LATEST POSTS

Friday, January 31, 2014

YAJUE MAGONJWA YA KUAMBUKIZA KWA WATOTO

LEO tutaangazia magonjwa hatari kwa watoto na tutajadili kwa kwa kifupi tu, baadhi ya maradhi hayo.
 
POLIO (ugonjwa wa kupooza wa watoto):

Polio hutokea zaidi kwa watoto walio na umri chini ya miaka miwili. Ugonjwa huu unaosababishwa na vijidudu vya virus, huanza kama mafua, homa, kutapika na maumivu ya misuli kwa mtoto.
Mara nyingine, hizi ndizo dalili zinazoonekana tu. Lakini, wakati mwingine sehemu fulani ya mwili hulegea au kupooza. Mara nyingi hii hutokea kwenye mguu au mkono mmoja. Baada ya muda mguu au mkono uliopooza huwa mwembamba na haukui kwa haraka kama huo mwingine.

TIBA:
Ikiwa ugonjwa umekwishaanza hakuna dawa itakayoweza kuondoa kupooza. Dawa za kuua vijidudu hazisaidii. Tuliza maumivu kwa asprini au Astaminofeni na kukanda misuli inayouma kwa maji moto.

KINGA:
Mweke mtoto mgonjwa kwenye chumba tofauti mbali na watoto wengine. Mama ni lazima anawe mikono kila mara baada ya kumgusa. Kinga iliyo nzuri kuliko zote kwa polio, ni zindiko la polio.

Hakikisha kuwa watoto wamezindikwa kuzuia polio kwa matone akiwa na umri wa miezi miwili, mitatu na minne.

Mtoto aliyelemazwa na polio ni lazima ale chakula bora na kufanya mazoezi ili kuipa nguvu misuli iliyobaki. Kwa mwaka wa kwanza, nguvu inaweza kurudi kidogo.

Msaidie mtoto ajifunze kutembea kwa jinsi anavyoweza. Weka nguzo mbili ili aweze kuegemea. Baadaye, mtengenezee magongo ya kutembelea.

KIFADURO:
Kifaduro hutokea wiki moja au mbili baada ya kukaa karibu na mtu aliyenacho. Huanza kama mafua kwa homa, makamasi hutoka puani na kikohozi.

Wiki mbili baadaye, kifaduro hutokea.
Ghafla, mtoto huanza kukohoa harakaharaka sana bila ya kuvuta pumzi mpaka kohozi linapovutika hutoka, na hewa huingia haraka kwenye mapafu yake kwa mlio wa ajabu unaoitwa kifaduro.
Baada ya hiki kifaduro, anaweza kutapika katikati ya nyakati hizi za kukohoa mtoto huwa mzima kabisa.

Kifaduro huchukua miezi 3 au zaidi.
Kifaduro ni cha hatari hasa kwa watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja kwa hiyo wazindikwe mapema.
Watoto wadogo hawapati kikohozi chenye kifaduro kamili kwa hiyo ni vigumu kuwa na uhakika kama wana kifaduro au hapana.
Ikiwa mtoto mchanga anazimia anapokohoa au macho yake yamevimba panapokuwepo wagonjwa wa kifaduro kwenye sehemu yake, mtibu haraka kama mgonjwa wa kifaduro.

TIBA:
Katika hatua za mwanzo za kifaduro, erythoromycin, tetracyline au ampisilini zinaweza kusaidia. Chroramphenicol husaidia pia lakini, ina hatari zaidi. Ni muhimu.

Kwa wagonjwa wa kifaduro ambao wamezidiwa sana, Phenobarbital inaweza kusaidia hasa ikiwa kikohozi kinamzuia kulala au kinasababisha degedege.

Chanzo: GPL

0 comments: