BUNGE Maalumu la Katiba, jana limechukua sura mpya baada ya baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo, kutaka kuzipiga ndani ya Ukumbi wa Bunge, Mjini Dodoma.
Hali hiyo ilimfanya Mwenyekiti wa muda, Bw. Pandu Ameir Kificho, kuahirisha shughuli za Bunge hilo kabla ya muda wake hadi jioni ili kupata muda wa kujadili mtikisiko huo bungeni.
Baadhi ya wajumbe walidai kuna dalili za upendeleo ambao unafanywa kwa wajumbe ili kupewa nafasi za kuzungumza kutokana na itikadi za vyama.
Mjumbe Bw. Christopher Ole Sendeka aliingia katika mvutano na mjumbe wa Kamati ya Kanuni, Bw. Abubakar Hamis Bakari juu ya uwasilishaji majedwali ya marekebisho ya kanuni.
Awali Bw. Ole Sendeka alipewa nafasi ya kuzungumza na Bw. Kificho ili aweze kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya kifungu cha 58 cha kanuni hizo kilichokuwa kikijadiliwa.
Baada ya Bw. Ole Sendeka kuwasilisha mabadiliko yake, alisimama Bw. Bakari ambaye alipaswa kujibu hoja hiyo kutokana na nafasi yake ya ujumbe wa kamati ya kanuni.
Bw. Bakari alikataa kupokea hoja ya Bw. Ole Sendeka na kudai kuwa, hayakuwa yamewasilishwa kwa kufuata taratibu za uwasilishwaji wa mabadiliko ya majedwali.
Alisema kamati haina mapendekezo hayo hivyo haiwezi kujibu jambo lisilojadiliwa na kukitupia lawama kiti cha Mwenyekiti wa muda akidai kimekuwa kikitaja majina ya wajumbe na kuwapa nafasi ya kuzungumza wakati hawapo kwenye utaratibu wala hawakuwa wameomba toka awali.
Aliongeza kuwa, si kwa Bw. Ole Sendeka pekee, bali hata Bw. Kificho, amekuwa akitaja wajumbe wengine wakiwamo Bw. Peter Serukamba na Bi. Ummy Mwalimu ambao wote hawakuwa wamewasilisha majedwali ya mapendekezo ya marekebisho toka awali.
"Mheshimiwa Mwenyekiti, Ole Sendeka hayupo katika orodha ya walioleta mapendekezo lakini nashangaa wewe unampa nafasi ya kuzungumza wakati hakuwapo kwenye orodha yetu, kamati hatuwezi kumpa nafasi ya kujibu hoja yake hatuitambui.
"Mwenyekiti ukiendeleza huu mtindo wa kuruhusu kila anayetaka kuzungumza hapa azungumze hatutofika, tutatumia miezi sita kutengeneza kanuni, hivyo lazima uwe na maamuzi, wanaoleta mapendekezo hivi sasa hatupokei," alisema Bw. Bakari.
Baada ya kumaliza kuzungumza, Bw. Kificho aliingilia kati na kusema jambo hilo linaweza kuwa limechanganywa na sekretarieti inayoandaa na kwamba yeye binafsi amepewa majina ya waliopeleka marekebisho hivyo anashangaa kuona kama hayapo kwa wajumbe hao.
Bw. Kificho alimruhusu Bw. Ole Sendeka azungumze tena ambapo katika mazungumzo yake, alisema mapendekezo yake aliyawasilisha mapema na kwamba kama Bw. Bakari ana itikadi zake za vyama, asimuhusishe humo.
Bw. Ole Sendeka alisema yeye ana uzoefu wa kanuni na alifuata taratibu akiwa na wenzake, Bw. Serukamba, Bi. Mwalimu na kama mapigo yao yanawaumiza wajumbe wengine wavumilie tu.
"Mheshimiwa Mwenyekiti, tuliopo hapa ni wajumbe, nilijua na mimi si dhaifu kwenye kanuni bali najua haki yangu, nilitimiza wajibu wangu, kama mapigo yetu yanawaumiza wavumilie.
Aliongeza kuwa, kazi yao si kupeleka majina kwa Bw. Hamisi na kama ana chama chake na hoja zao zinamuuma, asimame na kuwaweka wazi kuwa yupo katika msimamo gani lakini yeye amewasilisha kama taratibu zinavyomtaka.
Kauli ya Bw. Ole Sendeka iliibua sintofahamu ndani ya Bunge hilo ambapo baadhi ya wajumbe walianza kuzomea na wengine wakisimama na kutaka wapewe nafasi ya kuzungumza na kuwasha vipaza sauti.
Hali hiyo ilimfanya Bw. Kificho awasihi wajumbe waache kuingiza masuala ya vyama katika Bunge hilo na kudai wajumbe wote walioingia bungeni wamewakilisha makundi.
"Niwaombe wajumbe tujitahidi sana, tusioneshe misimamo ya vyama, tumepata heshima kubwa ya kuwapo humu ndani hivyo si vyema kuanza kuonesha vidole kwa sababu huyu ni CCM, sijui CUF au CHADEMA itaibua hisia ambazo si nzuri," alisema.
Aliongeza kuwa; "Mheshimiwa Ole Sendeka naona ulimi umekwenda mbali kidogo ukamgusa mheshimiwa Bakari, mimi naona hili jambo limekwenda nje hivyo naomba tuwe makini," alisema Bw. Kificho.
Baada ya kauli hiyo, wajumbe walianza kupiga kelele wakitaka Bw. Ole Sendeka kumwomba radhi Bw. Bakari wengine wakimtaka asifanye hivyo.
Bw. Kificho alitoa nafasi nyingine kwa Bw. Bakari kuzungumza, ambapo katika mazungumzo yake ndipo fujo hizo zilipoibuka baada ya kusema alichokizungumza yeye ni kwa faida ya Bunge na nchi na kwamba taratibu ni kuwasilisha mapema mapendekezo na kwamba majina ya akina Ole Sendeka hayakuwapo.
"Mimi nilizungumza vizuri na kuweka utaratibu mzuri wa kupokea majedwali haya, Mheshimiwa Mwenyekiti kwa bahati mbaya mdogo wangu Ole Sendeka anadai kanuni anazijua vizuri, ninachosema sifikiri kama ana uzoefu wa kujua kanuni kunishinda mimi.
"Toka mwaka 1980 nipo katika mabunge haya hivyo sifikirii kama mtu katoka Simanjiro miaka kumi iliyopita anaweza akaja hapa na kusema anajua kanuni kunizidi... sitaki aniombe radhi, ninachotaka kumfahamisha kwamba kuna watu wana ujuzi zaidi kuliko yeye hivyo awe makini katika mazungumzo yake,” alisema Bw. Bakari.
Kauli hiyo ilizidisha mgawanyiko ndani ya Bunge hilo ambapo baadhi ya wajumbe walisimama na kuanza kupiga meza wengine wakizomea, kurushiana maneno na kutaka kurushiana makonde.
Hali hiyo ilisababisha askari ambao ni wapambe wa Bunge kusogea karibu ili waweze kutuliza vurugu lakini wajumbe bado waliendelea kurushiana maneno.
Vurugu hizo zilionekana kusambaa ukumbini ambapo wajumbe wengine walionekana kurushiana maneno, hali iliyopelekea Bw. Kificho kuahirisha semina hiyo.

0 comments:
Post a Comment