LATEST POSTS
Sunday, June 21, 2015
KUTANA NA MWANAMKE HUYU ALIYEJIGUNDULIA DAWA YA MICHEPUKO
Msichana
aliyetajwa kwa jina la Abbie Bartlett, wa Ibiza Hispania, amewashangaza
wengi baada ya kumvalisha mpenzi wake Leon Connolly fulana maalum yenye
ujumbe unaowaponda wasichana wengine na kumsifia yeye kwa lengo la
kujihami na wezi wa penzi lao.Abbie alifanya hivyo baada ya kuona kuwa mpenzi wake
anataka kusafiri na kwamba wangekuwa mbali kwa muda mrefu hivyo alitaka maandishi pekee yawe ujumbe wa kutosha.Nampenda mpenzi wangu Abbie, nawachukia wasichana wa Ibiza, kwa hiyo tafadhali kaa mbali na mimi.
Yanaeleza maandishi yaliyo kwenye fulana hiyo ikiwa na picha zao
Saturday, June 20, 2015
MJAMZITO AJIFUNGUA BAADA YA KUBEBA MIMBA KWA MIAKA 5
An
Abuja-based woman, Mrs Adenike Kolawole, (pictured left) who was barren
for 27 years, has reportedly given birth to a baby boy after carrying a
5-year pregnancy. Is that even possible
According to PM News, Mrs Adenike gave birth on Sunday October 26th at Evangelical Church of
Cherubim and Seraphim located at Pipeline Road, Mafon area, Ejigbo, Lagos during the church’s Sunday service. Narrating her story to PM news, Mrs Kolawole said she suffered miscarriage in the early period of her marriage and afterwards found it difficult to conceive \
Cherubim and Seraphim located at Pipeline Road, Mafon area, Ejigbo, Lagos during the church’s Sunday service. Narrating her story to PM news, Mrs Kolawole said she suffered miscarriage in the early period of her marriage and afterwards found it difficult to conceive \
MAAJABU YA DUNIA!! NYOKA WAMFANYIA MTU MASAJI KWA GHARAMA YA DOLA 47
UNAPENDA kufanyiwa
masaji na nyoka? Unaweza kukaza roho na usiogope kung’atwa? Kama ndio
basi nenda nchini Indonesia utaipata kwa raha zako. Masaji hiyo inapatikana Bali Heritage Reflexology and Spa huko Jakarta, Indonesia ambako wanaweza kukuondolea uchovu wako wa siku nzima kwa massage ya nguvu inayofanywa na nyoka mkubwa.
Masaji
hiyo inafanyika kwa nyoka huyo kuwekwa juu ya mwili wa mteja na mengine
huachiwa yeye nyoka afanya yake. Ili kupata huduma hii mteja hutakiwa
kulipa dola 47 ambazo ni zaidi ya shilingi 76,000 za Tanzania
MASTAA WAFANYA KUFURU KWENYE HARUSI YA BABA HAJI WA BONGO MUVI!
SAA chache kabla ya kuanza kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, staa wa sinema za Kibongo, Haji Adam ‘Baba Haji’ ameangusha bonge la harusi baada kufunga ndoa na mrembo aliyetajwa kwa jina la Latifa Sharji wiki moja iliyopita huku mastaa wakifanya kufuru kama kawaida yao.
Katika pati hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kibao wa Bongo Movies huku gazeti hili nalo likijipenyeza ndani, waalikwa walikula na kunywa hadi wakasaza kabla ya muda wa zawadi na kusakata muziki.Kwenye shughuli hiyo, kadiri watu walivyokuwa wakipiga ulabu ndivyo sherehe ilivyokuwa ikichangamka na mastaa kujikuta wakiserebuka muziki kwa kwenda mbele.
Baadhi ya wasanii walioongoza kutunza ni tajiri mfupi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ambaye alimwaga fedha taslimu Sh. milioni 2 akifuatiwa na Single Mtambalike ‘Richie’, Jacob Steven ‘JB’, Vincent Kigosi ‘Ray’ na wengine waliokuwa fedha za kudunduliza.
Kwa upande wa mastaa wa kike, Kajala Masanja ‘Kay’ aliongoza kwa kumwaga mkwanja akifuatiwa na Jacqueline Wolper Massawe, Wastara Juma, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ na watoto wengine wa mjini.
Hadi gazeti hili linaanua jamvi ukumbini hapo usiku mnene, baadhi ya mastaa walikuwa wakiendelea kusakata rhumba na kupiga kinywaji
BREAKING NEWSSSS: KOCHA WA TAIFA STARS MAART NOOIJ NA BENCHI LAKE LOTE LA UFUNDI WAFUTWA KAZI
Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao
chake cha jana pamoja na mambo mengine kilipitia mwenendo wa timu ya
Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya
Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmini ya mwenendo wa timu.
Kamati ya Utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo;
1. Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia Juni 21, 2015.
2. Benchi lote la ufundi la Taifa Stars limevunjwa kuanzia Juni 21, 2015.
3. Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Juni 20, 2015

Kocha Mkuu wa Taifa Stars Maart Nooij akisindikizwa na ulinzi mkali usiku huu baada ya kumalizika kwa mchezo wa Tanzania na Uganda wa kuwania kufuzu fainali za CHAN katika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar ambapo Taifa Stars ilichapwa 3-0.
Kamati ya Utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo;
1. Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia Juni 21, 2015.
2. Benchi lote la ufundi la Taifa Stars limevunjwa kuanzia Juni 21, 2015.
3. Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Juni 20, 2015

Kocha Mkuu wa Taifa Stars Maart Nooij akisindikizwa na ulinzi mkali usiku huu baada ya kumalizika kwa mchezo wa Tanzania na Uganda wa kuwania kufuzu fainali za CHAN katika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar ambapo Taifa Stars ilichapwa 3-0.
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wanaongoza kwa utoaji wa mimba kwa njia za kienyeji
Moses
Mongo ambaye ni Mratibu wa Kanda ya Ziwa kutoka Taasisi ya Umoja wa
Mataifa (UNA-TANZANIA) amesema wanafunzi wa Vyuo Vikuu wanaongoza kwa
utoaji wa mimba kwa njia za kienyeji kwa kutumia mwarobaini na bluu ya
kuweka kwenye nguo nyeupe.
Mongo alisema katika utafiti walioufanya mwaka 2014 katika Vyuo Vikuu vinne Kanda ya Ziwa wamebaini wanafunzi kutoa mimba kienyeji.
“Utafiti
tuliofanya 2014 kwa kuzungumza na wanafunzi kila Chuo au Shule
tumebaini wapo wanafunzi waliotoa mimba na wapo waliofariki kwa kutoa
mimba lakini kwa kificho”—Moses Mongo.
Mongo alisema
katika mazungumzo na wanafunzi hao walieleza kuwa suala la utoaji wa
mimba ni la kawaida na matumizi ya kondomu huwa ni pale wanapoanza
uhusiano kabla ya kuzoeana.
Mufti mpya kupatikana ndani ya siku saba
Baraza Kuu la Waislamu nchini (Bakwata), limesema litatangaza mrithi wa Mufti wa Tanzania ndani ya siku saba kuanzia jana.
Akizungumza
kwa njia ya simu, Katibu mkuu wa Bakwata, Sheikh Suleiman Lolila,
alisema utaratibu unaendelea kuhakikisha katika kipindi hicho jina la
Mufti mpya linapatikana.
Kuchaguliwa
kwa kiongozi huyo mpya wa waumini wa dini ya Kiislam nchini, kunafuatia
kufariki kwa aliyekuwa Sheikh mkuu, Mufti Issa Shabani Bin Simba usiku
wa kuamkia Juni 15 katika Hospitali ya TMJ ya jijini Dare s Salaam.
Mufti
Simba alizikwa siku ya pili yake katika makaburi ya Nguzo nane mjini
Shinyanga, ambapo mazishi yake yaliongozwa na Rais Jakaya Kikwete na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, kidini na vyama vya
siasa.
“Mchakato
wa kumpata Sheikh Mkuu wetu utakamilika ndani ya siku saba kuanzia
sasa, wananchi na waumini wa dini ya kiislam wawe wavumilivu katika
kipindi hiki,” alisema Sheikh Lolila.
Katibu
mkuu huyo hakutaka kuweka wazi sehemu wanapokutana wajumbe wa Baraza la
Ulamaa ambao ndilo lenye mamlaka ya kumchagua kiongozi.
Hata
hivyo, baadhi ya watu wanaotajwa kushika nafasi hiyo ni Kadhi Mkuu,
Sheikh Abdallah Mnyasi na manaibu wake Sheikh Abubakar Zuber na Sheikh
Ali Muhidin Mkoyogile.
Wengine
ni Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Salum Ferej, Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga,
Ismail Makusanya, Sheikh wa Mkoa wa Kigoma, Hassan Kiburwa na Kadhi wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Hamid Masoud Jongo.
CHANZO: NIPASHE
Askari Azua Taharuki baada ya kufyatua risasi hewani Mahakamani Sumbawanga
TAHARUKI
imeibuka katika majengo ya Mahakama ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani
Rukwa na kusababisha shughuli za mahakamani hapo, zikiwemo za
kusikilizwa mashauri mbalimbali kusimama kwa muda wa takribani dakika
20.
Mtafaruku
huo ulitokea baada ya askari kupiga risasi hewani mahakamani hapo
wakati wakimsaka mahabusu aliyedaiwa kutoroka katika chumba cha mahabusu
mahakamani hapo na kujificha darini.
Mwandishi
wetu alishuhudia askari polisi wakiwa na bunduki mikononi wakihaha
kumsaka mahabusu huyo ambaye alidaiwa kutoroka kupitia upenyo uliopo
katika chumba cha mahabusi mahakamani hapo.
Mkasa
huo ulianzia saa 5 asubuhi na kudumu kwa dakika 20. Hata hivyo,
mahabusu huyo hakuweza kuonekana licha ya jitihada za baadhi ya polisi
kupanda darini kupitia chumba cha mahakama namba mbili bila ya
mafanikio.
Hekaheka
za kumsaka mahabusu huyo zilianza pale baadhi ya watumishi wa
mahakamani hapo na mahakimu kudai kusikia vishindo kwenye dari ambapo
mara moja mahabusu waliokuwa kwenye chumba mahakamani hapo walihesabiwa.
Katika
chumba hicho walitakiwa wawe mahabusu 10 lakini walipohesabiwa kwa mara
ya kwanza ilibainika kuwa alikuwa amekosekana mmoja ndipo msako mkali
ulipoanza huku askari wakihaha kumsaka darini.
Hata
hivyo walipohesabiwa mara ya pili ilibainika kuwa hesabu yao ilikuwa
imetimu kwamba walikuwa 10 lakini haikubainika nani miongoni mwao
alikuwa ametoroka. Hata mahabusu wenyewe hawakuwa tayari kumtaja.
Habari
za kuaminika kutoka mahakamani hapo zinaeleza kuwa baada ya watumishi
wa mahakama hiyo wakiwemo askari polisi na mahakama kusikia vishindo vya
miguu darini waliamini ilikuwa ni ya mahabusu anayedaiwa kutoroka
katika mazingira ya kutatanisha siku tatu zilizopita
Friday, June 19, 2015
MAKONDA KUONYESHA AJIRA KATIKA MICHEZO LEO
MH: PAUL MAKONDA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI,
Anawaomba Wanakinondoni wote na wakazi wa DSM katika
kuandaa maandalizi ya Team za Wilaya ya Kinondoni zitakazo kuwa na
wachezaji watakao lipwa mshahara; katika:
1.Mpira wa miguu
(Football).
2.Netball.
3.Basketball.
(Football).
2.Netball.
3.Basketball.
Kushirikiana nae katika uzinduzi wa ligi hizo leo jumamosi, saa moja asubuhi Viwanja vya Leaders.
Ambapo atazikabidhi Team 138 vifaa vya michezo.
SET 2 ZA JEZZY NA MIPIRA 2 KWA KILA TEAM.
SET 2 ZA JEZZY NA MIPIRA 2 KWA KILA TEAM.
WATAKUWAPO WATAALAMU WAKUPIMA AFYA ZA WACHEZAJI NA WATU WENGINE, KUTAKUWA PIA NA ZOEZI LA KUCHANGIA DAMU KWA ATAKAE PENDA.
TEAM ZOTE ZIKISHACHEZA KWA PAMOJA BAADAE WASHINDI WATAUNDA TEAM ZA WILAYA....
KWA MAELEZO ZAIDI FIKA VIWANJA VYA LEADERS MAPEMA leo(JMOS TAR 20 JUNE/2015) .
KIPAJI CHAKO AJIRA YAKO....
AJIRA SI BOMU.BOMU NI KUTOTUMIA KIPAJI CHAKO.
SERIKALI HAZIWEZI KUAJIRI WATU WOTE KATIKA AJIRA ZA OFISINI.
AJIRA INAJUMUISHA KUAJIRIWA NA KUJIAJIRI.NJOONI TUJIAJIRI TUPUNGUZE UGUMU WA MAISHA.
INAWEZEKANA...TUTIMIZE WAJIBU
















































