini.
Tarehe 17 nikafanya uamuzi, sasa nipo uwanjani, naomba niwaambie sijaja Mwanza hivihivi nimekamilika, nilipotoka nimeaga.”
Lembeli aliongeza: “Nimezoea kusema msemo wangu huu, hebu kunja ngumi... koroga... peoples,” umati wa watu uliitikia “Power”.
Kabla hajahutubia, Lembeli alibisha hodi Mwanza kwa kusema: “Hodi…hodi, aliitikiwa kwa sauti na umati uliohudhuria: “Karibu baba, karibu.”
Bulaya ampa salamu Wasira
Akihutubia baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama, Buyala alianza kwa kuwauliza wananchi: “Nikamtoe? Nauliza, nikamtoe? Nikamtoe nani?” wananchi walijibu kwa sauti kubwa: “Wasira... kamtoe Wasira.”
Bulaya alisema ni bora kama Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika, Stephen Wasira anamsikia akaondoka kama alivyomshauri Makongoro Nyerere.
“Makongoro Nyerere alisema, awamu ya kwanza upo, awamu ya pili upo, ya tatu upo ya nne upo ya tano mwisho wake umefika sasa,” alisema Bulaya.
Alisema kwa Mkoa wa Mara yupo mwenyekiti wake, Vicent Nyerere ambaye atafanya naye kazi kwa karibu na kwamba yeye na wenzake wa Chadema ni muziki mnene na jeshi kubwa.
Lissu na kabila la CCM
Akihutubia kwenye mkutano huo, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu aliwalinganisha, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Andrew Chenge na Spika Anne Makinda kwamba hawana tofauti na mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli, kwa sababu wote ni kabila moja la CCM.
“Nimefanya mikutano mingi, kila mahala nilipokwenda nilikuwa naambiwa Dk Magufuli kabila lake ni Msukuma, wengine Msubi na wapo waliosema Mzinza, mimi naomba niwaambie kwamba kabila moja la CCM ndilo la Dk Magufuli,” alisema Lissu.
Alisema Dk Magufuli ndiye aliyeuza nyumba za Serikali nchi nzima, kauli ambayo ilitiliwa mkazo na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari ambaye alisema watumishi wa umma wanaishi kwenye nyumba za vichochoroni kutokana na Dk Magufuli kuuza nyumba za Serikali.
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Chadema, Arcado Ntagazwa ambaye aliwahi kuwa waziri na naibu waziri kwa miaka 15 alisema: “Safari hii kwa Chadema na washirika wao wa Ukawa ni moja kwa moja Ikulu.
Goli la mkono laibuka
Ntagazwa alisema: “Mambo ya kusema goli la mkono, watambue kwamba Oktoba ndiyo mwisho wa ufisadi,”
Kauli hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ambaye alisema mwaka huu goli la mkono litawageukia wao... “Wakijifanya wao ni watoto wa kihuni makamanda wa Chadema ni wahuni zaidi yao.”
Kuhusu kucheza rafu, Mwalimu alisema wanaotarajia kucheza rafu kwenye uchaguzi mkuu ni wazi kwamba wameshindwa kucheza uwanjani.
“CCM kutangaza kushinda hata kwa goli la mkono ni wazi kwamba wameshindwa kucheza uwanjani sasa sisi tutawafuata hukohuko nje ya uwanja na tutawabana,” alisema Mwalimu.
Wenje, Kiwia watamba
Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje na Highness Kiwia, walisema kwa sasa wapo likizo ya miezi miwili na wanatarajia kuapishwa tena kuwa wabunge baada ya uchaguzi.
Kiwia alisema: “Mimi ndiye rais wa Jamhuri ya watu wa Ilemela, sina shaka tumemaliza kura za maoni sasa nasubiri tena kuwa Mbunge wa Ilemela.”
Akihutubia, Nyerere ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Mjini, alisema kazi inaendelea na kinachofanyika sasa ni kuhakikisha CCM inaondoka madarakani Oktoba.
Leo viongozi hao wa Chadema watakuwa na mkutano mwingine mjini Mbeya na baadaye Arusha na Jumatatu ni Dar es Salaam.

Auawa baada ya kuwachoma visu wenzake kwenye daladala

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mosha Mahona ameuawa na wananchi baada ya kuwachoma kwa kisu abiria watano waliokuwa kwenye daladala linalofanya safari zake kati ya Posta na Ubungo Simu 2000.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa moja usiku katika eneo la Magomeni Usalama na Mahona aliuawa kwa kushambuliwa na wananchi baada ya kudhuru abiria wenzake.
Kamanda Wambura alisema Mahona alikuwa ndani ya daladala hilo lililokuwa likitokea Posta kwenda Kituo cha Simu 2000 ndipo alipotoa kisu hicho na kuwashambulia wenzake sehemu mbalimbali ya miili yao.
“Mahona aliuawa na wananchi baada ya kuwachoma kwa visu abiria watano ambao walipelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu. Majeruhi hao wanaendelea vizuri,” alisema Wambura.
Wambura alisema baada ya Mahona kufanya kitendo hicho walianza kumshambulia na kusababisha kifo chake.
Aliwataja abiria waliochomwa visu kuwa ni; Daudi Mwenera, Geogre Nomani, Bakari Andrew, Zawadi Mwaipopo na Eda Kiwege.
Alisema polisi wanaendelea na uchunguzi ili kujua sababu ya marehemu huyo kufanya kitendo.
Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
Hilo ni tukio la kwanza la aina yake kwa abiria kuchoma visu wenzake.
 

Bulaya: Nilikataa ahadi ya uwaziri

Mchuano mwingine mkali unatarajiwa kuwapo
Mchuano mwingine mkali unatarajiwa kuwapo katika Jimbo la Bunda Mjini ambako Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira atavaana na Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya (pichani). 

Mbunge wa Viti Maalum alihama juzi CCM na kujiunga Chadema, Ester Bulaya amesema licha ya kuahidiwa vyeo vingi ukiwamo uwaziri na ukuu wa wilaya ili asihame CCM, aliamua kuviacha ili aweze kuwasaidia Watanzania wa chini ambao wameonewa na serikali ya chama hicho kwa miaka 50 iliyopita.
Akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyikia katika Viwanja vya Stendi ya zamani mjini Bunda jana, Bulaya alisema wakati chama chake cha zamani kilipogundua mikakati yake ya kuhamia Chadema, makada wake walimwendea wakimsihi asitoke, bali abakie ili apatiwe ukuu wa wilaya au uwaziri.
Bulaya aliyeambatana na Mbunge wa Kahama, James Lembeli ambaye pia alijiunga na Chadema juzi, alisema baada ya kutafakari kwa muda mrefu uhalisia wa maisha ya Watanzania hasa wa vijijini na jinsi ambavyo Serikali ya CCM imekuwa ikiwatendea, aliamua kuachana na ahadi hizo na kujiunga na Chadema kwa kuwa inalenga kuwakomboa Watanzania. “Ngojeni niwaambie, niliahidiwa ukuu wa wilaya na uwaziri ilimradi tu nisihame CCM. Lakini nikaona yote hayo ni upuuzi, bali cha muhimu ni kuwakomboa Watanzania, nikaachana nayo yote nikaja Chadema,” alisema.
Bulaya aliyejigamba kukulia na kufanya kazi ndani ya CCM, alisema chama hicho hakina sera zozote za kuwakomboa Watanzania badala yake kuna za kuwanufaisha wachache, jambo ambali yeye na Lembeli hawakulitaka.
Bulaya alitangaza azma yake ya kugombea ubunge katika Jimbo la Bunda Mjini, akisema tayari ameshajaza fomu za kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea nafasi hiyo.
“Niwaambie tu kwamba nimeshajaza fomu na kuirejesha na kesho (leo) nitashiriki kura za maoni. Inshallaah Mungu akinisimamisha nitagombea nafasi hiyo na nina uhakika wa kushinda,” alisema Bulaya.
Akihutubia mkutano huo, Lembeli aliwataka wakazi wa jimbo hilo kutoipigia kura CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao, badala yake waichague Chadema kwa nafasi zote bila kumsahau Bulaya kwa ubunge kwa kuwa ni mtu mwadilifu.
Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee akihutubia mkutano huo aliwataka Watanzania wakubali kula fedha wanazogawa na makada wa CCM ili wachaguliwe kwa nafasi mbalimbali za urais, ubunge na udiwani lakini kura zote waipatie Chadema.

source: Mwananchi

Tuesday, July 21, 2015

Gwajima akana kortini kumtusi Kardinali Pengo


Tuesday, July 21, 2015

Gwajima akana kortini kumtusi Kardinali Pengo

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima  
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amekana kumtolea lugha chafu Askofu wa Kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati akisomewa maelezo ya awali katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam jana.
Akisomewa maelezo na Wakili wa Serikali, Joseph Maugo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilfred Dyansobera, Gwajima alikana kutoa lugha chafu ila alikubali kuwa yeye ni askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, majina yake na kwamba aliitwa polisi Machi 27, 2015 kwa ajili ya kuhojiwa .
Maugo alidai upande wa mashtaka utawaita mashahidi saba kutoa ushahidi dhidi ya Gwajima pamoja na kuwasilisha vielelezo vitano.
Wakili wa Gwajima, Peter Kibatala aliomba kupewa maelezo ya mlalamikaji katika kesi hiyo.
Hakimu Dyansobera aliuagiza upande wa mashtaka kuwapatia maelezo ya mlalamikaji na kwamba kesi itaanza kusikilizwa kwa mashahidi upande wa mashtaka kutoa maelezo yao Agosti 10, mwaka huu.
Ilidaiwa kuwa kati ya Machi 16 na 25, mwaka huu kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Gwajima alitoa lugha chafu dhidi ya Pengo.
Akisoma maelezo ya awali, Maugo alidai kati ya Machi 16 na 25, Gwajima alitoa maneno machafu kwa Pengo.
Hata hivyo, Gwajima aliyakana maelezo hayo na kukubali maelezo yake binafsi ya kuitwa polisi.
Katika kesi inayomkabili Askofu  Gwajima na wenzake watatu, Maugo alisema nayo ilikuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali, lakini mshtakiwa mmoja hakuwapo mahakamani kutokana na kusumbuliwa na maradhi.
Alidai kwa mujibu wa sheria, mshtakiwa anatakiwa kuwapo mahakamani, hivyo aliomba ipangwe tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali, ambapo itasikilizwa Oktoba 8, mwaka huu.
Katika kesi hiyo, Gwajima  anakabiliwa na shtaka la kushindwa kuhifadhi silaha na risasi anazomiliki kihalali.
Kwa upande wa washtakiwa wenzake, akiwamo mlinzi wake, George Mzava, Yekonia Bihagaze na Mchungaji Georgey Milulu, wao wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa wakimiliki bastola aina ya Berretta pamoja na risasi 20 kinyume cha sheria.
Wanadaiwa kuwa Machi 29, mwaka huu katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni A walikutwa wakimiliki bastola hiyo yenye namba CAT 5802 bila ya kuwa na kibali kutoka mamlaka husika.
Pia wanadaiwa kuwa siku hiyo, washtakiwa hao pia walikutwa wakimiliki isivyo halali risasi tatu za bastola pamoja na risasi 17 za bunduki aina ya Shotgun. Washtakiwa wako nje kwa dhamana

LEMBELI AITOSA RASMI CCM, AHAMIA CHADEMA


Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kahama mkoani Shinyanga, Mhe. James Daudi Lembeli.

v Mbunge wa jimbo la Kahama mkoani Shinyanga, Mhe. James Daudi Lembeli ametangaza rasmi hii leo kuachana na Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendelo (CHADEMA).

MAUAJI YA RISASI, TAJIRI J4 MWANZA ABANWA

IKIWA ni takriban zaidi ya wiki moja imepita baada ya Mkurugenzi wa Mabasi ya J4 Express, Juma Mahende ‘J4” kudaiwa kuua kwa kuwapiga risasi wafanyabiashara wenzake wawili, kigogo huyo amebanwa na polisi kuhusiana na mauaji hayo.


Ally Mohamed enzi za uhai wake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, DCP Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa polisi bado wanafanya uchunguzi wa ndani juu ya tukio hilo huku mtuhumiwa wakimshikilia.
“Tunafanya uchunguzi wa ndani ili kubaini sababu za J4 kuwaua watu hao…waliuawa kikatili na silaha iliyotumika ni bastola aina ya Brown yenye namba 00092890,” alisema Mkumbo.
J4 ambaye mabasi yake yanayofanya safari kutoka Mwanza kwenda mikoa mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi, anadaiwa kuwapiga risasi wafanyabiashara wawili, Ally Mohamed Abeid na Claude Steven Sikalwanda wakazi wa Jiji la Mwanza Julai 13, mwaka huku chanzo cha tukio hilo kikitajwa kuwa ni kudhulumiana katika biashara.

Cloud Steven enzi za uhai wake.
Gazeti hili lililifuatilia tukio hilo ambalo limekuwa gumzo mjini Mwanza ambapo  liliweza kumpata Ramadhan Mohamed Abeid ambaye ni mdogo wa Ally Mohamed  aliyeuawa na alisimulia kama ifuatavyo:
“Siku ya tukio hilo kaka yangu  alinipigia simu saa 8:30 mchana akinitaka nimpelekee gari alilotaka kununua wakati huo akiwa Nyakato, wilayani Nyamagana jijini hapa.
“Nilipofika nilimkuta kaka yangu akiwa na Claude pamoja na mtu ambaye namfahamu kwa sura  ambapo waliku    wa wakimsubiri J4 ili awapatie fedha kutokana na biashara waliyokuwa wamefanya, tulikaa hapo mpaka saa 11 jioni.
“Walipoona J4 amechelewa kaka yangu aliomba twende mjini kutengeneza simu yake wakati huo wakiendelea kuwasiliana na J4 kuhusu biashara zao lakini alisikika kulalamika sana juu ya fedha zake, ilipofika saa moja kasoro  jioni nikaomba kwenda kufuturu, nikawaacha wakisubiri simu kwa fundi huyo ndiyo ukawa mwisho wa kuonana nao kwani walikuwa pamoja,” alisema Ramadhani.

Ally mohamed akizikwa.
Naye dada wa Claude,  Aziza Steven alisema usiku huo marehemu waliwahi kurudi nyumbani wakiwa katika hali ya kawaida na waliandaliwa chakula cha usiku wakala lakini Ally Abeid wakati anakula alikuwa anapigiwa simu na J4 akimtaka wakaonane ili kupeana pesa walizokuwa wamefanya biashara zao.
“Marehemu hakukubali kwenda usiku huo, akamtaka waonane kesho yake asubuhi, kutokana na mvutano huo Ally alivaa suruali na shati jeupe na  miguuni alivaa ndala wakaondoka wote huku Ally akisema wanaenda kuchukua shilingi milioni 25 kwa J4 walizokuwa wamekubaliana katika biashara zao, ikawa mara yao ya mwisho kuongea na kaka yao.
Baada ya Ally na Steven kuuawa ndugu zao Ramadhani na Aziza wakiwa pamoja mmoja wao alisema: “ Sisi tulipata taarifa usiku kuwa ndugu zetu wameuawa, tulikusanyika na saa 12 asubuhi tulikwenda Hospitali ya Rufaa Bugando tukaona miili yao ndipo tukaanza kufuata taratibu za kuweza kupata maelezo ya kitaalamu.
“Daktari mmoja alisema baada ya kuchunguza miili ya ndugu zetu, iligundulika Ally alipigwa risasi tatu kifuani na Steven alipigwa risasi moja kifuani na kusababisha vifo vyao papo hapo,” alisema Ramadhani.
Inadaiwa kuwa mara baada ya J4 kuwaua watu hao maeneo ya Nyakato kulikuwa na baadhi ya majirani ambao hawakuwa mbali sana na eneo la tukio waliliambia gazeti hili kwa masharti ya kutotaja majina yao kuwa risasi ndizo zilizowashitua wakaenda eneo la tukio.
“Tulipofika nyumbani kwa J4 tulimkuta  akiwa amesimama karibu na hao marehemu na baada ya muda mfupi polisi walifika eneo la tukio wakamkamata na  kumuingiza kwenye gari na maiti kisha wakaelekea Hospitali ya Bugando,” alisema shuhuda mmoja kwa sharti la kutotajwa jina.
Marehemu Claude alikuwa ni mkazi wa Nyansaka nje kidogo ya Jiji la Mwanza, alikuwa mfanyabiashara wa nafaka, ameacha mke pamoja na watoto wa nne, kwa upande wa Ally alikuwa akiishi maeneo ya Igoma na alikuwa akijishughulisha na shughuli za ujenzi lakini pia alikuwa mfanyabiashara wa  baa na gesti maeneo ya Igoma, ameacha watoto watatu na mke.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Malongo (pichani) amezihakikishia familia na ndugu wa marehemu waliouawa kuwa watahakikisha haki inatendeka kwa mshtakiwa kwani hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria.