LATEST POSTS

Friday, August 7, 2015

HIVI NDIVYO WASANII WALIVYOMUAGA RAIS JK MLIMANI CITY, DAR

Wasanii JK (1) Wasanii JK (2) Wasanii JK (3) Wasanii JK (4) Wasanii JK (5) Wasanii JK (7) Wasanii JK (8) Wasanii JK (9) Wasanii JK (11) Wasanii JK (12) Wasanii JK (13) Wasanii JK (14) Wasanii JK (15) Wasanii JK (16) Wasanii JK (17) Wasanii JK (18) Wasanii JK (19) Wasanii JK (20) Wasanii JK (21) Wasanii JK (22) Wasanii JK (23) Wasanii JK (24) Wasanii JK (25) Wasanii JK (26) Wasanii JK (27) Wasanii JK (28) Wasanii JK (29) Wasanii JK (30) Wasanii JK (31) Wasanii JK (32) Wasanii JK (33) Wasanii JK (34) Wasanii JK (35) Wasanii JK (36) Wasanii JK (37) Wasanii JK (38) Wasanii JK (39) Wasanii JK (40) Wasanii JK (41) Wasanii JK (42) Wasanii JK (43) Wasanii JK (44) Wasanii JK (45) Wasanii JK (46) Wasanii JK (47) Wasanii JK (48) Wasanii JK (49) Wasanii JK (50)
JANA usiku ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliwaaga kwa huzuni wasanii katika tasnia mbalimbali nchini na kuwaahidi kuendelea kuwa mlezi wao baada ya kumaliza muda wa kuongoza nchi siku 90 zijazo.
Usiku huo uliokuwa maalum kumuaga Rais Kikwete na kumkaribisha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli uliambatana na burudani na chakula cha usiku kwa pamoja.
Moja ya mambo aliyoyazungumza Rais Kikwete ni kuwasaidia wasanii katika kazi zao za sanaa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananufaika kupitia kazi zao.
“Nchini Marekani kuna msanii wa kike anaitwa Tylor Swift ambaye alifanikiwa kutoka kimuziki na kwa mwaka wa kwanza alilipwa zaidi ya dola milioni 40 kwa kazi zake za muziki. Akawa ana uwezo wa kumpata mwanaume yeyote. Kuna kipindi alikuwa na mmoja wa wanaounda Kundi la One Direction yote hiyo ni kufanikiwa kwa kazi zake.
“Leo hii wasanii wetu wanafanya kazi kubwa ya kurekodi, kutunga nyimbo na script lakini mwishoni kazi yake anamkabidhi mtu kwa malipo kiduchu na pesa nyingi anapata mwingine.
“Niwapongeze nimeshakaa na nyinyi vikao vingi kuhusiana na sanaa, nimesaidia kufunguliwa kwa studio ya kurekodia. Nikki wa Pili ameongea kuhusiana na kulipwa malipo kiduchu kutokana na miito ya simu. Utasikia kama unapenda wimbo huu bonyeza nyota! Msanii anapata hela ndogo wao wanatengeneza nyingi. Hilo nalifanyia kazi lipo Cosota kwa sasa.
“Najua hata kama nikimaliza muda wangu bado nitaendelea kuwa mlezi wenu kwa sababu nitakuwa mtu maarufu,” alisema Kikwete.
Katika hafla hiyo, wasanii walipata fursa ya kupiga picha (selfie) na Rais Kikwete sambamba na kucheza naye nyimbo mbalimbali za zamani za DDC zilizopigwa na msanii kutoka THT, Alice pamoja na Shakira.
Hafla hiyo ilifana pia pale alipopanda Dkt. John Magufuli na kwenda kwenye eneo la kupigia ngoma akiambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambapo naye alichukuwa gitaa na kuanza kutoa burudani kwa wasanii.

Thursday, August 6, 2015

NI ALIENS; WAHUSISHWA NA UPOTEVU WA WATU, NDEGE



Duniani kuna mambo mengi ya ajabu ambayo umewahi au hujawahi kusikia. Gazeti hili linapanda milima na kushuka mabondeni kisha kupaa angani kukuletea simulizi ya undani wa viumbe wa ajabu waishio au waonekanao angani. Ungana nami katika simulizi hii.
Huko nyuma niliwahi kudokeza kwenye gazeti tumbo moja na hili, Ijumaa Wikienda lakini sikuingia ndani ili kupata ukweli juu ya viumbe hao wa ajabu waishio angani. Wanaitwa Aliens. Wana muonekano kama binadamu isipokuwa hawafanani moja kwa moja na binadamu. Viumbe hao waliogundulika karne kadhaa zilizopita, wameshatengenezewa filamu nyingi na wasanii mbalimbali duniani (tutazichambua huko mbele).
Aliens wapo wa rangi tofauti kama kijani, weupe, weusi, njano, zambarau na kila aina ya rangi.
Inaaminika kuwa, Aliens wanaoishi angani wana akili nyingi kuliko binadamu. Wana mfumo wa kompyuta uitwao Alien Software  na  wapo juu  kiteknojia kuliko binadamu tatizo tuu hawavai nguo! Tofauti na binadamu ambaye anafanya kazi kwa hatua moja kwenda nyingine, Aliens wao hufanya mambo kinyume kabisa. Kwa mfano wakitaka kusema ‘naomba maji’ husema ‘maji naomba’ yaani cha nyuma kinakwenda mbele na cha mbele kinarudi nyuma. Kama tunavyowashangaa, nao pia wanatushangaa na kutuona viumbe wa ajabu.
Wachambuzi wa mambo ya anga walishaandika ripoti nyingi kuhusu viumbe hao ambao huja duniani na kurudi angani.
Swali ni je, viumbe hao wanaishi katika sayari gani? Wataalam hao wanalijibu swali hilo kwa kusema haijulikani moja kwa moja wanaishi sayari gani lakini kwa uhakika siyo kwenye mwezi (kumbuka mwezi siyo sayari).
Inawezekana bado hujaelewa simulizi hii. Bermuda Triangle ni eneo la pembetatu la bahari lililopo kati ya nchi tatu katika Bahari ya Atlantiki. Miaka kadhaa huko nyuma viumbe hao waliwahi kutua eneo hilo na kuweka historia (nitaisimulia huko mbele). Pia waliwahi kuonekana Kisiwa cha Bermuda, Pwani ya Mashariki mwa Marekani, Kisiwa cha Puerto Rico kilichopo Kaskazini mwa Carrebian na Fort Lauderdale huko Florida, Marekani.
Umewahi kusikia vitu mbalimbali duniani vikisemekana vimepotea katika mazingira ya kutatanisha? Aliens wanahusishwa na upoteaji wa meli baharini hasa za mizigo huku watu wakiamini huwa zinazama lakini uchunguzi ukifanyika meli hizo huwa hazionekani hata ndani ya maji baharini.
Aliens wanatajwa kuhusika na upotevu wa watu duniani ikiaminika kuwa labda watu hao walikufa lakini ukweli ni kwamba huchukuliwa na viumbe hao.Ndege za kijeshi zimeripotiwa mara nyingi kupotea au kutokuonekana milele katika eneo la Bermuda Triangle ikieleza kuwa Aliens ndiyo wahusika wa upotevu huo.
Ujio wa Aliens katika eneo la Bermuda Triangle ulisababisha kisiwa hicho kupata umaarufu duniani na kupewa jina la Devil’s Sea (Bahari ya Shetani) ambapo binadamu wamekuwa wakiamini au kujenga imani potofu kuwa shetani amekuwa na makazi katika eneo hilo na kuwapoteza wasafiri  wa majini. Wengine huhisi ni ushirikina.
Wapo binadamu wanaoamini kuwa Aliens walikuwepo duniani  tangu  enzi  hizo  kabla ya binadamu na hawajaondoka.
Si sehemu hizo pekee lakini wamekuwa wakitua maeneo mbalimbali duniani na kuna baadhi ya serikali duniani zinawajua.
Wataalam wa anga wanadai Aliens wako mbali kimaendeleo na wanafanya wanavyotaka.
>> Je, hawa ni viumbe gani? Ndiyo kwanza simulizi imeanza. Usikose kufuatilia wiki ijayo.

Chanzo: Global Publishers

Kwa Magufuli lazima wakae!

Magufuliii (3)-001Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Mgombea mwenza Samia Suluhu walipochukua fomu za kuwania urais kwenye ofisi za makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, juzi jini Dar.
LAZIMA wakae! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia umati mkubwa kujitokeza kumsindikiza mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), John Pombe Magufuli (pichani)kwenda kuchukua fomu ya urais Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Posta-Mpya, jijini Dar, Amani linakupa mchapo kamili.

Magufuliii (1)-001Wakionesha mkoba wenye fomu za kuwania urais.

Juzi, Magufuli (pichani) akiambatana na mgombea mwenza, Samia Suluhu wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Phillip Mangula na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana walianza msafara kuanzia kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba kuelekea makao makuu hayo ya NEC kuchukua fomu hiyo.Wakizungumzia msafara huo uliosimamisha shughuli zote kwa muda, baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar walisema kutokana na muitikio mkubwa wa wanachama na wasio wanachama waliojitokeza, ni dhahiri itakapofika siku ya uchaguzi, Oktoba 25, mwaka huu, wapinzani lazima wakae kwani Magufuli ni jembe.
“Lazima wakae wapinzani, tena na hivi wanavyoanza kugawanyika mara sijui katibu mkuu wao Slaa amejiengua hawaiwezi CCM hata kidogo.

IMG_0057-001
Mwenyekiti wa CCM taifa, Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza makao makuu ya CCM taifa jijini Dar, wakati wa uchuaji fomu hizo.

“Magufuli ni msafi, hana doa hata moja. Utendaji wake wa kazi umetukuka. Kila Mtanzania anajua namna ambavyo amekuwa akisimamia sheria katika ujenzi wa barabara, kupushi mambo yaende kwenye mstari na hata kuwafokea hadharani watumishi wanaozembea kazini,” alisema Kery Masabwite mmoja wa wakazi wa Dar na kuongeza:
IMG_0487-001
Umati wa watu waliofurika kushuhudia Magufuli akichukua fomu ya kuwania urais.

“Watu wengi ambao si wanachama wa CCM wameguswa sana uteuzi wa Magufuli. Kama hiyo haitoshi, kuna wafuasi wa Chadema na Ukawa ambao hawakufurahishwa na Edward Lowassa kuingia kwenye chama chao, wote wamekihama na watapigia kura CCM.”

Magufuliii (2)-001Wakati akielekea kuchukua fomu NEC kisha kurejea kuhutubia katika Ofisi Ndogo za CCM Lumumba kuhutubia, maelfu ya watu waliojitokeza kumsindikiza walisikika wakimpa jina jipya Magufuli kwa kufupisha jina lake na kuita JM wakimaanisha John Magufuli ukiachana na yale ya Tingatinga, Jembe na Burdoza yaliyozoeleka.

Magufuliii (4)-001Aidha, jina hilo la JM lilikaziwa maana na mnajimu Hassan Yahya Hussein ambaye hivi karibuni alizungumza na Amani na kueleza kuwa utabiri wake unaonesha kuwa mtu mwenye mvuto wa urais wa Tanzania lazima kwenye majina yake kuwe na heruf J, M na N.

Magufuliii (5)-001“Huo ndiyo ukweli na hata kwa marais waliotangulia, wote majina yao yameanzia herufi J, M na N. Hivyo hata ajaye lazima jina lake liwe na herufi hizo,” alisema mnajimu huyo ambapo Magufuli anazo mbili, J na M (JM).

Magufuliii (6)-001Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM taifa, Nape Nnauye.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika ofisi hizo ndogo za CCM mara baada ya Magufuli kuchukua fomu, Rais Jakaya Kikwete alisema tukio hilo lilikuwa muhimu kwake hivyo isingekuwa rahisi kutokuwepo.

Magufuliii (8)-001Katibu Mkuu wa CCM taifa, Abdulrahman Kinana.

“Kuchukua fomu kwa wagombea wetu ni moja ya shughuli muhimu katika chama ndiyo maana niko hapa leo, najivunia pia juzi kuwepo Australia, walinipongeza kwa kuongoza kwa demokrasia na kuwapa watu uhuru wa kuchagua chama wakitakacho. Watanzania wajiandae kwa uzinduzi rasmi wa kampeni tutakaoufanya Agosti 22, mwaka huu,” alisema Kikwete.
Mbali na Kikwete, shughuli hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM kuanzia wilaya hadi taifa akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

Dk. Slaa: Natishwa

 Slaa(2)

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, ambaye tayari amekwishakujivua uanachama wa chama hicho, amesema maisha yake binafsi pamoja na ya familia yake sasa yapo hatarini.
Hatua hiyo ya Dk. Slaa kufichua hatari hiyo inayomkabili dhidi ya maisha yake aliiweka bayana mwishoni mwa wiki katika mawasiliano yake na chumba cha habari cha Kampuni ya Raia Mwema Ltd, inayochapisha gazeti la kila wiki la Raia Mwema na gazeti hili la Raia Tanzania, linalochapishwa kila siku.
Slaa alilieleza Raia Tanzania kwamba kuna juhudi kubwa zinazofanywa na watu ambao hakuwa tayari kuwataja, akisema juhudi hizo zinalenga kutengeneza mizengwe ya kila aina na kisha kumdhuru, lakini hata hivyo, akisema haogopi chochote na kama ni “Mapenzi ya Mungu yatimizwe.”
“Ni dhahiri ninatengenezewa mizengwe ya kila aina. Inaonekana maisha yangu na ya familia yangu sasa yako hatarini. Nimekuambia (mwandishi wa gazeti hili) ili ikitokea chochote ujue siyo bahati mbaya. Sijawahi kuogopa na wala sitaogopa. Mtetezi wangu ni Mungu aliyehai na nina hakika atanilinda kama yanayopangwa siyo mapenzi yake. Kama ni mapenzi yake yatimie na isiwe kama ninavyotaka mimi,” alisema Dk. Slaa. 

Ilivyokuwa kujivua uanachama
Maisha ya Dk. Slaa yapo hatarini ikiwa ni takriban wiki moja tangu ajiuzulu wadhifa wake wa Katibu Mkuu Chadema na kisha kujivua uanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Katika uamuzi wake wa kujiuzulu na kisha kujivua uanachama, Dk. Slaa pia aliweka bayana kwamba anastaafu shughuli za kisiasa, akifanya hivyo kutokana na uongozi wa juu wa Chadema kumkaribisha “kwa mizengwe” ndani ya chama hicho aliyekuwa kada wa CCM, Edward Lowassa, ambaye sasa ndiye mgombea wao pekee wa urais.
Dk. Slaa hakubaliani na namna Lowassa alivyokaribishwa Chadema bila kufuata utaratibu waliokubaliana ndani ya vikao vya chama hicho.
Taarifa ambazo gazeti hili lilizipata wiki iliyopita zinasema, miongoni mwa mali za Chadema ambazo Dk. Slaa alizirejesha baada ya uamuzi wake wa kujiuzulu na kujivua uanachama, ni pamoja na gari alilokuwa akitumia kwa nafasi yake ya Katibu Mkuu. Mbali na gari hilo, alirejesha pia nyaraka nyingine za chama hicho.
Raia Tanzania lilipata taarifa za kurejeshwa kwa mali hizo za Chadema na kupiga kambi Ijumaa iliyopita, maeneo ya Ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam hadi liliposhuhudia tukio hilo la kihistoria.
Majira ya saa 3.15 hivi, gari aina ya Noah lenye namba za usajili T 217 BUZ liliingia katika Ofisi za Chadema likiwa na watu wawili na gazeti hili liliwashuhudia wakiteremka na mkoba mwekundu na kisha kuingia ofisini.
Wakati huo nje ya ofisi, kulikuwapo pikipiki moja iliyokuwa ikizunguka Mtaa wa Ufipa kana kwamba inafanya doria.
Baada ya muda mfupi, saa 3:20 hivi, watu hao walitoka nje ya Ofisi ya Chadema wakiwa mikono mitupu, wakaingia kwenye gari lao na kuondoka eneo la Ufipa. Raia Tanzania lilishuhudia pikipiki hiyo iliyokuwa ikifanya doria ikiingizwa ofisini humo muda mfupi baadaye.
Kuhusu kurudisha kadi yake ya uanachama wa Chadema Ijumaa usiku, Dk. Slaa aliliambia Raia Tanzania akisema: “Sikuwahi kurudisha kadi ya CCM, kwa nini nirudishe kadi ya Chadema? Kadi ni mali yangu na hili nimekuwa nikilieleza mara kwa mara.”
Mbali na kauli hiyo ya Slaa, moja ya vyanzo vyetu vya habari kutoka Makao Makuu Chadema kilieleza; “Hilo sasa ni suala ambalo confirmed (ni rasmi). Dk. Slaa amejivua nafasi yake ya Ukatibu Mkuu na kujivua pia uanachama wa Chadema. Amekerwa na namna mambo yalivyofanyika hovyo, bila kujali misingi ya utawala na maadili katika chama.” 
Dk. Slaa aliacha uanachama wa CCM na kuingia Chadema mwaka 1995 baada ya kutoridhishwa na mchakato wa kusaka wabunge ndani ya chama hicho.
Mwaka huo 1995 alishinda ubunge kupitia Chadema na kudumu bungeni hadi mwaka 2010 alipogombea urais na kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Jakaya Kikwete, huku matokeo ya kura za urais yakigubikwa na tuhuma za uchakachuaji.
Tangu gazeti hili lilipoweka hadharani wiki iliyopita ukweli kwamba mwanasiasa huyo anayekubalika zaidi nchini ameacha nafasi ya Katibu Mkuu wa Chadema, kumekuwa na uzushi mwingi katika mitandao ya kijamii nchini.
Uamuzi wa kujiuzulu wadhifa wake Chadema kwa kutoridhishwa na kupokewa kwa Lowassa kwenye chama hicho bila masharti, umefuatiwa na juhudi kubwa kutoka kwa watu mbalimbali kukanusha taarifa hizo kwa malengo ambayo hayajaeleweka wazi, lakini Ijumaa Dk. Slaa aliliambia Raia Tanzania kwamba ameamua kukaa kimya na kutojibizana na watu hao, asije akawa kama wao.
“Nimezoea kusimamia maadili ninayoyaamini. Nimeheshimu na kutii dhamira yangu daima kwa kuwa naamini Mungu huzungumza nasi kupitia dhamira zetu ndiyo maana binadamu tuko tofauti na viumbe wengine. Watasema mengi, propaganda daima hazijengi,” alisema Dk. Slaa na kuongeza:
“Wanaotumia propaganda kuhalalisha uamuzi mbovu, hawajui madhara wanayoyasababisha.
“Nitakuwa sina tofauti na wao nikipoteza muda kujibu kila kinachoandikwa kwenye mitandao. Nakuhakikishia sitakwenda chama kingine, bali nimestaafu siasa ili nitumikie taifa langu kwa njia nyingine,” alimwambia mwandishi wetu.
Akizungumzia taarifa zilizozagaa kwamba angezungumza na waandishi wa habari, Dk. Slaa aliliambia Raia Tanzania kwa kifupi: “Sina mpango huo, sina papara, najua kuna mengi yatasemwa. Wakati ukifika nitayazungumzia.”
Kutokana na uamuzi huo wa Dk. Slaa ni dhahiri sasa Chadema kinakabiliwa na wakati mgumu wa kusaka mrithi wa Katibu Mkuu huyo wa zamani aliyekuwa amekifikisha chama hicho katika kilele cha siasa Tanzania, na tayari watu wa karibu na Lowassa wameanza kujipanga kwa ajili ya kuinasa nafasi hiyo ya Katibu Mkuu. 

Makongoro Nyerere ashangaa
Katika hatua nyingine, mmoja kati ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyekuwa akiwania kuteuliwa na chama hicho kupeperusha bendera kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, Makongoro Nyerere, amesema Chadema kitapata wakati mgumu kumsafisha mgombea wao wa urais, Edward Lowassa.
Makongoro na Lowassa ni miongoni mwa makada 32 wa CCM waliokatwa majina yao na Kamati Kuu ya chama hicho mjini Dodoma mwezi uliopita.
Akizungumza na Raia Tanzania jana, Makongoro alisema uamuzi wa Lowassa kuhamia Chadema ni wa kidemokrasia na haki ya kila Mtanzania.
“Huo ni uamuzi binafsi, uheshimike. Lakini chama chake kipya kitapata wakati mgumu sana kumsafisha kutokana na tuhuma za ufisadi anazoandamwa nazo.
“Chadema walikubalika mioyoni mwa wananchi kutokana na hoja ya ufisadi dhidi ya Lowassa. Hiyo sabuni au brashi ya kumsafisha haipo hata Nakumatt,” alisema Makongoro, mmoja kati ya wanaCCM wachache waliokuwa wakimnyooshea kidole Lowassa wakati wa kusaka wadhamini ndani ya chama hicho.
Kuhusu uamuzi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa kuachana na siasa, Makongoro alisema hilo si jambo jema hata kidogo.
“Tuna muhitaji. Taifa linamuhitaji. Wanasiasa wa aina yake wanatakiwa kuendelea kutoa mchango kwa mustakabali mwema wa taifa letu. Ninamshauri asiache siasa, aje CCM tujenge taifa,” alisema. 

Chanzo: Raia Tanzania