LATEST POSTS

Monday, March 10, 2014

MAMBO SITA USIYOYAFAHAMU KUHUSU NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA

 

 
Kuna mambo ambayo watu hawajafahamishwa kuhusu ndege ya shirika la ndege la Malaysia (Malaysia Airlines) safari namba Flight 370 ambayo imepotea ikiwa eneo la juu ya bahari katika Ghuba ya Thailand na watu 239.
Ndege hiyo aina ya Boeing 777 iliyopotea Jumamosi asubuhi wiki iliyopita na kutoonekana mpaka leo imewababaisha wataalam wengi duniani wa mambo ya usalama wa vyombo vya anga.
Hata hivyo, pamoja na mkanganyiko huo, gazeti la Wall Street Journal limeorodhesha mambo ambayo watu wengi hawayafahamu kuhusiana na kupotea kwa ndege hiyo.
 
Mambo hayo ni yafuatayo:
  1. Ndege zote za Boeing 777 zina kisanduku maalum cha kutunza kumbukumbu za mawasiliano ya marubani wa ndege na waongoza ndege walioko ardhini (black box) ambacho hakiwezi kuharibika katika mlipuko wowote unaoweza kutokea kwenye ndege.
  2. Kijisanduku hicho (black box) kina nguvu za kurusha mawimbi kuonyesha kilipo kwa siku zisizopungua 30 baada ya kuanguka baharini.
Hata hivyo, wataalam wameshindwa kunasa mawimbi ya chombo hicho na hivyo kuwa na wasiwasi kwamba huenda kimeharibiwa na nguvu kubwa isyokuwa ya kawaida.
  1. Sehemu nyingi zilizoharibika za ndege huwa zinaelea juu ya maji baada ya ndege kuanguka baharini au majini.
Katika tukio hili hakuna kilichoonekana, na hivyo kuzua hofu kwamba ndege hiyo huenda imetoweka katika eneo la Dunia.
  1. Iwapo kombora lingeipiga ndege hiyo, basi kombora hilo lingeonekana katika vyombo vya uchunguzi vya kijeshi na vya usalama wa safari za anga. Hii ni pamoja na kwamba huenda imepigwa na kombora na kuikatakata ndege hiyo katika vipande vidogo-vidogo.
Katika nadharia hii, hakuna dalili zozote zilizonaswa na vyombo vya ulinzi na usalama kuonyesha kulikuwa na kombora lililohusika.
  1. Pamoja na eneo ambalo ndege hiyo ilikata mawasiliano na kupotea kufahamika, bado wataalam wameshindwa kujua iko wapi.
Kufahamu eneo la tukio, mwelekeo na kasi ya ndege hiyo, bado hakujasaidia kupatikana kwa ndege hiyo, hivyo kuzidisha hofu inayowachanganya wataalam.
  1. Iwapo Flight 370 ilitekwa, isingeacha kuonekana kwenye vyombo vya kudadisia nyendo za vyombo vya angani (radar).
Nadharia ya kutekwa haina msingi wowote, kwani ndege zinazotekwa huwa hazitoweki katika radar.
 
HITIMISHO: Ndege hiyo ya Boeing 777 haikulipuka angani, bali imetoweka!
 
Kutoka Urambonews.com
Binafsi, katika habari ambazo zimenifanya kichwa changu kuuma kwa kuwaza na kuwazua ni hii. Na nimekua nikiifuatilia ili kujua hatma yake ni nini? Mwanzoni tulikuwa tukihisi kuwa imetekwa lakini wataalamu wanasema kama imetekwa lazima ndege hiyo isingeacha kuonekana kwenye radar. Haya basi labda imeangukia baharini tunaambiwa kuwa ndege ikiangukia baharini Sehemu nyingi zilizoharibika za ndege huwa zinaelea juu ya maji baada ya ndege kuanguka baharini au majini. Lakini hadi leo hii Katika tukio hili hakuna kilichoonekana baharini na hivyo kuzua hofu kwamba ndege hiyo huenda imetoweka katika eneo la Dunia.
 
Sasa hapa ndipo mimi najiuliza maswali, enheeee! kwamba huenda ndege hiyo imetoweka katika eneo la dunia, imekwenda wapi sasa? Na je, ni lazima Ndege iangukie baharini? Wataalamu waangalie basi na kwenye maeneo ya misitu minene minene huenda iliangukia huko tusikazanie baharini tu. Ndege imetoweka katika eneo la dunia, Mmh!Mungu mwenyewe ndio anayo majibu. Tunamwomba Mungu atuonyeshe iliko ndege hii jamani. Tunakuomba baba, tuonyeshe. Wewe pekee ndio unaweza.
Daah! Pole kwa Nchi husika, Wanandugu na Dunia nzima kwa ujumla maana wote tumeguswa kwa kweli.

0 comments: