LATEST POSTS

Tuesday, December 10, 2013

HEBU CHEKI MISHONO YA KITENGE KUTOKA NIGERIA.

Wadau, hebu angalieni mishono hii bomba ya vitenge kutoka Nigeria kisha amua mwenyewe ni mshono upi kati ya hii unadhani unaweza ukauvaa mahali popote kama vile Nyumbani, kanisani, kazini kwa kitchen party n.k

Mwanamke kitenge babu wee na tena ni  ni alama ya uafrika.

 
Latest Nigerian Ankara StylesLatest Nigerian Ankara StylesLatest Nigerian Ankara Stylesankara beautiful styleankara stylelatest ankara fashionLatest Nigerian Ankara Stylesankara fahionstyles of ankaraankara style fashion ankara styles beautiful nice ankara cloth ankara design Latest Nigerian Ankara Styles ankara attire for nigerianankara fashion wear


Read the original post and more here http://iloverelationship.com/latest-nigeria-ankara-styles/
 

Monday, December 9, 2013

UNHCR ULYANKULU WATOA MSAADA WA GARI LA WAGOJWA, PIKIPIKI MOJA NA COMPUTER - ULYANKULU

UNHCR Ulyankulu wametoa msaada wa gari moja la wagonjwa katika kituo cha afya Ulyankulu, Pikipiki moja katika kituo chga polisi Ulyankulu na Computer moja kwa Mkuu wa makazi Ulyankulu ili kusaidia shughuli za maendeleo Wilayani Kaliua.
Angalia yaliyojiri katika tukio hilo katika picha.

Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Mhe. Maketta akisaini kitabu cha wageni
 
Aliyesimama ni  Ndg. Nyamwalle aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua akisema neno katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano
 
 

 Pikipiki na gari vilivyotolewa kwa Kituo cha afya Ulyankulu na Pikipiki kwa ajili ya kituo cha polisi Ulyankulu

 

 Misaada iliyotolewa na UNHCR kama inavyoonekana katika picha


 Dr.Revocatus Masanja, aliyekuwa Mganga Mkuu Kaliua
 
 Kaimu Mkurugenzi Ndg. Nyamwalle (katikati) akiwa na Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua muda mfupi kabla ya zoezi la kukabidhiwa vifaa halijaanza.

MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU WA TANZANIA - BARA YAFANA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiambatana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakiwasili katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanzania Bara leo.…


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiambatana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakiwasili katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanzania Bara leo.
Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal akiwasili katika Uwanja wa Uhuru kwa maadhimisho ya sherehe za uhuru wa miaka 52 ya Tanzania Bara.
Rais Kikwete akiwa amesimama kikakamavu wakati Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Rais Jakaya Kikwete akikagua vikosi mbalimbali vya majeshi wakati wa maadhimisho hayo.
Mojawapo ya kikosi cha majeshi kikisubiri kukaguliwa na Mhe. Rais Kikwete.
Vikosi mbalimbali vya majeshi vikipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete kutoa heshima zao.
Rais Kikwete akichukua 'notes' wakati sherehe zikiendelea.
Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal (kushoto) akiwa na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amaan Karume.
Mama Salma Kikwete (kushoto) akibadilishana mawazo na Rais wa Zanzibar Dk. Mohammed Shein.
Rais Kikwete (kushoto) akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda.
Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa (katikati) akisalimianan na Rais Shein.
Rais Kikwete akihutubia wakati wa maadhimisho hayo.
Makundi mbalimbali ya vijana yakitoa burudanai ndani ya Uwanja wa Uhuru.
Picha ya Rais Shein iliyotengenezwa na vijana.
 
Wananchi wa Tanzania Bara (Tanganyika) leo wameadhimisha miaka 52 ya uhuru wake uliopatikana Desemba 9, 1961. Sherehe za maadhimisho hayo zimefanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam amabapo mgeni rasmi alikuwa Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Viongozi mbalimbali wamehudhuria sherehe hizo.

Chanzo: Global publishers