LATEST POSTS

Monday, July 6, 2015

Jaji Ramadhani: Mniombee mapenzi ya Mungu yatimie

Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani  

Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jaji mstaafu Augustino Ramadhani amewataka Watanzania kuendelea kumwombea ili mapenzi ya Mungu ya kumfanya kuwa kiongozi wa Taifa yatimie.
Jaji Ramadhani alisema hayo jana wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Dayosisi ya Dar es Salaam. Katika sherehe hizo, mgombea huyo alikuwa mgeni rasmi akiambatana na Dk Mwele Malecela ambaye pia anawania nafasi hiyo.
Jaji Ramadhani, ambaye ni mchungaji wa kanisa hilo alisema haikuwa mapenzi yake kutangaza nia ya kugombea urais, bali alipata msukumo kutoka kwa Mungu mwenyewe.
“Kila siku watu wananipongeza kwa kujitokeza kuwania urais. Ninawaambia safari bado ni ndefu, wazidi kuniombea ili mapenzi ya Mungu yatimie,” alisema.
Azungumzia rushwa
Kiongozi huyo alisema rushwa imekuwa tatizo kubwa nchini na kubainisha kuwa yeye anachukia na hata Mungu pia haipendi.
Alisema CCM imekuwa ikipambana na rushwa chini ya msemo wake ‘rushwa ni adui wa haki’ na kuwataka wananchi wabadilike na kuepuka rushwa.
Awali akimkaribisha Jaji Ramadhani, Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa alimpongeza kwa kujitokeza kuwania urais, akisema kati ya waliojitokeza, yeye ameonekana kuwa na karama nyingi.
Alisema Jaji Ramadhani amekuwa ni Kasisi wa Kanisa la Anglikana, aliwahi kuwa Brigedia Jenerali, alikuwa Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu na pia ni Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu.
“Tuko nyuma yako, tunakuombea kwa Mungu ushinde nafasi ya urais ili utende haki na kupambana na rushwa,” alisema Askofu Mokiwa.
Askofu Mokiwa alisisitiza kuwa wala rushwa wote wafungwe bila huruma ili kuondoa tatizo hilo.
Alipoulizwa kuhusu Jaji Ramadhan kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo licha ya kuwa yeye ni kasisi tu wa kanisa hilo, mjumbe wa kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo, Mchungaji John Kamoyo alisema uamuzi huo unatokana na uhusiano kati ya Jaji Ramadhani na Askofu Mokiwa.
“Majibu ya swali hilo ni mengi, lakini nadhani ni uhusiano tu kati ya Askofu Mokiwa na Jaji Ramadhani. Kuna mambo mengi lakini nisingependa kueleza hapa,” alisema Mchungaji Kamoyo.

Mbunge ajivua uanachama Chadema

Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi ametangaza kujivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). 

Sumbawanga. Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi ametangaza kujivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Akizungumza mjini Mpanda katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili, jana Arfi aliwaeleza wananchi wa Mpanda kuwa uanachama wake ndani ya Chadema utakoma mara tu baada ya kuvunjwa Bunge Julai 9.
Pia, alitumia mkutano huu kuwaaga wananchi wa jimbo hilo akisema hatagombea tena nafasi hiyo aliyoitumikia kwa miaka 10.
Arfi alifafanua kuwa hayuko tayari kugombea jimbo hilo kupitia chama chochote cha siasa na kauli hiyo imelenga kuondoa uvumi uliokuwa umeenea kwamba alikuwa na nia ya kugombea kupia ama ACT – Wazalendo au CCM.
Alisema amekuwa akishangazwa na kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya wanachana na wapenzi wa Chadema kuwa hajafanya lolote kwenye chama hicho.
Alisema kama kuna mtu anayekifahamu vizuri chama hicho ni yeye, hivyo haoni sababu za watu kumbeza.
Alisema alikuwa ameamua kukaa kimya na kuwa akiamua ‘atamwaga mboga’ ili watu wafahamu upungufu ulioko ndani ya chama hicho.
Alisema hagombei katika jimbo hilo na kama kweli chama hicho kina nguvu, basi kilitetee, akisisitiza kuwa ana uhakika jimbo hilo litakwenda CCM kwa kuwa wananchi wa Mpanda Mjini walikuwa na mapenzi na mtu siyo chama.
Arfi aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema kabla kujiuzulu wadhifa huo, aliwahi kuhusishwa kusuka mpango wa kumwezesha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kupita bila kupingwa katika kinyang’anyiro uchaguzi wa mwaka 2010 katika Jimbo la Katavi kwa kuwashawishi baadhi ya wagombea kuondoka majina yao.
Hata hivyo, Arfi amekuwa akikanusha tuhuma hizo, hali ambayo pia ilisababisha kutokuelewana na baadhi ya viongozi wenzake na kusababisha kujiuzulu nafasi yake ya umakamu mwenyekiti.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walionyesha kushtushwa na kauli ya mbunge huyo kujiondoa Chadema lakini wakasema ametimiza haki yake ya kikatiba kuchagua sehemu iliyo sahihi kwake.
Mmoja wa wananchi hao, Abdallah Hussein alisema: “Arfi amekuwa mvumilivu sana ndani ya Chadema lakini anayo ya moyoni sasa kwa muda mrefu amekaa kimya aliogopa ya Zitto Kabwe yasimtokee, sasa ameweka bayana msimamo wake acha tuheshimu mawazo yake.”

Kikwete: Msimchague huyu

Rais Jakaya Kikwete  

Tanga. Rais Jakaya Kikwete amewataka viongozi wa dini nchini kuwahimiza waumini wao kuwachagua wanasiasa wasiokuwa waovu, wasiofanana na uovu au hata kuukaribia.
Amewataka kuepuka makundi ya kisiasa na wasiwape mwanya wanasiasa wenye dhamira ovu katika kutafuta madaraka kwa thamani yoyote na wawakemee wale wanaotaka kupata madaraka kwa gharama yoyote.
Alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 125 tangu kuingia kwa injili katika ukanda wa Pwani ya Tanga na Milima ya Usambara uliofanyika katika Viwanja vya Mbuyukenda jijini hapa.
“Wanasiasa wanaotaka madaraka kwa njia yoyote ile, muwanyanyapae, wakatalieni kwa macho makavu, hawa si watu wema watatufikisha pabaya,” alisema Rais Kikwete.
Alisema hayo baada ya Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dk Stephen Munga kumweleza kwamba akiwa mkuu wa nchi anao wajibu wa kuhakikisha Taifa linavuka kwa amani na usalama katika kipindi hiki kigumu cha uchaguzi.
Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alisema katika kipindi hiki, viongozi wa madhehebu ya dini wasijiingize katika makundi ya wanasiasa kwa sababu mambo yakiharibika itakuwa hakuna pa kukimbilia.
Aliwataka viongozi wa dini watumie nyumba za ibada kuliombea Taifa livuke salama katika kipindi hiki kigumu badala ya kuwapangia vyama au viongozi wa kuwachagua.
“Tunawategemea kuwahimiza na kuwakumbusha kutumia haki na wajibu wao vizuri, muwahimize na kuwakumbusha kuwa watatakiwa kufanya mambo matatu muhimu; Kwanza, kujiandikisha, pili, kujitokeza kwenda kupiga kura na tatu kuchagua viongozi wazuri, wasiokuwa waovu, wasiofanana na uovu na kuukaribia uovu, watakaosukuma mbele gurudumu la maendeleo na kujali masilahi mapana ya jamii husika na nchi yetu.”
“Viongozi wa dini muwe kama mimi, nina wagombea wa urais 42, kama nitaonyesha kuwa upande wa mgombea yeyote kati yao, basi nitakuwa nimeharibu mchakato mzima wa uchaguzi.
“Tusiwape mwanya wanasiasa wenye dhamira ovu kuwafarakanisha Watanzania. Tuendelee kukemea matumizi mabaya ya fedha, rushwa, hila, ghiliba na hujuma katika uchaguzi. Tunapaswa kufanya hivyo tena zaidi sasa, wakati wa michakato ya ndani ya vyama vya siasa na baadaye wakati wa uchaguzi,” alisema.
Alisema hiki ni kipindi nyeti na kwamba, viongozi wa dini pamoja na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kufahamu kuwa Tanzania haina kinga ya milele ya amani na utulivu, kama itavurugwa haitakuwa lulu ya Afrika tena kama ilivyo sifa yake.
“Tuwakemee wanasiasa wapenda madaraka kwa gharama yoyote, ambao watataka kutumia fedha kununua ushindi au ubaguzi wa rangi, kabila, dini na kadhalika, kuwabagua wapinzani wao na kujijenga kisiasa. Nawaomba msiwasikilize wala kuwaendekeza kwani mchezo wao ni mauti yetu. Wakatalieni kwa macho makavu na kwa kweli muwanyanyapae,” alisema.

Rais Kikwete ambaye wiki hii atakuwa na kibarua cha kuongoza vikao vya kuwachuja wagombea kupitia CCM, alisema hawapaswi kukaa kimya dhidi ya watu wanaokiuka maadili na kuchochea mifarakano katika Taifa.
“Hawa si watu wema, watatufikisha pabaya. Hawaitakii mema nchi yetu. Kamwe tusiruhusu wachezee dini zetu ambazo ni mhimili muhimu sana wa amani yetu,” alisema.
Alisema tofauti na ukabila ambao pamoja na ubaya wake, unaweza kuhusisha eneo dogo, dini zinahusisha nchi nzima.
“Hakuna mtu, dini wala eneo litakalonusurika. Tutapoteza ile sifa yetu ya kihistoria ya kuwa lulu na mfano wa amani katika Afrika. Tusikubali kumchukiza Mungu akatukasirikia na kutuadhibu kwa jambo ambalo liko ndani ya uwezo wetu kulizuia lisitokee. Kwa kweli mambo yakiharibika, hatuwezi kumlaumu mtu mwingine yeyote, bali sisi wenyewe. Katu hatuwezi kusema ni mapenzi ya Mungu, bali itakuwa ni makosa yetu wenyewe.”
Aliwaomba viongozi wa dini: “Limeni mraba wenu vizuri nasi tulime wetu. Msiwape nafasi viongozi wa siasa na hata wa dini kutumia majukwaa ya dini kuendeleza masilahi yao ya kisiasa na hasa kupandikiza chuki katika jamii. Msiwe sehemu ya makundi ya wagombea au vyama vya siasa. Mnatakiwa msiwe na upande, muwe juu ya pande zote. Hapo ndipo mtakapofanya vizuri kazi yenu ya ulezi na kuponya Taifa iwapo kutatokea matatizo.”
Kauli ya askofu
Askofu Munga mbali na kueleza historia ya kuingia kwa injili katika eneo la Pwani ya Tanga na Milima ya Usambara, alisema kanisa hilo litaliombea Taifa livuke salama katika Uchaguzi Mkuu... “Tunakuahidi kukuombea wewe na nchi ivuke kwa amani na salama. Wewe kama mkuu wa nchi una mzigo mzito wa kuhakikisha unatuvusha vyema.”
Alisema kilele cha maadhimisho ya miaka 125 ya kuingia kwa Injili kitakuwa Julai 12, mwaka huu katika Kanisa la Makao Makuu ya Dayosisi mjini Lushoto na zaidi ya vijana 125 watatembea kuanzia Tanga hadi Lushoto kwa kupita njia ambazo Wamisionari walipitia kwa miguu wakati wakieneza injili.
Alisema katika kipindi cha miaka 125, KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki imeendesha huduma nyingi za kuisaidia jamii ikiwa ni wajibu wake wa kutobagua kwa itikadi za kidini wala rangi.

Saturday, July 4, 2015

WANACHAMA WAWILI WA CUF WAPIGWA RISASI ZANZIBAR




Muonekano wa wanachama hao wa CUF waliopigwa risasi.

Wanachama wawili wa CUF wamepigwa risasi na watu waliofunika nyuso zao mchana wa leo wakati wa kuandikisha kupiga kura Makunduchi, Zanzibar, wamelazwa Hospitali ya Arahma.

(CHANZO: ITV NA JAMII FORUMS)


Mayai ya kwale kama kikombe cha Babu, Serikali iko kimya

Miaka ya hivi karibuni kulikuwa na gumzo kubwa hapa nchini na hata nje ya nchi juu ya tiba ya kimaajabu maarufu kama ‘kikombe cha babu.’
Tiba hiyo ya kikombe ilikuwa ikitolewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapile kijijini Samunge Wilaya ya Loliondo. Taarifa za tiba hii zilienea kwa haraka nchi nzima hali iliyowafanya wananchi wengi kila kona kuelekeza macho, masikio na mioyo yao kwenye tiba hii.
Kutokana na uvumi wa maajabu ya kikombe cha Babu, baadhi ya watu walidiriki hata kuwatorosha wagonjwa wao hospitalini.
Wengine wakaacha matibabu na dozi walizopangiwa hospitali kwa magonjwa mbalimbali, yakiwemo yale sugu na kuamua kukimbilia kikombe cha babu kwa imani, kina uwezo zaidi.
Pia, ikumbukwe kwamba kikombe hakikuwa na tiba sahihi kwani hata Serikali kupitia Wizara ya Afya na taasisi zake zilishindwa kutoa uthibitisho wa kisayansi juu ya ukweli wa tiba ile. Hivi sasa kumeibuka tiba ya ‘mayai ya kwale’ ambayo inavuma kila kona na imekuwa gumzo kila mahali. Tiba hii ni ya kimaajabu kwani uvumi uliopo ni kwamba mayai ya kwale yana uwezo wa kutibu magonjwa yote sugu.
Kasi ya kushauri wagonjwa na hata wasio wagonjwa kutumia mayai haya badala ya kwenda hospitali kwa uchunguzi wa afya zao inaongezeka na maelekezo yanayopatikana mitaani juu ya kutumia tiba hii ni ya ajabu na yanatofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Nilishuhudia mtu mmoja akimwelekeza mgonjwa kuwa alipaswa kuyapasua mayai na kuyapondaponda pamoja na magamba yake na kisha ayanywe katika hali ya ubichi. Mwingine aliambiwa ayapasue na kisha ayakoroge pamoja na asali au maziwa kisha anywe, wengine wanaelekezwa kuyachemsha kama mayai ya kawaida na kisha kula kiini cha ndani. Uvumi huu unaenea kwa kasi mitaani.
Kutokana na kuvuma kwa tiba hii, mayai haya hivi sasa yanaonekana kusakwa kila mahali na yanauzwa kati ya Sh15,000 hadi 20,000 kwa trei.
Uvumi wa tiba hii hauna tofauti na ule uliozuka nchini juu tiba maarufu kama ‘kikombe cha Babu’. Watu wengi walikatisha matibabu kwenye hospitali mbalimbali na kuamua kwenda Kijiji cha Samunge kwenda kupata kikombe cha babu na kufanya kuwe na misururu mirefu ya watu waliokesha usiku na mchana. Hii ilizusha adha kubwa hasa kutokana na kutokuwepo na maandalizi ya vyoo hivyo watu kujisaidia ovyo vichakani.
Adha ya safari ndefu na kukaa kwenye foleni kwa zaidi ya siku tatu, kulifanya wenye afya mbaya kushindwa kuhimili na hata kupoteza maisha.
Katika mazingira haya ya kuibuka tiba za ajabuajabu ambazo hazijathibitishwa kitaalamu, ni vyema Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ikatoa ufafanuzi.
Isisubiri hadi watu wapoteze maisha halafu ndiyo ianze kuja na maelekezo tena yanayopingana na yale ambayo jamii inaamini. Kuchelewa kunafanya wengi wapoteze fedha na hata kuacha tiba sahihi na kukimbilia kitu ambacho kinavumishwa tu.
Serikali haipaswi kukaa kimya wakati watu wakiendelea kutibiana kwa vitu ambavyo havijathibitishwa kitaalamu.

Kama Serikali ingechukua hatua mapema, watu wasingepoteza maisha kupitia kikombe cha babu.
Uvumi huu wa tiba ya mayai ya kwale hauna tofauti na Kikombe cha Babu.
Katika ulimwengu huu wa utandawazi na soko huria, ni kawaida kusikia mambo mapya yakiibuka kila kukicha, lakini kama mambo hayo yanagusa afya zetu, hatuna budi kuwa makini na waangalifu zaidi.

Unatumia Nokia XL na unapata shida kudownload Whatsaap? Ufumbuzi huu hapa.

kizuri kula na wenzako.
Nilipopata simu ya Nokia Xl baada ya ile ya aina ya Samsung niliyokua nikiitumia awali tena nikiwa nimeetumia ndani ya kipindi kifupi sana toka nilipoinunua ( kama miezi mitano hivi), nilichanganyikiwa sana hasa kwa kukumbuka pesa yangu niliyotoa kununua simu ile aina ya samsung iliyonizimikia ghafla kama mshumaa. Nilijuta nikaona bora ile hela ningenunulia walao mifuko ya simenti nikafanyia kitu cha maana.
Mungu si Athumani, nilidunduliza pesa nikafanikiwa kununua simu nyingine aina ya Nokia Xl. Sasa nilikuja kupata shida sana kupata application ya Whatasaap kwenye simu hii. Nilihangaika sana lakini hatimaye nikapata msamaria mwema ambaye naye anatumia Nokia Xl. Nilipomuuliza kama katika simu yake hiyo anatumia whatsaap, alinijibu ndio. Nikapatwa na shauku ya kujua alifanyaje maana mie nilihangaika mno na kushirikisha wadau kadhaa ikiwepo na kugugle lkn ilinishindikana. Alinipa jibu rahisi sana, kwamba download kitu kitu kinachoitwa 1 Mobile Market kisha download whatsaap kupitia application hiyo. Nilipojaribu, ndani ya dakika kumi tu, kitu cha whatsaap kikawa hewani. Nilichekeleaje. Si mnajua tena whatsaap ndio mpango mzima siku hizi. Kama simu haina whatsaap ya kazi gani? Maana siku hizi tukienda dukani kununua simu cha kwanza hua tunauliza hivi, "Eti kaka/dada, hii simu ina whatsaap?". Sasa unainunua halafu unafika nyumbani, whatsaap hamna. Weee!Unachanganyikiwaje. Tafadhali, jaribuni hii kitu then mkifanikiwa mrudi hapa kutoa ushuhuda.

Nawapedeni sana fans wangu.

Teddy Chacha.

Nyumba ya mwandishi wa Nyerere yauzwa kinyemela

 
 Nyumba ya Paul Sozigwa iliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam

Nyumba ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Mwalimu Julius Nyerere, Paul Sozigwa imeuzwa katika mazingira ya kutatanisha na mke wake Monica Kuga baada ya mwanahabari huyo kupata maradhi ya kupoteza kumbukumbu.
Kuga aliiuza  nyumba hiyo kwa Mahamood Duale kwa Sh600 milioni mwaka 2010, huku watoto wake wanne wa Sozigwa wakipinga uuzwaji huo wakidai kuwa baba yao aliwakabidhi nyumba hiyo mwaka 1998.
Mtoto wa mwisho wa Sozigwa ambaye pia ametajwa kama msimamizi wa mirathi, Moses alisema wana vielelezo vya wosia aliowaachia baba yao akiwa Finland kabla ya tatizo lake la kupoteza kumbukumbu halijawa kubwa.
“Tulirekodi kila kitu na ushahidi wa maandishi upo, baba alisema nyumba ile ni ya watoto na siyo yake wala ya mke wake. Lakini pia tulirekodi sauti yake, tunashangaa kwanini mama ameiuza,” alisema Moses.
Kwa maelezo ya wanafamilia hao, Kuga aliachana na Sozigwa mwaka 1974 na kufungua kesi ya kudai talaka mahakamani jambo ambalo baba yao alilipinga.
“Alitaka kuachana na baba tena sisi tukiwa wadogo ili wagawane mali, lakini baba hakukubali, tunashangaa iweje leo arudiane naye halafu auze nyumba?” alihoji Moses.
Moses alieleza kuwa mama yao alimchukua Sozigwa na kuishi naye kama kisingizio cha kujihalalishia  uuzwaji wa nyumba hiyo iliyopo maeneo ya Kurasini, karibu na shule ya Sekondari ya Jitegemee.
“Mama alimkana baba na wameachana kwa miaka zaidi ya 34 na aliidai talaka hadi mahakamani kwa nguvu, halafu baba alipoanza kuumwa anadai anataka kumlea kumbe ni ujanja wake  tu, alitaka kuuza eneo la familia,” alidai mtoto huyo.
Kwa mujibu wa wanafamilia hao, Kuga alighushi hati ya nyumba hiyo na kuiuza kwa Duale lakini baadaye aliwataka wampe hati halisi ili amkabidhi Duale.
Lakini baada ya kuona kuwa hawezi kuipata, kwa kushirikiana na Duale walianza kumsumbua Moses na hatimaye walimfungulia kesi mahakamani.
Hata hivyo, baada ya Duale kuzungumza na wakili wa familia ya Sozigwa, aliambiwa ukweli kuwa hiyo nyumba ina utata wa wanafamilia hali iliyomsababishia Duale mshtuko hadi kupooza.
“Huyu Duale alizungumza na wakili wetu, akaambiwa ukweli kuwa asinunue hiyo nyumba kwa kuwa haina hati na alipoonyeshwa hati halisi alishtuka na kupata kiharusi kwa sababu alikuwa ameshalipa fedha zote,” alisema Moses.

Akiendelea kusimulia, Moses alisema mauzo ya nyumba hiyo yana utata na kuna dalili ya rushwa kwani yameidhinishwa na baraza la ardhi la Wilaya ya Temeke ambalo kwa kawaida, lina haki ya kuidhinisha mauzo ya nyumba yenye thamani ya Sh50 milioni na chini ya hapo, wakati thamani halisi ya nyumba hiyo ni Sh900 milioni.
“Tunashangazwa na kitendo cha mama kuuza nyumba hiyo kwa Sh600 milioni wakati tathmini iliyofanywa mwaka 2010 ilionyesha kuwa ina thamani ya Sh900 milioni,” alisema Moses.
Moses ambaye alizungumza kwa niaba ya ndugu zake watatu, Salome, Irene na Ephata alisema licha ya mama yao kuuza nyumba kwa mamilioni ya fedha lakini alikataa kusaidia kutoa fedha za kumpeleka baba yao nchini Finland kwa matibabu. “Ilitubidi kutembeza bakuli hadi kwa Rais Jakaya Kikwete ili tupate msaada wa matibabu ya mzee,” alisema.
Mwananchi lilizungumza na Kuga ambaye alisema anawashangaa watoto wake kwa kushindwa kujua sheria zinavyofanya kazi na kuanza kumrushia tuhuma zisizo na ukweli kuwa ameuza nyumba kwa ujanja.
“Hii kesi imeenda mahakamani  hadi mahakama kuu na nimeshinda mara tatu, lakini hawa wanaona kuwa wao ndiyo wana haki ya nyumba ambayo mimi na baba yao tuliijenga, wanakata rufaa kila siku,” alisema. Alieleza pia sababu za kuishi na Sozigwa licha ya kuwa walitengana kwa zaidi ya miaka 34.
Alisema baada ya kuona hali ya mumewe huyo siyo ya kuridhisha aliamua kurejea kumtunza na siyo kwa ajili ya nyumba. “Nilimhurumia mzee nikaamua kuishi naye ili nimlee na ndiyo hapo tulipokubaliana naye tuiuze nyumba,” alisema.
Kuga ambaye aliwahi kugombea ubunge wa Temeke kwa tiketi ya DP mwaka 1995, alisema watoto wake hao walifikia hatua ya kuficha hati halisi ya nyumba hiyo ili kuzuia uuzwaji.
Lakini hata hivyo, Kuga alisema yeye na wakili wake walitoa matangazo kwenye magazeti kuwa hati hiyo imepotea ili kupata kibali kutengeneza hati mpya ili waweze kuiuza nyumba hiyo.
“Hali ya baba yao ni mbaya lakini naona na hawa watoto hali yao ni mbaya zaidi kwa sababu hawajui kitu wanachokifanya; nyumba ni yetu mimi na mzee wao kinawauma nini? Alihoji.
Kadhalika Kuga alisema mpaka sasa Duale tayari ana hati na ameshakuwa mmiliki kamili wa nyumba hiyo.

Chanzo: Mwananchi

Wanne wahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kumuua albino

Mbeya. Washtakiwa wanne kati ya watano wa kesi ya kumuua mtu mwenye ulemavu wa ngozi (albino) Henry Mwakajila mwaka 2008 wilayani Rungwe, wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa mjini hapa jana.
Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Nyanda za Juu Kusini aliwataja waliohukumiwa kuwa ni Hakimu Mwakalinga na Leonard Mwakisole wote wakazi wa Kijiji cha Kiwira wilayani Rungwe na Gerard Kalonge na Asangalwisye Kayuni wa Kijiji cha Mbembati wilayani Ileje.
Mshtakiwa aliyenusurika kwenye kesi hiyo ni Mawazo Figomole ambaye alikuwa mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo ambaye aliachiwa huru baada ya ushahidi kutojitosheleza dhidi yake.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda hiyo, Dk Mary Revila alisema mahakama imeridhika pasipo shaka na ushahidi ulitolewa dhidi ya washtakiwa hao na kwamba, wanastahili kunyongwa hadi kufa huku akisisitiza kwamba ushahidi kwa mshtakiwa namba nne haukujitosheleza.
Awali, ilielezwa mahakamani hapo kwamba Februari 5, mwaka 2008, washtakiwa hao walimteka marehemu Henry akiwa katika Shule ya Sekondari Ukukwe wilayani Rungwe na kwenda kumuua.
Ilielezwa kwamba Mshtakiwa Kayuni ambaye ni mganga wa jadi maarufu kwa jina la Katiti alikutwa na utumbo uliodaiwa kuwa wa binadamu na hatimaye Mkemia Mkuu wa Serikali alithibitisha kwamba ulikuwa wa marehemu Henry.
Ilifafanuliwa kwamba mshtakiwa Kalonge alikutwa na vidole vinne na mifupa 10 iliyodaiwa kuwa ya binadamu na baadaye Mkemia Mkuu wa Serikali kuthibitisha kuwa ilikuwa ya marehemu Henry.

Chanzo: Mwananchi

Friday, July 3, 2015

Vurugu za Bungeni!! WABUNGE WATANO WAMEPEWA ADHABU YA KUTOINGIA BUNGENI,YUMO TUNDU LISSU,JOHN MNYIKA.....





Wabunge watano wamepewa adhabu ya kutokuhudhuria vikao vya mkutano wa 20 wa bunge, kwa madai ya kukiuka kanuni za bunge na kusababisha vurugu hali iliyopelekea spika wa bunge kuahirisha bunge. 

Adhabu hiyo imetolewa na kamati ya haki maadili na madaraka ya bunge ambapo waliosimamishwa ni Mh Tundu Lissu, Mh John Mnyika, Moses Machali, Pauline Gekul na Mh Felix Mkosamali ambao hawataweza kuhudhuria vikao vya bunge hili hadi litakapovunjwa na wabunge wengine wawili Mh Peter Msigwa na Mh Rajab Mbarouck Mohamed wamezuiliwa kuingia vikao viwili vya bunge ambapo akisoma maamuzi hayo mjumbe wa kamati hiyo Mh Hassan Ngwilizi amesema. 

Vurugu hizo zilitokea wakati waziri wa nishati na madini Mh Simba Chawene akiwasilisha muswada wa sheria ya petroli bungeni mjini Dodoma ambapo wabunge wa upinzani walianza kuomba muongozo wa spika huku Mh Chawene akiendelea kusoma muswada huo lakini baada ya muda alishindwa kuendelea baada ya kuzidiwa na kelele za wabunge hao hali iliyosababisha spika wa bunge Mh Anne Makinda kuahirisha bunge. 

Mara baada ya kikao cha bunge kuahirishwa nje ya ukumbi wa bunge mbunge wa Ubungo Mh John Mnyika akazungumzia suala hilo kwa niaba ya wabunge wa kambi ya upinzani bungeni ambapo amesema kambi ya upinzania haiko tayari kuua ndoto za watanzania za kuondokana na umaskini kwa kutumia rasilimali zao na hapa anafafanua zaidi sababu za wao kupinga miswada hiyo. 

Waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu na bunge Mh Jenista Mhagama amekanusha madai ya miswada hiyo kujadiliwa kwa siku moja na kudai kuwa ingeweza kujadiliwa hadi pale ambapo wabunge wangefikia muafaka na kuongeza kuwa ndiyo maana serikali iliamua isomwe mwishoni baada ya miswada mingine yote kujadiliwa.

Thursday, June 25, 2015

MKULIMA ATUMIA MABASI YA ABIRIA KUSAKA WADHAMINI

Dar/Mikoani. Kada wa CCM, Elidephonce Bilohe (43), mkulima anayeomba kupitishwa na chama chake kuwania urais, amesema anatumia usafiri wa mabasi ya umma kuzunguka mikoani kusaka wadhamini.
Wakati Bilohe akitumia usafiri huo, wagombea wenzake wanatumia au walitumia mabasi waliyokodi na kuyafanyia maboresho ndani, magari madogo na ndege kutafuta wadhamini 450 kutoka mikoa 15 inayotakiwa kwa mujibu wa taratibu za CCM.
Akizungumza na Mwananchi jana, Bilole alisema ameshafika mikoa tisa ambayo ni Dodoma, Kigoma, Geita, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Tabora, Morogoro na Dar es Salaam, tangu alipochukua fomu hiyo Juni 9.
“Huko kote nimekuwa nikienda kwa kutumia usafiri wa mabasi ya abiria na daladala. Kwa kweli nimepata ushirikiano mzuri kutoka kwa makatibu wa CCM, nawashukuru sana,” alisema.
Bilohe alisema atakwenda mikoa 15 tu kama inavyotakiwa na chama chake, tofauti na watiania wengine ambao baadhi wamekwenda zaidi ya mikoa 20.
“Kwenda mkoa mmoja natumia siku mbili ama tatu kufika na kupata wadhamini. Gharama ni nyingi sana, lakini kwa kuwa nimeshaamua kuwatumikia Watanzania nitakwenda,”alisema.
Alisema Watanzania wamekuwa wakimtia matumaini katika safari yake hiyo na kuwaomba wamuombee ili aweze kuifanikisha kwa mafanikio.
“Naomba Watanzania wenzangu mniombee katika safari hii. Nitawavusha kuwapeleka kwenye nchi ya ahadi,” alisema Bilohe aliyejiunga na chama hicho mwaka 2003.
Alisema kuwa atazirudisha fomu hizo Juni 30 au Julai Mosi kulingana na ratiba yake ya kukusanya wadhamini.
Jumla ya makada 39 wamejitokeza kuwania nafasi hiyo na Bilohe ndiye mgombea pekee aliye na elimu ndogo ya darasa la saba, tofauti na sheria ya nchi inayotaka mgombea wa nafasi hiyo ya juu kisiasa awe na shahada.
Bilohe ni mmoja wa makada wachache waliojitokeza kuomba ridhaa ya CCM ambao hawajawahi kushika madaraka makubwa serikalini au ya kisiasa.
Katika kinyang’anyiro hicho kuna mawaziri wakuu watatu, mawaziri 12 wa sasa, Jaji Mkuu mstaafu, maofisa wa juu wa Idara ya Usalama wa Taifa, maofisa waandamizi wa Serikali ambao wamestaafu na wabunge.
Mkoani Pwani, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe amesema kiongozi anayetaka kuwa rais mwaka huu ni lazima alingane kiuadilifu na viongozi wanne wa urais waliotangulia kuiongoza Tanzania kwani hao wote hawakujilimbikizia mali na wanachukia ubadhirifu, rushwa na ufisadi.
Membe alirejea kauli yake kuwa ana sifa zote za kumrithi Rais Jakaya Kikwete na hivyo ameitaka Kamati Kuu kutolikata jina lake ili Tanzania isonge mbele kiuchumi na kiutamaduni.
Membe alipata wadhamini 21,000 na kusema kuwa mkoa huo umevunja rekodi kwa kutoa idadi hiyo ikilinganishwa na mikoa 26 aliyokwishapita.
Waziri huyo alisema akipata urais tu, utakuwa mwisho wa mauaji ya watu wenye ulemevu wa ngozi na kwamba ataanza kumsaka muuaji wa kwanza wa albino na akimkamata tu utakuwa mwisho wa tabia hiyo kwa wengine.
Kadhalika, Membe alisema endapo CCM itampitisha na kuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao na kushinda, jambo la kwanza ni kufufua viwanda na kujenga vipya ili kuweza kuzalisha ajira za kutosha.
Alisema atakuwa mkali katika kukataza viongozi kujihusisha katika ulaji rushwa huku akibainisha baadhi ya vipaumbele kuwa ni utawala bora na uchumi wa viwanda.
Akizungumza na wakazi wa Manispaa ya Morogoro mtaa wa Makongoro mjini hapa mara baada ya kukabidhiwa fomu za wadhamini 950, Membe alisema kuwa Kamati Kuu ya CCM haitakuwa imefanya makosa wala kujuta endapo itamteua kupeperusha bendera ya chama hicho, akiwa na lengo kuu kuzalisha ajira kwa vijana kwa kufufua viwanda vilivyokufa sambamba na kujenga vipya.
Lowassa avunja rekodi
Mkoani Arusha, Edward Lowasa ameendelea kuvunja rekodi ya idadi ya watu wanaojitokeza kumdhamnini baada ya kupata wadhamini 120,392 jana.
Rekodi hiyo ya Arusha imezipiku ile iliyowekwa na mkoa ya Iringa alikodhaminiwa na wanachama 58,562.
Mbunge huyo wa Monduli aliwasili jijini Arusha saa 9:00 alasiri na kupokelewa kwa mbwembwe zilizoambatana na nyimbo mbalimbali za wasanii kadhaa nchini. Lowassa aliongozana na mkewe Regina na viongozi kadhaa wa CCM.
Mara baada ya kuwasili uwanjani hapo, Lowassa alifanyiwa maombi rasmi na wazee wa kimila wa jamii ya Wamaasai, maarufu kama Malwaigwana.
Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha, Isaack Joseph alisema waliomdhamini waziri huyo mkuu wa zamani ni wanachama hai kutoka wilaya zote saba za kichama mkoani Arusha.
Kwa CCM, mkoa wa Arusha una wilaya za Arusha Mjini, Karatu, Longido, Monduli, Ngorongoro, Arumeru Mashariki na Arumeru Magharibi.
Marupu adhaminiwa na wanafunzi
Katika hatua nyingine, mgombea mwingine, Maliki Marupu amesema amelazimika kutumia mkoa maalumu wa vyuo vikuu kupata wadhamini ili kukwepa changamoto ya fedha za kuzunguka katika mikoa mbalimbali.
Marupu ambaye ni mwanafunzi wa shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu Mzumbe alilieleza Mwananchi jana kuwa anatarajia kukamilisha idadi ya wadhamini 450 kwenye Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro.
Alipoulizwa kama haoni kuwa kwa kutumia mkoa huo wa vyuo vikuu pekee atakuwa amekosa sifa kwa kushindwa kutembelea mikoa mingine 14 zaidi inayotakiwa, Marupu alisema hata hao wanafunzi wanaunda mkoa wa vyuo vikuu kuna mikoa yanayotoka, hivyo haoni shida kumdhamini.
Marupu, mwenye umri wa miaka 34, alisema endapo angefuata mikoa ya kijiografia ingekuwa shida kwake kutokana na kukosa fedha.
Alisema katika mzunguko wake alipata changamoto za watu walioko katika ofisi za wilaya wakisubiri kudhamini wagombea kwa malipo ya Sh20,000 au 30,000, hivyo akaamua kuwakwepa na kudhaminiwa na wanafunzi wenzake.
Mwanafunzi huyo alisema licha ya kukamilisha idadi ya wadhamini, atakwenda nyumbani kwao Ukerewe kutafuta baraka za wazee kabla ya kuwasilisha fomu zake Dodoma.
Makada nane warejesha fomu
Jumla ya makada wanane wamerudisha fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais, huku Boniface Ndengo akisema amekumbana na tatizo la kuombwa fedha na wanachama kwa ajili ya wamdhamini.
Wengine waliorejesha fomu jana ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani.
Akizungumza mjini hapa mara baada ya kurejesha fomu hizo, Ndonge alisema katika mchakato wa kukusanya wadhamini amebaini wananchi wa kawaida nao ni zao la rushwa. “Unafika mahali wananchi wanakataa kukudhamini kwa sababu hauna pesa ya kuwapa. Mimi niliwaambia sina fedha ila ninataka kuwatumikia. Waliniambia mbona fulani katoa kiasi fulani wewe hutoi,”alisema.
Alilalamikia makada wenzie waliochukua fomu kuandikwa mara nyingi katika vyombo vya habari na wengine kutopewa nafasi.
Ndonge alisema alifanikiwa kupata wadhamini 602 katika mikoa 20 aliyoenda.
Katika hatua nyingine, Waziri Chikawe aliwaomba msamaha waandishi wa habari kuwa hataweza kuzungumza nao kutokana na kukimbilia majukumu mengine.
Kwa mujibu wa ratiba ya chama hicho mwisho wa kuchukua fomu na kurudisha ni Julai 2 saa 10:00 jioni. Kazi hiyo ilianza Juni 3.
Wazee wa CCM bado
Kufanyika kwa kikao cha Baraza la Ushauri wa Wazee wa CCM kunasubiri uwepo wa wajumbe wake muhimu ambao kwa sasa wako safarini.
Kikao cha wazee hao ndio kitakuwa msingi wa uamuzi wa Kamati Kuu kuwapata wanachama watano ambao majina yao yatapelekwa kupigiwa kura na Halmshauri Kuu na Mkutano Mkuu wa CCM.
Kikao hicho cha Baraza la Usahauri linaloundwa na wenyeviti na makamu wenyeviti wastaafu wa CCM kipo chini ya uenyekiti wa Ali Hassan Mwinyi, ambaye aliongoza Serikali ya Awamu ya Pili, huku katibu wake akiwa Pius Msekwa.
Wengine wanaounda baraza hilo linalotambuliwa na katiba ya CCM ni Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk Salmin Amour, Rais msataafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, Makamu Mwenyekiti wa CCM mstaafu, John Malecela na Amani Abeid Karume ambaye ni Rais mstaafu wa Zanzibar.
Katika mahojiano na gazeti hili jana kuhusu mkutano wao, Msekwa alisema: “Kikao hakijafanyika, wazee wapo safarini. Wengine wapo huko, wengine kule, mimi nipo Dodoma, nitarejea Dar es Salaam baada ya vikao vya Bunge kumalizika.Alipotakiwa kueleza kama kwa mazingira hayo kikao hicho kitafanyika lini, Msekwa alisema: “Kikao kitafanyika tu, kipo kwenye ratiba. Watu wenye busara husubiri ratiba ikamilike, iko ratiba nasi tunafuata ratiba.”

BREAKING NEWZZZ: DOGO JEMBE ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS KUPITIA CCM

 Nimeamua kuchukua fomu ya kugombea urais wa Tanzania. Karibu uwe sehemu ya kampeni yangu, kuhakikisha nchi yetu inapata kiongozi ambaye anaelewa changamoto za Watanzania, na yuko tayari kushirikiana nao kuzitatua.

Rais Kikwete Awashangaa Wanasiasa Wanaokosoa Kitendo cha Serikali Yake Kukopa Fedha Nje


RAIS Jakaya Kikwete amewashangaa wanasiasa wanaokosoa kitendo cha Serikali yake kukopa fedha nje ya nchi kuwa kinazidisha deni la taifa, kwamba hawana ufahamu na kufafanua kuwa katika kuharakisha maendeleo ya nchi, kukopa ni jambo la kawaida.
 
Alisema hata mataifa makubwa yaliyopiga hatua kubwa kwenye maendeleo yamekuwa yanakopa na akasisitiza kuwa uamuzi wa serikali kwenda nje kukopa amekuwa anaufanya ili kupata fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu ambayo itaifanya nchi ipige hatua kubwa kimaendeleo.
 
Alitoa mfano kuwa hata kama mtu anaeendesha duka ni lazima akakope benki kama anataka kuendeleza duka lake, kama hatafanya hivyo kwa kuamini kuwa fedha anazopata kwa kuuza bidhaa zitalitunisha duka hilo basi asubiri miujiza ya kumpatia faida.
 
Aliyasema hayo wakati akizungumzia uamuzi wa serikali yake kuwenda kukopa nje kwa ajili ya kujenga miundombinu mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa mkongo wa taifa ambao alisema lengo lake ni kuweka misingi ya miundombinu wakati taifa linapoelekea kwenye utekelezaji wa ujenzi wa viwanda vya kisasa.
 
Rais Kikwete alisema baada ya kufanya uamuzi huo aliamua pia kuwekeza kwenye utafiti kwa kuhakikisha kuwa Serikal inatenga fedha kwa ajili ya kuwasomesha watafiti, kununua vifaa vya utafiti na kukarabati vituo vya utafiti ambayo alisema vingi vilikuwa kwenye hali mbaya.
 
“Tulianza na Sh bilioni 10, tunashukuru sasa hivi tupo kwenye Sh bilioni 60 na naamini kuwa Rais atakayekuja ataendeleze juhudi hizi kwa kutenga fedha zaidi kwa ajili ya tafiti maana nikiangalia hali ya baadaye ya maendeleo ya nchi hii inategemea watafiti, wanasayansi na wabunifu,” alisema Rais Kikwete.
 
Rais alisema anajivuna kwamba anaondoka madarakani wakati shughuli za utafiti zimepata uhai na kwamba juhudi zilizofanywa na Serikali yake za kuwaendeleza wabunifu zimezaa matunda mengi kwani kwa sasa nchi ina watafiti wazee na vijana wanaofanya mambo makubwa yanayotambulika kimataifa.
 
Alisema fedha zilizotolewa na serikali yake zimesaidia kusomesha watafiti 517 katika kozi za shahada ya uzamili na uzamivu na vituo 20 vimekarabatiwa na miradi 70 ya utafiti imetekelezwa.
 
“Ndio maana nasema kiongozi anayekuja asipoliendeleza hili, mwambieni mzee unatuletea matatizo.”
 
Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk Hassan Mshinda alisema kongamano hilo la nne limewakusanya wanasayansi, watafiti, watunga sera na wabunifu mbalimbali.
 
Alisema mada 80 zitajadiliwa ikiwemo tafiti mbalimbali zilizofanywa na watafiti wa ndani, kujadiliana changamoto za kupeleka utafiti sokoni na upatikanaji wa teknolojia na jinsi ya kuhuisha sayansi asili na sayansi ya kisasa.
 
Dk Mshinda alimshukuru Rais Kikwete kwa kujali na kuwapa umuhimu watafiti kuliko miaka ya nyuma na akasema kuwa anaamini kuwa msingi uliowekwa utaendelezwa na awamu ijayo.
 
Alisema juhudi zilzofanyuwa na Rais Kikwete zimeungwa mkono na nchi za Sweden na Finland ambao nao sasa wameamua kutoa fedha kusaidia juhudi za serikali katika kufanya tafiti.

Malkia Elizabeth wa Uingereza atoa tuzo kwa vijana wawili wa Kitanzania

Malkia Elizabeth wa Uingereza jana alitoa tuzo ijulikanayo kama ‘The Queen’s Young Leader Award’ kwa vijana wawili wa Tanzania. Vijana hao ni Given Edward na Angela Benedicto Mnagoza
CIREv0ZW8AAv1zd
“Today I received a award from Queen Elizabeth II of United Kingdom. It was awesome and very inspiring,” ameandika Given kwenye ukurasa wake wa Facebook. “Before the awarding ceremony, I met with UK Prime Minister, Mr. David Cameron at 10 Downing Street I got a chance to visit Twitter offices and BBC and conduct and interview with BBC Swahili. After that we headed to Buckingham Palace where we received the award from Queen Elizabeth II and met various public figures. Dinner was at St.James Palace hosted by The Duke of York. The day as awesome1 — at Buckingham Palace.” Watu mbalimbali wamewapongeza watanzania hao kwenye mitandao ya kijamii. Chini ni maelezo kuhusu tuzo hiyo na sababu za vijana hao kupewa. The Queen’s Young Leader Award aims to recognise exceptional people aged 18­29, who are taking the lead in their communities and using their skills to transform lives. Winners of this prestigious Award will receive a unique package of training, mentoring and networking, including a one­week residential programme in the UK during which they will collect their Award from Her Majesty The Queen. 

With this support, Award winners will be expected to continue and develop the amazing work they are already doing in their communities. This year there were 1800 youth nominated for the award. The Advisory Panel shortlisted the names and another panel made of personnel from 3 partner organizations (The Royal Commonwealth Society, Comic Relief and The Queen Elizabeth Diamond Jubilee Trust) made final decisions and chose the winners. 60 youths have been awarded this award of which in Tanzania there are two Given Edward and Angela Mnagoza:­ 1) Given Edward He has been awarded for his leadership activities in Tanzania and for his project which provides a platform for students in Tanzania to discuss subjects online. You can view it at www.myelimu.com. He created it last year in February and up to now we have more than 700 students registered. 

It’s for students in O level and A level. He currently work at Tanzania Youth Vision Association as the Head of Research and Information, whom he has been working with for 4 years now. He also work with the Youth of United Nations in carrying out different activities and events. 

Past achievements have also been helpful. He was awarded the best delegate in Dar es Salaam Model United Nations Conference 2012; and last year he was among 200 youth selected across Africa to attend the Africa Model United Nations Conference in Addis Ababa, Ethiopia. 2. Angela Benedicto Mnagoza Following the death of her mother and her aunt, Angela worked in domestic service where

she was abused and exploited by her employer. She now promotes the rights of child domestic workers, educating this marginalised workforce and attempting to change attitudes towards them. 

WHAT WILL AN AWARD WINNER RECEIVE? Mentoring As a Queen’s Young Leader you will be allocated a mentor with relevant experience and expertise who will support you over the course of the year to continue and develop your work. Online learning Online learning will be provided with materials relevant to your area of interest, as well as serving as a place for you to meet and share experiences and knowledge with other Queen’s Young Leaders. 

One­week residential programme in the UK The Award winners will have the opportunity to meet with inspiring people and visit organisations in the UK that have expertise in areas such as media and communications, social action and advocacy. During this week, Awards will be presented by Her Majesty The Queen at Buckingham Palace.