LATEST POSTS

Tuesday, October 13, 2015

DUUH! ETI DP: MTIKILA ALIAWA KABLA YA AJALI



mtikila2
Mti ambao gari liliugonga kwa juu kabla ya kupinduka.

Akizungumza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye ofisi ndogo ya chama hicho nyumbani kwa marehemu, Mikocheni B jijini Dar, Mluya alisema hata watu waongee vipi, lakini uchunguzi wao umeonesha kwamba, kiongozi wao aliuawa tofauti na eneo la ajali na mwili kwenda kutupwa pale.

ROHO YAKE ILIWINDWA KWA SIKU 40
Mluya alisema: “Ndugu mwandishi, Mchungaji Mtikila kama kufa alikuwa afe muda mrefu sana pengine siku arobaini zilizopita (mpaka siku ya kifo cha kweli), kwa sababu amewindwa na watu ambao hatujajua lengo lao kubwa lilikuwa nini!
“Kila alikokwenda kwa shughuli za kichama kulikuwa na timu ya watu inayomfuatilia.”

mtikila4
...Baada ya Kupinduka

MARA YA KWANZA
“Tarehe siikumbuki, lakini ni Septemba mwanzoni. Tulikuwa Bunda, Mara kwenye shughuli za chama, kuna watu ambao walikuwa hawaeleweki walitufuata mpaka hotelini.
“Baada ya kubaini hilo, nilimuuliza mwenyekiti kuhusu ratiba aliyokuwa nayo ya kuzungumza kwenye runinga ya Staa TV.
“Alinipa ratiba. Baada ya kumaliza kuzungumza, nilimwambia Bunda si mahali pa kulala hivyo nilimshauri aondoke, aende Mwanza. Na nilimwambia dereva wake aondoke bila kuaga.”

mtikila4 (2)
WAKIWA NJIANI

“Lakini cha ajabu, wakiwa njiani wakielekea Mwanza kuna gari liliwafuata kwa nyuma kwa mwendo ambao waliutulia shaka. Dereva wa mwenyekiti alipokuwa akiongeza mwendo, naye anaongeza, akipunguza naye anapunguza.
“Ilibidi dereva amwambie mwenyekiti naye akamtaka dereva aongeze kasi hadi Mwanza.”
“Katika ratiba yetu tulitaka kufanya ziara za kichama kuanzia  Oktoba 18,  mwaka huu kwa kuanzia mkoa wa Kigoma na kwingineko. Pamoja na kufuatiliwa kote kule mwenyekiti hakuwa na roho ya uoga hata kidogo. Alimtanguliza sana Mungu.
“Kwa hiyo wasiwasi mkubwa wa kufuatiliwa na watu hao ulianza Mara na Mwanza kwa nyakati tofauti.
“Septemba 11, mwaka huu ndiyo tarehe ambayo sasa nilianza kukariri matukio hayo hatua kwa hatua. Siku hiyo tulikwenda kwenye Kijiji cha Usangu mkoani Pwani kwa ajili ya kufanya kampeni ya mgombea udiwani. Baada ya kumaliza tuliamua kurudi Dar lakini njiani dereva akasema kuna watu hawajui wanakuja nyuma yetu.”

WAPOTEA NJIA KWA KUFUATILIWA
“Tulijikuta tukipotea njia na kutokea mjini Kisarawe (Pwani). Pale tulifika kituo cha mafuta ambapo tulikuta gari aina Toyota Land Cruiser VX limepaki kama vile ni watu pia walikuwa wakitufuatilia.
“Lengo la kusimama pale lilikuwa kupata chakula lakini hatukufanya hivyo kulingana na mazingira. Tukaanza safari ya kurudi Dar. Tulipofika Pugu Sekondari, gari lile lilitupita kwa kasi na kupotea.
“Tulipofika Tazara gari lile lilionekana na wakati huo yalikuwa mawili. Kilichotushangaza ni upya wa magari lakini eti namba zinaanzia na A. Mimi nilifikiria kwamba, pengine ni za idara  ya  usalama  wa  taifa  zilikuwa doria  mbalimbali hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi.
“Ndugu mwandishi, mimi ninafanya kazi ya siasa, niko makini sana. Niliwaambia wenzangu kuwa tunafuatiliwa.
“Ndani ya gari sisi tulikuwa na viongozi wa kuwapeleka Temeke. Lakini baada ya kufika huko lile VX tulikutana nalo. Tulipomuacha yule tuliyempeleka kule, tukawa tunampeleka mchungaji nyumbani kwake (Mikocheni) lakini bado lile gari lilikuwa likitufuatilia.”

WAPIGA CHENGA
“Tulipofika maeneo ya Msasani kwa Mwalimu (Julius Nyerere) dereva alikunja kona kuelekea kwa mchungaji na lile gari likakunja kona na kurudi lilikotoka.”

SIKU NYINGINE
“Siku iliyofuata tulipanga mipango yote ambapo sasa tulisema Oktoba 18, mwezi huu tuanze ziara ya mkoa wa Kigoma  na maeneo  mengine ya Kanda ya Ziwa.
“Mimi niliondoka kuelekea Shinyanga, yeye (Mchungaji) aliandaa safari ya kwenda Njombe kwenye kampeni ya mgombea Ubunge Jimbo la Njombe.”

OKTOBA 2, 3, 2015
“Mwenyekiti aliondoka Dar Oktoba 2, kuelekea Njombe. Oktoba 3, alinipigia simu asubuhi na kunijulisha kuwa  jana yake walipata ajali maeneo ya Makambako wakati wanakwenda.
“Nilimuuliza alipata matibabu, akajibu kuna viongozi wa Njombe walifika na kumchukua hivyo yuko sawasawa.”

TAARIFA YA AJALI
“Siku hiyo hiyo walifanya kampeni na jioni yake walianza safari ya kurejea Dar. Walipofika Mkoa wa Pwani, saa kumi na moja alfajiri, Mchungaji Mgaya alinipigia simu na kuniambia walikuwa njiani wanarudi Dar, wamepata ajali mbaya sana. Lakini hakuniambia kama mchungaji amefariki dunia.
“Nilianza kufuatilia tukio hilo na kuuliza kama kuna msaada wowote wameupata, akasema mpaka muda huo polisi walikuwa hawajafika. Mimi napenda sana kufungua mitandao ya kijamii, nilipofungua nikakuta picha zilishasambaa kwenye mitandao kitu ambacho nilijiuliza usiku huo huyo mpigapicha alikuwa wapi?”

SHAKA KUBWA YA DP
“Sisi DP, mashaka yetu makubwa ni mazingira mazima ya namna kiongozi huyo alivyofariki dunia. Hata mtoto hawezi kudanganywa kwa namna hiyo. DP ina taasisi ya kufanya uchunguzi iitwayo Liberty International Foundation iliyokuwa ikisimamiwa na marehemu. Ipo kazini kwa sasa ili kubaini ukweli wa kifo cha mwenyekiti na tutaweka wazi kila kitu.”
“Laini pia tunaitaka serikali kufanya uchunguzi na kutoa taarifa hadharani.”

MWENYEKITI KIJIJI AIBUKA NA YAKE
Uwazi pia lilifika aneo la ajali na kujionea kwa macho mazingira yake na kupata maelezo kutoka kwa baadhi ya mashuhuda.
Joshua Mohamed Msigala ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Msolwa, Chalinze, Pwani palipotokea ajali. Yeye anasimulia mambo aliyoelezwa na mmoja wa majeruhi, Mchungaji Patrick Mgaya siku ya tukio.
“Kwanza kabisa waandishi wa habari mmefanya vizuri kufika eneo la tukio na kujionea hali halisi. Nawaeleza hali halisi ilivyokuwa mpaka mimi kufika eneo la ajali.
“Siku hiyo asubuhi ya saa kumi na moja na nusu kama sikosei, nikiwa nyumbani nilipigiwa simu na dereva mmoja wa lori anayenijua. Akasema ameona ajali maeneo yangu lakini hajui kama kuna waliokufa au la!”

MWENYEKITI AWAHI NA BODABODA
“Kusikia hivyo, nilichukua bodaboda ili niwahi. Nilifika ndani ya dakika kama kumi tangu kutokea kwa ajali. Nilikuta mwili wa Mtikila umelala pembeni ya gari huku wengine watatu waliodai walikuwa ndani ya gari wakiwa wamesimama tu.
“Ila kati ya hao watatu, mmoja alijitambulisha kuwa ni Mchungaji Mgaya, yeye wakati nafika alikuwa akiongea kwa simu.”

ALICHOAMBIWA NA MCHUNGAJI
“Nilimuuliza mchungaji ilikuwaje? Akasema wakati wanapata ajali hiyo, marehemu Mtikila na wengine wawili walichomoka ndani ya gari hali iliyosababisha kifo cha Mtikila. Hata hivyo, kwa upande wangu sikuamini kama wote walichomoka kutoka kwenye gari bali mazingira yalionesha walitoka wenyewe.
“Mchungaji alizidi kuniambia kuwa, gari lilipaa juu zaidi ya futi kumi na kugonga mti kisha likapinduka na kulalia paa (kwenye Uwazi siku ya tukio, mchungaji alisema gari lilibiringika).
“Lakini pia siamini, kwani pamoja na kuona alama katika mti sikubali kama zilisababishwa na ajali kwani kama ni hivyo gari lingekuwa limepondeka zaidi juu lilikoangukia tofauti na lilivyokuwa likionekana.”

KILICHOMSHANGAZA ZAIDI MWENYEKITI
Mwenyekiti huyo alizidi kusimulia kushangaa kwake: “Kitu kingine kinachonishangaza ni kwamba, kwa maelezo yao gari liliacha barabara likawa linaendeshwa pembeni kwa umbali wa meta mia moja (urefu wa uwanja wa mpira). Kwa nini dereva asipunguze mwendo ambapo angefanya hivyo gari lisingefika kwenye mti.”
“Kinachoshangaza kingine ni kwamba, hakuna majeraha yaliyoonekana kwa macho kwa walionusurika hata kuonesha kwamba walikatwa na vioo wakati wakirushwa nje kutoka ndani ya gari. Hata viti vya mbele vilikuwa vilevile, havikuharibika na kama majeruhi walirushwa nje walipitia wapi?”

WALIOFIKA AWALI

Mwenyekiti huyo alisema anawashukuru askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wa Kambi ya Kizuka na Sangasanga waliokuwa wakipita ambapo walifika kutoa msaada.
“Baadaye mimi nilifanya mawasiliano na Polisi wa Kituo cha Chalinze (Bagamoyo) ambapo walifika eneo la tukio. Pia polisi wa mkoa nao walifika na saa 12:30 asubuhi majeruhi na mwili wa marehemu walipelekwa Hospitali Teule ya Rufaa Tumbi.”
Naye Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Msolwa, Joseph Hamad kwa upande wake alisema alipokea taarifa saa 3 asubuhi na alipowasiliana na mwenyekiti alimwambia yupo katika eneo la tukio.
Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho waliohojiwa na Uwazi walisema wameshangazwa na ajali hiyo iliyosababisha kifo cha Mchungaji Mtikila na kuitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina.

SIMU YA MTIKILA YAZUA UTATA
Mpaka tunakwenda mitamboni, familia ya Mtikila ilisema, jana ilitarajia kufuatilia simu ya marehemu kwani haijulikani ilipo na pia kujua walipo dereva (George Ponella) na msaidizi wake (Ally Mohamed) ambapo awali, dereva alishikiliwa na jeshi la polisi.

Chanzo: Global Publishers

KIGAUNI KIMEMNOGESHAJE PENNY.


sexy Penny


MH370? Plane wreckage containing 'many skeletons' found in the Philippines

A Plane wreckage containing 'many skeletons' and painted with the Malaysian flag has reportedly been found in the Philippines, prompting speculation it could be missing MH370.

Police confirmed they had received reports of the discovery in thick jungle on the remote island of Sugbai.

Mailonline reports that,an audio technician, Jamil Omar, phoned police in Malaysia to say his aunt, Siti Kayam, had stumbled upon the wreckage while she and others were hunting for birds.

Police commissioner Jalaludin Abdul Rahman, said the woman claimed she climbed into the smashed fuselage and saw skeletons.He said:

'Jamil claimed his aunt had entered the aircraft wreckage, which had many human skeletons and bones.'She also found a Malaysian flag measuring 70 inches long and 35 inches wide.'
Speculation grew that the wreckage could belong to the missing Malaysia Airlines flight that disappeared in March last year with 239 people on board.

Police remain reserved about the report, mindful of confirmation by French authorities that part of an aircraft wing – a flaperon – found on the island of Reunion in the west of the Indian Ocean earlier this year had been confirmed as being from MH370.

ALA KICHAPO, ACHIMBIWA KABURI

Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Juma Rajabu, 23, (pichani) mkazi wa Kijiwe Samli Wilaya ya IIala, Dar nusura auawe baada ya kula kichapo maeneo ya Buguruni Sheli, hali iliyofanya afikishwe na polisi Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam kwa matibabu.


kaburi (3)
Chanzo chetu kilisema kijana huyo alipigwa hadi kupoteza fahamu na wabaya wake waliodai kuwa aliwaibia na baada ya kichapo waliamini kuwa amefariki dunia.
“Vijana wale baada ya kumpiga naye kupoteza fahamu wakajua kuwa wamemuua, hivyo wakamuacha palepale hadi polisi wa doria walipofika na kumchukua,” kilisema chanzo ambacho hata hivyo haikuelezwa alituhumiwa kuiba nini.

kaburi 
Habari zinasema baadhi ya watu wanaomfahamu kijana huyo walifikisha habari nyumbani kwao wakidai kuwa ameuawa na maiti yake ipo Hospitali ya Amana, hivyo maandalizi ya mazishi yakafanyika.
“Jumamosi asubuhi familia yao baada ya kupata taarifa za ‘msiba’ waligawana majukumu, wapo waliokwenda kuchumba kaburi, wapo waliokwenda kununua sanda na upishi wa chakula ulifanyika,”alisema mama mzazi wa  kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Tatu Mohamed  (65).
Bi Tatu alisema  kila aliyepewa  jukumu lake  lilifanya na  waliokwenda Hospitali ya Amana walipofika walimkuta Juma akiwa hai ila akiwa ameumizwa na kushonwa nyuzi kadhaa sehemu mbalimbali za mwili wake.
“Watu waliokwenda Amana walituarifu kwa simu kwamba Juma hajafariki dunia, hivyo shughuli za msiba zikasitishwa mara moja na watu wakatangaziwa na wakatawanyika.
Alipohojiwa na gazeti hili Juma alisema kuwa alipigwa na  na watu asiowajua baada ya kusingiziwa kuwa ni mwizi.

Source: Global Publishers

Monday, October 5, 2015

TASWIRA ZA MSIBA NYUMBANI KWA MTIKILA

Sehemu maalum iliyoaandaliwa kwa ajili ya wageni kuandikisha majina yao.Rafiki wa karibu wa marehemu Mch. Christoppher Mtikila, Anyambilile Mwakatole akizungumza na wanahabari msibani hapo.
Ndugu, jamaa na marafiki wakilia kwa hudhuni msibani.

PICHA NA BONIPHACE NGUMIJE NA GABRIEL NG'OSHA/GPL

TAARIFA YA POLISI KUHUSU KIFO CHA MCHUNGAJI MTIKILA

Christopher-Mtikila
Marehemu Christopher Mtikila enzi za uhai wake.

Mnamo tarehe 04/10/2015 majira ya saa 05:45hrs huko Msolwa Kata ya Bwilingu barabara kuu ya Dar es Salaam – Morogoro, Wilaya ya Ki-Polisi Chalinze, Mkoa wa Pwani. Gari No. T.189 AGM aina ya Toyota Corolla likiendeshwa na George Steven Ponera miaka 31, mkazi wa Mbezi Mwisho Dar es Salaam liliacha barabara kisha kupinduka na kusababisha kifo cha Christopher Mtikila miaka 62, mpangwa, mchungaji wa Kanisa la Assemblies, na mwenyekiti wa Chama cha siasa DP mkazi wa Kinondoni “B” Dar Salaam.
Katika ajali hiyo, watu watatu waliokuwamo ndani ya gari hilo na marehemu Mchungaji Mtikila walijeruhiwa ambao ni Ally Mohamed miaka 42 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam, yeye alipata maumivu shingo, mabegani na kifuani, mwengine ni Patrick Mgaya miaka 37 ambaye ni mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God mkazi wa Mbagala Dar es Salaam ambaye alikuwa na michubuko midogo usoni na kuumia kichwani, pamoja na George Steven miaka 31 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam ambaye alipata michubuko kidogo eneo la mabegani. Majeruhi wote walipatiwa matibabu katika Kituo cha afya Chalinze na badae wawili kati yao katika Hospitali teule ya Tumbi na waliruhusiwa kutokana na hali zao kuendelea vizuri.
Baada ya kutokea kwa hiyo ajali, timu maalum ilifika katika eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji wa ajali hiyo ikiongozwa na Mkuu wa utawala wa Traffic kuu Dar es Salaam SACP J. Kahatano, pamoja na mimi mwenyewe, Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoa wa Pwani na kuwashirikisha wataalamu wa Forensic Makao Makuu ya Polisi ACP Kashindye na Dokta A. Makata.
Uchunguzi wa mwili wa marehemu tayari umefanyika, na taarifa ya Daktari aliyefanya uchunguzi huo katika Hospitali ya Rufaa tumbi Kibaha jana tarehe 04/10/2015 umeonyesha kuwa, kifo cha marehemu kimesababishwa na kuvunjika kwa mbavu nane (8) upande wa kushoto na kuingia kwa damu kwenye mfumo wa hewa na kusababisha kushindwa kupumua.
Kabla ya ajali hiyo kutokea marehemu na wenzake tarehe 02/10/2015 jioni waliondoka Dar es Salaam kwenda Mkoa wa Njombe na kufika tarehe 03/10/2015 alfajiri kwa ajili ya kampeni za Chama chao cha DP. Wakiwa huko walipata ajali kwa kugonga magari mawili yaliyopata ajali na kusababisha uharibifu wa gari lao.
Kulingana na taarifa ya Mkaguzi wa magari ya tarehe 03/10/2015 huko Njombe walishauriwa walitengeneze kwanza kabla ya kulitumia tena.
Tarehe 03/10/2015 saa 21:30hrs waliondoka Njombe kwenda Dar es Salaam na ilipofika saa 05:45hrs katika eneo la Msolwa ndipo wakapata ajali hii.
Uchunguzi uliofanywa kwa kukagua tukio na kuwahoji majeruhi walionusurika (katika eneo hilo hakuna watu wengine walioshuhudia tukio hilo kwa kuwa si eneo la makazi ya watu, ni mbuga). Ajali hii imeonyesha kuwa imesababishwa na sababu zifuatazo:
  1. Mwendo kasi, dereva mwenyewe anakubali kwamba alikuwa mwendo kasi licha ya kuwepo kwa alama zinazooonyesha kwenda mwendo wa Km 50 kwa saa. Aidha baada ya kuacha barabara kuu, gari hilo lilikwenda umbali wa mita 125 kabla ya kupinduka hali inayoashiria kuwa lilikuwa kwenye mwendo kasi.
  2. Uchovu wa dereva kutokana na safari ndefu kwa kuendesha gari mchana na usiku kucha kabla ya kuanza safari walikuwa wakishughulikia matengenezo ya gari hilo ambapo hakupata muda wa kupumzika.
  3. Kutofunga mkanda ya usalama. Katika uchunguzi inaonyesha marehemu hakufunga mkanda kwa kuwa alirushwa nje kupitia kioo cha mbele (wind screen).
  4. Ubovu wa gari. Gari hilo lilipata ajali tarehe 03/10/2015 na moja ya sehemu muhimu iliyoharibika ni mfumo wa usukana (steering system) yawezekana halikupata matengenezo kikamilifu na hivyo kuchangia kutokea kwa ajali hiyo.
Hivyo nitumie fursa hii kuwaomba wananchi kuwafichua maderva wanaokwenda mwendo kasi kupitia namba 08007575 ama 0715 009953 au 0658 376012. Aidha niwatake madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kwa wale watakao kaidi Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani hatutasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengi.

Asanteni kwa kunisikiliza.
Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani
Kamishina Msaidizi Jafari Ibrahim.

Sunday, October 4, 2015

TANZIA: MCHUNGAJI MTIKILA AFARIKI DUNIA




Mch.Christopher Mtikila.

Mwili wa marehemu Mtikila baada ya ajali hiyo.
mtikila

Gari alimokuwa Mtikila wakati wa ajali.
Mwanasiasa mashuhuri nchini na Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party (DP), Mch.Christopher Mtikila amefariki dunia na watu wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Msolwa kilichopo Chalinze mkoani Pwani alfajiri ya leo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema Mtikila amefariki majira ya saa 11:45 alfajiri ya leo katika kijiji cha Msolwa, Chalinze.
Amesema gari alilokuwa amepanda Mtikila lilikuwa linatoka mkoani Morogoro kwenda Dar es Salaam, ndani ya gari hilo kulikuwa na watu wanne ambapo wengine watatu wamejeruhiwa vibaya na kupelekwa katika Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha, Pwani kwa matibabu.

Wednesday, September 2, 2015

MTIKISIKO UKAWA

  Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Serena hoteli jijini Dar

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, amevunja ukimya kwa kueleza kile kilichomsukuma kujiuzulu wadhifa huo, sambamba na kujivua uanachama wa chama hicho. Katika kuvunja kwake ukimya huo, Dk. Slaa aliweka hadharani namna viongozi wenzake ndani ya Chadema, akiwamo mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Profesa Abdallah Safari walivyoyumbisha kusimamia misingi ya namna ya kumpokea Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond, Edward Lowassa.


Wandishi wa habari wakifuatilia kwa karibu tukio hilo.
Mbali na hayo, mengine aliyoweka wazi ni namna Lowassa alivyoratibu mipango yake ya kuhamia Chadema akiwa bado CCM, akifanya hivyo kwa kumtumia Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, Gwajima ndiye “mshenga” wa Lowassa kwa Chadema na kati ya hoja alizozitumia kumshawishi Dk. Slaa kumkubali Lowassa ni kwamba, mwanasiasa huyo aliyeokosa urais CCM, anaungwa mkono na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na ndani ya Kanisa Katoliki, maaskofu 30 kati ya 34, wamehongwa na wamemkubali Lowassa.
Ilivyokuwa na Kama ambavyo wahenga wanasema kimya kingi kina mshindo, ndivyo ilivyokuwa kwa kimya cha Dk. Slaa. Mshindo wa kimya hicho ulianza kujidhihirisha mapema, katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, alikofanyia mkutano huo, ambapo mpaka saa saba mchana idadi kubwa ya waandishi wa habari walikuwa tayari wamefika katika eneo hilo, kushiria kuwa tukio hilo litakuwa na ukubwa wa aina yake.

Dk. Slaa aliyewasili ukumbi wa mkutano saa 8:05 mchana, jana, Jumanne, aliweka bayana uamuzi wake wa kuzungumza na waandishi wa habari, akisema, kwa kuwa ikifika mahali ukweli unatakiwa kusemwa ni lazima usemwe, kutokana na upotoshwaji uliofanywa na watu mbalimbali wakiwamo baadhi ya viongozi wakuu wa Chadema, kwamba alikuwa amepumzishwa (likizo) na viongozi wa chama hicho.

“Nataka nianze na kusema mimi sikuwa likizo, sikupewa na mtu yeyote, niliamua kuachana na siasa Julai 18, 2015 usiku saa tatu, baada ya kuona yanayofanyika ndani ya chama changu sikubaliani nayo,” alisema Dk. Slaa.

Alisema alishiriki katika majadiliano ya kumakribisha Lowassa ndani ya Chadema lakini kwa kuweka misingi ambayo chama kilitakiwa kwanza kuizingatia kabla ya kufikia uamuzi wa kumkaribisha, baada ya kukatwa katika mbio za kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Baada ya tarehe 11 Julai, Lowassa alipokatwa mshenga wa Lowassa, Askofu Josephat Gwajima alinipigia simu kuniambia sasa kule Dodoma mambo yameisha, nikamwambia awasiliane na Mwenyekiti (Mbowe), tukawasiliana na naye baadaye tukakutana naye, nikawaeleza msimamo wangu kwamba ni lazima kusikia mtu ana nini, tukakutana na vijana wake ili tujue ana nini,” alisema na kuongeza; “Nikasema msingi wa kwanza ni lazima atangaze kutoka CCM, akijiondoa aseme anakwenda chama gani, na atumie nafasi hiyo kujisafisha na tuhuma zote zinazomkabili katika nchi hii, kwa sababu Chadema kimeaminika, ukipokea mtu ambaye hajajisafisha unakuwa unapokea na uchafu wake. Hilo halikufanyika mpaka alipopokewa Julai 28. Siwezi kumsafisha mtu ninayekaa naye meza moja.”

Dk. Slaa anasema msingi wa pili aliokipa chama chake kabla ya kumpokea ni kupima kama Lowassa ni rasilimali (asset) au mzigo (liability) kwa chama hicho, kwa kuwa walikuwa wameambiwa kwamba angekuja na viongozi wengi kutoka CCM. “Nikawauliza anakuja na nani, yeye peke yake au na wafuasi, na kama wafuasi ni wa aina gani, vijana wa boda boda wanaoshabikia tu au ni viongozi serious (makini). Nikaambiwa anakuja na wabunge 50, wenyeviti wa CCM mikoa 22 na wenyeviti wa wilaya 88, nikakiri hili litakuwa tetemeko, nikahitaji kupewa majina, Katibu Mkuu makini hawezi kupokea idadi tu, na tulikuwa tunakwenda kwenye uchaguzi wa kura za maoni, ilikuwa lazima nijue nani anagombea wapi, vinginevyo uta – destabilize (utayumbisha) chama,” alisema na kuongeza kwamba; mpaka chama hicho kinampokea Lowassa hakuna hata moja kati ya misingi hiyo iliyotekelezwa.

Kuhusu ushiriki wake katika kikao cha kumpokea Lowassa, alisema aliombwa kuitisha kikao cha Kamati Kuu ya dharura, lakini akaeleza msimamo wake kwamba hajapata jibu la upembuzi kama Lowassa ni mtaji au mzigo.

“Asubuhi ya Julai 27, Mwenyekiti alinipigia simu kunieleza sijaridhika akaomba tukutane asubuhi tuzungumze ili tusije tukatofautiana na Mwenyekiti, kwangu mimi tangu mwaka 2004 sijawahi kutofautiana na mwenyekiti, tulifika pale akiwepo Tundu Lissu, na mshenga wake Gwajima, tukabishana tangu saa 3 asubuhi mpaka saa 9 alasiri, wapo hapa waseme kweli, mimi sikukubaliana nao tangu mwanzo, nawaomba viongozi wangu wawe wanyoofu na wenye hofu ya Mungu,” alisema.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, baadaye walitakiwa kwenda nyumbani kwa Lowassa lakini alikataa akisema hawezi kwenda nyumbani kwa mtu wa CCM katika mazingira ya u-Katibu Mkuu wa Chadema. Aliongeza kwamba baada ya hapo, iliundwa kamati ya watu wachache kumshawishi (Slaa), ambayo ilikaa tangu saa 9 mpaka saa 12 jioni lakini akawapa masharti yale yale.

“Tuliporudi kwenye kikao taarifa ya kikao kile haikutolewa. Nikaandika barua ya kujiuzulu nikampa Makamu Mwenyekiti Profesa Safari akaichana, nikaandika nyingine nikampa Makamu Mwenyekiti Zanzibar, akaniambia Dokta usihangaike mambo haya yamepangwa,” alisema.

Akizungumzia watu waliokuja Chadema, alisema wote wamekuja wakiwa makapi baada ya kuwa wameshindwa kwanza kwenye mchakato wa awali wa CCM (kura za maoni) na hata huko walikotoka si wasafi. “Watu kama Sumaye hawakuwa safi, mimi mwenyewe nilimwita fisadi bungeni, alichukua Shamba la Magereza Kibaigwa, na yeye mwenyewe alifikia hatua ya kusema CCM wakimteua Lowassa yeye atahama chama, sasa yuko naye, najua dhambi haihalalishiwi na dhambi nyingine, lakini maneno hayo yalitamkwa na nani, Watanzania walimwita Sumaye ziro,” alisema.

Aliendelea kuwaponda wana CCM waliohamia kuwa ni kama makapi ambao hawataongeza thamani yoyote kwa chama hicho akiwataja Mgana Msindai na Matson Chizii kuwa ni sehemu ya makapi ambayo hayataongeza thamani yoyote kwa Chadema. “Kuna watu wanasema ondoa CCM kwanza hata ikiwezekana kuweka mkataba na shetani, mimi ni Padri Mkatoliki, hata kama nimestaafu, nikubali kuweka mkataba na shetani mradi tu niondoe CCM. Unaondoa CCM kwa program serious na watu makini au unaondoa na watu wale wale?” alihoja Dk. Slaa.

Chadema na tuhuma za ufisadi Mbali na kuhoji endapo waliohamia Chadema kutoka CCM wameongeza thamani yoyote kisiasa; Dk. Slaa aliyesimama imara akizungumza kwa saa 1.32 alisema; “Chadema iliaminika miongoni mwa Watanzania kwa kutoyumbishwa na kusimamia uadilifu. Sasa leo Chadema wanathubutu kusema etu usimtuhumu mtu? Upuuzi mtupu! Kama tusingemtuhumu Mramba (Waziri wa Fedha wa zamani, Basil Mramba) leo angekuwa Segerea?

“Kama tusingemtuhumu Yona (Waziri wa Viwanda wa Nishati na Madini, Daniel Yona) leo angekuwa Segerea? Ni lazima tuhuma zitolewe ndipo serikali iwajibike. Kwa kawaida binadamu lazima kwanza awe na ‘reasonable doubt’ sio ‘absolute doubt’,” alisema Dk. Slaa. Alinukuu kifungu kimoja cha Biblia kinachosisitiza kuwa ni makosa na dhambi kupotosha watu huku akiitupia lawama Serikali ya CCM kwa kumlea Lowassa kwa miaka mingi bila kumshughulikia akisema: “CCM ni waoga na ndio maana wamlea mtu huyu na leo wanatuletea matatizo.”

Dk. Slaa ambaye alisema hajawahi kutofautiana na Mwenyekiti wa Chadema, Mbowe, vikaoni tangu mwaka 2004, aliwashangaa viongozi wa Chadema kwa majaribio yao ya kuwapotosha Watanzania kwa kutaka waamini kuwa kwa Lowassa na watu wake kuhamia Chadema, wamekuwa watu wasafi.

“Ni kama vile choo; kwetu Watanzania choo ni sehemu chafu ingawa kwa wenzetu ukiingia chooni unakuta kuna glasi ya ‘wine’. Samahani kwa mfano huo lakini sina mfano mwingine. Sasa leo mtu aende chooni achote kile kilichomo ndani ya choo na kukihamishia chumani anakolala, utasemaje? Ni kwamba choo kimehamia chumbani. “Na kwa kuwa ili aweze kuchota kinyesi kilichomo chooni atalazimika kwanza kukikoroga, basi kile kilichomo chumbani kitakuwa kinanuka zaidi ya hata choo chenyewe,” alisema Dk. Slaa.

Suala la kashfa ya Richmond

Kuhusu kashfa ya kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond, kashfa ambayo aghalabu Lowassa na wapambe wake hawapendi kuisikia hata kidogo, Mbunge huyo wa zamani wa Karatu alisema yeye na wabunge wengine wa Bunge la Tisa wanalifahamu zaidi kwa kuwa waliiishi kashfa hiyo.

Dk. Slaa aliwatupia lawama wabunge wa CCM kwa kutopenda kusoma nyaraka mbalimbali huku pia akiwalaumu waandishi wa habari kwa kutokufanya utafiti na kuandika habari za kina.

“Hebu mwambieni Lowassa aache kulalamika. Ajitokeza hadharani na kusema Richmond ni ya nani? Amtaje hadharani huyo mkubwa anayedai kuwa alimzuia kuvunja mkataba, ni nani. Juu ya Waziri Mkuu kuna Makamu wa Rais na Rais, sasa ni nani kati ya hao, 
“Juzi juzi hata leo walikuwa wakinitisha eti nisizungumzie masuala haya wakidai kuwa nitapotea kisiasa; nini kupotea kisiasa, niko tayari kupotea katika siasa za Tanzania hata nipotee kabisa duniani kuliko kuikana dhamira yangu.

“Msingi wa Richmond ukitaka kuujua ni ripoti ya Kamati ya Mwakyembe (Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge, Dk. Harrison Mwakyembe),” alisema Dk. Slaa Alisema kamati hiyo iliomba ridhaa ya Rais iweze kupitia nyaraka za Baraza la Mawaziri na kufahamu kwamba katika Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichoketi Februari 2, 2006 (takriban mwezi mmoja na nusu tangu Lowassa ateuliwe kuwa Waziri Mkuu), kilitoa mapendekezo ya namna ya kushughulikia kwa dharuala tatizo la umeme lililokuwa limeikumba Tanzania.

Alisema suala hilo lilianzia tangu wakati wa Rais Benjamin Mkapa ambapo Baraza la Mawaziri lilielekeza namna ya kulitatua, kisha suala hilo likarithishwa kwa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 112 cha Katiba, Waziri Mkuu ndiye mwenye nguvu katika utendaji wa serikali na baada ya kikao cha Februari 2, 2006, saaa 10 jioni ya siku hiyo hiyo, Ibrahim Msabaha (aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati huo), akafuta mchakato ulioanzia kwenye Serikali ya Mkapa na kubarikiwa na Baraza la Mawaziri.

“Tujiulize Msabaha alipata wapi nguvu ya kufanya hivyo kama si kwa bosi wake (Waziri Mkuu)? Mimi mwenyewe, Februari 5 au 6 mwaka 2008 wakati wa kashfa ya Richmond, nililetewa rushwa hotelini kwangu saa 12 asubuhi. Lowassa alijiuzulu uwaziri mkuu Februari 8, 2008.

“Nililetewa Sh. milioni 500 ili ripoti isipitishwe. Nikamuuliza aliyeniletea, kama mimi unanipa Sh. milioni 500, wewe una shilingi ngapi?” alisema huku akihoji Dk. Slaa na kumtaka Lowassa ajitokeze na kueleza jinsi ripoti ile ilivyoibiwa, ingawa hakufafanua zaidi akisema hizo ‘ni silaha za akiba’. Alisema amewahi kuwaambia wote wawili, Lowassa na Sumaye kwamba rushwa huanzia kichwani, moyoni kabla ya kutolewa mikononi na kwamba katika sakata la Richmond, Lowassa aliingilia mchakato kwa kumtumia msaidizi wake binafsi kupeleka maelekezo kwa Msabaha.


“Leo anasema mwenye ushahidi apeleke mahakamani la sivyo afunge mdomo wake; mimi ninasema Lowassa anatafuta urais wa nchi hii nafasi ambayo hawezi kupewa mtu mwongo; mwongo hakubaliki kuwa Rais,” alisema.
Dk. Slaa alikumbushia pia ufisadi wa Kampuni ya Meremeta iliyodaiwa kuwa ni mali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kabla wajanja ‘hawajaidaka’ na kuitumia kuibia fedha za umma akisema Lowassa alimuonya akimwambia nyaraka anazoziandika na kuziwasilisha bungeni zinaiaibisha serikali.

“Nikamjibu, nikasema hapana. Tuwatafute kwanza wanaoiba Meremeta hapo itatusaidia hata kufahamu nani alisababisha mradi wa magari wa Nyumbu ukafilisika. “Baadaye akaniita kule Speaker’s Lounge bungeni, tukawa wawili, akaja na mtu mwingine ambaye leo sitamtaja, wakaanza kunitishatisha na nikawaona na wale vijana wao, nikaogopa. Nikawaambia nyie ni mafisadi vichwani, moyoni na ndani ya nafsi zenu. “Baada ya hapo nikafungua mlango nikakimbia kuokoa maisha yangu. Nani anaweza kumwambia Lowassa wewe ni fisadi? Ni watu wachache sana wenye ujasiri huo lakini mimi nilimwambia,” alisema.

Dk. Slaa aliwashangaa wananchi wanaoshabikia ujio wa Lowassa kutaka urais kupitia Chadema akidai kuwa atawasaidia kutatua shida mbalimbali, akisema: “Nendeni Monduli (Jimbo la Lowassa), hakuna maji kule! Sasa atawaletea vipi maji Watanzania wote? Nendeni Karatu (Jimbo ambalo Slaa alikuwa Mbunge kwa miaka 15) mfananishe na Monduli .“Watu wa Karatu watakwambia ukweli kuwa akiwa Waziri Mkuu, alibadili hata mpaka wa Monduli na Karatu na hadi leo kuna ugomvi. Mtu kama huyo atawezaji kutatua matatizo ya wakulima na wafugaji kama yeye mwenyewe ni chanzo?”

Dk. Slaa pia liponda ujenzi wa shule za kata ambao wapambe wa Lowassa huutumia kama kete ya mafanikio yake kiuendaji, akisema mpango huo ulibuniwa mwaka 1990 nchini Thailand naye akiwa ni mmoja wa wajumbe walioshiriki wakati huo ukiitwa Education For All (EFA). Urafiki wa Lowassa na Lawrence Masha Kuhusu uhusiano uliopo kati ya Lowassa na aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, ambaye naye kwa sasa yupo Chadema, Dk. Slaa alisema ulianzia wakati wa mchakato wa kuhalalisha zabuni ya Richmond.

Alisema Lowassa, Msabaha na Masha walishiriki kikamilifu kusimamia mchakato uliorudiwa zaidi ya mara tatu kuiwezesha Richmond kupata zabuni ya kufua umeme wa dharura nchini kinyume cha sheria ya ununuzi. Alisema kampuni nane zilizoomba zabuni hiyo zote hazikuwa na sifa lakini wakubwa hao wakalazimisha Richmond kupewa mkataba ndani ya siku 10 badala ya siku 45, kwa mujibu wa sheria na kwamba uetetezi wa Lowassa kwamba alichukua hatua, si kweli na mtu mwongo hafai kuwa Rais.

Alisema hata baada ya kashfa ya Richmond kujulikana, Lowassa na Rostam Aziz walishinikiza kampuni hiyo irithiwe na Dowans, kampuni nyingine feki kutoka Costa Rica. “Kamati ya Mwakyembe ilipotaka kuifahamu Dowans ya Costa Rica, iliambiwa kuwa Mkurugenzi wake aitwaye Zamora aliisajiri siku moja pamoja na kampuni zake nyingine 99 huku pia akiwa ni mwenyekiti wa kampuni nyingine 52 tofauti. “Hadi leo Dowans wanalipwa Sh. milioni 153 kila siku. Lowassa aje kutuambia ni nani anayepokea fedha hizo. Ninafahamu kuwa hata fedha za kampeni sasa zinatolewa na Rostam Azizi, mtu aliyewahi kunipigia simu akiniambia; ‘dokta, omba Mungu ndani ya dakika tano hautakuwapo duniani’.

“Lowassa aje atuambie kwa nini Scotland Yard wanamtafuta kwa utoroshaji wa Pauni milioni 400. Mtu huyu leo anataka kuwa Rais! Haikubaliki na niseme wazi kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote lakini ni Mtanzania na nitapiga kelele watu hawa wajulikane.

“Lowassa aje hadharani aseme ana hisa kiasi gani kwenye kampuni mbalimbali nchini ambazo hakuziandikisha kwenye Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,” alisema. Alihoji uadilifu wa Sumaye aliyepora eneo la ujenzi wa Makao Makuu ya Wilaya ya Mvomero huko Morogoro na kuihodhi ardhi ambayo hadi leo haitumiki na sasa makao hayo makuu yamejengwa pembebi ya Barabara ya Dodoma – Morogoro.

Ahitimisha hoja zake

Katika kuhitimisha hotuba yake hiyo ya saa moja na nusu, Dk. Slaa aliwasihi vijana aliowaimarisha ndani ya Chadema kutopiga kura kwa ushabiki bali watafakari na kufanya uamuzi sahihi huku akiponda hoja za kufunguliwa kwa babu Seya na watuhumiwa wa ugaidi Zanzibar, akisema si za msingi kwa Watanzania wa sasa.
“Nilisema tangu awali kuwa nimestaafu siasa. Kwa sasa sina chama, bali nina nchi. Nimeombwa na vyama vitano tofauti nijiunge nigombee uraisa, lakini nikasema hapana, tatizo la Watanzania si urais wa Dk. Slaa; ni uadilifu wa viongozi.

“Ndio maana nitaendelea kupiga kelele nje ya vyama vya siasa kwa kuwa kuna viongozi ambao si waadilifu wanataka kuchukua taifa letu. Kwa mfano mshenda wa Lowassa (Askofu Gwajima) alikuja kwangu, akaniambia ninapaswa kumuunga mkono Lowassa kwa sababu anaungwa mkono na wengi. “Nikamuuliza akina nani hao? Akanijibu kuwa kuna fedha kutoka kwa Rostam Aziz, anaungwa mkono na KKKT na kwamba kati ya maaskofu 34 wa Katoliki, 30 wamehongwa!

“Nikamwambia akili yake imepumbazwa. Nikawasikitikia maaskofu wangu kwamba kama ni kweli wamehongwa, basi taifa letu linaangamia. Mshenga (Gwajima) akaniambia kuna askofu alitaka gari zuri la kiaaskofu, ndani ya dakika 20, akapewa. “Nikajiuliza hawa watu wanatoa wapi fedha? Inamaana hata hawaziweke benki kwa sababu huwezi ndani ya dakika 20 ukanunua gari la Sh. milioni 60,” alimaliza Dk. Slaa hotuba hiyo huku akisisitiza kuwa zipo silaha nyingine za akiba atazitumia mara baada ya Lowassa na Sumaye kujibu hoja hizo.

Dk. Slaa alisema huenda maneno yake yakaonekana kuegemea upande fulani kwa sasa, lakini hiyo ni kutokana na ukweli kuwa ukweli lazima utakuwa upande tofauti na uongo.
chanzo: global publishers

Saturday, August 22, 2015

Sumaye aitikisa CCM, aungana na Lowassa UKAWA

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu maamuzi yake ya kujiondoa uanachama wa CCM.Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu maamuzi yake ya kujiondoa uanachama wa CCM.

Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye leo Ametangaza rasmi kujivua uanachama wake ndani ya Chama cha Mapinduzi na kuhamia umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA bila kutaja  ni chama gani rasmi atakachojiunga.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es  Salaam jioni ya leo Sumaye amesema kwamba  ametoka CCM ili kukijenga chama Mapinduzi  na kuufanya upinzani kuwa na nguvu zaidi kwa kuwa ndani ya CCM amekuwa ni kama sisimizi.
“Haikuwa kazi rahisi kufanya uamuzi wa kujiunga na UKAWA,nilipata kazi sana kutoka katika familia yangu  akiwemo mke wangu”Amesema Sumaye
Amesema  mara baada ya kuingia  mfumo wa vyama vingi  Siasa imekuwa ikitawala   kila kitu hivyo mtumishi wa  serikali anatakiwa ajinyenyekeze kwa mwanasiasa ili kulinda usalama wake kazini suala ambalo ni kosa kubwa .
“Ni ndoto kuamini  mkuu wa Wilaya  atashughulikia  kazi za kisiasa kwa  kufuata haki labda  aamue kujilipua na kuweka kibarua chake hatarini”Amesema  Sumaye.
Sumaye amezungumzia pia mchakato wa kumpata rais ndani ya CCM ambapo amedai mwenyekiti wa chama hicho aliingia na majina yake mfukoni  hivyo yeye pamoja na watia nia wengine38 kukatwa katika mchakato huo.
Amesema alichukua fomu ya urais ndani ya CCM ili kujenga sura mbili ambazo ni Sura ya Utawala na Kujenga  Chama Mbadala kwa CCM. Ametolea mfano nchi ya Marekani ina vyama viwili ambavyo  vimeaminika kwa wananchi na rais lazima atokane na vyama hivyo ambavyo ni Democratic na Republican
Nchi nyingine ni Uingereza ambayo pia ni lazima Kiongozi atoke katika vyama hivyo ambavyo ni Conservative na Labour.
Amesema umuhimu wa kuwa na  chama Kingine kikubwa ni kuwa  lazima wananchi wakichoke chama kilichokuwa madarakani hata kama kiwe kinafanya vizuri hivyo umuhimu wa kuwa na chama cha Pili ni wananchi kuwa na chaguo la Pili wakikichoka chama tawala hivyo kuwa na chama mbadala.
Katika hatua nyingine amesema kwamba hatoki CCM kwa sababu eti hakuchaguliwa kugombea urais anatoka CCM ili kukiimarisha chama hicho  kwa kufanya upinzani kuwa mkali zaidi. Amesema kuwa atamsaidia Lowassa na ukawa katika safari yake ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Chama cha Mapinduzi kimekumbwa na mpasuko wa wanachama wake kukihama na kutimkia Upinzani kwa madai mbalimbali ikiwemo kutoridhishwa na mchakato wa kura za maoni kwa kuwa baadhi ya makada wamepita kwa rushwa   pamoja na umaarufu.

Kumekuchaa!

CCM

NI kweli kumekucha! Kipyenga cha kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu 2015 kimepulizwa. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema leo ndiyo siku ambayo wagombea udiwani, ubunge na urais wa vyama vyote wanaruhusiwa kuanza kujinadi kwa wapigakura, Risasi Jumamosi lina kila kitu.
Jiji la Dar es Salaam ambalo linaaminika kuwa na wapiga kura wengi kuliko majiji mengine manne nchini kote (Arusha, Mwanza, Tanga na Mbeya), hali ni ya msisimko tangu juzi (Ijumaa) ambapo baadhi ya barabara zilianza kuwekwa sawa kwa ajili ya kuruhusu wagombea kupita na magari yao kwenda kwenye viwanja vya kampeni.
lowassa 
CCM, UKAWA NDIYO GUMZO
Kampeni jijini Dar zinazotazamwa kwa macho makubwa ni mbili. Ya Chama Cha Mapinduzi (CCM, mgombea wake John Magufuli) ambayo itasimamisha jiji kesho kwenye Viwanja vya Jangwani vilivyopo wilayani Ilala na ile ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema, mgombea wake Edward Lowassa) chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) zitakazofanyika Agosti 29, 2015 huku vyama vingine navyo vikianza leo nchini kote.

BARABARA YA MOROGORO
Mhandisi mmoja wa Halmashauri ya Jiji la Dar ambaye alisema yeye si msemaji mkuu, alilidokeza gazeti hili kwamba, upande mmoja wa Barabara ya Morogoro (kutokea Kariakoo kwenda Mbezi) utakula kitanzi kuanzia mchana wa kesho ili kuwezesha magari ya msafara wa wana CCM, mgombea wake, John Magufuli na wapambe kuweza kuingia kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya kuzindua kampeni ambayo rais anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete ‘JK’ atakuwepo.

WASIO NA KAZI MUHIMU MJINI
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar ambao kesho watakuwa hawana kazi za muhimu mjini, wametakiwa kujituliza majumbani mwao ili kukwepa usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na usafiri wa umma kuingiliwa na misafara ya kampeni, hususan kwa Barabara ya Morogoro.
Akitoa maelekezo kwa wakazi wa Jiji la Dar alipozungumza na wanahabari ofisini kwake, Ilala juzi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik alisema Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleimani Kova ataweka mambo yote hadharani.

KAMANDA KOVA
Kwa mujibu wa Kamanda Kova, ni vyema wananchi wakatambua kuwa polisi wamejipanga kuhakikisha ulinzi unakuwepo kwa asilimia mia moja.
“Polisi haitamuonea mtu. Ila nawaomba wale wanaotaka kutumia wingi wa watu na misafara kufanya uhalifu waachane na mawazo hayo kwani jeshi la polisi lipo macho saa ishirini na nne.”
Aidha, Kamanda Kova alipiga marufuku tabia za baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar kuwazomea wanachama waliovaa mavazi yenye utambulisho wa vyama vyao.

CCM WATAMBA NA ‘HAPA NI KAZI TU’
Tayari wana-CCM wamekuwa wakiutumia msemo wa mgombea wao kwamba atafanya kazi kwa kiwango cha juu ‘hapa ni kazi tu’ kujifagilia kwamba, ushindi ni wao wakimpamba mgombea huyo kuibuka na ushindi wa kishindo.

UKAWA WAO NI ‘SAFARI YA MABADILIKO’
Wakati CCM, wakitamba na msemo wao huo uliojipatia umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii na mitaani, Ukawa wao wanasimamia ‘slogani’ ya Safari ya Mabadiliko ambayo mgombea wake, Edward Lowassa amekuwa akiitumia tangu alipojiunga na umoja huo Julai, mwaka huu.

NI KAMA SIMBA NA YANGA
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar, walipozungumza na gazeti hili kuhusu kuanza kwa kampeni nchi nzima leo, walisema ni kama refa amepuliza kipyenga tayari kuanza kwa mpira wa fainali ya timu kubwa mbili za Simba na Yanga.

Wednesday, August 19, 2015

OSCAR PISTORIUS KUACHIWA IJUMAA

Mwanariadha Oscar Pistorius.

AP_oscar_pistorius_reeva_steenkamp_jt_140302_16x9_992
Oscar Pistorius akiwa na mpenzi wake Reeva Steenkamp.

oscar-pistorius-800Oscar Pistorius akiwa mahakamani wakati wa kesi yake.

Mwanariadha mahiri wa nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius anatarajiwa kuachiwa Ijumaa hii baada ya kuonyesha tabia nzuri akiwa gerezani. Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani mwaka uliopita kwa kosa la kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp katika usiku wa Siku ya Wapendanao 'Valentine's Day'.
 oscar Pistorius ametumikia kifungo cha miezi 10 pekee gerezani kati ya miaka mitano aliyohukumiwa. Baada ya kuachiwa, Pistorius anatarajiwa kuwa akitumikia muda wake uliobaki akiwa katika kifungo cha nje.
Wakati akitoa hukumu ya staa huyo, Jaji Thokozile Masipa alisema kuwa kiongozi wa mashtaka nchini Afrika Kusini alishindwa kuthibitisha kuwa Pistorius alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp alipompiga risasi nyumbani kwake akidhani kuwa ni mwizi.

Meninah aolewa kimyakimya

Nyota wa muziki wa kizazi kipya, zao la BSS 2012 Meninah Abdulkarim.


WENYE wivu wajinyonge! Nyota wa muziki wa kizazi kipya, zao la BSS 2012 Meninah Abdulkarim, anadaiwa kufunga ndoa kimyakimya mwishoni mwa wiki iliyopita na mtu anayetajwa kulelewa tangu utotoni na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini aliyejiuzulu, Profesa Sospeter Muhongo, Risasi Mchanganyiko limetonywa.
Chanzo chetu makini kimearifu kuwa shughuli hiyo ilifanyika Agosti 16 mwaka huu ikimaliziwa na sherehe kubwa iliyofanywa nyumbani kwao, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Meninah-Copy“Ebwana Meninah kaolewa na jamaa mmoja ambaye tumeambiwa ni mtoto wa Muhongo, ambaye alikuwa naye kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu sasa, ndoa hiyo ilikuwa ya siri maana sisi hatukujua kabisa, ila nilikuwa naenda zangu mjini mara nikakutana na magari ya harusi ndiyo nikajumuika na mimi kula ubwabwa,” kilisema chanzo chetu ambacho kilishuhudia shughuli nzima.
Inadaiwa kuwa bwana harusi amelelewa kwa muda mwingi wa maisha yake na Profesa Muhongo kiasi kwamba watu wa karibu na familia hiyo walifahamu ni mtoto wake wa kumzaa. Hata hivyo, haikuweza kujulikana mara moja uhusiano baina ya Profesa na bwana harusi huyo, anayedaiwa kuwa ni mfanyabiashara mzuri hapa nchini.
Gazeti hili liliwasiliana na kaka yake Meninah ambaye pia ni meneja wake, Atik Abdulkarim ambaye alikiri dada yake kufunga ndoa, lakini akashangaza baada ya kudai hafahamu jina la shemeji yake, ingawa alisema ni kweli mume ni mtu aliyelelewa na Profesa Muhongo.
“Ni kweli Meninah kaolewa jana (Jumapili), ila jina la bwana harusi mimi silijui maana nimezoea kumuita shemeji tu,” alisema Atik.

Chanzo: Global Publishers

Tuesday, August 18, 2015

Urais ACT – Wazalendo sarakasi tupu

 Ofisa Mwandamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi 
Ofisa Mwandamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), George Kashura (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo, Samson Mwigamba fomu za uteuzi wa mgombea urais na makamu wa rais kwa niaba ya wagombea wa nafasi hizo kupitia chama hicho, Dar es Salaam jana.

Sintofahamu imetanda ndani ya Chama cha ACT – Wazalendo juu ya hatima ya mgombea wa urais baada ya mgombea aliyependekezwa na kuchukuliwa fomu ya kuomba uteuzi, Profesa Kitila Mkumbo kuikataa nafasi hiyo.
Mapema jana saa 4.30 asubuhi, Katibu Mkuu wa chama hicho, Samson Mwigamba alitinga katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua fomu bila ya kuwa na Profesa Kitila na kueleza kuwa mgombea wao huyo yupo safarini.
Mwigamba alisema alikwenda kuchukua fomu hiyo kwa niaba ya chama na bila kusindikizwa na viongozi wengine kwa kuwa walikuwa kwenye vikao vya ndani vilivyokuwa vikiendelea.
Muda mfupi baada ya Mwigamba kuchukua fomu hizo, Profesa Mkumbo aliandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa anawashukuru makada na Kamati Kuu ya chama hicho kumwamini na kumtaka agombee urais lakini kwa sasa hayupo tayari.
Katika ujumbe huo ambao baadaye alikiri kuuandika, Profesa Mkumbo alisema Kamati Kuu ilituma ujumbe maalumu nyumbani kwake juzi kuzungumza na familia na jamaa zake juu ya ombi hilo na kubainisha kuwa amekuwa akitafakari uwezekano wa kugombea nafasi hiyo baada ya juhudi za kutafuta mgombea kushindikana.
“Nimefanya mawasiliano mapana katika familia, ndani ya chama, chuoni ninapofanyia kazi, kanisani kwangu na kwa watu na taasisi mbalimbali ninazohusiana nazo.
“Baada ya tafakari na mawasiliano mapana, nasikitika kusema kwamba sina utayari na maandalizi ya maana ya kisaikolojia, kifamilia na kisiasa kuniwezesha kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi huu,” alisema Profesa Mkumbo.
Alisema anajua bayana amewaangusha lakini anaamini kwamba wafuasi hao wataheshimu uamuzi wake, hivyo hawataacha kuthamini mchango alioutoa katika chama hicho kwa sababu amekataa kugombea urais.
Alishauri chama kiwaombe wanachama wengine waandamizi kuchukua jukumu hilo, akiwamo Mwenyekiti, Anna Mghwira, huku akiwataka makada wa ACT –Wazalendo kutomtuhumu kwa lolote juu ya uamuzi wake.
Kukataa kwa Profesa Mkumbo kunakipa kazi chama hicho kutafuta mbadala wa mgombea huyo ambaye ni moja ya waasisi wa chama hicho chenye makao yake makuu, Kijitonyama jijini hapa.
Hata hivyo, Mwigamba alipoulizwa mbadala baada ya mgombea waliyemchukulia fomu kukataa, alisema hawadhani kuwa Profesa Mkumbo atakataa na ikitokea hivyo watamtafuta kada mwingine agombee.
“Mwigamba alisema mgombea mwenza aliyetarajiwa ni kada wa muda mrefu wa ACT – Wazalendo aitwaye Hawra Shamte.
Alipotakiwa kueleza kwa kina iwapo jina la mgombea mwenza huyo ni linahusiana na Mhariri wa gazeti hili, Hawra Shamte, Mwigamba alisema: “Siyo huyo na kiufupi yeye (mgombe mwenza) na mgombea urais tutawatangaza baada ya kikao cha dharura cha Kamati ya Uongozi kukamilika leo (jana) au kesho (leo).”
Shamte alipoulizwa kuhusu mpango huo, alisema hajui jambo hilo na kwamba jina hilo huenda halihusiani naye kwa kuwa yeye si mwanachama wa chama chochote.
Makada wavamia ACT
Baada ya taarifa ya Profesa Mkumbo kukataa kuzagaa, makada zaidi ya 200 wa ACT – Wazalendo walitinga katika ofisi cha chama hicho wakiwa katika maandamano wakishinikiza agombee.
Maandamano hayo yalianzia jirani na Ofisi ya Tume ya Sayansi na Teknolojia Kijitonyama, wilayani Kinondoni hadi katika ofisi za chama hicho zilizopo umbali wa kilomita moja.
Waandamanaji hao wakiwa na bendera za chama hicho walifika katika ofisi za chama hicho saa 6.10 mchana na kutishia kuvunja mlango wa ofisi lakini walizuiwa na wenzao waliokuwa ofisini.
Baada ya azma hiyo kushindwa, waliendelea kuimba nyimbo mbalimbali za kumshinikiza Profesa Mkumbo kuwania urais huku wakiwa na mabango yenye ujumbe wa aina mbalimbali ukiwamo “…Bora ofisi ifungwe kama hatuwezi kusimamisha mgombea urais.”
Wengi wa waandamanaji hao ambao ni vijana kati ya miaka 20 na 30 waliendelea kuimba: “Zitto na Kitila turudishieni chama chetu kama mmeshindwa kuweka mgombea urais. Kitila Mkumbo tumia busara na hekima wewe ni rais 2015.”
Katika hali ya kushangaza, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Shaaban Mambo aliingia katika ofisi hizo saa 6.30 mchana na kupokewa kwa shangwe na vijana ambao waliimba huku wakisema, “karibu Profesa Kitila, Kitila, Kitila.”
Baada ya Mambo kuingia ndani, ndipo baadhi ya vijana wakaanza kuwaeleza wenzao kuwa yule hakuwa Profesa Kitila.
Baadaye ofisi za chama hicho ziligeuka ‘uwanja wa vita’ kwa vijana hao baada ya kuanza kugombania maji na biskuti zilizokuwa zikitolewa katika ofisi hiyo.
Mmoja wa wafuasi wa chama hicho aliyekuwa akigawa vinywaji hivyo alishindwa kuhimili vurugu za vijana hao na kuamua kuwarushia juu chupa za maji na biskuti.

Majimbo Ukawa hadharani, 12 bado moto

Wananchi wa Unguja wakimshangilia mgombea urais Wananchi wa Unguja wakimshangilia mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara yuliofanyika katika Uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti, Zanzibar jana.

Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimetangaza mgawanyo wa majimbo 253 kati ya 265 ya ubunge huku 12 yaliyokuwa kwenye mvutano yakibaki kiporo.
Katika mgawanyo huo uliotangazwa kwa wanahabari jana, Chadema kimepata majimbo 138, sawa na asilimia 73 ya majimbo yote huku CUF ikichukua 99, NCCR – Mageuzi 14 na NLD matatu.
Hiyo ni pamoja na kujumlisha majimbo 51 ya Zanzibar ambayo yote yalikwenda kwa CUF isipokuwa moja lililoachwa kwa Chadema.
Mgawanyo huo ambao umechapishwa katika ukurasa wa 36 wa gazeti hili, umetangazwa wakati mgombea urais wa Ukawa akihutubia mkutano wake wa nne wa kujitambulisha kwa wananchi katika Uwanja wa Demokrasia, Kibandamaiti, Zanzibar; baada ya kufanya hivyo katika mikoa ya Mbeya, Arusha na Mwanza.
Majimbo hayo yalitangazwa na wawakilishi wa makatibu wakuu wa umoja, John Mnyika (Chadema), Nderakindo Kessy (NCCR – Mageuzi), Shaweji Mketo (CUF) na Masudi Makujunga (NLD) waliokutana katika Ofisi za Makao Makuu ya za NCCR – Mageuzi.
Miongoni mwa majimbo ambayo hayajagawanywa ni, Segerea, Kigamboni, Mbarali, Geita Vijijini, Gairo, Mtwara, Mpwapwa na Geita Mjini, Mwanga na Serengeti ambalo Katibu Mkuu wa NCCR – Mageuzi, Mosena Nyambabe jana alichukua fomu kuliwania.
Taswira ya mgawanyo
Chadema ambacho katika uchaguzi uliopita kilipata majimbo 24 dhidi ya manne ya NCCR-Mageuzi na mawili ya CUF Bara, kimeachiwa majimbo karibu yote katika mikoa ya Mara, Shinyanga, Geita, Njombe, Rukwa, Arusha, Manyara, Singida, Katavi huku Cuf ikibeba mkoa wote wa Lindi na NCCR-Mageuzi ikibeba ngome ya Kigoma.
Katika mgawanyo huo, NLD ambayo haikuwa na jimbo hata moja imeachiwa majimbo matatu tu ya Lulindi, Masasi na Ndanda mkoani Mtwara.
Katika mkutano huo, Kessy alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya majadiliano ya muda mrefu, kuhusu kuachiana majimbo ya ubunge kwa vyama vinavyounda Ukawa.
Mnyika alisema katika uchukuaji wa fomu za Tume ya Uchaguzi, hatatambuliwa mgombea kutoka vyama hivyo, nje ya makubaliano yaliyofikiwa na Ukawa.
Akizungumzia mvutano wa baadhi ya majimbo, mfano Segerea, Mnyika alisema wananchi wanatakiwa kuvuta subira.
Vigezo
Mketo alitaja vigezo sita vilivyotumika katika mgawanyo huo kwa chama husika kuwa ni matokeo ya Uchaguzi wa Serikali Mitaa, matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, kukubalika kwa mgombea, hali ya kisiasa ndani ya jimbo na mtandao wa chama husika.
“Taarifa hii ni rasmi kutoka CUF kwani kila chama kilitoa mapendekezo ya majimbo ndani ya vikao vya Ukawa na yalijadiliwa kupima vigezo hivyo kwa hivyo tunaomba viongozi wote waheshimu uamuzi uliofikiwa,” alisema Mketo.
Agosti 2014, viongozi wakuu wa vyama vinavyounda Ukawa walisaini makubaliano (MoU) ya kusimamisha mgombea mmoja kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge na urais wa Muungano na Rais wa Zanzibar.
Lowassa Zanzibar
Wakati huohuo, mgombea urais kupitia Chadema na Ukawa, Edward Lowassa jana alitambulishwa Zanzibar na kusema umefika wakati wa kuikomboa nchi dhidi ya mfumo kandamizi wa CCM.
Alisema jukumu la awali ni kuiondoa CCM madarakani na kutoa nafasi kwa rais kupitia Ukawa ili kuikwamua Tanzania kimaendeleo.
“Mkituchagua mimi na Maalim Seif (mgombea urais wa Zanzibar) mtaiona Tanzania inakwenda kasi ya ajabu, haijawahi kutokea. Hatuwezi kushindwa na Rwanda! Hatuwezi kuachwa na Malawi! Hatuwezi kushindwa na Kenya na Uganda! Tupeni nafasi tuikwamue nchi yetu kutokana na ufukara na umaskini,” alisema.
Kama ilivyokuwa katika mikoa ya Mbeya, Arusha na Mwanza, Lowassa alionya kuhusu mwenendo aliouita wa hujuma na ubadhirifu wa CCM hasa katika uchaguzi, akisisitiza kuwa hakuna msaada wowote wa kukinusuru chama hicho kikongwe kwa sasa kisiondoke madarakani kwa kuwa muda wake umekwisha.
“Ninawasihi ndugu zangu wale mliobaki CCM njooni haraka muungane nasi kuikomboa nchi hii, wakati ni huu, hakuna namna ya kuzuia wimbi hili la umma katika safari hii ambayo inaelekea katika ushindi wa kihistoria na mwisho wa utawala wa CCM,” aliongeza.
Lowassa aliweka msisitizo juu ya azma ya kusimamia kikamilifu mapendekezo ya Katiba kwa mujibu wa maoni ya wananchi kama yalivyowasilishwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba.
“Hatuhitaji kusimama na batili ambayo haikuwa chaguo wala mapendekezo ya wananchi walio wengi, tutalinda masilahi ya Zanzibar katika Muungano kama nchi kamili yenye heshima yake,” alisema Lowassa.
Alisema iwapo atachaguliwa, Serikali yake itahakikisha haki za masheikh waliopo kizuizini zinapatikana haraka iwezekanavyo.
Mgombea mwenza, Juma Duni Haji alisema upepo mkali wa mabadiliko na nguvu isiyozuilika ya Ukawa dhidi ya CCM ni ujumbe tosha kwamba mwisho wa chama hicho umewadia.
“Someni yaliyojiri Urusi, Ukraine, Misri na kila pembe ya mabadiliko duniani, muangalie ni wapi dola iliposhinda nguvu za umma,” alihoji Duni ambaye hivi karibuni alijivua uanachama wa CUF, alikokuwa Makamu Mwenyekiti na pia kujiuzulu uwaziri katika Baraza la Mawaziri Zanzibar.
Maalim Seif
Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alimtahadharisha Rais Jakaya Kikwete juu ya matumizi mabaya ya vyombo vya dola.
“Ndugu yangu, rafiki yangu kipenzi, Rais Kikwete nakuomba umechukua nchi kwa amani ondoka kwa amani,” alisema huku akilaumu tabia ya watu aliowaita “Janjaweed”, waliodaiwa kumpora Abdi Seif Hamad fomu ya kugombea Ubunge kupitia CUF katika Jimbo la Shaurimoyo jana.
Abdi ni miongoni mwa watu waliohama CCM siku za karibuni na kujiunga CUF kwa matarajio ya kuungwa mkono na Ukawa.
Mamia ya mashabiki jamii wa Kimasai walimiminika katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume kumlaki Lowassa na katika hali ambayo haikuzoeleka, walionekana kupiga saluti wakiwa wamejipanga barabarani wakati msafara wa viongozi wa Ukawa ukipita Barabara ya Kiembe Samaki, Mwanakwerekwe kuelekea Kibandamaiti.
Wamasai hao walimiminika kwa wingi uwanjani hapo na kupata fursa ya kuburudisha umati wa watu kwa wimbo wa Kimasai wenye maana ya ‘tunampenda Lowassa’.
Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema safari ya Ukawa ni ndefu, imepitia majaribu mengi lakini bado umoja huo uko imara hivyo wananchi hawana budi kujitokeza kwa wingi kuunga mkono umoja huo kuelekea ukombozi wa pili wa Tanzania.
“Ndugu zangu tumetoka mbali tutasimama imara kuhakikisha safari yetu inafikia tunakohitaji katika mafanikio na ushindi na hatimaye kushika uongozi wa nchi,” alisema.
James Mbatia
Mwenyekiti wa NCCR, Mageuzi, James Mbatia alisema: “Tumeshawaagiza mawakili wetu kurekodi kila tukio kila udhalimu na kila uonevu, tunamuomba Bensouda (Fatou, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa) kufutilia namna zote za uvunjaji wa haki na ifikapo Novemba tunampeleka yeyote ICC.”
Khamis Mgeja
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja aliwahamasisha Wana-CCM kujiunga na Ukawa na kumpigia kura Lowassa, wakielewa kwamba hatima ya chama hicho kikongwe imewadia.
Wengine wachukua fomu za uraisi
Wakati mkutano wa Ukawa ukiendelea, wagombea wengine wa urais Zanzibar walijitokeza jana katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kuchukua fomu za kugombea nafasi hizo.
Waliojitokeza ni Juma Ali Khatib wa Tadea na Said Soud Said wa Chama cha Wakulima (AFP). Khatib ni Katibu Mkuu wa Tadea na Soud ni mwenyekiti wa AFP.
Imeandikwa na Kelvin Matandiko, Borrice Bwire (Dar) na Hussein Ali (Zanzibar).

Chanzo: Mwananchi