Rais
Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za Rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa
Tabora Bibi Fatma Mwassa kufuatia kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Urambo Bibi
Anna Magoa kilichotokea tarehe 24 Septemba, 2013 katika hospitali ya
Taifa ya Muhimbili jijini Dar-Es-Salaam.
Katika
salamu hizo, Rais amemuelezea Bibi Magoa kuwa alikuwa kada na
mchapakazi hodari ambaye ameacha pengo kubwa katika Chama na Serikali.
“Kwa
hakika umepoteza moja ya nguzo zako mkoani Tabora. Bibi Anna amekua
kada na mtumishi wa kutumainiwa katika Chama chetu cha Mapinduzi na
serikali kwa ujumla. Tumeondokewa na mtu muhimu na mchapa kazi hodari”
Rais amesema na kumuomba Bibi Fatma Mwassa kumfikishia salamu za pole
kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki zake wote.
Rais
pia amewatumia salamu za pole wafanyakazi na wananchi wa Urambo ambao
marehemu amekuwa akifanya nao kazi tangu alipohamia Wilayani humo Mwaka
2010.
Marehemu ameacha mtoto mmoja wa kike na wajukuu wawili. Mwili wake unatarajiwa kusafirishwa leo kwenda Mkoani Iringa kwa maziko.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu
Dar-Es-Salaam, Tanzania
25 Septemba, 2013
0 comments:
Post a Comment