Mmoja
wa washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents akihojiwa na Msanii
Joti mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu hapo kesho huku
mjukuu wake pia akifanikiwa kuingia hatua hiyo pia.
Washiriki
wa Shindano la kusaka vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama
Tanzania Movie Talents wakiwa kwenye mazoezi wakati walipokabidhiwa
muswada (script) kwaajili ya kuifanyia mazoezi na kwenda kuonyesha uwezo
wao kwa majaji.
Msanii
wa Vichekesho Joti akihojiana na Mmoja wa washiriki wa shindano la
Tanzania Movie Talents mara baada ya kutoka kwa majaji, shindano
limeingia hatua ya pili leo kwa kuchagua washiriki 30 ambao watatafutwa
washiriki 15 bora hapo kesho.
Mshiriki
namba 00554 akihojiwa na msanii Joti mara baada ya kufanikiwa kuingia
hatua ya tatu hapo kesho ambapo watapatikana washindi kumi na tano bora
na hatimaye kupata washindi watatu bora wa kanda ya kati ambapo kila
mmoja atajinyakulia kitita cha shilingi laki tano za kitanzania
Baadhi
ya washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents wakibadilishana
mawazo mara baada ya kupatikana kwa washiriki 30 ambao wataendelea na
mashindano hapo kesho kwaajili ya kupata washiriki 15 bora.
Mmoja
wa washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents akiwa amenyongonyea
mara baada ya safari yake katika mashindano kuishia leo kutokana na
kukosa nafasi ya kuingia katika hatua ya tatu hapo kesho.Picha na
Josephat Lukaza wa Proin Promotions – Dodoma
Washiriki
wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni babu na mjukuu wake
kiuhalisia wakipongezana mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu
ya kutafuta washiriki 15 bora na hatimaye kupatikana washindi watatu
bora wa kanda ya kati ambapo kila mmoja ataondoka na kitita cha shilingi
laki tano za kitanzania.
……………………………………………………………………………..
Leo
Shindano la Tanzania Movie Talents limeingia ya hatua ya pili ya mchujo
ambapo washiriki 30 wameweza kupatikana kwaajili ya kuendelea na
shindano hilo hapo kesho ambapo washiriki 15 ndio watachukuliwa kwaajili
ya kuendelea na mashindano hayo na hatimaye kupatika washindi watatu
bora ambao watawakilisha kanda ya Kati na kwa kila mshindi mmoja kuibuka
na kitita cha shilingi laki tano (500,000/=).
Mpaka
sasa washiriki 30 wameshapatikana kwa kanda ya Kati na hatimaye kesho
washindi watatu watapatikana na kuiwakilisha kanda ya Kati katika
fainali kubwa itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na hatimaye mshindi
katika fainali hiyo kujinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50 za
kitanzania (50,000,000/=)
Katika
Washindi 30 waliopatikana leo, washiriki wawili wameweza kuonyesha
vipaji vyao huku washiriki hao wakiwa ni ndugu kabisa, washiriki hao ni
babu na mjukuu wake wa kike ambao wameweza kufanikiwa kuingia hatua ya
tatu kesho ambapo washindi wa Kanda ya Kati watapatikana.
Shindano
la Tanzania Movie Talents linatarajiwa kumalizika kesho Kanda ya Kati
Mkoani Dodoma na hatimaye kuhamia Kanda ya Juu Kusini ambapo usaili
utafanyika Mkoani Mbeya na usaili wa Kanda ya Juu Kusini utaanza tarehe
19 April 2014 saa 1 asubuhi na wakazi wa Kanda ya Juu Kusini wanaombwa
kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuonyesha vipaji vyao na kuweza kuitumia
fursa hii, Vilevile fomu za usaili zitapatikana Siku hiyohiyo ya usaili
na fomu hizo hazina gharama yoyote ile
0 comments:
Post a Comment