LATEST POSTS

Monday, December 9, 2013

MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU WA TANZANIA - BARA YAFANA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiambatana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakiwasili katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanzania Bara leo.…


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiambatana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakiwasili katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanzania Bara leo.
Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal akiwasili katika Uwanja wa Uhuru kwa maadhimisho ya sherehe za uhuru wa miaka 52 ya Tanzania Bara.
Rais Kikwete akiwa amesimama kikakamavu wakati Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Rais Jakaya Kikwete akikagua vikosi mbalimbali vya majeshi wakati wa maadhimisho hayo.
Mojawapo ya kikosi cha majeshi kikisubiri kukaguliwa na Mhe. Rais Kikwete.
Vikosi mbalimbali vya majeshi vikipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete kutoa heshima zao.
Rais Kikwete akichukua 'notes' wakati sherehe zikiendelea.
Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal (kushoto) akiwa na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amaan Karume.
Mama Salma Kikwete (kushoto) akibadilishana mawazo na Rais wa Zanzibar Dk. Mohammed Shein.
Rais Kikwete (kushoto) akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda.
Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa (katikati) akisalimianan na Rais Shein.
Rais Kikwete akihutubia wakati wa maadhimisho hayo.
Makundi mbalimbali ya vijana yakitoa burudanai ndani ya Uwanja wa Uhuru.
Picha ya Rais Shein iliyotengenezwa na vijana.
 
Wananchi wa Tanzania Bara (Tanganyika) leo wameadhimisha miaka 52 ya uhuru wake uliopatikana Desemba 9, 1961. Sherehe za maadhimisho hayo zimefanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam amabapo mgeni rasmi alikuwa Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Viongozi mbalimbali wamehudhuria sherehe hizo.

Chanzo: Global publishers




0 comments: