Mwandishi wa Habari wa ITV na Radio One Ufoo Saro amejeruhiwa kwa risasi na mtu mmoja anaedaiwa kuwa mchumba wake ambaye inasemekana anafanya kazi UN. Katika tukio hilo ambalo limetokea katika maeneo ya Kibamba jijini Dar-es-saalam.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Kamanda Wambura amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya Alfajiri leo.
Kamanda
wambura ameongeza kuwa mwanaume aliyefanya tukio hilo anafanya kazi Umoja wa Mataifa (UN)
huko Sudani ila bado haijafahamika kwamba anafanyia kitengo gani (japo kwa habari za mtaani zinasema mtu huyo ni mwanajeshi ila bado hazijathibitishwa)
Kamanda
Wambura alisema kuwa, inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao
ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi
wa Ufoo Saro (mama mkwe) na ndipo mwanaume huyo alipomshutumu mama mkwe
wake kwamba anamtetea mwanae ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama yake
na Ufoo Saro Risasi ya kichwa na kumuua papo hapo na kisha akampiga
Ufoo Saro risasi mbili moja ya tumboni na ingine ya mguuni na kudhani
kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya
kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.
Kwa sasa Ufoo yupo katika hospitali ya Muhimbili chumba cha wagonjwa mahututi.
Urambonews inatoa pole kwa familia ya Bi.Ufoo Saro na tunamwomba Mwenyezi Mungu ampe afueni/ahueni. Na mama Ufoo Saro apumzike kwa amani.
0 comments:
Post a Comment