LATEST POSTS

Sunday, August 16, 2015

Ndege ya Indonesia yatoweka na abiria 54


Mamlaka nchini Indonessia inasema kuwa ndege moja ya abiria iliowabeba watu 54 wakiwemo watoto watano imepoteza mawasiliano na idara ya kituo cha udhibiti safari za ndege.
Maafisa wa idara ya uchukuzi wanasema kuwa ndege hiyo inayomilikiwa na huduma ya Trigana Air ililikuwa ikielekea katika mji wa Oksibil mashambani,mashariki mwa jimbo la Papua kabla ya kutoweka.
 
 
Msemaji wa wizara hiyo amesema kuwa hatua za kuisaka ndege hiyo zimeanza na zinashirikisha mamlaka ya eneo hilo na kwamba hali mbaya ya hewa katika milima ya eneo hilo inaathiri harakati hizo.
Waandishi wanasema kuwa taifa la Indonesia lina rekodi mbaya ya ajali za ndege huku ajali mbili zikiwa tayari zimeripotiwa mwaka mmoja ulioipita.
 
Ndege ya Indonesia Air ilianguka katika bahari ya Java mwezi Disemba ilipokuwa ikitoka Sura Baya kuelekea Singapore na hivyobasi kuwaua watu wote 192 walioabiri chombo hicho.
Vilevile ndege moja ya kijeshi ilianguka katika makaazi ya watu huko Medan Sumatra mnamo mwezi Julai na kuwaua zaidi ya watu 140 ikiwemo watu kadhaa ardhini.

Chanzo: BBC SWAHILI

FLAVIANA MATATA NA MASSAWE WAFUNGA NDOA

flaviana ndoa (1)
Mwanamitindo Flaviana Matata na Deogratius Massawe baada ya kufunga pingu za maisha jana.
flaviana ndoa (2)
Massawe akimbusu mkewe.
flaviana ndoa (3)
Mwanamitindo Flaviana Matata akiwa katika pozi na mumewe Deogratius Massawe.
flaviana-ndoa-(1) flaviana-ndoa-(2)MWANAMITINDO Flaviana Matata jana alifunga ndoa na Deogratius Massawe katika Kanisa la St. Joseph lililopo jijini Dar. Ndoa hiyo ilifuatiwa na sherehe zilizofanyika katika Hoteli ya Serena, Dar

NIKKI WA PILI : Zaidi ya mwanamuziki

Mwanamuziki kutoka kundi la weusi ,Nikki wa Mwanamuziki kutoka kundi la weusi ,Nikki wa Pili

Mara nyingi tumezoea kuona wasanii wakijishughulisha na kazi za sanaa pekee na ni wachache ambao wanafanya kazi za sanaa na wakati huohuo wakajishughulisha na shughuli nyingine za kitaalamu.
Wengi wa wasanii wa Tanzania hawajaenda shule, huku baadhi yao wameishia elimu za sekondari. Hali hii ni tofauti na msanii Nickson Simon au Niki wa pili ambaye yeye kwa upande wake amesoma elimu ya juu na kuwa na shahada ya pili na sasa anaendelea na masomo yake ya shahada ya tatu ya PhD katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Tofauti na usanii msanii huyu pia ni mchambuzi wa masuala ya siasa nchini lakini pia ni mtangazaji mshiriki katika kipindi cha Cloud 360.
Kwa mujibu wa Niki wa Pili, aliingia katika uchambuzi wa masuala ya kisiasa bila kutarajia baada ya kualikwa siku moja na kuonekana kwamba alifaa, hivyo waandaaji waliomwomba ili awe mchambuzi ndani ya kipindi hicho cha runinga.
Anasema kwa kuwa shahada zake amesomea masuala ya maendeleo, imemuwia rahisi kwake kuchambua masuala ya kisiasa ingawa yeye si mwanasisasa na hatarajii kuingia huko.
“Haukuwa mpango wangu ni kitu ambacho kimetokea ghafla, sijawahi kujiona kama mchambuzi lakini kumbe vile unavyotoa mawazo yako kuna mapokeo ambayo wengi wanayapokea inakuwa tofauti,” anasema.
Hata hivyo, Nikki wa Pili anasema anapenda vijana wenye uthubutu, hata alivyosikia idadi kubwa ya wasanii wanajiunga katika siasa aliwaunga mkono.
Anasema ni kitu kizuri kwani inaonyesha kwamba vijana wapo tayari kwa mawazo mapya, lakini jambo la msingi ni lazima watu wawe makini wachunguze na watambue au wafanye utafiti kujua historia zao zikoje na je? Kilichowavutia ni kwenda kuitumikia jamii au kwa ajili ya masilahi yao binafsi.
“Nafikiri kwa wabunge vijana wameonekana wakichapa kazi, ukiangalia mfano kina January Makamba, David Kafulila, Zito Kabwe, Halima Mdee na hata John Mnyika wamefanya vizuri, kwa hiyo unajua vijana wana mwamko wapo tayari kupokea mambo mengi kufanya mabadiliko,” anasema Nikki na kuongeza kwamba ni vizuri kuwa na rais kijana kwa sababu asilimia kubwa ya taifa ni vijana hivyo kiongozi anatakiwa kufanana na wale anaowaongoza.
Mchango alioutua kuendeleza muziki
“Nimejaribu kufanya kwa kiwango fulani katika ushawishi. Kwanza, nimeshiriki harakati za kuishawishi Serikali itambue kikatiba umuhimu wa sekta ya sanaa.”
Anasema pia kuwa ameshiriki mstari wa mbele kama mfano kupinga unyonyaji unaofanywa kupitia milio ya simu na alitangaza kujiondoa Kampuni ya Spice VAS Africa na Push Mobile mwaka jana na baadhi wakafuata baada ya kuelimisha kuhusu unyonyaji huo.
Kwa mujinu wa Niki wa Pili, wasanii wengi bado hawafahamu hata makadirio ya faida au mapato yanayoingia kupitia milio ya nyimbo zao jambo ambalo ni hatari sana kwani kampuni za simu zinachukua asilimia 60, mzalishaji anachukua 31 na mpaka hatua ya mwisho msanii anapata asilimia mbili hadi sita pekee.
“Harakati za kujiondoa huko zinaathiriwa na mfumo, inahitaji safari ndefu ya ushiriki wa Serikali na uamuzi wa wasanii wenyewe. Kwa hivyo, akimaliza PhD nitakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuendeleza harakati hizo, ili siku moja tuone muziki wetu unaondolewa mizizi ya unyonyaji.
“Anasema mbali na harakati hizo, amekuwa muelimishaji wa fursa za ajira kupitia semina iliyoandaliwa na Clouds Media Group.
Semina hiyo iliitwa Fursa, pia ni balozi wa kupinga rushwa, mtetezi wa haki za binadamu na mwanaharakati wa ulinzi wa mtoto dhidi ya unyanyasaji.
Harakati alizowahi kuzifanya
“Baada ya kumaliza Shahada yangu ya Uzamili, nilipata nafasi ya kufanya kazi katika shirika la kimataifa linalojihusisha na Ulinzi wa Mtoto Dhidi ya Unyanyasaji na Utelekezwaji barani Afrika (African Networking for Prevention and Protection Against Childrens).
Muziki
Niki wa Pili anasema ili muziki wa Tanzania usonge mbele na kuchuana na ule wa kimataifa unahitaji kufanyiwa utafiti wa kina.
Anasema iwapo taasisi zilziowekwa kusimamia sanaa hapa nchini zitaifanyia kazi mikakati hiyo, sekta hiyo itaingiza pato kubwa la taifa na kuongeza ajira kwa vijana walio wengi.
Nikki anasmea licha ya wasanii mbalimbali kujitangaza kimataifa, wanatumia nguvu kubwa sana ambayo iwapo utafiti ungefanyika nguvu hizo ingekuwa ni ziada kwa kuvuka mipaka zaidi.
“Hakuna utafiti, ukitaka kuongelea muziki wa Tanzania ni ngumu kwa sababu hakuna takwimu, huwezi kujua baadhi ya mambo yahusuyo sanaa kwa kuwa kuna vitu vya msingi vya kuweza kufanyiwa kazi lakini vimeachwa tu,” anaanza kwa kusema Nikki.
Nyota huyo anasema wasanii nchini wana malengo ya kuwa namba moja Afrika ndiyo maana wanahangaika kwa fedha ndogo wanazozipata kupitia shoo za kila siku.
Anasema hiyo ndiyo sababu ambayo hata kundi la Weusi wameamua kusaidia, huku wasanii wengine wakiangalia namna ya kutoka kwa kutafuta kolabo na wasanii wa kimataifa ili kuzifikia ndoto zao kwani wanahitaji kufika mbali zaidi ili muziki upanuke, hivyo nguvu za ziada kutoka kwa taasisi hiyo zikiongezwa lengo litafikiwa.
Hata hivyo, Nikki anasema changamoto za mitandao kuzikabili ni mtihani, lakini pia imefungua kitu kipya kwao ambapo sasa wanaweza kuuza muziki wao online, “zamani ilichukua wiki moja muziki kufika vijijini lakini kwa sasa ndani ya sekunde kadhaa unaweza kuwauzia mamilioni ya watu muziki wako.
“Kinachotakiwa kufanya ni namna tunavyotumia faida katika teknolojia hizi lakini pia vilevile kuangalia namna ya kupunguza madhara ya teknolojia.”
Nikki anasema ili kufikia katika viwango vinavyofaa kuna mambo ambayo yanatakiwa kufanywa na taasisi zilizopewa dhamana ikiwamo kuangalia namna soko linakoelekea wapi na namna ya kuweza kuingia huko, mfano soko la muziki wa Afrika lakini ili uweze kuingia huko msanii anatakiwa awe na video nzuri, nchi ina maprodyuza lakini bado hawana viwango.
“Mfano Diamond au Weusi wakienda kutengeneza video Afrika Kusini wanalipa mamilioni ya fedha, lakini bado hatupati kitu wala nchi haipati kitu fedha ya ndani inatoka nje ya nchi, kuna kila sababu sasa Tanzania isomeshe maprodyuza wakubwa wawasomeshe wakafikia viwango fulani ili na sisi tupate watu wanaoweza kufanya kazi kubwa zaidi ili hata wasanii wa nje nao pia watamani kufanya kazi na sisi wakaja kufuata ule ubora wa video kwa hiyo nchi itaingiza kipato kikubwa,” anasema Nikki.
Licha ya hayo aliyoyaongea, Nikki anasema Rais atakayepewa ridhaa na Watanzania, anatakiwa kuzingatia kwamba robo ya Watanzania wamejiajiri kupitia sekta ya sanaa.
“Rais ajaye nataka nimwambie kwamba kuna zaidi ya wasanii milioni moja Tanzania, ambayo ni asilimia kubwa ya nchi sanaa inaweza kuajiri watu wengi, ninapopiga muziki wangu Dj anapata kipato, prodyuza na wengineo kwa hiyo kuna mzunguko mkubwa, hivyo ana uwezo wa kuutumia muziki ili kutatua tatizo la ajira nchini.”

Waziri atembeza mkong’oto, wengine wawili waanguka

 Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Dk 
Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Dk Titus Kamani

Mawaziri wawili wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete wameanguka kwenye marudio ya kura za maoni zilizofanyika juzi, huku matokeo ya Jimbo la Busega yakikwama baada ya Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Dk Titus Kamani kumshambulia msimamizi wa uchaguzi.
Walioanguka ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid (Rufiji) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mazingira), Dk. Binilith Mahenge (Makete), huku Dk Raphael Chegeni akiongoza kwenye Jimbo la Busega.
Vurugu kubwa Busega
Hali ilikuwa mbaya jimboni Busega ambako baada ya Dk Kamani na wafuasi walizuia matokeo kutangazwa na kuibuka kwa vurugu zilizosababisha polisi kuingilia kati na kukamata watu wanne walioonekana kumuunga mkono.
“Napigania haki yangu,” alisema Dk Kamani baada ya kutulia kwa vurugu ambazo zilihusisha kupigwa kwa msimamizi wa kura hizo za maoni, Jonathan Mabiya.
“Huu ni ushindani. Uchaguzi uliopita tulikubaliana na matokeo na tulisaini, lakini uongozi umesema turudie, leo hatujasaini wanataka kutangaza kwa nguvu, hatujakubaliana.”
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya, licha ya matokeo kutotatangazwa alisema watu hawana budi kukubaliana na matokeo na kusema kitendo cha Dk Kamani kwa kuhusika kwenye vurugu hizo ni cha kibinadamu.
“Aliyeshinda ameshinda tu hakuna namna. Kilichofanywa na Waziri Kamani kumpiga msimamizi huyo ni mambo ya binadamu tu… lakini walioshindwa lazima wakubali matokeo na lazima yatangazwe,” alisema Mzindakaya.
Halmashauri Kuu ya CCM iliagiza kurudiwa kwa kura za maoni za ubunge kwenye jimbo hilo baada ya kubaini kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni. Katika kura za Awali, Dk Kamani na Dk Chegeni, kila mmoja kwa wakati wake alijitangaza kuwa mshindi, lakini baada ya matokeo rasmi kutangaza Dk Chegeni aliibuka mshindi kwa kupata kura 13,048 dhidi ya 11,829 za Dk Kamani.
Jana, vurugu zilianza saa 4:00 asubuhi baada ya Dk Kamani, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Simiyu, kuingilia kati wakati Mabiya, ambaye ni katibu wa Wilaya ya Meatu, akianza kutangaza matokeo.
Vurugu hizo zilisababisha wafuasi wanne wa Dk Kamani kukamatwa na polisi. Walikuwa wakigomea ujumlishaji matokeo, lakini baada ya kushindwa kuzuia, walianza kupiga huku wakitukana, hali iliyosababisha ofisa wa polisi Wilaya ya Busega aliyefahamika kwa jina moja la Nyaoga, kutoa onyo.
Hali iliyosababisha wananchi waliokuwa kwenye uwanja wa ofisi za CCM wilayani Busega, kushangilia huku wakiimba: “Tuna imani na Chegeni, Chegeni jembe, Kamani siyo chaguo letu.”
Baada ya Polisi waliokuwa na silaha kuimarisha ulinzi, Mabiya alisimama kutangaza matokeo lakini akakatishwa baada ya kurukiwa na watu walioonekana kumuunga mkono Waziri Kamani na kupigwa makonde mbele ya polisi na Mzindakaya.
Kipigo hicho kilimfanya Mabiya akimbilie ndani ya ofisi za chama hicho na kuacha askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakitumia nguvu kudhibiti watu hao.
Wakati wote wa vurugu hizo, Dk. Chegeni alikuwa amesimama pembezoni mwa ofisi za chama hicho akishuhudia matukio hayo, lakini baadaye akaondoka akiwa amepanda gari lake huku akishangiliwa.
Baada ya polisi kufanikiwa kutuliza ghasia, Mabiya alisimama tena kutangaza matokeo hayo, lakini Dk Kamani alimfuata na kumshambulia kwa makonde, hali iliyozua tafrani kubwa zaidi.
Wafuasi wanne wa waziri huyo walikamatwa.
Lakini mtu wa karibu na Dk Kamani alikanusha waziri huyo kumshambulia msimamizi wala kuhusika kwenye vurugu.
“Hivi unamfahamu mheshimiwa Kamani? Ni mtu muadilifu na wala asingeweza kupigana,” alisema mtu huyo baada ya Waziri Kamani kutopatikana kuzungumzia suala hilo.
“Tunachokipinga sisi ni Chegeni kushinda usiku mzima na viongozi wa wilaya wakihesabu kura wakati watu wetu sisi hawakuwapo. Tunauliza ameshindaje, hawasemi.”
Alilaumu kitendo cha polisi kukamata watu watatu waliokuwa wanamuunga mkono Dk Kamani wakati kwenye vurugu hizo kulikuwa na watu wa pande zote.
Dk Kamani aliondoka eneo hilo saa 5:12 na gari aina Toyota Land Cruiser huku kukiwa na ulinzi mkali wa polisi. Matokeo ya awali ya kura hizo yalionyesha kuwa Dk Chegeni alikuwa anaongoza kwa tofauti ya takriban kura 2,300.
Chegeni anena
Akizungumzia sakata hilo, Dk Chegeni alisema:“Sikutarajia kama mwenyekiti wa CCM wa mkoa, mbunge na waziri aliyekuwa mgombea urais na mzee wa familia kumpiga msimamizi wa uchaguzi.
“Kitendo cha kumshambulia msimamizi wa uchaguzi ni aibu na kinadhalilisha nafasi na utu wake. Akiwa kiongozi. alipaswa kusoma alama za nyakati siyo kupiga watu. Kama nisingekomaa mimi lolote lingeweza kutokea maana uchaguzi uliopita alichakachua.”
Rufiji
Kwenye jimbo la Rufiji, katibu wa CCM wa wilaya, Musa Liliyo alisema Waziri Seif alishindwa baada ya kupata kura 5,010 dhidi ya Mohamed Mchengerwa aliyeshinda kwa kupata kura 6,002.
Katibu huyo aliwataja wagombea wengine walioshiriki uchaguzi huo na kura zao kwenye mabano kuwa ni Hassan Sule (325), Shaaban Matwebe (126), Mohamed Salehe Afif (121), Jamal Rwambo (78) Juma Kiolobele (51) na Tano Seif Mwera (17). Hata hivyo, Dk Seif alikubali matokeo hayo akisema hayatasababisha ahame CCM.
“Haiwezekani katika baadhi ya vituo, inaonyesha idadi ya watu waliojiandikisha ni 300, lakini waliopiga kura ni 800, huu ni uhuni mkubwa unaokivuruga chama chetu cha CCM,” alisema Dk Seif.
Dk Seif anabainisha kuwa hatishwi na matokeo hayo kwa kuwa kwa taratibu za CCM, wingi wa kura si kigezo cha mwisho mtu kupitishwa na chama kugombea nafasi aliyoshinda.
Kwa mujibu wa Dk Seif, mwanasiasa yeyote aliyebobea hawezi kuhama chama kwa sababu ya kushindwa kwenye uchaguzi, hivyo hafikiri kabisa kuondoka CCM ila ametoa wito kwa viongozi kuzitazama upya taratibu za namna ya kupata haki pale mtu anapokuwa ameonewa.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Rufiji, Musa Nyelesa amekiri kuwepo kasoro katika uchaguzi huo na kubainisha kuwa hata hivyo idadi ya wapigakura ilikuwa ndogo ikilinganishwa na uchaguzi uliopita.
Nyelesa alikitahadharisha chama hicho kuwa makini ili CCM iendelee kuwa chama cha wananchi, vinginevyo kitakuwa chama cha matajiri na wafanyabiashara wakubwa ambao hutumia fedha nyingi kupata madaraka.
“Tumeshuhudia genge kubwa la wahuni waliotoka Dar es Salaam kuja kusimamia kura hapa Rufiji. Hawa watu wametumia kila aina ya mbinu kuhakikisha kuwa mtu wao anapita katika mchakato huu, hii si sawa, ila kwa kuwa nina imani na chama changu najua kitarekebisha hizi kasoro,”alisema Nyelesa.
Kuhusu ushindi huo, Mchengerwa alisema: “Matokeo hayo ni faraja kwa Wanarufiji na yamenipa somo kwamba natakiwa kuwatumikia Wanarufiji na si kuwa kiongozi wao.”
Makete
Waziri mwingine, Dk.Binilith Mahenge ameanguka baada ya kupata kura kura 7,885 huku Dk Norman Sigala King akipata kura 8,838.
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Njombe, Hosea Mpagike aliwataja wagombea wengine kuwa ni Bonic Mhami, aliyepata kura 124, Fabian Nkinga (74) na Lufunyo Nkinda (42).
Matokeo hayo yanasubiri kupitishwa na Kamati Kuu ya CCM.
Ukonga
Jimboni Ukonga, matokeo ya marudio ya kura za maoni yameendelea kumpa ushindi Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa baada ya kupata kura 10,965 dhidi ya mpinzani wake Ramesh Patel aliyepata kura 6,960.
“Huwezi kutofautisha Ukonga na Silaa, wananchi wananikubali. Ndiyo maana niliamua kukaa kimya wakati haya yote yakitokea kwa sababu mimi ni kiongozi wa CCM ninajua nini ninachokifanya,” alisema Silaa.
 
Chanzo: Mwananchi

JK, Magufuli warusha kijembe ‘kwa Ukawa’


Rais Jakaya Kikwete akijaribu Trekta 
 Rais Jakaya Kikwete akijaribu Trekta alilozawadi na Wadau wa Sekta ya Ujenzi wakati wa sherehe za kumuaga iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Rais Jakaya Kikwete amesema anaamini mgombea wa urais kupitia CCM, Dk John Magufuli ndiye atakayeshinda katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu, na kwamba vuguvugu la kisiasa linaloendelea hivi sasa ni moto wa mabua.
 Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM alikuwa akihutubia watendaji wa Wizara ya Ujenzi na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo katika hafla ya kumuaga, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Kauli ya Rais Kikwete inaweza kutafsiriwa kuwa ni vijembe kwa vyama pinzani, hasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vinavyoendelea na pilikapilika zake tangu kumpokea Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliyehamia Chadema kutoka CCM na kuteuliwa kuwania urais, huku nao wakitupia vijembe CCM.
“Sishangai chama chako kimekuteua kuwa mgombea wa urais wa chama hicho ambacho ndiyo chama changu na mimi ndiyo mwenyekiti wake, nina imani Mwenyezi Mungu akijalia, kazi iliyobakia tutaikamilisha kwa salama. Huo mwingine ni moto wa mabua tu, hauwaki ukadumu,” alisema Rais Kikwete na kushangiliwa na wahandisi hao.
Jina la Lowassa lilikatwa pamoja na wagombea wengine 38 wa CCM walioomba kuteuliwa kuwania urais kupitia chama hicho katika vikao vyake vya Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu, vilivyoketi makao makuu yake mjini Dodoma.
“Huwezi kulazimisha, hata ukilazimisha hayawi,” alisema Rais Kikwete na kuamsha shangwe nyingine uwanjani hapo huku akiwaambia: “Mtampata mwenzenu, inshallah;… ombi langu mpeni ushirikiano rais ajaye, kwani kutokana na kazi yenu nchi imefikia mahali pa kuanza ‘ku-take off.”
Kikwete aliyewasili uwanjani hapo saa 5:02 asubuhi na kuanza kupokea taarifa za utekelezaji za atendaji wakuu wa taasisi saba zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi katika miaka 10 inayomalizika, kabla ya Dk Magufuli kumkaribisha kutokana na utendaji wake, taifa likimpata Dk Magufuli litanufaika kwani ni kiongozi mzuri.
Rais Kikwete aliyetumia takriban dakika 47 kutoa hotuba ya kuwaaga wafanyakazi wa wizara hiyo, alimsifu na kumshukuru Dk Magufuli akimwelezea kuwa ni msikivu aliyefanya kazi nzuri, iliyomfanya alale usingizi usio na mawazo.
Vile vile, Rais alitumia muda huo kuwaeleza wananchi kuwa mara atakapotoka madarakani atakwenda kuishi kijijini kwake Msoga, wilayani Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani na kwamba asingependa watu wamfuate fuate huko.
Alisema akirejea kijijini kwake atafuga ng’ombe na kulima mananasi kwa kuwa ana eneo la ekari 1000 lililopo katika kijiji cha Kibindu alilopewa wakati akiwa mbunge wa Chalinze na kwamba akikaa kijiji atakuwa na utulivu wa kutosha hivyo wasimfuatefuate.
Tangu Lowassa aenguliwe katika kinyang’anyiro cha kuingia Ikulu kwa tiketi ya CCM na baadaye kujiunga na Chadema, kumekuwapo na vuguvugu la wanachama wengi wa CCM kukihama chama hicho na kumfuata.
Akiwahutubia mamia ya wafuasi wa Ukawa muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), makao makuu ya Chadema, Lowassa alisema rafiki yake Kikwete ndiye aliyeharibu uchumi, lakini akasema asingetaka kutoa mashtaka bila kutoa takwimu.
“Wakati Rais Benjamini Mkapa anaondoka madarakani, bei ya sukari ilikuwa Sh650, leo ni Sh2,300, kutoka 650 hadi 2,300 ameharibu uchumi, hajaharibu?” aliuliza na kujibiwa, “ameharibuuu.”
Magufuli
Akimkaribisha Rais Kikwete, Dk Magufuli katika hotuba yake iliyochukua dakika 12 na sekunde 26, alisema kuwa anashanga kwa nini wataalamu hao wa ujenzi hawajamwandalia sherehe ya kumwaga kama walivyofanya kwa Rais, lakini akasema anaamini wana matumaini fulani, hivyo watakuwa wanajiandaa kumfanyia sherehe ya kumpokea mara baada ya kuingia Ikulu mwishoni mwa mwaka huu akiwaomba wasimsahau katika ‘ufalme wao’.
“Kama ndiyo hivyo basi Mungu awabariki, tuliombee taifa tupite salama katika uchaguzi” alisema Dk Magufuli.
Dk Magufuli naye alimtupia kijembe mmoja wa wagombea urais kupitia vyama vya upinzani aliyesema kuwa akiingia Ikulu anawasaidia waendesha bodaboda akisema mtu huyo kasahau kujiuliza vyombo hivyo vya usafiri vililetwa na nani.

Chanzo: Mwananchi

Wednesday, August 12, 2015

CCM, Ukawa gumzo

Mazungumzo kuhusu siasa na hasa Uchaguzi Mkuu, idadi ya watu waliojitokeza kujiandikisha kupiga kura na idadi kubwa ya watu wanaojitokeza kwenye mikutano ya hadhara ya wanasiasa ndiyo hali iliyoenea kila kona ya nchi kwa sasa, kitu ambacho wachambuzi waliohojiwa na gazeti hili wamekielezea kuwa ni kuongezeka kwa mwamko wa wananchi katika masuala ya siasa.
Wachambuzi hao, ambao waliohojiwa na Mwananchi kwa nyakati tofauti, wameeleza kuwa mwamko huo pia unatokana wananchi kutaka mabadiliko, uamuzi wa kada wa CCM, Edward Lowassa kuhamia Chadema na umoja wa vyama vya upinzani ambavyo vimeamua kuunganisha nguvu kwenye uchaguzi, kitu ambacho kimewafanya wananchi waone kunaweza kuwa na ushindani wa kweli safari hii.
Tangu mchakato wa uchaguzi uanze ndani ya vyama, mazungumzo ya wananchi wa kawaida kwenye mikusanyiko mbalimbali kama sokoni, maskani, kwenye vyombo vya usafiri na mitandao ya jamii imekuwa ikitawaliwa na siasa na hasa baada ya CCM kuanza kutafuta mgombea wake wa urais.
Ufuatiliaji huo wa habari za siasa uliongezeka zaidi baada ya kumteua Dk John Pombe Magufuli kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho tawala na jina la Lowassa kutoingia tano bora, kitu kilichomfanya atangaze kujivua uanachama na kuhamia Chadema.
Wanasiasa hao wawili pia wamevuta maelfu ya watu kwenye mikutano yao ya kutambulishwa kwa wanachama, kutangaza kuhama chama na kuchukua fomu za kuwania urais, huku mbunge wa zamani wa Chadema, Zitto Kabwe akivuta mamia ya watu kwenye mikutano yake ya kukitangaza chama kipya cha ACT Wazalendo.
Idadi ya watu wanaotangaza kuhama chama kimoja na kwenda kingine imekuwa ikiibua mijadala mara kwa mara, huku bendera za vyama vikuu vya kisiasa—CCM, Chadema, CUF na NCCR Mageuzi—zikipepea maeneo mengi.
Wakati mwaka 2010 waliojiandikisha kupiga kura mwaka 2010 walikuwa milioni 11.5, mwaka huu idadi inaweza kuwa maradufu baada ya makisio ya watu waliotarajiwa kujitokeza kujiandikisha kuwa milioni 24 huku Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ikieleza kuwa imefikia idadi iliyotarajiwa au kupita malengo kwenye baadhi ya mikoa.
Pamoja na ukweli kwamba kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25 kinatakiwa kitawaliwe na habari na mijadala ya kisiasa, wachambuzi wanazungumzia mwamko wa mwaka huu kuwa ni mkubwa zaidi kulinganisha na chaguzi zilizopita.
Kauli za wasomi
Akizungumza na Mwananchi kuhusu hali hiyo ya siasa kushika nafasi kubwa katika mijadala mbalimbali, Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha (Ruco) alisema wananchi sasa wameamka na kutambua haki yao ya kupigakura, na hivyo wanataka kuitumia kudai mabadiliko waliyoyakosa kwa muda mrefu.
“Kuongezeka kwa umasikini, vijana kukosa ajira, ufisadi na kuongezeka kwa rushwa kumewaamsha wananchi kwa kiasi kikubwa na kuamka kwao kunatokana na kukua wa utandawazi,” alisema Profesa Mpangala.
“Ukiongea na wananchi wengi, wanakwambia kuwa wanataka mabadiliko. Wana matatizo mengi na wanaamini kuwa wakichagua kiongozi mzuri anaweza kuondoa matatizo yanayowakabili.”
Hata hivyo, Profesa Mpangala alisema tatizo lililopo ni wananchi kuamini kuwa mtu mmoja ataweza kuwaletea mabadiliko na kusahau kuwa mabadiliko watayaleta wenyewe, akieleza kuwa ili mabadiliko yatokee ni lazima kubadilisha mfumo wa utawala.
“Wanatakiwa kutazama mfumo maana chama kitakachoingia Ikulu kitaweza kuleta mabadiliko kama mfumo wa utawala utakuwa mzuri. Chama kinaweza kuwa na mgombea mzuri, lakini akashindwa kuleta kipya kwa sababu ya mfumo,” alisema.
Kauli ya Profesa Mpangala juu ya Watanzania kutaka mabadiliko inaungwa mkono na Richard Mbunda ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambaye alisema mwamko huo pia unatokana na ugumu wa maisha kwa watu wengi.
“Ninatembea maeneo mbalimbali ya nchi yetu na kuzungumza na watu. Nilichokibaini ni wananchi kuchoshwa na maisha wanayoishi. Wanahoji wazi iweje maisha yao yawe duni na ya wengine yawe ya juu. Watanzania sasa si watu wa kufuata upepo tu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma,” alisema Mbunda.
“Wanaona tatizo kubwa tulilonalo ni la kimfumo na wanaamini kuwa wakichagua kiongozi wa aina fulani hali yao ya maisha itabadilika.”
Alisema kitendo cha Ukawa kumsimamisha Lowassa kimeibua changamoto mpya kwa sababu ni mgombea anayekubalika na watu wengi na wengi wanaamini kuwa akiwa rais ataweza kuwavusha.
“Hata Magufuli amefanya mengi ikiwa ni pamoja na kujenga barabara nyingi na wananchi wanamfahamu. Wagombea hawa wanaufanya uchaguzi wa mwaka huu kuwa wa kihistoria,” alisema.
Dk Benson Bana ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) naye alimtaja Lowassa kama chachu inayowafanya Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi.
“Mabadiliko ni hali ya kutoka katika hali uliyokuwa nayo kwenda katika hali nzuri zaidi. Watu hawajaanza kuyataka mabadiliko leo, wamekuwa wakiyataka kila uchaguzi. Wapo wanaomuonea huruma Lowassa na kuona kuwa dhamira yake ya kuhama CCM kwenda Chadema ni ya kweli na kuna jambo anataka kulifanya,” alisema.
Alisema CCM imekaa madarakani kwa muda mrefu na kufikia hatua ya kujisahau, jambo ambalo linawafanya wananchi kutaka mabadiliko.
“Binadamu siku zote hupenda mabadiliko. Hili suala la watoto wa viongozi nao kupewa uongozi, wananchi wanaliona na linawaudhi na wanaona CCM kama uwanja fulani hivi wa kubebana. Hawasemi tu ila wanayaona haya na wanayatafakari,” alisema.
“Mfumo wa CCM kujiendesha unatakiwa kutazamwa upya maana chama kineonekana kama cha (katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman) Kinana na (katibu wa itikadi na uenezi wa CCM), Nape (Nnauye),” alisema na kusisitiza kuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho, Philip Mangula amebaki kushughulikia masuala ya nidhamu. Hivi utapata kura kwa kushughulikia nidhamu?”
Alisema wanachotakiwa kukifanya Watanzania ni kuzichambua sera za CCM na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kama zinaweza kutatua matatizo yanayowakabili, si kutazama sifa za mgombea mmoja mmoja.
“Wagombea wote wanakuja na lugha za kuwasaidia machinga, waendesha bodaboda, mamantilie na tatizo la ajira. Hizo ni lugha za kutafuta kura tu. Wanachotakiwa kutueleza wagombea wote ni mkakati watakaoutumia kumaliza matatozo hayo,” alisema.
Hoja za kuwapo mwamko pia zilitolewa na mchambuzi wa masuala ya siasa na utawala na mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Hamad Salim.
“Watanzania wanataka mabadiliko na wapo wanaodhani watayapata kupitia CCM na wanaodhani watayapata nje ya CCM kutokana na kuyasubiri ndani ya chama hicho tawala kwa muda mrefu,” alisema Salim.
Alisema kitendo Lowassa kuhamia Ukawa kumeibua mihemko na ushindani mpya wa kisiasa nchini, na kwamba hilo limekuwa moja ya sababu ya wananchi wengi kujiandikisha.
“Ila si wote wanaojiandikisha kupigakura watapiga kura kuchagua viongozi, wapo watakaotumia shahada zao katika masuala yao binafsi,” alisema.
Profesa Damiani Gabagambi wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(Sua) anaouona mwamko huo kwa vijana waliozaliwa mwishoni mwa miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya tisini, akisema wengi wanataka mabadiliko lakini hawajui yataletwaje.
“Miaka ya nyuma wananchi walikuwa hawapigi kura wakiamini kuwa nguvu ya upinzani ni ndogo, ila kitendo cha vyama vinne kuungana na kusimamisha mgombea mmoja kimewazindua  na sasa wanauona ushindani wa kweli. Ila wapo waliojiandikisha ili wapate shahada tu kwa matumizi mbalimbali,” alisema.
Katika uchaguzi wa mwaka huu, watu saba wamejitokeza kuwania urais kumrithi Rais Jakaya Kikwete ambaye amemaliza vipindi vyake viwili vya miaka mitano kila kimoja.
Wakati CCM imemsimamisha Dk Magufuli, vyama vinne vinavyounda Ukawa vimekubaliana kumsimamisha Lowassa, hali inayofanya uchaguzi wa mwaka huu uonekane kuwa ni vita vya kihistoria baina ya wawili hao.
Pia mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila amechukua fomu za kugombea urais sambamba na Chifu Lutayosa Yemba (ADC), Macmillan Lyimo (TLP), Hashimu Rungwe (Chauma) na Fahami Dovutwa (UPDP).
Mgombea wa nane anatarajiwa kutoka chama kipya cha ACT Wazalendo.

chanzo: Mwananchi

Aliyejiita ‘Mungu’ afariki akiwa na wake 35, watoto 95

 

Jehova Wanyanyi 
Jehova Wanyanyi

Wahenga walisema; “duniani kuna mambo.” Jamaa mmoja aliyejiita ‘mungu’ huko nchini Kenya, Jehova Wanyanyi amefariki duniani na kuacha wake 35 na watoto zaidi ya 95.
Wanyonyi alizaliwa mwaka 1924 magharibi mwa Kenya, karibu na Mlima Elgon ambako anatambuliwa kama Mlima Sayuni.
Wanafamilia na waumini wa kiongozi huyo wa dini aliyoianzisha na kuiongoza, wanasisitiza kuwa ‘mungu’ wao bado yupo hai, ingawa uongozi wa Serikali ya kijiji alichokuwa akiishi unasema Wanyanyi alifariki dunia Julai 18 mwaka huu.
Taarifa za kufariki dunia kwa Wanyanyi zilianza kusambaa tangu Julai mwaka huu, lakini ndugu zake walikuwa wakisisitiza kuwa mungu wao hajafa na kwamba hakuna mwenye mamlaka ya kuhoji mahali alipo.
Baadhi ya viongozi katika eneo alilokuwa akiishi Wanyonyi wanasema kuwa ‘mungu’ huyo alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa katika Hospitali ya Kitale baada ya kuzidiwa.
“Wanafamilia walikuja kwangu kuomba kibali cha mazishi, baada ya aliyejiita Jehova Wanyonyi kushikwa na ugonjwa akiwa njiani kwenda Cherangany Nursing Home Kitale mjini,” alisema Chifu Kipsomba Daniel Busienei alipozungumza na gazeti la The Standard la Kenya.
Chifu Busienei alisema wanafamilia walikwendea kumwomba kibali ya mazishi ili waende hospitali wakachukue mwili wa Wanyonyi kwa kuwa wasingekabidhiwa maiti hiyo bila ya kuwa na kibali hicho.
“Nilimwambia msaidizi wangu awape kibali, waende wakampumzishe Wanyonyi,” alisema Chied Busienei.
Msaidizi wa chifu, Paul Bett anathibitisha kuwa alitoa kibali kwa familia hiyo Julai 19, siku moja baada ya uvumi kuenea kuwa Wanyonyi amefariki dunia.
“Alifariki dunia Julai 18, akiwa njiani kuelekea hospitali na kijana wake ndiye aliyekuja kuomba kibali siku iliyofuata,” alisema Bett.
Wiki mbili zilizopita vyombo vya habari vilizuiliwa kuingia katika makazi ya Wanyanyi yaliyopo katika Kijiji cha Chemororoch, Jimbo la Soy kwa maelezo kwamba ‘mungu’ wao alikuwa mzima wa afya.
Waandishi hao walifika katika eneo  hilo baada ya kupata taarifa kuwa Wanyonyi amefariki dunia. Baadhi ya wanafamilia wakiwamo watoto na wake zao, walisema kuwa mungu wao mwenye enzi alikuwa salama.
Awali, ilielezwa kuwa Jehova amelazwa katika Hospitali ya Cherangany kabla ya kusafirishwa kwenda katika Hospitali ya Rufaa ya Moi huko Eldoret.
Hata hivyo, utata wa kifo hicho uliongezeka baada ya waandishi wa habari kushindwa kuliona jina la ‘mungu’ huyo katika orodha ya majina ya watu waliokuwa wamehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti. 
Utata wa kifo cha mungu huyo aliyekuwa kiongozi wa huduma ya Lost Israelites of Kenya, yenye wafuasi wengi katika mpaka wa majimbo ya Uasin Gishu na Kakamega, ulichochewa na maoni tofauti yaliyokuwa yakitolewa na watu mbalimbali.
Msemaji wa familia ya kiongozi huyo, Eliab Masinde aliendelea kukanusha kuwa mauti imemchukua mungu wao, licha ya uongozi kuthibitisha kifo hicho.
Masinde alisema: “Jehova ni mzima, ingawa hali yake si nzuri sana, amelazwa katika moja ya hospitali jijini Nairobi akipatiwa matibabu kwa usimamizi wa watoto wake wawili.”
“Alikuwa na maumivu ya mgongo kwa muda mrefu, lakini alipelekwa hospitali na watoto wake huko Nairobi. Mungu huwa hafi, kama angekuwa amekufa, tungeshapata taarifa,” alisema Masinde.
Msemaji huyo wa familia ambaye pia ni mwangalizi wa madhabahu wa huduma hiyo, alisema majirani wa Wanyonyi waliomwona alipokuwa akipelekwa hospitali ndio walioeneza uvumi wa kifo chake.
Mkazi mmoja wa kijijini hapo, ambaye hakutaka kutaja jina kwa kuihofia familia ya mungu huyo, alisema kiongozi huyo alifariki ingawa wanafamilia wanaficha suala hilo.
“Jehova alikuwa ana maumivu ya mgongo kwa muda mrefu, alikuwa anatembelea kiti cha magurudumu kabla hajatoweka. Alikuwa ni mzee na tunachokijua, familia inatawa kumweka mrithi wake kwa siri,” alisema.
Anaongeza kuwa Jehova ana wafuasi wengine nchini Uganda na kwamba inawezekana mwili wake umepelekwa huko kwa ajili ya mazishi.
Tangu taarifa za kifo hicho kutolewa, waumini wengi wamekuwa wakifika nyumbani kwa kiongozi wanayemtaja kuwa ni ‘mungu aliye hai’ kumwombea ili apate nafuu haraka.
Baadhi ya wananchi wamekuwa na maoni tofauti kuhusu kifo hicho, huku wengine wakisema haiwezekani mungu kufariki dunia.
John Paul alisema kupitia mtandao kuwa: “Inakuwaje mungu akafa au kuugua? Kama kweli alikuwa mungu, hakupaswa hata kuugua, achilia mbali kifo.”
Wanavyoabudu
Waumini wa Wanyanyi, husujudu mbele yake na kuomba wanachotaka. Mwandishi wa BBC, Muliro Terewa aliingia katika kanisa hilo na kumsikia muumini akisali:
“Mungu mkuu, uliyekuwepo, upo na utakuwepo Jehova. Wewe ndiye aliyezungumzwa kwenye Biblia katika Kitabu cha Isaya 11. Tunakuheshimu kwa sababu kama ulivyosema mwisho umekaribia, tunaomba utuongoze kwenda mbinguni.”
Akihojiwa na BBC, Wanyonyi alisema:”Mimi ni masikini nina watoto 95 wa kuwalisha. Waangalie watoto hawa, hawajala kitu chochote asubuhi hii, nahitaji dola 13 (Sh26, 000) niwanunulie mikate.”
‘Mungu’ huyo alisema aliingia kwenye mwili wa mwanadamu miaka mingi iliyopita kama ilivyoandikwa katika vitabu vitakatifu.
Aliongeza: “Jehova nilimtuma mwana wangu kuwaokoa watu wake lakini wanakataa, hivyo nimeamua kuja mwenyewe labda watu wanaweza kuacha uovu wao.” Alihadharisha kuwa kama hawatakubali na kubadilika, ataagiza moto kutoka mbinguni uwachome, lakini wanaoamini kuwa yeye ni mungu hawataungua.
Waumini wa Wanyanyi wanasema wameshuhudia ‘mungu’ wao akifanya miujiza, ukiwamo ule wa mume na mke waliokuwa wakiugua Ukimwi kupona kabisa.
Hata hivyo, wakati waumini wake wakipaza sauti kuwa Wanyonyi ni ‘mungu’, baadhi ya watu walitishia kumuua iwapo wangemtia mikononi mwao.
“Wanyonyi ni nabii wa uongo. Ni miongoni mwa manabii wa uongo waliosemwa kwenye Biblia,” alisema Mchungaji Julius Makona.
Patrick Busolo alisema: “Wanyanyi siyo Mungu, anajikusanyia mali tu kwa kutumia imani aliyowajengea waumini wake. Anawalazimisha watu wamfanyie kazi ili aweze kuishi vizuri.”
Wanyanyi alisema kuwa aliuteremsha Ukimwi duniani kama adhabu kwa wanadamu wanaodharau amri za Mungu.
Wakati ikithibitika kuwa ‘mungu’ Wanyanyi amefariki dunia, kazi iliyobaki ni kwa waumini wake kumteua kiongozi mwingine atakayesimamia mamia ya waumini wa dhehebu hilo.
Pia, itakumbukwa kwamba, ‘mungu’ huyo alikuwa akisisitiza kwamba hakuna Mungu mwingine isipokuwa yeye pekee aliyeumba vitu vyote. Kiongozi ajaye atasema  ametoka wapi?
Bila shaka jibu wanalo waumini wa The Lost Israelites, wanaoomboleza kifo cha ‘mungu’  wao.
 
Chanzo: Mwananchi

Dk Slaa aikana twitter inayomzushia mazito

 

Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa 
 Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa

Wakati kukiwa na taarifa zinazosambaa mtandaoni zikimuhusisha Dk Willibrod Slaa na akaunti ambayo imekuwa ikitoa msimamo wake wa kujitenga na shughuli za siasa pamoja na Ukawa, katibu huyo mkuu wa Chadema amekanusha taarifa hizo akisema hajawahi kuwa na akaunti ya twitter.
Hii ni mara ya pili kwa Dk Slaa kuzungumza na gazeti hili, lakini akikatakaa kufafanua mambo mbalimbali yanayohusu sakata lake na Chadema, akiahidi kuwa kufanya hivyo baadaye, huku akiweka bayana kuwa hajawahi kuwa na akaunti ya twitter.
Dk Slaa, aliyekuwa anatajwa kuwa mgombea urais wa Chadema, hajaonekana hadharani katika matukio makubwa ya kichama tangu Chadema na Ukawa walipomkaribisha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa na kumteua kuwa mgombea urais anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja huo.
Mara ya mwisho kuonekana kwenye shughuli za chama hicho ni katika kikao cha Kamati Kuu wakati Lowassa alikaribishwa kufanya majadiliano na kujibu hoja za wajumbe.
Lakini baada ya hapo Dk Slaa hakuonekana wakati wa kutambulishwa kwa Lowassa kwa waandishi wa habari, tukio la kuchukua na kurudisha fomu za urais ndani ya chama na tukio la juzi la kuchukua fomu za urais kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Wakati hayo yakiendelea, kuna akaunti ya twitter yenye jina la “Dr Willibrord Slaa” ambayo imekuwa ikitoa kauli mfululizo zikiwa na ujumbe mbalimbali unaoendana na mazingira aliyomo sasa mwanasiasa huyo.
 Agosti 10, kulitumwa ujumbe zaidi mara 10, mmojawapo ukijaribu kuwaaminisha watu kuwa hiyo ni akaunti halisi ya Dk Slaa.
“Ndugu zangu Watanzania, hii ni akaunti yangu rasmi, bila shaka yoyote na naomba ninachoandika hapa kifikishwe kwa Watanzania popote walipo,” unasema ujumbe huo.
Taarifa nyingine zilizotumwa kwenye akaunti hiyo ya twitter ni pamoja na ile iliyoeleza kuwa   Dk Slaa ameomba ulinzi kutoka nchi na mashirika ya kimataifa na atazungumza kupitia runinga na redio pindi atakapopata ulinzi.
Akizungumza na gazeti hili jana, Dk Slaa alisema hajawahi kutuma taarifa yoyote kwenye mitandao ya kijamii.
“Sijawahi ku-operate (kuendesha) kitu chochote kwenye akaunti ya twitter, sina akaunti kama hiyo,” alisema Dk Slaa.
Mbali na kukanusha kumiliki na kuendesha akaunti hiyo, Dk Slaa alirudia kauli yake ya wiki iliyopita kuwa atatoa msimamo wake muda muafaka utakapofika, baada ya kuulizwa swali kuhusu hatma yake ndani ya Chadema na kisiasa kwa ujumla.
“Subira yavuta heri, sasa ili uipate hiyo heri unatakiwa kuvumilia. Kwa hiyo wakati ukifika nitazungumza tu na Watanzania,” alisema.
Alipoulizwa ni wapi alipo kwa sasa, alisema yupo Dar es Salaam anapumzika, lakini akasisitiza kuwa ipo siku ataweka wazi mustakabali wake kisiasa.
Dk Slaa alisema yeye na mke wake Josephine Mushumbusi wanatarajia kusafiri kwenda nje ya nchi katika siku chache zijazo, ingawa hakuweka wazi nchi anayotarajia kuitembelea, lakini akasema atarejea baada ya wiki moja.
 

Gardner amkejeli Jide!

captain56
Mtangazaji maarufu Gardner G. Habash akiwa na demu mjamzito.

REVENGE! Katika kile kinachoonekana kama kejeli kwa mke wake wa zamani aliyekorofishana naye, mtangazaji maarufu Gardner G. Habash, ametundika picha kwenye akaunti yake katika mtandao wa Instagram ikimuonyesha akiwa amempakata mwanamke mjamzito.

Gardner, mume wa ndoa wa nyota wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo, anayesadikika kuwa na matatizo ya uzazi, aliiweka picha hiyo akiificha sura ya mwanamke huyo, lakini akionyesha kulishika tumbo huku akiachia tabasamu na kusindikizia na maneno kuwa mambo mazuri yako mbioni kuja.
Katika maoni mbalimbali ya wadau waliozungumzia suala hilo, baadhi walimpongeza kwa kumpata mwanadada na kumpa ujauzito, huku wengine wakihoji kama huyo ndiye shemeji au wifi yao.
Wapo waliokwenda mbali zaidi na kudai mtangazaji huyo wa zamani wa Times FM, alikuwa amefanya kitendo hicho makusudi ili aweze kumkejeli Jide, ambaye alikaa naye kwa muda wa miaka kumi pasipo kupata mtoto.
“Jamani hivyo siyo vizuri maana anamkejeli tu dada yetu Jide, sijui anaona raha gani kumuumiza mwenzake moyo,” aliandika mdau mmoja.
Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Gardner na kutaka kufahamu kuhusu ukweli wa picha hiyo na kama alikuwa na lengo la kumkejeli mwandani wake huyo wa zamani.
“Yaa, ni kweli picha nimeweka mimi..lakini si kwa lengo la kumkejeli Jide, kwa nini nimkejeli? Mimi sina matatizo naye mbona, ni picha tu nimeweka..
“Huyo ni shemeji yangu, mke wa mdogo wangu mmoja kifamilia. Lakini usijali, wiki hii nitamwonyesha picha nzima ili watu wamtambue na nitawaeleza kwa kirefu,” alisema Gardner, ambaye pia ni mdau mkubwa wa muziki.
Wawili hao waliingia katika mtafaruku miezi kadhaa iliyopita na tangu wakati huo, hakuna hata mmoja kati yao aliyeweza kuzungumzia suala hilo moja kwa moja zaidi ya mafumbo wanayoyatoa kupitia akaunti zao katika mitandao ya kijamii. Jide hakupatikana kuzungumzia picha hiyo.

TIBA YA HEDHI ILIYOFUNGA (AMENERRHOEA)


Wiki hii nilitumiwa maswali mawili ambayo yaliulizwa na watu wengi nikaona niyaandikie tiba zake ingawa si kwa undani zaidi lakini kwa kufanya hivi inaweza kukusaidia Kama wewe una tatizo hili la hedhi kufunga, tafuna ufuta kiasi cha kijiko kimoja kila siku mara tatu. Fanya hivyo hadi upate hedhi. Ni bora zaidi kula ufuta kabla ya zile siku ambazo hedhi hutoka na uendelee wakati inapotoka.
Dawa hii ni nzuri lakini haishauriwi kwa watu wanaotafuta ujauzito kwani unaweza kuwa nao ikasababisha matatizo, kama unaona hedhi yako imefunga, pima kwanza ukiona huna mimba ndiyo utumie tiba hii.

KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA
Kuna watu wengi huielezea hali hii lakini huwa hawajui tiba yake, wengine husema huenda ana minyoo, lakini kumbe ni tatizo ambalo hutibiwa kwa njia rahisi.
Hali ya kujisikia kuwa unataka kutapika lakini hutapiki ni kawaida sana hasa wakati unaposafiri kwa chombo kama meli au ndege, hali ya ujauzito, kupata harufu mbaya, kuona au kuhisi kinyaa baada
ya kuona kitu au chakula fulani kibaya chenye ladha na harufu mbaya.
TIBA: Chukua kijiko kimoja kidogo cha unga wa pilipili manga, koroga ndani ya glasi yenye maji halafu ukamulie ndimu nusu kisha kunywa, hakikisha maji yamechemshwa tayari kwa kunywa, si kila maji unayokutana nayo.
Ukiona hali inajirudia ifanye kuwa dozi, uwe unakunywa asubuhi, mchana na jioni.

chanzo: global publishers

Monday, August 10, 2015

Ama zao au zetu – Lowassa

MGOMBEA urais wa Chadema ambaye pia anawakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, amesema vyama vinavyounda umoja huo visipochukua dola katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, havitaweza kuchukua tena kwa miaka 50 ijayo.
Akizungumza Makao Makuu ya Chama Cha Wananchi (CUF) Buhuruni jijini Dar es Salaam jana mbele ya maelfu ya wananchi waliojitokeza kumpokea alipofika katika ofisi hizo kwa mara ya kwanza, Lowassa alisema ni lazima Ukawa wahakikishe wanashinda uchaguzi mwaka huu.
Lowassa alisema ni lazima umoja huo uhakikishe kuwa wanafanikiwa kuingia Ikulu katika uchaguzi huu kwa sababu wakifanya kosa, hawataweza kufanikiwa hadi baada ya miaka 50.
Kauli hiyo ya Lowassa ilikuwa ni ya kuunga mkono kauli iliyotolewa na mgombea mwenza wake, Juma Duni Haji, aliyedai kwamba balaa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama watashinda uchaguzi huo, litakuwa la kihistoria.
"Nimetumwa na uongozi kuja kuungana na Lowassa hadi kuhakikisha tunaingia Ikulu. Naamini tutafika. Tusipofika mwaka huu tutasubiri miaka 50 ijayo maana hilo balaa lake kwa hawa jamaa litakawa halipimiki," alisema Duni, kauli ambayo Lowassa aliiunga mkono.
Lowassa aliwasifu viongozi wa Ukawa akisema ni imara na hodari kwani pamoja na misukosuko waliyopitia, lakini wameshinda na bado wapo pamoja wakisubiri ushindi utakaopatikana mapema asubuhi ya Oktoba 25 mwaka huu.
Alisema viongozi hao wa Ukawa hawahongeki bila kufafanua ni nani aliyejaribu kuwahonga, na kuongeza kwamba wakiendelea namna hiyo Ikulu ni yao mwaka huu.
Alisema Ukawa watakwenda Ikulu kupitia masanduku ya kra na si kwa maandamano akiwataka wananchi na wanaUkawa kutunza shahada za kupigia kura.
Akizungumzia safari yake ya leo kwenda kuchukua fomu katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Lowassa aliwataka wanachama na wapenzi wake kujitokeza kwa wingi akiwasihi kuwa na busara ili waondokane na sifa ya kuitwa wakorofi.
"Wanasema tuna fujo. Sasa kesho (leo) tujitokeze kwa wingi kwenda kuchukua fomu, lakini tuwe waungwana tusitukane wala kugombana na mtu ili tusiwape kisingizio. Muwe na nidhamu wasipate hoja ili tuwashinde mapema asubuhi," alisema Lowassa ambaye katika mkutano wa kutambulishwa Ukawa, alitahadharishwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kuwa: “Ujiandaa, maana huku kuna mabomu (ya machozi). Lakini huenda wewe (polisi) watakuheshimu kidogo.”
Lowassa alipotaka kuwapa pole wanaCUF kutokana na kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wao, Profesa Ibrahim Lipumba, wanachama walimtaka kuachana na suala hilo kwani wameshalisahau na hawajadhurika kwa chochote.
Kwa upande wa mgombea mwenza wa Ukawa, Duni, alisema hawakuja kwenye vyama kutafuta vyeo ndiyo maana aliamua kuachia nafasi ya Uwaziri na Makamu Mwenyekiti wa CUF ili kuunganisha nguvu na Lowassa na hatimaye kuingia Ikulu.
Mwenyekiti wa Chadema, Mbowe, alisema zimetumika nguvu nyingi za fedha kuhakikisha Ukawa wanasambaratika lakini kwa kuwa ulikuwa mpango wa Mungu, bado wapo pamoja na imara.
"Tumeweza kufika hapa tulipo na safari yetu imebaki kidogo tufike tunapotaka kwa kuwa malengo yetu yanafanana na tumepata baraka kutoka kwa Mungu ila akitokea kiongozi kati yetu akaona malengo yetu hayafai kuliko fursa binafsi, huyo hatufai, bora aende," alisema Mbowe katika kauli iliyoonekana kama ni kijembe kwa Profesa Lipumba na Dk. Slaa walioondoka Ukawa.
Alisema mgombea wao wiki chache zilizopita alikuwa CCM na mgombea mwenza alikuwa CUF lakini wamewapa nafasi kutokana na kuwa sio walafi wa madaraka na wao ni familia moja.
Joto la uchaguzi Arusha, Mwanza nyuzi 100
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole, akijiuzulu wadhifa wake huo, kada mwingine wa chama hicho, Dk. Raphael Chegeni, ametangaza kuvunja urafiki wa kisiasa na mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.
Taarifa za kujiuzulu kwa Ole Nagole zimethibitishwa jana baada ya kuwepo uvumi kwa muda mrefu kuwa alikuwa na mpango wa kufanya hivyo na kumfuata Lowassa Chadema.
Sambamba na Ole Nangole, makada wengine walioachia uongozi ndani ya CCM mkoani Arusha jana ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa, Robinson Meitinyiku na Katibu Mwenezi wa chama hicho Mkoa, Isack Kadogoo.
Raia Tanzania linafahamu kwamba mipango ya viongozi hao kuondoka CCM ilianza mara baada ya vikao vya juu vya chama kulikata jina la Lowassa mjini Dodoma katika harakati zake za kuwania urais kupitia chama hicho.
Wadau mbalimbali wa siasa za Arusha waliliambia gazeti hili jana kuwa viongozi hao wamejiuzulu ili kwenda kuongeza nguvu ya kampeni za urais za Lowassa  ndani ya Chadema.
"Hawa waliokuwa mstari wa mbele kwenye kampeni za Lowassa ndani ya CCM na alipokatwa kugombea urais, walifedheheka sana," alisema mmoja wa watu wa karibuna Ole Nangole.
Vikao vya mkakati wa kuhama CCM vilikuwa vikifanyika kwa siri katika Hoteli ya Milestone jijini Arusha na jana jioni ilidaiwa kuwa walikuwa safarini kwenda Dar es Salaam kumsindikiza Lowassa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua fomu za kugombea urais.
Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Mjini, Ferous Bano, alithibitisha kujiuzulu kwa viongozi hao huku akisistiza kuwa ndani ya CCM kuna viongozi mahiri zaidi ya hao waliojiuzulu na kwamba kuondoka kwao hakuna madhara.
“Hawa (waliojiuzulu) ni kama tikiti maji. Yaani ni tunda kubwa ukilitazama lakini ndani ni maji tu, hakuna lolote. CCM kwa sasa haihitaji viongozi matikiti maji na itaendelea kubaki imara siku zote," alisema Bano.
Alisema hajasikitishwa na kuhama kwao kwani wamedhihirisha udhaifu wao katika uongozi.
Bano alisema mlango upo wazi kwa kiongozi yeyote anayetaka kuondoka CCM huku kukiwa na taarifa kwamba yupo kiongozi mwingine atakayeondoka wiki hii.
 
Chegeni amtosa Lowassa
Wakati hali ikiwa hivyo jijini Arusha, mkoani Mwanza, Mjumbe wa Halmashuri Kuu ya CCM Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa kambi ya Lowassa Kanda ya Ziwa, Dk. Raphael Chegeni, ametangaza kuvunja urafiki wao huo wa kisiasa.
Akizungumza jijini Mwanza jana, Dk. Chegeni, ambaye alimshinda Mbunge wa Busega anayemaliza muda wake, Dk. Titus Kamani kwenye kura za maoni, alisema urafiki huo umevunjika baada ya Lowassa kuhamia Chadema na kwamba sasa ameelekeza nguvu kubwa kushirikiana na wanaCCM wengine kumnadi mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Dk. John Magufuli.
“Siwezi kuwa na rafiki wa kisiasa nje ya CCM, rafiki yangu mzuri ni ambaye yuko ndani ya CCM kwa hiyo Lowassa si rafiki yangu tena," alisema Dk. Chegeni na kuongeza:
"Tulikuwa na kambi 38 za wawania urais, lakini mchakato ulikamilika baada ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kumchagua Dk. Magufuli kuwa mgombea wetu wa urais, huyo ndiye tingatinga la Chama Cha Mapinduzi.
"Nilimtetea Lowassa kwa sababu nilikuwa naamini atakuwa Rais, lakini tukamchagua Dk. Magufuli, hivyo tulivunja kambi zote Dodoma na kubaki na moja, ya Dk. Magufuli. Kwa sasa jukumu letu kubwa wanaCCM ni kumuunga mkono akivushe chama chetu na kufufua matumaini ya Watanzania."
Akizungumzia kura za maoni Busega, Dk. Chegeni alisema mshindani wake wa karibu, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Kamani, hana sababu ya kulalamikia matokeo kwani katika uchaguzi suala la kushinda na kushindwa ni la kawaida na kwamba yeye amewasamehe wote waliojaribu kuvuruga uchaguzi huo.
Chanzo: Raia Tanzania

YANAYOJIRI VIUNGA VYA SIASA LOWASSA ACHUKUWA FOMU YA KUWANIA URAIS KUPITIA UKAWA.









 
Pilika pilika za uchaguzi nchini Tanzania zimeendelea huku Edward Lowassa, ambaye ni mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Chadema na kuungwa mkono na umoja wa vyama vya upinzani nchini humo, UKAWA, akifika ofisi ya Tume ya Uchaguzi kuchukua fomu ya urais. 

Lowassa alindamana na mgombea mwenza Juma Duni Haji pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka vyama mbali mbali vya upinzani.

Waliotemwa Chadema washinda ACT Wazalendo

Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chadema, Chiku Abwao )kushoto) akuongea na wafuasi wa ACT - Wazalendo baada ya kupitishwa na chama hicho kugombea ubunge Jimbo la Iringa Mjini
 
Kada aliyewania ubunge kupitia Chadema katika Jimbo la Kalenga na kutemwa kwenye kura za maoni, Mwanahamisi Muyinga ameibuka mshindi wa kura hizo katika jimbo hilohilo kupitia chama cha ACT-Wazalendo.
Katika uchaguzi uliofanyika katika Kata ya Mlandege mwishoni mwa wiki iliyopita, Muyinga aliibuka mshindi kwa kupata kura 10 akifuatiwa na Daniel Mwangili aliyepata kura saba, huku Edward Mtakimwa na Kiduo Mgunga wakipata kura tatu kila mmoja.
Mbali na Muyinga, wengine waliotemwa Chadema na kushinda ACT ni aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kunduchi, Janeth Rithe na Dickson Ngh’illy aliyewahi kugombea Jimbo la Temeke mwaka 2010. Ofisa wa Habari wa ACT- Wazalendo, Abdallah Khamis alisema jana kuwa Ngh’illy ameshinda katika jimbo jipya la Kibamba baada ya kupata kura 19 kati ya 29 zilizopigwa. Alisema kabla ya kura hizo kupigwa, mgombea mmoja alijitoa na kuacha nafasi hiyo ikiwaniwa na Ngh’illy, Monalisa Ndala na Edna Mwango aliyeambulia kura mbili. “Rithe ameshinda baada ya kupata kura 38 kati ya 58 Jimbo la Kawe, huku Mohamed Ngulangwa akiibuka kidedea Jimbo la Temeke baada ya kupata kura 80 kati ya 93,”  alisema Khamis.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Muyinga aliwashukukuru wapigakura na wakazi wa Kalenga kwa kumuamini na kumpa fursa ya kupeperusha bendera ya chama hicho na kwamba hatawaangusha.
“Nawashukuru kwa kunipa heshima hii. Nataka kuwaeleza kuwa mimi natoka ukoo wa machifu, nimeomba ruhusa ya kuifanya kazi hii katika Jimbo la Kalenga na nimeruhusiwa,” alisema Muyinga na kuongeza:
“Nawafahamu wakazi wa Kalenga kwa zaidi ya asilimia ya 90. Najua kuwa wanategemea kilimo na mimi nimesoma mambo ya kilimo, nitatumia taaluma yangu kuwaletea maendeleo.”

Friday, August 7, 2015

Polisi yakamata bunduki 16 za Stakishari






Jeshi la Polisi limesema limeshakamata bunduki 16 kati ya 21 zilizoporwa kwenye Kituo cha Stakishari.
Bunduki hizo ziliporwa Julai 12 wakati watu wanaoaminika kuwa ni majambazi walipovamia kituo hicho cha polisi, Ukonga – Dar es Salaam na kuua askari wanne na watu wengine watatu.
Jana, Naibu Kamishna wa Kanda ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaambia waandishi wa habari kuwa zaidi ya majambazi 10 wameshakamatwa na polisi wanaendelea kuwahoji kuhusu tukio hilo.
“Silaha zilizokuwa zimebaki ni tano, 16 zimeshakamatwa na hizo tano ndizo tunafanya bidii ya kuzipata. Niwahakikishieni kuwa zitapatikana,” alisema Sirro.
Alisema watuhumiwa waliovamia kituo hicho walikuwa zaidi ya 15 na walitumia mbinu mpya ambayo Polisi hawakuitegemea.
Wakati huohuo; Jeshi la Polisi limewakamata watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya ofisa wa Polisi, Elibariki Palangyo yaliyotokea nyumbani kwake Yombo Kilakala, usiku wa Agosti.
Katika tukio jingine, polisi inawashikilia watu wanne wakituhumiwa kukutwa na vipande vinne vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh30 milioni juzi, saa 1.30 usiku huko Tandale kwa Mtogole.

Mke wa Dk Slaa afunguka



Mke wa Dk Willibrod Slaa, Josephine Mushumbusi 
 Mke wa Dk Willibrod Slaa, Josephine Mushumbusi
 
Siku moja baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuzungumza na gazeti hili na kusema yupo salama, mke wake, Josephine Mushumbusi amekanusha tuhuma zilizozagaa kuwa ndiye aliyemshauri kiongozi huyo wa Chadema kujiuzulu na kumzuia kushiriki vikao muhimu vya chama.
Tetesi hizo zilivuma kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari baada ya Dk Slaa kutoonekana katika vikao muhimu vya Chadema na Ukawa, kuwa Mushumbusi hakupendezwa na kitendo cha Lowassa kupitishwa kuwania urais chini ya mwavuli wa Ukawa na badala yake alitaka Dk Slaa ndiye awe mpeperusha bendera.
Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo Mushumbusi amezikanusha, aliamua alimfungia ndani Dk Slaa kama moja ya mbinu za kumzuia asishiriki shughuli za kichama, tuhuma ambazo amezikanusha.
“Bosi wako akija kukuomba ushauri utamsaidia, lakini akija akakuambia ameshafanya maamuzi unaweza kupingana naye?” alihoji Mushumbusi akianza kutoa maelezo yake na kuendelea:
“Wakati wa vikao nilikuwa namwona (Dk Slaa) anachelewa kurudi kila siku, siku moja akaja akaniambia uamuzi aliouchukua na mimi sikuwa na la kusema, nikachukua shuka nikajifunika.”
Katika mahojiano yake ya kwanza na Mwananchi baada ya kuzagaa kwa tetesi hizo, Mushumbusi pia alikana kumfungia Dk Slaa ndani ya nyumba, akisema wakati maneno hayo yalipokuwa yanazagaa, alikuwa nje ya nchi na wala hakujua kinachoendelea.
“Mwenyewe najiuliza nini kinaendelea, siwezi kufanya kitu kama hicho. Nyumba yangu ina milango miwili, nawezaje kumfungia mtu, tena mwanamume, hata watoto siwezi kuwafungia. Kuna mambo mengine mwanamke huwezi kuyafanya kwa mwanamume. Mwanamume ni mwanamume tu,” alisema.
Alisema viongozi wa Chadema, ndugu, jamaa na marafiki walikuwa wanafika nyumbani kwake na walikutana na Dk Slaa na kuzungumza naye... “Kama ningekuwa nimemfungia wangezungumza naye vipi?”
Mushumbusi alisema mwanamke anaweza kufanya chochote lakini kuna baadhi ya mambo ambayo mwanamume akiamua ni vigumu kumzuia.
Akifafanua tuhuma za kumshinikiza Dk Slaa kujiuzulu Chadema, Mushumbusi alisema kiongozi huyo wa Chadema ana uamuzi wake na yeye ni msaidizi tu ambaye hana uamuzi wa mwisho kwenye familia.
Hata hivyo, alisema endapo angeamua kumshawishi, uwezo wa kufanya hivyo anao lakini yeye ni mwanamke mwadilifu anayependa mafanikio ya mumewe.
“Kwani unanionaje? Mimi ni ‘strong’ (nina nguvu), ningetaka ningefanya hivyo, nisingeshindwa,” alisema.
Pamoja na hayo, Mushumbusi alilalamika kuwa tuhuma hizo dhidi yake zimesababisha asisikilizwe kama ilivyokuwa awali.
Bila kufafanua kwa undani, alisema kuna kundi linalounda propaganda hizo ili abadili mtazamo kuhusu mumewe lakini jambo hilo haliwezi kutokea.
“Nilisema nitampenda kama alivyo, sitajali chochote wala akiwa katika hali gani au chama gani. Kazi yangu ni kumtia moyo ili kile atakachofanya kifanikiwe,” alisema.
Auza mkaa
Mbali na kukanusha vikali tuhuma hizo, Mushumbusi alisema alikwishajitoa kwenye masuala ya siasa kwa miaka miwili sasa na badala yake ameamua kufanya biashara ya kuuza mkaa.
“Nimenyamaza kimya, nimekaa kando ninaendelea na biashara yangu ya kuuza mkaa, nipo mbali na siasa na sitaki kujua kinachoendelea, kwanza hata mchakato wenyewe siujui,” alisema.
Aliwashauri wanawake kuacha kushabikia masuala yanayotokea ndani ya ndoa yake na kuwataka wavae viatu anavyovivaa na wajue kuwa anapitia wakati mgumu.

Chanzo: Mwananchi