WANANCHI
waishio maeneo ya Vijijini endapo watapata elimu kuhusu matumizi ya
Nishati mbadala,watakuwa katika nafasi nzuri ya kutunza mazingira
yanayoharibiwa kwa kasi kutokana na matumizi ya kuni katika kukaushia
tumbaku na matumizi ya Nyumbani.
Akifungua mafunzo kwa walimu wa Umeme Vijijini wa Vyuo vya Maendeleo ya
Jamii,Mkuu wa Wilaya ya Uyui,Bi Lucy Mayenga katika Hotuba yake
iliyosomwa na Katibu Tawala,Bw.Bibangamba John,ameeleza ni lazima elimu
ya matumizi sahihi ya Nishati mbadala itolewe ili wananchi wasizidi
mazingira.
Ameeleza wananchi wanatumia sana kuni na kuharibu mazingira lakini
matumizi ya Nishati mbadala yatawasaidia sana kuokoa na kutunza
mazingira ambayo ni muhimu kwa ustawi wa maisha yao.
Mayenga amesisitiza kwa wshiriki hao kuhakikisha kweli wanaipeleka elimu
hiyo kwa wananchi wengi waishio vijijini vinginevyo itakuwa ni kazi
bure.
Kwa upande wake Afisa Kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na
watoto,Pius ligo,amesema Wakala wa Nishati Vijijini,REA, wanataka
wananchi wasitumie Nishati inayoharibu mazingira.
Amesema mafunzo hayo yanayotolewa kwa washiriki kutoka Mikoa Tisa Nchini
yatatumika kueneza elimu ya matumizi ya Nishati mbadala kwa wananchi wa
Vijijini kupitia washiriki hao na hivyo kuleta ustawi wa maisha ya
wengi
Mafunzo hayo yanayochukua Wiki mbili yanayoendeshwa na wakala wa Nishati
Vijijini,REA kwa kushirikiana na Wizara ya maendeleo ya
Jamii,yatawapeleka washiriki kufunga Nishati katika zahanati ya Miyenze
ambayo itakuwa ni sehemu ya mafunzo yao.
CHANZO: TABORA YETU
0 comments:
Post a Comment