LATEST POSTS

Monday, December 9, 2013

PICHA 20 ZA MAANDAMANO YA KUMPINGA ZIARA YA DK.SLAA HUKO KIGOMA...WAKATI AKIWA KATIKA MKUTANO

KATIBU MKUU WA CHADEMA DK.WILLBOARD SLAA AMEWEZA KUKUTANA NA MAANDAMANO WAKATI AKIWA KATIKA ZIARA YAKE HUKO KIGOMA



HAPA ILIKUWA MWANZO WA MKUTANO WAKE WAKATI AKIWA ANAINGIA NA KUANZA ZIARA YAKE


NA HAYA NDO MABANGO YA ALIYOWEZA KUKUTANA NAYOO AKIWA MKUTANONI













































                             


BAADHI YA VIJANA WALIWEZA KUKAMATWA NA  POLISI AMBAO WALIFIKA HAPO KWA AJIRI YA KUFANYA VURUGU KATIKA MKUTANO WA DK.SLAA






HII NI BAADHI YA WANACHAMA WALIWEZA KUCHOMA KADI ZAO NA BENDERA YA CHAMA CHA CHADEMAA





HII NDO KIGOMA NA NA HAPA ENEO LA TUKIO BAADHI YA WATU WENGINE WAKIWA WANASHANGAA SITOFAHAMU YA LINALOENDELEAA  UWANJANI 


HUYU NDO MWANADADA ALIYENUSURIKA KUBAKWA BAADA YA KUKATISHA KARIAKOO AKIWA AMEVAA KIMINI





Mrembo aliyevaa kivazi cha ajabu kilichoacha wazi sehemu zake nyeti akisaidiwa na wasamaria wema baada ya kuvaa khanga.
MREMBO wa haja ambaye jina halikupatikana amenusurika kubakwa na wanaume baada ya kuvaa kivazi kilichoacha wazi sehemu kubwa ya maungo yake nyeti.


Mrembo huyo akizongwa na vijana wa Kariakoo.
  Tukio hilo lilijiri sehemu yenye mkusanyiko mkubwa, Kariakoo jijini Dar ambapo mrembo huyo alikuwa kwenye ‘shopping’ kwa ajili ya sikukuu ijayo ya Krismasi.




Akisaidiwa kuingia kwenye gari.
Likiwa linarandaranda maeneo hayo, Ijumaa Wikienda lilinasa laivu tukio hilo ambapo mrembo huyo alivuliwa nguo hadharani na kuacha ‘vitu’ njenje vikishuhudiwa hata na watoto waliokuwa wakimzomea.

Wanaume hao waliokuwa wakiongezeka na kuanza kumshika sehemu nyeti, walisababisha dada huyo kuanza kutoka nduki ambapo alizama kwenye duka moja kisha akasitiriwa kwa khanga na mama mmoja msamaria mwema.


Akiwa ndani ya gari.
Alipotoka bado wanaume waliendelea kumzingira ambapo ilimlazimu kutoa shilingi elfu hamsini kisha kurukia kwenye ‘kenta’ iliyomuondoa eneo hilo na haikujulikana alikoelekea kwa sababu gari hilo lilichomoka mbio huku akiwa amekoma ubishi wa kutembea nusu utupu.



Vijana wakilizonga gari alilopanda mrembo huo. maeneo ya kariakooo waliotaka kumfanyia kitu mbaya mrembo  huyu




source gumzo la jiji

Sunday, December 8, 2013

PATA UNDANI WA MAISHA YA NELSON MANDELA NA FAMILIA YAKE

Wakati Nelson Mandela anaongoza Afrika Kusini dhidi ya ubaguzi wa rangi na baadaye kuwa kiongozi maarufu duniani baada ya kutoka jela, inabidi tujiulize ni watu gani ambao walikuwa karibu naye kifamilia, kiroho na kuumia naye na waliomfahamu zaidi ya wote?

Mandela na mkewe Winnie wakiwa na mjukuu wao mara baada ya Mandela kutoka jela

Baba yake Mandela alimwacha akiwa na miaka tisa baada ya kufariki mwaka 1927, baadaye alilelewa na Chifu Jongintaba kabla ya kutoroka baada ya kutaka kuozwa akiwa bado mdogo.
Wakati anaanzisha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na kupigania usawa, ilikuwa dhahiri Mandela alihitaji kuwa na mwanamke mkakamavu na jasiri.
Mandela ameishi na wake watatu katika maisha yake – EvelynMase, Winnie Madikizela na wa mwisho, Graca Machel alimuoa akiwa anatimiza miaka 80.
Mandela amekuwa kipenzi kwa watoto na masuala ya elimu na kwa kudhihirisha hilo aliaanzisha Mfuko maalumu wa elimu kwa ajili ya watoto, ukiwa ni sehemu ya mafanikio katika maisha yake.
Nelson Mandela ni baba wa watoto sita, wanne akiwazaa kwenye ndoa ya kwanza na Evelynna wengine wawili kwa mkewe wa pili, Winnie.
Watoto wa Mandela wamepitia katika kipindi kigumu na wana kitu cha kipekee katika maisha yao, kwani kuna wengine ambao hawakupata kuonana na baba yao maisha yao yote, kwani alikuwa jela katika kipindi cha uhai wao.
Mabinti wa Mandela waliozaliwa kwa mke wa kwanza waliitwa Makazawie.  Mkubwa alikufa miezi tisa baada ya kuzaliwa na mwingine aliyemfuata ilibidi apewe heshima ya jina hilo kwa ajili ya dada yake.
Mwingine, Madiba Thembikile (Thembi) alikufa kwa ajali ya gari mwaka 1969 akiwa na miaka 25. Mandela alikuwa jela kipindi hicho na hakuruhusiwa kuhudhuria mazishi ya mwanawe.
Makgatho alikufa mwaka 2005 baada ya kuugua ugonjwa wa Ukimwi.
Ndio maana Nelson Mandela amekuwa mwanaharakati mkubwa wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo na alianzisha kampeni dhidi ya ugonjwa huo aliyoiita 46664 AIDS Campaign, jina likitokana na namba yake akiwa jela.
Mandela na Evelyn walidumu katika ndoa kwa miaka 13 na kuachana mwaka 1957. 
Waliachana kwa sababu mwanamke huyo alikuwa Shahidi wa Yehova na imani yao iliwataka wasishabikie masuala ya siasa. Mwanamke huyo alifariki dunia mwaka 2004.
Mwaka 1958 Mandela alimuoa Winnie Madikizela.  Ingawa sehemu kubwa ya muda wa ndoa yao aliutumia akiwa jela.
Winnie alikuwa mwanamke shupavu kwani naye alikuwa mwanasiasa machachari.
Walifanikiwa kuzaa mabinti wawili Zenani (Zeni) –aliyezaliwa mwaka 1958, na Zindziswa (Zindzi) – aliyezaliwa 1960.
Zeni aliolewa na mtoto wa mfalme, Prince Thumbumuzi Dlamini. Zindzi alijiandikia historia mwaka 1985 pale alipotoa hotuba ya kupinga baba yake kutolewa jela kwa masharti.
Kutokana na tofauti za kisiasa na za kibinafsi, Mandela na Winnie walilazimika kuachana mwaka 1994.  
Mwaka 1988 alipotimiza miaka 80 ya kuzaliwa, Mandela alimuoa Graca Machel (Mjane wa Rais wa Msumbiji, Marehemu Samora Machel ambaye aliyekufa kwenye ajali ya ndege inayodhaniwa ilitunguliwa na Makaburu mwaka 1989.
Nelson Mandela alikuwa akiishi katika nyumba yake iliyoko Qunu. Pamoja na kwamba ana nyumba nyingi sehemu mbalimbali duniani, lakini sehemu aliyoipenda ni kijijini kwao katika jimbo la Transkei.
Chanzo: Mwananchi

UYUI WAOMBA HALMASHAURI MBILI

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora wamepeleka mapendekezo ya kuigawa kuwa na halmashauri mbili.
Mapendekezo hayo yalifikiwa kwenye kikao cha baraza maalumu la madiwani kilichoketi makao makuu ya wilaya, Kata ya Isikizya.
Katika kikao hicho madiwani wote walichangia michango yao ambapo walishauri kwa kauli moja kuwa wilaya hiyo igawanywe na kuwa na halmashauri mbili za Tabora na Igalula.
Wakichangia kwenye mjadala huo walisema kugawanywa wilaya hiyo kuwa na halmashauri mbili ni faida kwa wananchi, hasa ikizingatiwa hali ya jiografia kwenye wilaya hiyo siyo nzuri.
“Agizo letu kama madiwani tunapeleka mapendekezo ya kuwa na halmashauri mbili za Igalula na Tabora. Hii itasaidia kusogeza huduma kwa wananchi wetu,” alisema mmoja wa madiwani hao.
Chanzo: Tanzania Daima

MARAIS KUINGIA KWA KADI, MAZISHI YA MANDELA


Qunu, nyumbani kwa MandelaTISHIO la vitendo vya kigaidi vinavyotokea kwenye maeneo mbalimbali hapa duniani, vimeifanya Serikali ya Afrika Kusini, kutoa kadi kwa marais na viongozi watakaohudhuria mazishi ya baba wa taifa hilo, Nelson Mandela.
Mandela aliyefariki Desemba 5, atazikwa Desemba 15 kijijini kwake Qunu, eneo alilolichagua kabla ya mauti yake.
Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya kimataifa, usalama katika miji ya Afrika Kusini, unatarajiwa kuimarishwa zaidi kuliko hata ule unaotumika kwa marais wa Marekani wanapofanya ziara kwenye mataifa mbalimbali.
Taarifa hizo zinabainisha kutokana na idadi kubwa ya watu kuhudhuria mazishi hayo, utawala wa nchi hiyo umebuni mbinu hiyo ya utoaji kadi kwa watu watakaokuwa eneo la maziko wakiamini itasaidia kuimarisha ulinzi.
Mazishi hayo yanatarajiwa kuvunja rekodi ambapo yanalinganishwa na yale ya Papa John Paul II mwaka 2005, ambayo yalihudhuriwa na wafalme watano, malkia sita wa falme mbalimbali na marais wapatao 70 na mawaziri kadhaa, wakiwamo wafuasi wake zaidi ya milioni mbili.
Ratiba ya kutoa heshma za mwisho yatangazwa
Chanzo: Tanzania Daima

Thursday, December 5, 2013

ELIMU YA MATUMIZI YA NISHATI MBADALA KUNUSURU MAZINGIRA

 
WANANCHI
 
 waishio maeneo ya Vijijini endapo watapata elimu kuhusu matumizi ya
 
 Nishati mbadala,watakuwa katika nafasi nzuri ya kutunza mazingira 
 
yanayoharibiwa kwa kasi kutokana na matumizi ya kuni katika kukaushia 
 
tumbaku na matumizi ya Nyumbani. 
 
Akifungua mafunzo kwa walimu wa Umeme Vijijini wa Vyuo vya Maendeleo ya 
 
Jamii,Mkuu wa Wilaya ya Uyui,Bi Lucy Mayenga katika Hotuba yake 
 
 
iliyosomwa na Katibu Tawala,Bw.Bibangamba John,ameeleza ni lazima elimu 
 
ya matumizi sahihi ya Nishati mbadala itolewe ili wananchi wasizidi 
 
mazingira. 
 
Ameeleza wananchi wanatumia sana kuni na kuharibu mazingira lakini 
 
matumizi ya Nishati mbadala yatawasaidia sana kuokoa na kutunza 
 
mazingira ambayo ni muhimu kwa ustawi wa maisha yao. 
 
Mayenga amesisitiza kwa wshiriki hao kuhakikisha kweli wanaipeleka elimu 
 
 hiyo kwa wananchi wengi waishio vijijini vinginevyo itakuwa ni kazi 
 
bure. 
 
Kwa upande wake Afisa Kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na 
 
watoto,Pius ligo,amesema Wakala wa Nishati Vijijini,REA, wanataka 
 
wananchi wasitumie Nishati inayoharibu mazingira. 
 
Amesema mafunzo hayo yanayotolewa kwa washiriki kutoka Mikoa Tisa Nchini 
 
 yatatumika kueneza elimu ya matumizi ya Nishati mbadala kwa wananchi wa 
 
Vijijini kupitia washiriki hao na hivyo kuleta ustawi wa maisha ya 
 
wengi 
 
Mafunzo hayo yanayochukua Wiki mbili yanayoendeshwa na wakala wa Nishati 
 
Vijijini,REA kwa kushirikiana na Wizara ya maendeleo ya 
 
Jamii,yatawapeleka washiriki kufunga Nishati katika zahanati ya Miyenze 
 
ambayo itakuwa ni sehemu ya mafunzo yao.
 
CHANZO: TABORA YETU

Monday, December 2, 2013

HAKIMU WA WILAYA ALIYESIMAMISHWA AKUTWA NA MAJALADA THELATHINI NYUMBANI KWAKE

ALIYEKUWA Hakimu Mkazi  wa Mahakama ya wilaya ya Urambo Mkoani Tabora Oscar Bulugu,  anayekabiliwa na tuhuma tatu za kuomba na kupokea Rushwa amejikuta matatani baada ya kukutwa akiwa na majalada ya Kesi zaidi ya Thelathini nyumbani kwake.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Tabora, Fidelis Kalungura, imeeleza kuwa Hakimu huyo alipekuliwa na Maafisa wa TAKUKURU na kukutwa na majalada yapatayo Thelathini na Moja ya kesi mbali mbali.
Kalungura aliongeza kuwa  TAKUKURU ilichukua jukumu la kufanya upekuzi nyumbani kwa Hakimu Bulugu baada ya wananchi kupeleka malalamiko ya mara kwa mara wakidai kutotendewa haki na Mahakama ya Wilaya ya Urambo.
Katika malalamiko yao wananchi wamekuwa wakidai kuwa wanapofika Mahakama ya Wilaya ya Urambo wanakosa huduma kwa  kuwa majalada ya kesi zao hayaonekani kwa makarani kwa vile  yapo kwa  Hakimu aliyesimamishwa.
Kufuatia malalamiko hayo  TAKUKURU iliamua kufanya uchunguzi  wa kina na baada ya kujiridhisha walienda kupekua nyumbani kwa Hakimu huyo na kukuta akiwa na majalada hayo
Mwezi Aprili mwaka huu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,(TAKUKURU),Mkoani hapa ilimkamata na  kumfikisha Mahakamani Hakimu mkazi mfawidhi huyo,Oscar Bulugu kwa tuhuma tatu za kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni tano.
Hakimu  Bulugu Katika kesi yake inayomkabili  anatuhumiwa kuwa alitenda makosa hayo kati ya Mwezi Machi 15 mwaka huu  hadi Machi 22 huko wilaya ya Urambo akiwa ni Hakimu Mkazi Mfawidhi.
Katika kesi hiyo upande wa mashitaka ulidai kuwa Machi 15 mwaka huu mtuhumia akiwa ni Hakimu wa  wilaya ya Urambo alimshawishi Lucas Raymond Changala ampe fedha hizo ili kumpa dhamana ndugu yake aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya wizi wa fedha za benki ya NMB.

Mwanasheria wa TAKUKURU katika shauri hilo,  Simon Mashindia,  alidai katika shtaka la pili kuwa tarehe 18 Machi Mwaka huu hakimu huyo ambaye ni mtuhumiwa alipokea shilingi milioni moja toka kwa Changala kama malipo ya awali ili aweze kumpa dhamana Phillipo Raymond aliyekuwa mtumishi wa benki ya NMB tawi la Urambo anayetuhumiwa kuiba zaidi ya shilingi milioni mia moja.

Mwanasheria huyo wa TAKUKURU alidai katika shitaka la tatu kuwa tarehe 21/03/2013  mtuhumiwa huyo alipokea tena shilingi milioni moja ikiwa ni endelezo la malipo aliyoomba aweze kumpa dhamana mtumishi huyo wa NMB tawi la Urambo.
CHANZO: TABORA YETU

TUSIADHIMISHE SIKU BALI TUDHAMIRIE KUUTOKOMEZA UKIMWI

Kila Disemba Mosi ni siku ya Ukimwi Duniani ambapo watu kwenye maeneo mbalimbali hukutana kwa lengo la kupeana elimu ya kujikinga na kupiga vita ugonjwa wa UKIMWI. Siku hii iliasisiwa na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) mwaka 1998 na inaendelea kuadhimishwa kila Desemba mosi kwa uratibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Ukimwi (UNAIDS).
Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayoadhimisha siku hiyo, ambapo Rais Jakaya Kikwete atawaongoza wananchi wake, hususan wakazi wa Dar es Salaam ambako Siku ya Ukimwi Duniani inaadhimishwa kitaifa.
Maadhimisho hayo yalianza Novemba 25 kwa wadau wa ukimwi kufanya maonyesho ya shughuli za wadau kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini humo.
Hapa Tanzania maadhimisho ya siku hiyo yanabebwa na kaulimbiu ya ‘Tanzania bila maambukizi mapya ya VVU; vifo vitokanavyo na ukimwi na unyanyapaa inawezekana.’
Tunaungana na watu wote duniani wanaoadhimisha siku hii kwa kukumbuka ndugu, jamaa, marafiki, wazazi na wenza wetu waliotangulia mbele ya haki kutokana na ugonjwa huu.
Ni wazi kwamba ukimwi ni janga la dunia hususani kwa nchi zinazoendelea Tanzania ikiwemo, kila familia hapa nchini kwa namna moja ama nyingine inalo kovu linalotokana na ukimwi.
Yamefanyika makongamano mengi makubwa na madogo yanayoelezea jinsi ya kujikinga na maambukizi mapya ya VVU, kutowaambukiza wengine, kuishi kwa matumaini na kutowanyanyapaa walioathirika.
Hivi sasa taifa lipo kwenye mkakati wa kudhibiti ukimwi kwa kufikia azima ya sifuri tatu, yaani maambukizi mapya sifuri, vifo sifuri na unyanyapaa sifuri ifikapo mwaka 2015.
Mkakati huo unahimiza utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) na maazimio yaliyowekwa kwenye mkutano maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi uliofanyika mwaka 2001 nchini Marekani.
Tunakumbuka pia mwaka 2007 Rais Kikwete alianzisha kampeni ya kupima kwa hiari VVU ili kubaini walioathirika, ambapo yeye na mkewe walipima kwanza.
Ni kampeni iliyoleta hamasa kwa kiasi kikubwa na kupunguza kasi ya unyanyapaa uliokithiri katika jamii, hali iliyoharakisha vifo kwa wapendwa wetu huku wengine wakihofia kupima, kwa sababu dawa hazikuwepo.
Hivi sasa tunaweza kusema kasi ya maambukizi mapya imepungua baada ya wananchi kupata elimu sahihi ya kujikinga na kutumia dawa za kufifisha makali ya ugonjwa huo ikiwemo kupungua sana kasi ya unyanyapaa.
Tanzania Daima Jumapili tunawahimiza Watanzania wote kushirikiana katika kutokomeza maambukizi mapya ya VVU ili kuwa na taifa salama. Ni kweli tukiamua tunaweza kuufanya ugonjwa wa ukimwi kuwa historia.

KESI ZAUKATILI NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA KUSIKILIZWA MIEZI MITATU

NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki, amesema kuanzia mwakani kesi zitakazohusiana na ukatili wa kijinsia, mashauri yake yatasikilizwa ndani ya miezi mitatu  hadi kutolewa hukumu.
Kairuki alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa kijitabu cha mwongozo wa kuwasaidia wanawake  waliofanyiwa ukatili kilichoandaliwa na Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC).
Alisema ili kuhakikisha hilo linafanikiwa kutakuwa na vikao maalumu katika mahakama zinazoendesha kesi hizo, hatua ambayo alisema imeafikiwa na nchi zote za Maziwa Makuu.
“Ni kweli kumekuwepo na ucheleweshaji wa kesi hizi, hali inayowafanya walalamikaji kuachana na kesi hizo kwa kuona kuwa wanapotezewa muda wao, ndio  maana kwa pamoja nchi hizo ziliamua  kuja na azimio moja, ili kuona watuhumiwa wa makosa haya wanashughulikiwa mara moja,” alisema.
Pamoja na mikakati hiyo, Kairuki alitoa wito kwa asasi zinazoshughulika na masuala ya kuwatetea kinamama na watoto  kushirikiana na viongozi wa dini ambao wataweza kuwahubiria  waumini wao umuhimu wa kuishi kwa amani na katafuta suluhu ya matatizo kwa amani.
Mwenyekiti wa WLAC, Nakazael Tenga, alisema wakati takwimu za utafiti wa afya  Tanzania ya mwaka 2010 zikionyesha asililimia 39 ya wanawake wote Tanzania wameathirika kwa namna moja au nyingine na ukatili wa kimwili tangu wakiwa watoto, mkoa wa Dodoma umeonekana kuongoza kwa vitendo hivyo kwa asilimia 70.
Mkoa wa Mara ambao awali ulikuwa ukiongoza sasa hivi vitendo vimepungua na kufikia asilimia 66.4, Ruvuma (50.8) na Morogoro (50.1), takwimu ambazo Tenga alisema haziridhishi kwani karibu kila mkoa nchini unakabiliwa na titizo hilo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa WLAC, Theodosia Muhulo, alisema ipo haja ya kuanzishwa mahakama ya familia ambayo itakuwa ikishughulikia kesi zote zinazohusiana na migogoro ndani ya familia.
CHANZO: TANZANIA DAIMA

Sunday, November 24, 2013

LULU ASEMA 'DIAMOND HANA HADHI YA KUTEMBEA NA MIMI, HATA IWEJE'

Msanii wa filamu bongo,na mwenye jina kubwa kuliko umri wake,Elizabeth Michael aka LULU, ameonesha msimamo mkali baada ya msanii wa bongo fleva mwenye jina la madini expensive Naseeb Mohamed au DIAMOND kufanya kila aina ya mbinu ikiwemo ile ya kutaka kumuagizia msanii huyo gari expensive aina ya nissan murrano yenye thamani ya shiling million zaidi ya 60,ambapo hata hivyo mbinu yake iyo imeonekana kugonga mwamba baaada ya Lulu kukataa kata kata kutoka na staa huyo anayetamba na ngoma ya my number one.

Kwa kumaanisha kuwa hataki kutoka na staa huyo, Lulu alilazimika kubadilisha namba ya simu yake ya mkononi ili kuepuka usumbufu kutoka kwa bwana mdogo huyo ambaye kila kukicha amekuwa akiwindwa na wasichana warembo ili tu waonje sukari yake. 

Pia inasemekana lengo la diamond kutaka kutoka na Lulu ni kutaka kukuza jina lake(kiki) kwa kuwa anaamini staa huyo ana jina kubwa na lenye mvuto hivyo kumfanya na yeye aogelee kwenye dimbwi la umaarufu na kuongelewa zaidi na watu,na kuwa ishu iyo ndo itakuwa habari ya mujini yaan yeye kutoka na lulu.

Baadhi ya watu wameonyesha kushangzwa sana na msimamo mkali wa binti huyo,kwa kuwa waliamini hakuna staa yeyote bongo mwenye ubavu wa kupindua kwa diamond,kama ilivyokuwa kwa Wema,Jokate,Aunt,Wolper na baadhi ya mastaa ambao dogo huyo aliwamega kiulaini. 

Watu wanahaha kumjua mwanaume anayempa jeuri Lulu hadi kufikia hatua ya kuchomoa kwa diamond..
 
SOURCE: MSEMA UKWELI BLOG

Saturday, November 23, 2013

TUGHE TABORA KUTOWATETEA WATUIMISHI WASIOWAJIBIKA

CHAMA cha watumishi wa serikali Kuu na Afya,TUGHE,Mkoani Tabora,kimeeleza kuwa hakitawatetea watumishi wanaokwenda kinyume cha sheria,kanuni na taratibu za kazi zao.

Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Tabora,Bw.Ezra Lema,amesema kutokana na hali hiyo watumishi ni lazima wafuate mikataba yao ya ajira na kama inatokea wanaonewa hapo chama chao kitawatetea kwa nguvu zote.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati tendaji Mkoa,Mwenyekiti huyo amesema chama chake kitawatetea watumishi ambao waajiri wao hawakutimiza wajibu wao baada ya wao kutimiza wajibu wao.

Akiwazungumza viongozi wa matawi,Bw,Lema amesema ni muhimu wakapata elimu ya mahusiano kazini  ili wafanye kazi zao kwa ufanisi zaidi tofauti na ilivyo sasa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wanawake wa chama hicho mkoa wa Tabora,BI. Plaxeda  Mkwira, amesema wanawake wa chama hicho wengi hawajui haki zao na wanafanya jitihada za kuwaelimisha kuzijua haki zao.

Kikao hicho pia kiliazimia kwa viongozi kutembelea wanachama wao kwenye matawi na kutoa elimu kwao kwani ndio muhimu na kukifanya chama hicho kuwa imara zaidi.
 
SOURCE: TABORA YETU

UJENZI WA BARABARA YA MOROGORO KUKAMILIKA 2014.

KUSEMA UKWELI, TUMETOKA MBALI. HAPA TULIPOFIKA, TUMEPIGA HATUA.

Moja ya kituo ambacho kitatumika kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi kilichopo Magomeni Usalama jijini Dar.

Barabara ya Morogoro ilivyo sasa.…

Moja ya kituo ambacho kitatumika kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi kilichopo Magomeni Usalama jijini Dar.

Barabara ya Morogoro ilivyo sasa.

Njia ambayo itatumika kwa ajili ya magari madogo huku pembeni kikionekana kituo kwa mbali.

Baadhi ya mafundi wakiendelea na ujenzi huo.

Meneja wa mradi huo Deo Muta akisikiliza maelezo kutoka kwa walinzi DART wanaolinda vituo hivyo wanaozuia watu wasifanye biashara na wala kupita ndani ya vituo.

Naye akitoa yake ya moyoni kuwa kuna walinzi hawafanyi kazi kama walivyopangiwa majukumu yao.

Eneo la Manzese likionekana kwa mbali.

 
Eneo hilo likionekana kwa ukaribu zaidi.

Daraja linalojengwa katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo.

                      Daraja hilo likionekana lilivyoingia hadi ndani ya kituo.
 
UJENZI unaoendelea katika Barabara ya Morogoro, jijini Dar utakamilika ifikapo mwakani.
Akizungumza na mtandao huu meneja wa mradi huo kutoka DART, Deo Muta ‘Mzee wa Mi’ alisema kuwa ifikapo katikati ya mwaka 2014 mradi huo wa kutengeneza barabara kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi utakuwa umekamilika kutokana na jinsi ujenzi unavyokwenda haraka haraka.
“Sisi kama DART tunategemea kukabidhiwa barabara na Kampuni ya STRABAG inayojenga  katikati ya mwaka 2014 hivyo tunawaomba wanachi hasa wanaokaa au kufanya biashara pembezoni mwa barabara hii waendelee kuwa kando na watuvumilie  hadi pale mradi huu utakapokuja kukamilika hiyo mwakani” alisema Deo Muta.
RESOURCE: GLOBAL PUBLISHERS