LATEST POSTS

Friday, April 17, 2015

Mbinu za Uandishi Bora

Kwa kuwa waandishi wengi wamesoma katika vyuo mbalimbali vya uandishi wa habari, imeonekana  kuwa kuna haja ya kuwa na mwongozo wa uandishi bora na aina za mitindo inayotumika na kukubalika.
Mwongozo huu umejikita katika matumizi fasaha na sanifu ya lugha ya Kiswahili ambayo ndiyo msingi katika uandishi wa habari.
Ifahamike kuwa kila  kampuni  ya uchapishaji wa magazeti au vitabu na kampuni za televisheni na redio huwa na mtindo wao wa kuandika au kutangaza habari ambao ni tofauti kidogo na vyombo vingine katika matumizi ya lugha ya Kiswahili. Hata hivyo ziko mbinu ambazo ni za jumla kwa kila mwandishi ambazo hana budi kuzifuata kama kwa mfano matumizi ya tahajia ya maneno, miundo ya sentensi na mpangilio wa maneno. Tofauti zinazojitokeza ambazo hutumiwa na wachapishaji ama wa magazeti au wa vitabu zinazojulikana kama ‘House style’ ni ndogo na haziwezi kuathiri sana uandishi kwa jumla.
Maelezo yafuatayo yametokana na utafiti pamoja na ushauriano baina ya wataalamu wa lugha.
 Maelezo
Msingi wa maelezo yaliyoandikwa umezingatia miongozo iliyowahi kutolewa na Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita) siku za nyuma kama ilivyoandikwa katika machapisho yao kama kitabu cha “Jifunze Kiswahili Uwafunze Wengine,’ pamoja na ‘Mwongozo wa Uandishi’.
Kwa kuanzia ningependa kufafanua baadhi ya maneno yanayokanganya kiasi fulani wasomaji wengi kutokana na kushindwa kuyapambanua. Sababu kubwa ya mkanganyiko huu ni athari ya lugha za asili katika Kiswahili sanifu pia ni misingi mibovu wa sarufi ya Kiswahili inayosababishwa na walimu wa shule za msingi wasiokuwa na ujuzi wa kutosha katika taaluma katika fani ya Fonolojia, Fonetiki, Mofolojia, Semantiki na Sintaksia. Pia wako wale wanaoathiriwa na lugha za kigeni kama Kiarabu na Kiingereza. Lugha hizi za kigeni kimetufanya tuione lugha ya Kiswahili kama chotara wa lugha nyingine wakati lugha hii ina misingi ya lugha ya Kibantu. Nitaanza kufafanua baadhi ya maneno nna vifungu vya maneno kwa utaratibu wa kutumia alfabeti. Kwa mfano:
     A
Ajali/ajari:
Ajali ni tukio lenye madhara yanayotokea ghafla.
Ajari  ni malipo  kwa kazi ya ziada na jina linalofahamika ni ovataimu ambalo limetoholewa kutoka     katika neno la Kiingereza la ‘overtime’.
Aidha/au /ama:
Neno aidha asili yake ni  Kiarabu na tangu likopwe, matumizi yake hayajabadilika. Kuna wakati tunalitumia kama waaidha. Watumiaji wengi wanafuata mtindo wa Kiingereza wa ‘either ... or’. Tunasoma kwa mfano: “Wataalamu  wa Kichina watabaki aidha bara au visiwani. Matumizi sahihi ni “Wataalamu wa Kichina watabaki ama bara au visiwani.
        Maana ya aidha ni tena, basi, zaidi ya hayo, vilevile. Kwa mfano:
Kabla ya kwenda sokoni nitapitia aidha benki kuchukua   fedha. 
Ahirisha/hairisha:
Neno sahihi ni ahirisha.
Kuahirisha maana yake ni kuchelewesha jambo kwa makusudi ili lifanyike baadaye.
Adhima/azma:
Neno adhima si neno sahihi la Kiswahili ila liko neno adhimisha ambalo maana yake ni kufanya sherehe ya kukumbuka kwa tukio fulani kama vile siku ya kuzaliwa, siku ya kufunga ndoa, siku ya kupata uhuru, n.k.
Neno lingine linalofafana na hilo ni adhimu ( kiv) –enye sifa, iliyotukuka, tukufu, jalili.
Azma ni jambo linalokusudiwa kufanywa, makusudio au lengo. Wakati mwingine huandikwa kama azima.
Alimradi/ilimradi:
Haya ni maneno yenye maana moja. Maana yake ni ili, iwapo, kwa masharti kwamba,  mradi.
Aidha:
Maana ya aidha ni vilevile, pamoja na hayo, pia, isitoshe n.k. Kuna wakati tunachanganya aidha na au katika sentensi moja. Hii inatokana na athari ya Kiingereza ya kutumia ‘either … or’... Kwa usahihi inatakiwa iwe ‘ama / au’ tunapotaka kulinganisha mambo.
B
Budi:   
Neno hili likisimama peke yake lina maana ya hiari. Tukisema ,”Wakulima ni budi walime” tuna maana  kuwa wakulima ni hiari walime.Tunatakiwa kusema “Wakulima ni lazima walime au wakulima hawana budi kulima. Kwa usahihi tunasema “Wakulima hawana budi kulima” (yako maneno yanayofanana kimuundo kama sina budi, hatuna budi, hawana budi , huna budi)
Baadaye/baadae :
Neno sahihi ni baadaye
       D
Digiti/Digitali:
Digiti ni nomino na limetoholewa kutoka kwa neno ‘digit’ lenye maana ya tarakimu.  Neno hili ni nomino na ni sahihi. Digitali ni kisifa (adjective). Kwa kawaida tunatohoa nomino na wala siyo kisifa. Hivyo neno sahihi ni ‘digiti”.                          
Durusu/rudufu:
Haya ni maneno yanayochanganywa na yana maana tofauti. Kudurusu ni kupitia tena maandishi  yaliyoandikwa kwa madhumuni ya  kusahihishwa au kuboreshwa  na kutoa toleo jipya. 
Rudufu ni kufanya nakala, kufanya kitu madhubuti k.v kurudufu nyuzi kuwa imara.
Darubuni:
Ni chombo  cha kuonea mbali; kionea mbali yaani ‘Telescope/binoculars’.
Dahili/sajili: Maana ya kudahili ni kutaka kujua habari za watu kwa kuulizauliza au kudadisi. Kusajili ni kuweka orodha ya kmbukumbu za vitu au watu kwa kuviandika katika daftari maalumu.
F
Fedha/pesa/hela:
Haya ni maneno yenye maana moja lakini yana asili tofauti. Maneno mengine yanayofanana na hayo ni sarafu, fulusi, faranga ambayo hutumika katika malipo. Maneno yote yanakubalika. Hata hivyo tuna mazoea ya kutumia neno fedha upande wa bara na pesa upande wa visiwani.
Fikiri /dhani.
Maneno haya yanafanana kwa kiwango fulani lakini wengi wetu huyachanganya  na kuyatumia kama visawe. Yana tofautiana kidogo. Fikiri ni kutumia ubongo kutatua jambo, kutafakari, kuwaza. Kudhani ni kufikiri bila kuwa na uhakika.
G
Ghairi-
Kuacha kutenda kilichokusudiwa.
Ghushi/gushi:
Neno sahihi ni ghushi
H
Hadubini:
Ni chombo  cha kuona vitu visivyoonekana kwa macho (Microscope).      
Hoteli/mahoteli :
Neno sahihi ni  hoteli.
Hovyo/ovyo:
 Neno sahihi ni ovyo           
Chanzo: Mwananchi

GWAJIMA APATA DHAMANA MAHAKAMA YA KISUTU, DAR



Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima leo amepata dhamana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar atarudi mahakamani hapo Mei 4, 2015. Josephat Gwajima ameshitakiwa kwa makosa mawili kutoa lugha ya matusi na kushindwa kutunza slaha.

Chanzo: Global Publishers

HALI ILIVYOKUWA NYUMBANI KWA GWAJIMA LEO


Askari wakiwa nyumbani kwa Gwajima.
Makamanda wa polisi wakiwa tayari kwa lolote.Gari lililombeba Gwajima likitoka ndani ya nyumba yake kuelekea kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano.Mawakili wa Gwajima wakisalimiana na mmoja wa maofisa wa polisi mara baada ya kufika eneo la tukio.Waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio.

Waumini wa Gwajima wakiwa wamezunguka nyumba wa askofu wao.
Kundi la wafuasi wa Gwajima wakifika nyumbani kwake mara baada ya polisi kuondoka eneo la tukio.
Baadhi ya watu waliokuwemo ndani ya nyumba ya Gwajima wakichungulia dirishani.
Baadhi ya waumini wa Gwajima wakifuatilia kwa makini hali iliyokuwapo.
Baadhi ya waumini wakiwa mbele ya nyumba ya Gwajima.Gari la polisi likiondoka eneo la tukio.Hapa wakishangilia ushindi baada ya polisi kuondoka eneo la tukio.
WAKATI taarifa zikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya jamii kuwa nyumba ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, imezingirwa na polisi, habari kamili ni kwamba zoezi la kumkamata askofu huyo lilishindikana baada ya kugoma kufungua geti lake.
Polisi hao waliokuwa na silaha walifika nyumbani kwa askofu huyo maeneo ya Salasala jijini Dar wakiwa kwenye magari zaidi ya manne ambapo walipiga kambi katika eneo hilo kwa saa sita huku njia hiyo ikiwa imefungwa kwa saa kadhaa kabla ya waandishi wa habari na baadhi ya waumini wa askofu huyo kuruhusiwa kupita.



Hata hivyo baada ya polisi hao kuzungumza na mawakili wa Gwajima na viongozi kadhaa wa kanisa hilo, waliamua kuondoka huku wakitoa amri kiongozi huyo afikie kituo kikuu cha polisi  kwa ajili ya mahojiano zaidi ambapo alifika na baadaye kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu ambapo taarifa za kina kuhusu kilichojiri huko zikiwa bado hazijapatikana.

Sunday, January 25, 2015

Escrow yapangua mawaziri 13


Hatimaye Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko 13 kwenye Baraza la Mawaziri yaliyohusisha mawaziri nane, manaibu watano, wakiwamo wapya wawili, ikiwa ni siku mbili kabla ya kuanza kwa Bunge, na ndani ya saa 48 kama gazeti hili lilivyoripoti Ijumaa iliyopita. 

Rais pia aliwaapisha mawaziri wote 13 akiwamo waziri mpya wa Afrika Mashariki, Dk Harrison Mwakyembe ambaye alisababisha hafla hiyo kuchelewa kwa kuwa alikuwa akitokea Davos, Uswisi.
Mabadiliko hayo, yanayoweza kuwa ya mwisho kwa Rais Kikwete, yamefanyika ikiwa imesalia miezi sita kabla ya kuvunjwa kwa Bunge kupisha Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba.
Rais amelazimika kufanya mabadiliko hayo baada ya mawaziri wawili, Profesa Anna Tibaijuka na Profesa Sospeter Muhongo, kuondoka kutokana na kuhusishwa na kashfa ya uchotwaji fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, ambayo pia imesababisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliackim Maswi kusimamishwa kazi, huku waziri wa zamani wa wizara hiyo, William Ngeleja akivuliwa uenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria.
Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, Kikwete amewaondoa mawaziri wawili wazoefu kutoka Ofisi ya Rais, Steven wasira na Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi, kuwapangia wizara nyingine, huku akimhamishia Dk Mary Nagu kwenye Ofisi ya Rais na Jenister Mhagama (Waziri Mkuu).
Akitangaza mabadiliko hayo jana, Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue alisema mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene, ambaye alikuwa naibu wa wizara ya Nishati na Madini kuanzia mwaka 2012 hadi 2014 na ambaye hadi jana alikuwa naibu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ameteuliwa kumrithi Profesa Muhongo kwenye wizara hiyo tata ya Nishati na Madini.
Simbachawene anakuwa waziri wa nne kushika wizara hiyo tangu Serikali ya Awamu ya Nne iingie madarakani na anaingia wakati Steven Masele, aliyekuwa naibu Waziri wa Nishati na Madini, akiwa amehamishiwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano). Nafasi ya Masele imechukuliwa na mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage ambaye ameteuliwa kwa mara ya kwanza.
Sefue alisema mbunge wa Ismani, William Lukuvi, ambaye tangu mwaka 2010 amekuwa Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Utaratibu na Bunge), ameteuliwa kuziba nafasi ya Profesa Tibaijuka ya uwaziri wa Kazi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Sura nyingine ngeni kwenye baraza hilo, kwa mujibu wa Sefue, ni ya mbunge wa Same, Anne Kilango Malecela, mmoja wa wazungumzaji wakubwa bungeni, ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu.
Alisema aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenista Mhagama amepanda kuwa Waziri wa Nchi, Sera, Uratibu na Bunge, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Lukuvi.
Nagu amehamia Uhusiano na Uratibu (Uwekezaji na Uwezeshaji) na Dk Harrison Mwakyembe anayehamia Afrika Mashariki (Uchukuzi).
Wengine ni mwanasiasa mkongwe, Steven Wasira aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo akitokea Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, wakati Samuel Sitta anakwenda Uchukuzi akitokea Wizara ya Afrika Mashariki.

Manaibu waziri wengine waliohamishwa ni Angella Kairuki, ambaye anakwenda Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akitokea Katiba na Sheria.
Ummy Mwalimu anakuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria akitokea Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).
Mabadiliko hayo yamekuja ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio manane ya Bunge, kutaka uteuzi wa Profesa Muhongo na Profesa Tibaijuka kutokana na kuhusishwa na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow.
Bunge liliagiza mamlaka ya uteuzi kutengua nyadhifa hizo pamoja na wenyeviti wa Kamati za Bunge, Nishati na Madini iliyokuwa chini ya Victor Mwambalaswa.
Wengine waliotakiwa kuvuliwa nyadhifa za Kamati kutokana na kashfa hiyo ni Andrew Chenge (Bajeti) na Kamati ya Sheria na Katiba iliyokuwa chini ya William Ngeleja.
Akizungumzia uteuzi huo, Kilango alisema: “Ninayajua matatizo ya walimu wenzangu na kwa kushirikiana na wenzangu tutaweza kuyatatua, kikubwa ni kushirikiana.”
Alisema kuwa kwa kushirikiana na Waziri wa Wizara hiyo watakuja na mipango na mikakati itakayolenga kuboresha sekta ya elimu.
Kwa upande wake, Lukuvi alisema kuwa anafahamu changamoto zinazoikabili wizara hiyo na atashirikiana na wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi.
“Ninachoomba ni ushirikiano kutoka kwa wananchi kwa kuwa ni imani yangu kuwa tukiunganisha nguvu zetu kwa pamoja kazi itafanyika vizuri”alisema Lukuvi.
Naye Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene alisema anatambua fika kuwa uchumi wa nchi yeyote unategemea nishati hivyo atahakikisha sekta hiyo inawaletea manufaa watanzania wote.
Simbachawene alisifu kazi ya Profesa Muhongo ana akasema atahakikisha anaikamilisha kwa kufikisha umeme kote vijijini.
Dk Slaa alonga

Akizungumzia mabadiliko hayo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema: “Hakuna jipya katika hayo mabadiliko, kwani tatizo lililopo ni mfumo na si viongozi, Watanzania wasitegemee lolote kutoka kwao.
“Kitendo hiki cha watu wanafanya makosa halafu wanaachiwa wanajiuzulu na kubaki na sifa zao.
Kama taifa hatuwezi kusonga mbele. Tunahitaji kuwashughulikia wanaorudisha nyuma maendeleo ya nchi.”
Katibu huyo aliongeza kusema: “Wahalifu bado wanapata fursa ya kukaa na kujadiliana na rais, hii haikubaliki. Washabainika wamefanya makosa kwa nini wasiwajibishwe mapema?”
TBC yawa kero
Shirika la Habari Tanzania (TBC) jana liliwakera Watanzania waliokuwa wakifuatilia matangazo ya moja kwa moja ya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.
Mabadiliko hayo yalikuwa yakitangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kutoka Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo yalihusisha mawaziri na manaibu mawaziri.
Matangazo hayo yalikuwa yakikatika mara kwa mara na wakati mwingine yakionyesha picha bila sauti jambo lililokuwa kero kwa watazamaji.
Hata hivyo, mkurugenzi mtendaji wa TBC, Clement Mshana alipotafutwa kuzungumzia matatizo yaliyojitokeza, alisema kwa kifupi “mimi sijui na nipo mkoani ninaendelea kufuatilia matangazo ya mabadiliko hayo” na kukata simu.
Katika hatua ya uapishwaji wa mawaziri na manaibu mawaziri hao ulioanza Saa 12.14 jana jioni muda mfupi baada ya kumalizwa kutangazwa matangazo yaliendelea vizuri.
Hali hiyo si ya kwanza kutokea kwani katika mijadala kadhaa ya mikutano ya Bunge matangazo yamekuwa yakikatika jambo lililokuwa likilalamikiwa na baadhi ya wabunge na wananchi kwa kukoseshwa fursa ya kutazama muhimili huo wa ukiendelea na shughuli zake.
Chanzo: Mwananchi

Mwenyekiti auawa, viungo vyapikwa kama mboga

Mwenyekiti  wa Kitongoji    cha  Songambele, Kata ya Ilela Tarafa Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi, Richard Madirisha (31), ameuawa kikatili kwa kuchinjwa  shingo na kutenganishwa na kiwiliwili na kisha kunyofolewa  viungo vya mikono na miguu na sehemu za siri  na kichwa chake na viungo hivyo kupikwa ndani ya safuria kama mboga.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari  mauaji hayo ya kikatili na  kutisha  yalitokea jana saa 5.30 usiku nyumbani kwa marehemu.
Kidavashari alisema, siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa amelala nyumbani kwake akiwa na mkewe  Meklina  Mussa na  ghafla walitokea watu watano ambao hawafahamiki na  kuvunja mlango na kuingia ndani ya nyumba.
Alisema watu hao waliodaiwa kuwa na mapanga  waliingia chumbani kwa marehemu  na kumlazisha mkewe ajifiche kwa kujifunika na shuka usoni.
 Alisema  baada ya mkewe kujifunika walianza kumchinja marehemu  kwa  kutumia panga huku mkewe akiwa anasikia jinsi marehemu  akilia kwa uchungu.
Kidavashari alisema baada ya kumchinja walichukua kichwa na kukiweka kwenye safuria na maji na kukipika kwenye moto uliokuwa unawake nje ya nyumba ya marehemu.
Alisema kisha walirudi ndani na kunyofoa sehemu za siri, mikono na miguu  na  kuziweka kwenye  safuria  jingine  kwenye moto   na kutokomea kusikojulikana huku  viungo hivyo vikiendelea kuchemka  ndani ya safuria hizo.
 Kidavashari alisema  mke  wa marehemu baada ya kuona watu hao wametokomea alitoka nje na kwenda kutoa taarifa kwa majirani ambao walifika kwenye eneo hilo  na kukuta viongo hivyo vikiwa  vinaendelea kuchemka  kwenye sufuria hizo huku kiwiliwili chake kikiwa ndani ya chumba chake

 Amesema uchunguzi wa  awali umebaini kuwa chanzo cha mauwaji  kimetokana na visa vya marehemu na mtu mmoja ambae walikuwa wakiishi nae Tabora  ambae  alikuwa akimtuhumu marehemu  kuwa amemnyanng'anya  mwanamke ambae walikuwa  na mahusiano nae ya kimapenzi ambae marehemu aliamua   kuhama nae kijijini  hapo na kuhamia nae kijiji cha Songambele  Wilaya Mlele

 Kamanda Kidavashari  alieleza   jeshi la polisi Mkoa wa Katavi limewakamata na linawashikilia  watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo ya kikatili.

Samahani wadau kwa picha hizi za kutisha ila hakuna jinsi ni lazima kuziposti.
 


 Chanzo: Mwananchi

Saturday, January 24, 2015

VIDONGE HATARI VYAUZWA KA NJUGU PHARMACY DAR!

Hali inatisha! Vidonge vinavyodaiwa ni vya kutoa mimba vimezagaa kwenye maduka ya madawa baridi ‘famasi’ jijini Dar na kuuzwa kinyume cha sheria iliyowekwa na wahusika kwa kuwa hairuhusiwi kuuziwa dawa hizo pasipokuwa na kibali cha daktari.


Wauzaji wa moja ya duka la dawa linalouza dawa za kutolea mimba.

Kikosi chetu cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers Ltd kiliingia kazini kuzisaka famasi zinazodaiwa kujihusisha na biashara ya dawa hizo zilizotajwa kwa jina la Misoprostol 200.

ENEO LA KWANZA
Zoezi lilianzia kwenye famasi za Mwenge, Dar (majina yanahifadhiwa kwanza) ambapo OFM walikwenda kwa lengo la kutaka kununua dawa hizo ambapo muuzaji wa kwanza ambaye ni mwanaume alikiri kuziuza kwa bei ya sh 10,000.

Kamanda wa OFM (kulia) akimbana kwa maswali mmoja wa wauzaji hao.

Katika famasi nyingine maeneo hayo, muuzaji wa pili aliiuza kwa  sh 25, 000 huku akikiri kuwa anauza dawa hizo kinyume cha sheria.“Naziuza kimakosa tu maana haziruhusiwi kuuzwa pasipokuwa na kibali cha daktari. Ili umuuzie mtu lazima aje na cheti cha dokta kinachoonesha anahitaji kuzitumia na matumizi yake rasmi ni kwa ajili uchungu endapo mjamzito anataka kujifungua baada ya kazidisha miezi bila kuzaa,” alisema mfamasia huyo bila kujua anazungumza na makachero wa OFM.
Moja ya dawa zinazutumika kutolea mimba ikiwa mkononi mwa kamanda wa OFM.
ENEO LA PILI
Baada ya hapo, OFM ilitua maeneo ya Tandale ambapo ilihitaji huduma hiyo kwenye famasi mbalimbali huku tukio zima likirekodiwa hatua kwa hatua.OFM waliingia kwenye famasi hiyo kwa awamu na kuulizia vidonge hivyo kama vinapatikana na kutajiwa bei ya sh 20,000.
OFM waliomba kupata maelekezo ya matumizi yake ambapo mhudumu mwanamke, alitoa maelekezo:
“Hizi dawa huwa naziuza sana kwa watu mbalimbali kama wanafunzi na wake za watu kwa lengo la kutolea mimba. Vidonge vingine huingizwa sehemu za siri na nyingine unameza. Isipokuwa ukikosea tu kidogo kuziweka zinaweza kuharibu mfumo mzima wa uzazi hivyo unahitajika umakini mkubwa mno.”
Makamanda wa OFM wakichukua maelezo zaidi kutoka kwenye duka hilo la dawa.
ENEO LA TATU
Maeneo ya Magomeni OFM ilibaini dawa hizo zinauzwa sh 15,000 hadi sh 30,000. Hata hivyo, OFM walinunua vidonge hivyo (vielelezo vipo ofisini) kwa bei ya sh 25,000 kwenye duka moja lililopo Magomeni-Kagera.
ZINA MADHARA?
Kwa mujibu wa mtaalam wetu wa afya na uzazi, athari za utoaji mimba kwa kutumia dawa hizo ni pamoja na kuharibu taratibu za kimaumbile kwenye kizazi na kusababisha ugumba.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid.

MAGONJWA SUGU
Pia mtoaji mimba huwa na hatari ya kupata magonjwa sugu ya via vya uzazi yanayoathiri shingo ya kizazi na mirija ya mayai. Wanaotumia vidonge hivyo wana uwezekano wa kupata kansa ya uzazi hasa kwa wale wanaoingiza sehemu za siri.

SOURCE: GLOBAL PUBLISHERS

MARA BAADA YA MUHONGO KUJIUZULU NA JK KUTEUA WAPYA, ZITTO ATOA YA MAYONI!

Hiki ndicho alichokiandika Mhe. Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa Face Book mara baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter muhongo kutangaza kujiuzulu mapema leo.
Na hiki ndicho alichokiandika mara baada ya uteuzi wa Mawaziri na manaibu Mawaziri wapya.

Friday, January 16, 2015

Roda; binti aliyelipiwa kishika uchumba akiwa na miaka 15

“Natamani kuondoka eneo hili lenye mila na desturi nyingi potofu zinazoninyima haki, sina amani hata kidogo na moyoni mwangu sioni nuru ya maisha yangu”
“Kwa mfano tarehe 11.06.2014 alikuja mwanamume mmoja nyumbani kwetu akampa mama kilo moja ya sukari na Sh500 kama kishika uchumba ili anioe katika umri huu mdogo”.
Maneno haya ya kukata tamaa yanatoka kinywaji mwa Roda Damas (jina halisi limefichwa), mwanafunzi wa Shule ya Msingi Oldonyomurwa iliyopo Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.
Roda mwenye umri wa miaka 15 ni miongoni mwa watoto wa kabila la Wamasai ambaye anatakiwa kuolewa katika umri mdogo, baada ya wazazi wake kupewa kishika uchumba na mwanamme anayenuia kumuoa.
Hofu hii ya watoto wa jamii ya kifugaji ndiyo inayonifanya nitembelee maeneo yao kuujua ukweli wa yanayozungumzwa na nina bahatika kukutana na Roda anayezungumza nami huku akibubujikwa machozi.
Wilaya ya Siha hususan Kata za Orkolili, Makiwaru, Karansi, Gararagua na Biribiri, zina watoto wa kike wanaoishi kwa hofu ya kuolewa katika umri mdogo. Wengine wanaanzia hata miaka mitano.
Ndoa za utotoni
Roda anasema kwa jamii ya kifugaji si jambo la ajabu mtoto kuchumbiwa hata akiwa na umri wa miaka mitano, umri ambao hata anayechumbiwa hajui nini kinaendelea.
“Mwanamume anaweza kuja na kutoa kishika uchumba na mtoto ataendelea kuishi kwa wazazi wake na siku akimhitaji humchukua baada ya kutoa ng’ombe waliohitajika kama mahari.
“Kila nikipita nikikutana na huyo baba huniita mke wake na hata mama yangu huniambia huyo ndiye mume wako. Hii inaniumiza kwa sababu mimi nataka kusoma sitaki kuolewa.”
Hawa nao wako mtegoni
Roda ananisaidia kukutana na watoto wengine wawili, Neema na Evelyn wote wana miaka 14 na wana masaibu kama yake kwani tayari wameonyeshwa wachumba na wanatakiwa kukeketwa ili waolewe.
“Muda mwingi tunautumia kufikiria ni jinsi gani tutajitoa kwenye mikono ya wanafamilia wanaotaka kutuozesha,” anasema Neema.
Ndoa za utotoni Tanzania
Tanzania ni moja ya nchi zilizokithiri kwa ndoa za umri mdogo duniani. Kwa wastani, wasichana wawili kati ya watano huolewa kabla ya kufikisha miaka 18 .
Kwa takwimu za mwaka 2010 kutoka mashirika mbalimbali ya kijamii, asilimia 37 ya wanawake wenye umri wa miaka 20 hadi 24 waliolewa kabla ya kufikia miaka 18.
Mikoa inayoongoza kwa ndoa za utotoni ni Shinyanga asilimia 59, Tabora asilimia 58, Mara asilimia 55 na takwimu hizo zikionyesha Mkoa wa Kilimanjaro una tatizo hilo kwa asilimia 25.
Serikali inasemaje?
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Pindi Chana amewahi kunukuliwa akisema mkoani Mara kuwa suala la ndoa za utotoni na ukeketaji linatoa dosari kubwa katika harakati za kumkomboa mtoto wa kike.
Anasema Taifa linahitaji mchango wa kila mwananchi ili kufikia malengo ya mpango wa Taifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (Mkukuta) na utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025.
Alisema ndoa za utotoni na ukeketaji vinapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote na kuwa jamii inaweza kuondoa tatizo hilo kama italichukulia kwa uzito wa juu.

Wednesday, January 14, 2015

PROJECT MPYA, BOB JUNIOR NA WEMA. KAZI IPO


LICHA ya Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kuwahi kufikishwa kortini na Mbongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior, wamebambwa ‘live’ wakioneshana mahaba niue, Amani lina tukio zima.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akiwa mapajani mwa Mbongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior'.
TUJIUNGE TEGETA, DAR
Ishu hiyo iliyopigwa chabo na paparazi wetu hivi karibuni lilijiri ndani ya Ukumbi wa Club 71 uliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam ambapo Wema siku hiyo alimtambulisha msanii wake mpya anayesimamiwa na kampuni yake ya Endless Fame anayeitwa Ally Luna.

WAKUTANA
Katika tukio hilo, Wema ndiye aliyeanza kufika ukumbini humo akifuatana na timu yake, akiwemo Petit Man (kama kawa).

Muda mfupi baadaye, Bob Junior naye alifika ambapo alipokutana na Wema walianza kupeana mahaba huku wakigandana kwa zaidi ya dakika kumi.
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akizidi kupozi kimahaba na ‘Bob Junior'.

Mbali na Bob Junior, Wema alialika wasanii kibao kwa ajili ya kumsapoti ambao hata wao walipigwa butwaa baada ya kushuhudia tukio hilo.
Wakiwa katika chumba cha VIP, Wema aliendelea kuwa ‘veri klozi’ na Bob Junior hivyo kusababisha minong’ono ya hapa na pale.

MAPOZI
Katika tukio hilo, kilichowashangaza mashuhuda zaidi ni kitendo cha Wema kukaa mapajani kwa Mbongo Fleva huyo bila kujalia macho ya watu.


Wema Sepetu na ‘Bob Junior' wakiteta jambo.

SALAMU KWA DIAMOND NA ZARI?
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walikwenda mbali zaidi na kuanza kuhisi tabia hiyo ya Wema na Bob Junior ni salamu kwa aliyekuwa mwandani wake na kumwagana Nasibu Abdul ‘Diamond’ na ‘bebi’ wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘Zari’.
“Hapa naona kama sielewielewi maana ni mara ya kwanza kumwona Wema na Bob Junior wakigandana kiasi hiki tangu walipopelekana mahakamani kipindi kile na ukizingatia Sharobaro (Bob Junior) alikuwa hasimu wa Diamond aliyekuwa mpenzi wa Wema kipindi hicho,” alisema mmoja wa mastaa wakubwa (jina linahifadhiwa). Akaongeza:


Wema Sepetu akimchumu ‘Bob Junior.

“Nakuhakikishia hizi ni salamu kwa Diamond na yule Zari wake. Hapa Wema anajua kabisa salamu zitawafikia.”
Baadhi ya mastaa hao walionekana kulaani tukio hilo na kujaribu kumtahadharisha Wema juu ya ukaribu huo kwani kama Diamond atagundua atajua ni ishu za kulipizana visasi.
“Kwa vyovyote Diamond akigundua jambo hili litamfanya ukaribu wake na Wema kuzidi kuwa mgumu na kuurejesha ni ndoto kama wana mpango wa kurudiana.”

WENYEWE WANASEMAJE?
Paparazi wetu alipojaribu kuwadodosa wawili hao juu ya uhusiano wao, kila mmoja aliishia kucheka tu bila kutoa majibu ya kueleweka.

DAKTARI AMUONYA WEMA
Wakati huohuo, mmoja wa madaktari wa mastaa Bongo (jina lipo) amemuonya Wema kuhusu masuala ya mapenzi kwamba, kama ni kweli ameanzisha uhusiano mwingine si vizuri kwani bado akili yake haijatulia tangu amwagane na Diamond hivyo anahitaji muda ili kutuliza akili.
“Wema hatakiwi kuanzisha uhusiano wa kimapenzi kwa haraka, wala si vizuri kulipiza kisasi kwani anaweza kujikuta pabaya zaidi, haya mambo ya mapenzi yanatesa sana mastaa wengi na nimekuwa nikiwapa huduma za kisaikolojia,” alisema dokta huyo kwa sharti la kutotajwa gazetini.

TUJIKUMBUSHE
Mwaka 2011, Mahakama ya Mwanzo Kinondoni jijini Dar ilimhukumu Wema kwenda jela miezi sita au faini ya shilingi elfu 40 baada ya kupatikana na hatia ya kumtukana matusi ya nguoni Bob Junior ambapo alilipa faini na kuachiwa huru jambo lililoibua uhasama mkubwa kati yao.
Hivyo, tukio la kuonekana pamoja na kugandana kimahaba ni ishara njema kuwa sasa wapo vizuri na ule uhasama haupo tena!!

WASHTAKIWA WAWILI WA SAKATA LA AKAUNTI YA ESCROW WAPANDISHWA KIZIMBANI


WATU wawili Rugonzibwa Mujunangoma na Theophillo Bwakea wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashitaka ya rushwa baada ya kupokea mgao wa Sh. Milioni 485.1 kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow walizohamishiwa na James Rugemalira.
Katika kesi ya kwanza, aliyekuwa Mwanasheria wa Mamlaka ya Vizazi na Vifo (Rita) Mujunangoma ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Sheria Wizara Ardhi, Nyumba Maendeleo ya Makazi, alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Emmilius Mchauru.
Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai akisaidiana na Max Ari, ulidaiwa kuwa Februari 5, mwaka 2014 katika benki ya Mkombozi iliyopo Ilala jijini, mshtakiwa akiwa Mkuu wa Sheria wa wizara hiyo, alipokea rushwa.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alipokea rushwa ya Sh. Milioni 323.4 kama zawadi kupitia akaunti yake namba 00120102062001 kutoka kwa Mshauri binafsi wa kimataifa na Mkurugenzi wa zamani wa IPTL,James Rugemalira baada ya kuwa mjumbe katika menejimenti ya Rita wakati wa machakato wa kuipitisha IPTL kuiuzia Tanesco umeme.
Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alipokea zawadi hiyo kama ofisa wa muda wa kushughulikia masuala ya IPTL.
Mshtakiwa alikana mashitaka yake.
Swai alidai kuwa upande wa Jamhuri hauna pingamizi la dhamana na kwamba mahakama ijielekeze katika hati ya mashitaka fedha anazodaiwa kuchota mshtakiwa.
Hakimu Mchauru alisema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kujidhamini kwa Sh. Milioni 160 taslimu au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo ya fedha.
Pia wadhamini wawili wanaofanyakazi serikalini watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. Milioni 10 na mshtakiwa asitoke nje ya Dar es Salaam, bila kibali cha mahakama.
Mshtakiwa alitimiza baadh ya masharti ya dhamana ambapo hakimu alisema mahakama imempa dhamana ya muda hadi Januari 16, mwaka huu hati za mali zake zitakapohakikiwa.
Katika kesi ya pili, aliyekuwa mjumbe wa kitengo cha kuidhinisha Tanesco kununua umeme wa IPTL, Wizara ya Nishati na Madini, Injinia Bwakea kwa sasa mtumishi wa Wakala wa Umeme Vijijini(REA), alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi.
Swai alidai kuwa Februari 12, mwaka 2014 mshtakiwa akiwa Injia Mkuu wa REA, alipokea rushwa ya Sh. Milioni 161.7 kupitia akaunti namba 00410102643901 ya Tegeta Escrow kama zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Rugemalira.
Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alipokea zawadi hiyo baada ya kuwa mjumbe aliyeandaa sera zinazohusu sekta binafsi kuzalisha na kuuza umeme kwa Tanesco.
Mshtakiwa alikana mashitaka yake.
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana na kwamba upelelezi umekamilika.
Hakimu Moshi alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili kutoka serikalini au wanaofanyakazi katika taasisi zinazotambulika watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. Milioni 20 kila mmoja.
Pia alisema mshtakiwa asitoke nje ya Dar es Salaam,  bila kibali cha mahakama.
Mshtakiwa alitimiza masharti ya dhamana na kesi yake itatajwa Januari 26, mwaka huu.
Jana saa 2:00 asubuhi katika viunga vya mahakama ya Kisutu, watumishi na watu mbalimbali waliingia katika eneo hilo huku kukiwa na minong’ono kwamba wanaotuhumiwa ufisadi wa Escrow watafikishwa mahakamani hapo.
Pia waandishi wa habari waligawanyika katika makundi tofauti huku wakijadili na kutafatuta wadau wao kujua kuhusu ujio wa watuhumiwa hao.
Mapema jana saa 5:42 asubuhi vigogo hao walitinga mahakamani hapo na kwenda kusomewa mashitaka yao yanayowakabili.

MABAKI YA NDEGE YA AIRASIA QZ8501 YAZIDI KUPATIKANA


Picha zikionyesha mabaki ya ndege ya AirAsia QZ8501 iliyozama baharini.

Picha za mabaki ya ndege ya AirAsia yaliyowekwa na Waziri wa Ulinzi wa Singapore, Ng Eng Hen kwenye ukurasa wake wa Facebook leo
.
SEHEMU kubwa ya mabaki ya ndege ya AirAsia QZ8501 iliyoanguka baharini ikiwa na watu 162 mwaka jana yameonekana na kupigwa picha katika Bahari ya Java.
Mkuu wa Mamlaka ya Uokoaji na utafutaji Indonesia, Bambang Soelistyo, amesema mabaki hayo yameonekana jana, Jumanne.
Waziri wa Ulinzi wa Singapore, Ng Eng Hen, leo ameweka picha za ndege hiyo katika ukurasa wake wa Facebook na kuandika kuwa picha hizo zinathibitisha kuwa ndege iliyoanguka baharini ni AirAsia QZ8501.
AirAsia ilipoteza mawasiliano na waongoza ndege Desemba 28,mwaka jana ilipokuwa ikitokea Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singapore ikiwa na jumla ya watu 162.
Miili 40 tayari imepatikana kutoka Bahari ya Java ila wengi wa watu waliokuwa kwenye ndege hiyo wanadaiwa kuwa bado wamekwama ndani.
Mpaka sasa vifaa viwili vya kutunza kumbukumbu za ndege (black boxes) na mkiwa wa ndege hiyo vimepatikana na kupelekwa sehemu husika.

Tuesday, January 13, 2015

KABURI LA MAREHEMU ALIYEZIKWA NA KUKU TUMBONI SHINYANGA , LIMEFUKULIWA

Kaburi la marehemu Benadetha Steven aliyefariki dunia hivi karibuni kutokana na uvimbe tumboni aliyekuwa mkazi wa Mtaa wa Mapinduzi kata ya Ndala katika manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga aliyezikwa na kifaranga cha kuku tumboni na ndugu zake kwa madai kuwa wanaondoa mikosi katika familia.Pichani ni kaburi lake likiwa limefukuliwa na watu wasiojulikana-Picha na Kadama Malunde
 Kaburi la marehemu Benadetha limekutwa limefukuliwa huku sanda na jeneza likiwa linaonekana na alama za  nyayo za miguu ya watu na miguu ya mnyama aina ya fisi zikionekana katika kaburi hilo.Inasemekana kuna watu walionekana eneo la makaburi juzi wakiwa na gari na inadaiwa udongo umepelea pengine umechukuliwa-Picha na Kadama Malunde

Wananchi wakiwa kaburini ambapo walisikika wakisema :“Tunalaani kitendo hiki,tumekuta jeneza na  sanda ya marehemu inaonekana,tukaita polisi,hiki kitendo kimefanywa na binadamu tu maana kaburi lilikuwa refu sana,fisi hawezi kufukua,hapa kuna miguu ya watu na fisi,fisi nadhani alisikia harufu ya maiti,na fisi hawezi kuingia kwenye shimo,binadamu wamekosa utu”-Picha na Kadama Malunde

Wananchi wakiwa katika eneo la kaburi la marehemu kabla ya kuzika tena-Picha na Kadama Malunde

Mkuu wa upelelezi jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Musa Athuman Taibu(mwenye suti) akiwa kwenye kaburi la marehemu ambapo alisema jeshi la polisi halina mamlaka ya kufukua kaburi la marehemu bali mahakama pekee ndiyo yenye yenye mamlaka ya kutoa kibali cha kaburi kufukuliwa hivyo kuwaomba wananchi kufukia kaburi hilo badala ya kulifukua.
Benadetha Steven(35) alikuwa anaishi mtaa wa Mapinduzi kata ya Ndala,alifariki dunia Januari 1,2015,wakati akitibiwa uvimbe wa tumboni katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga na kuzikwa katika makaburi ya Masekelo ambapo mazishi yake yalileta utata baada ya ndugu wa marehemu kutoka mkoani Mara(Wakurya) kuingia kaburini na kuchana tumbo la marehemu kwa wembe kisha kuchinja kifaranga cha kuku kwa wembe na kuingiza kuku huyo kwenye tumbo la marehemu. Picha na Kadama Malunde

Monday, December 8, 2014

Kikwete apangua tena wakuu wa mikoa

Rais Jakaya Kikwete amempandisha cheo Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Daudi Ntibenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuwahamisha vituo vya kazi wakuu wengine sita wa mikoa kuanzia jana.
Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ilisema Ntibenda ataapishwa leo, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.
Wakuu wa mikoa waliohamishwa ni Elaston Mbwilo anayetoka Manyara kwenda Simiyu kuchukua nafasi ya Paschal Mabiti aliyepewa likizo ya ugonjwa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera anahamia Manyara kutoka Morogoro na nafasi yake inachukuliwa Dk Rajabu Rutengwe kutoka Tanga alikokaa kwa mwezi mmoja akitokea Katavi.
Magalula Magalula amehamishiwa Tanga kutoka Lindi ambako naye alikaa kwa mwezi mmoja akitokea Geita na nafasi yake inazibwa na Mwantumu Mahiza kutoka Pwani.
Mhandisi Evarist Ndiliko amehamishiwa Pwani kutoka Arusha alikohamia hivi karibuni kutoka Mwanza.
Katika taarifa yake, Balozi Sefue alisema wakuu wengine wa mikoa wanaendelea kubakia katika vituo vyao vya sasa vya kazi.
Uhamisho huo umekuja ikiwa ni mwezi mmoja kamili tangu Rais Kikwete alipofanya uteuzi wa wakuu wapya wanne wa mikoa na kuwahamisha sita huku wengine watatu wakipangiwa kazi nyingine.
Wakuu wa mikoa wanne wapya ni Dk Ibrahim Msengi (Katavi), Amina Masenza (Iringa), Halima Dendego (Mtwara) na John Mongella (Kagera).
Kabla ya kuteuliwa, Masenza alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mwanza; Dk Msengi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kilimanjaro na Mongela alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Walioachwa kwa ajili ya kazi nyingine ni Dk Christine Ishengoma (Iringa), Kanali Fabian Massawe (Kagera) na Kanali Joseph Simbakalia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, ambaye tayari ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA).

Source: Mwananchi.

Friday, December 5, 2014

Fahamu jinsi Ukimwi ulivyoanza hata kusambaa kila kona duniani

Wakati ugonjwa wa ukimwi ukipamba moto katika mataifa mengi ya Afrika, miaka ya 1980, ilizuka hofu kubwa na maswali mengi juu ya lilikoanzia.
Kwa mfano, hapa Tanzania ulipewa majina mengi, kama vile Juliana, silimu (wembamba), fire (moto) na mdudu. Ni ugonjwa ambao walioupata walionekana kukonda hadi kubakia mifupa na nywele kunyonyoka.
Mbali na hali hiyo, mgonjwa alipata matatizo ya ngozi kuharibika kwa kuwa kavu, vidonda ambavyo viliacha madoa meusi na kuharisha.
Sura za wagonjwa zilikuwa zinabadilika na kuonekana za kutisha na walionekana kuwa katika hali ya mateso mengi ya kukumbwa na maradhi mengi kabla ya kufa.
Inafahamika wazi kuwa binadamu lazima utafika wakati atakufa, lakini kwenye miaka ya 1980 hadi mwanzoni mwa 1990, ulionekana kuambkizwa Virusi Vya Ukimwi (VVU) ni sawa na kupewa tiketi ya kifo. Wengine walidiriki hata kujiua mara baada ya kubaini wameambukizwa.
VVU inaweza kuchukua miaka mitano hadi zaidi ya 10 ili kuonyesha dalili za kuugua, hatua ambayo inafahamika kuwa ni ya ukimwi.
Wengi wa waliopimwa na kuonekana wameambukizwa wakati huo walifika hatua ya kukonda na kuugua mapema kutokana na wasiwasi na msongo wa mawazo juu ya kifo.
Zipo dhana nyingi katika jamii zinazohusu jinsi Viruzi Vya Ukimwi (VVU) vilivyoanza kuenea kwa binadamu, hususani kwa Waafrika ambao ndio wanaonekana kuathirika zaidi na janga hili.
Zilikuwapo dhana nyingi sana na zote zimefanyiwa kazi na wataalamu wa afya. Baada ya uchunguzi wa kina dhana nne ndizo zilizofanyiwa utafiti wa kina baada kuonekana kuwa mojawapo inaweza ikawa ni chanzo.
Dhana zilizofanyiwa kazi ni nne nazo ni za madai ya hujuma zilizofanywa na wataalamu ili kuwaua Waafrika, ukatili wa kikoloni, matumizi ya chanjo na shughuli za uwindaji.
Hujuma dhidi ya Waafrika
Hii ilitokana na hisia za Waafrika wenyewe hasa ikizingatiwa kuwa wao ndio waliokuwa wanaathirika zaidi.
Hapa ikaonekana kuwa huenda wazungu ndio wamefanya njama ili kuwaangamiza Waafrika kama siyo kuwapunguza.
Uvumi huo ulienea na uchunguzi uliofanywa ulibaini kuwa watu weusi wanaoishi Marekani, wengi wao waliamini VVU ni silaha iliyotengenezwa maabara ili kuwamaliza nchini humo.
Nchini Marekani wengi wa waliokufa ni watu weusi hasa waliokuwa wanajihusisha na ushogo na hata wanaoshirikiana nao.
Baada ya utafiti wa kina ulionekana kuwa huo ni uvumi tu kwa kuwa haukuwepo uthibitisho wa kisayansi kuthibitisha jambo hilo.
Vilevile ilibainika kuwa historia ya ukimwi ulianza kuenea kwa binadamu miaka ya 1920. Wakati huo taaluma ya sayansi ya afya ilikuwa haina ufundi wa uhandisi jeni ambao unawezesha kutengeneza virusi.
Kwa sababu hiyo, dhana hiyo ikaonekana haina mashiko na kuwekwa kando.
Ukatili wa wakoloni
Wapo waliodhani VVU ilianza kuenea kwa Waafrika wakati wa ukoloni, ambapo vilikuwapo vitendo vya kikatili vya kulazimisha watu wafanye kazi hadi kuwasababishia kuumia huku wakiishi mazingira magumu yasiyo safi wala chakula cha kutosha.
Iliaminika kuwa katika mazingira hayo mfumo wao wa kinga ulishuka na kuwa rahisi kuambukizwa maradhi mengi yakiwamo ya bakteria na virusi.
Isitoshe walipougua walidungwa sindano za tiba, huku zikiwa hazijachemshwa hivyo kuwa rahisi kuhamisha maradhi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Isitoshe, iliaminika kwamba baadhi ya kambi walisambazwa wanawake malaya ili kuwaliwaza wanaume baada ya kazi ngumu.
Kwa sababu hiyo, mazingira haya yote yalikuwa ya hatari na ambayo yangeweza kueneza virusi haraka kwa watu.

Hata hivyo vigezo hivyo vyote havikuzingatiwa kwa sababu hayakuwepo mazingira ya chanzo cha kirusi. Isitoshe baada ya taaluma kubaini VVU anatokana na kirusi aliyeanzia kwa sokwe hayakuwapo mazingira ya mahusiano na wanyama hao.
Utoaji wa chanjo
Baadhi ya wataalamu wa afya walifikiri kuwa VVU ilianza kuenea kwa binadamu kutokana na utoaji wa chanjo ya polio. Chanjo iliyopewa nafasi kubwa ya kueneza VVU ni ile iliyotengenezwa kwa figo za sokwe na ilitolewa kwa mtu aimeze.
Chanjo ya namna hiyo ilitolewa kwa mamilioni ya watu Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC), Rwanda na Burundi mwanzoni mwa miaka ya 1950.
Kwa sababu hiyo ikadhaniwa kuwa zilichukuliwa figo za sokwe na katika utengenezaji wa chanjo, vikawapo pia virusi.
Dhana hiyo ilionekana kuwa siyo chanzo kwa sababu VVU ilianza kuenea hata kabla ya miaka ya 1950. Jambo jingine ni kwamba kwa namna chanjo hiyo ilivyokuwa inatengenezwa isingeweza ikabeba VVU. Kwa sababu hiyo dhana hiyo ikatupwa.
Dhana ya uwindaji
Ilionekana kuwa uwindaji na utumiaji wa nyama ya sokwe umekuwa ukifanyika kwa miaka katika misitu ya eneo la Afrika ya Kati, hususani nchini DRC.
Wawindaji wakati wa pilika za kumuua sokwe waliweza kupata majeraha mbalimbali yakiwepo ya kujikata, kujikwaa na kuchubuka ngozi.
Wakati wa kuchuna ngozi ama kukatakata nyama, ilikuwa rahisi damu ya sokwe kufikia vidonda na hapo virusi kufanikiwa kuhamia kwa binadamu.
Dhana hii ilikubalika kutokana na desturi za wawindaji na kwamba ulikuwapo hata kabla ya miaka ya 1920, ambayo inaaminika kuwa watu wa kwanza kufa kwa dalili za ukimwi walionekana ingawa wakati huo ugonjwa ulikuwa haufahamiki.
VVU ilianzaje?
Wataalamu wa afya wamefanya tafiti mbalimbali na kujiridhisha kuwa VVU vinatokana na mfumo wa mabadiliko ya kijeni wa kirusi aliyekuwa anaenea miongoni mwa sokwe.
Kirusi huyu anajulikana kama Simian Immunodeficiency Virus (SIV). Ni kirusi ambaye kama ilivyo VVU naye anadhoofisha mfumo wa kinga ya sokwe. SIV anaaminika kuwa sawa na VVU, lakini yeye ana uwezo wa kushambulia tu mfumo wa kijinga ya sokwe.
Wataalamu wanaeleza kuwa VVU ni SIV ambaye amejibadili mfumo ili aweze kuendelea na uzalishaji kwa kupitia mfumo wa kinga wa binadamu.
Inaaminika VVU ilianza kusambaa kwa binadamu mwaka 1920 katika mji mkuu wa DRC, Kinishasa. Hata baada ya SIV kujibadili na kuwa VVU anayeweza kuenea kwa binadamu amekuwa akijibadili hivyo kusababisha aina kadhaa za virusi.
Hii imesababisha viwepo aina mbili za virusi, VVU1 na VVU2. VVU1 inatabia zinazofanana na za SIV zaidi kuliko VVU2. VVU1 inapatikana zaidi nchini DRC.
Wiki ijayo makala hii itaendelea kwa kukueleza jinsi VVU ilivyoenea kwa kasi pamoja na madhila yake.

Source: Mwananchi