LATEST POSTS

Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

Thursday, June 25, 2015

Rais Kikwete Awashangaa Wanasiasa Wanaokosoa Kitendo cha Serikali Yake Kukopa Fedha Nje


RAIS Jakaya Kikwete amewashangaa wanasiasa wanaokosoa kitendo cha Serikali yake kukopa fedha nje ya nchi kuwa kinazidisha deni la taifa, kwamba hawana ufahamu na kufafanua kuwa katika kuharakisha maendeleo ya nchi, kukopa ni jambo la kawaida.
 
Alisema hata mataifa makubwa yaliyopiga hatua kubwa kwenye maendeleo yamekuwa yanakopa na akasisitiza kuwa uamuzi wa serikali kwenda nje kukopa amekuwa anaufanya ili kupata fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu ambayo itaifanya nchi ipige hatua kubwa kimaendeleo.
 
Alitoa mfano kuwa hata kama mtu anaeendesha duka ni lazima akakope benki kama anataka kuendeleza duka lake, kama hatafanya hivyo kwa kuamini kuwa fedha anazopata kwa kuuza bidhaa zitalitunisha duka hilo basi asubiri miujiza ya kumpatia faida.
 
Aliyasema hayo wakati akizungumzia uamuzi wa serikali yake kuwenda kukopa nje kwa ajili ya kujenga miundombinu mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa mkongo wa taifa ambao alisema lengo lake ni kuweka misingi ya miundombinu wakati taifa linapoelekea kwenye utekelezaji wa ujenzi wa viwanda vya kisasa.
 
Rais Kikwete alisema baada ya kufanya uamuzi huo aliamua pia kuwekeza kwenye utafiti kwa kuhakikisha kuwa Serikal inatenga fedha kwa ajili ya kuwasomesha watafiti, kununua vifaa vya utafiti na kukarabati vituo vya utafiti ambayo alisema vingi vilikuwa kwenye hali mbaya.
 
“Tulianza na Sh bilioni 10, tunashukuru sasa hivi tupo kwenye Sh bilioni 60 na naamini kuwa Rais atakayekuja ataendeleze juhudi hizi kwa kutenga fedha zaidi kwa ajili ya tafiti maana nikiangalia hali ya baadaye ya maendeleo ya nchi hii inategemea watafiti, wanasayansi na wabunifu,” alisema Rais Kikwete.
 
Rais alisema anajivuna kwamba anaondoka madarakani wakati shughuli za utafiti zimepata uhai na kwamba juhudi zilizofanywa na Serikali yake za kuwaendeleza wabunifu zimezaa matunda mengi kwani kwa sasa nchi ina watafiti wazee na vijana wanaofanya mambo makubwa yanayotambulika kimataifa.
 
Alisema fedha zilizotolewa na serikali yake zimesaidia kusomesha watafiti 517 katika kozi za shahada ya uzamili na uzamivu na vituo 20 vimekarabatiwa na miradi 70 ya utafiti imetekelezwa.
 
“Ndio maana nasema kiongozi anayekuja asipoliendeleza hili, mwambieni mzee unatuletea matatizo.”
 
Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk Hassan Mshinda alisema kongamano hilo la nne limewakusanya wanasayansi, watafiti, watunga sera na wabunifu mbalimbali.
 
Alisema mada 80 zitajadiliwa ikiwemo tafiti mbalimbali zilizofanywa na watafiti wa ndani, kujadiliana changamoto za kupeleka utafiti sokoni na upatikanaji wa teknolojia na jinsi ya kuhuisha sayansi asili na sayansi ya kisasa.
 
Dk Mshinda alimshukuru Rais Kikwete kwa kujali na kuwapa umuhimu watafiti kuliko miaka ya nyuma na akasema kuwa anaamini kuwa msingi uliowekwa utaendelezwa na awamu ijayo.
 
Alisema juhudi zilzofanyuwa na Rais Kikwete zimeungwa mkono na nchi za Sweden na Finland ambao nao sasa wameamua kutoa fedha kusaidia juhudi za serikali katika kufanya tafiti.

Saturday, June 20, 2015

Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wanaongoza kwa utoaji wa mimba kwa njia za kienyeji

Moses Mongo ambaye ni Mratibu wa Kanda ya Ziwa kutoka Taasisi ya Umoja wa Mataifa (UNA-TANZANIA) amesema wanafunzi wa Vyuo Vikuu wanaongoza kwa utoaji wa mimba kwa njia za kienyeji kwa kutumia mwarobaini na bluu ya kuweka kwenye nguo nyeupe.

Mongo alisema katika utafiti walioufanya mwaka 2014 katika Vyuo Vikuu vinne Kanda ya Ziwa wamebaini wanafunzi kutoa mimba kienyeji.

“Utafiti tuliofanya 2014 kwa kuzungumza na wanafunzi kila Chuo au Shule tumebaini wapo wanafunzi waliotoa mimba na wapo waliofariki kwa kutoa mimba lakini kwa kificho”—Moses Mongo.

Mongo alisema katika mazungumzo na wanafunzi hao walieleza kuwa suala la utoaji wa mimba ni la kawaida na matumizi ya kondomu huwa ni pale wanapoanza uhusiano kabla ya kuzoeana.

Askari Azua Taharuki baada ya kufyatua risasi hewani Mahakamani Sumbawanga


TAHARUKI imeibuka katika majengo ya Mahakama ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa na kusababisha shughuli za mahakamani hapo, zikiwemo za kusikilizwa mashauri mbalimbali kusimama kwa muda wa takribani dakika 20.
 
Mtafaruku huo ulitokea baada ya askari kupiga risasi hewani mahakamani hapo wakati wakimsaka mahabusu aliyedaiwa kutoroka katika chumba cha mahabusu mahakamani hapo na kujificha darini.
 
Mwandishi wetu alishuhudia askari polisi wakiwa na bunduki mikononi wakihaha kumsaka mahabusu huyo ambaye alidaiwa kutoroka kupitia upenyo uliopo katika chumba cha mahabusi mahakamani hapo.
 
Mkasa huo ulianzia saa 5 asubuhi na kudumu kwa dakika 20. Hata hivyo, mahabusu huyo hakuweza kuonekana licha ya jitihada za baadhi ya polisi kupanda darini kupitia chumba cha mahakama namba mbili bila ya mafanikio.
 
Hekaheka za kumsaka mahabusu huyo zilianza pale baadhi ya watumishi wa mahakamani hapo na mahakimu kudai kusikia vishindo kwenye dari ambapo mara moja mahabusu waliokuwa kwenye chumba mahakamani hapo walihesabiwa.
 
Katika chumba hicho walitakiwa wawe mahabusu 10 lakini walipohesabiwa kwa mara ya kwanza ilibainika kuwa alikuwa amekosekana mmoja ndipo msako mkali ulipoanza huku askari wakihaha kumsaka darini.
 
Hata hivyo walipohesabiwa mara ya pili ilibainika kuwa hesabu yao ilikuwa imetimu kwamba walikuwa 10 lakini haikubainika nani miongoni mwao alikuwa ametoroka. Hata mahabusu wenyewe hawakuwa tayari kumtaja.
 
Habari za kuaminika kutoka mahakamani hapo zinaeleza kuwa baada ya watumishi wa mahakama hiyo wakiwemo askari polisi na mahakama kusikia vishindo vya miguu darini waliamini ilikuwa ni ya mahabusu anayedaiwa kutoroka katika mazingira ya kutatanisha siku tatu zilizopita

Friday, June 19, 2015

MAKONDA KUONYESHA AJIRA KATIKA MICHEZO LEO




MH: PAUL MAKONDA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI,
Anawaomba Wanakinondoni wote na wakazi wa DSM katika kuandaa maandalizi ya Team za Wilaya ya Kinondoni zitakazo kuwa na wachezaji watakao lipwa mshahara; katika:
1.Mpira wa miguu
(Football).
2.Netball.
3.Basketball.
Kushirikiana nae katika uzinduzi wa ligi hizo leo jumamosi, saa moja asubuhi Viwanja vya Leaders.
Ambapo  atazikabidhi Team 138 vifaa vya michezo.
SET 2  ZA JEZZY NA MIPIRA 2 KWA KILA TEAM.
WATAKUWAPO WATAALAMU WAKUPIMA AFYA ZA WACHEZAJI NA WATU WENGINE, KUTAKUWA PIA NA ZOEZI LA KUCHANGIA DAMU KWA ATAKAE PENDA.
TEAM ZOTE ZIKISHACHEZA KWA PAMOJA BAADAE WASHINDI  WATAUNDA  TEAM ZA WILAYA....
KWA MAELEZO ZAIDI FIKA VIWANJA VYA LEADERS MAPEMA leo(JMOS TAR 20 JUNE/2015) .
KIPAJI CHAKO AJIRA YAKO....
AJIRA SI BOMU.BOMU NI KUTOTUMIA KIPAJI CHAKO.
SERIKALI HAZIWEZI KUAJIRI WATU WOTE KATIKA AJIRA ZA OFISINI.
AJIRA INAJUMUISHA KUAJIRIWA NA KUJIAJIRI.NJOONI TUJIAJIRI TUPUNGUZE UGUMU WA MAISHA.
INAWEZEKANA...TUTIMIZE WAJIBU