Dar es Salaam.Rais
Jakaya Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama, amewapandisha vyeo maofisa 28 kutoka Kanali na kuwa Brigedia.
Huku Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Samweli
Ndomba akiwataka maafisa hao kuchapa kazi kwa bidii ili kuongeza
ufanisi wa Jeshi.
Hatua ya Rais Kikwete kuwapandisha vyeo maofisa
hao imefanywa kwa mujibu wa kanuni za Majeshi ya Ulinzi inayompa mamlaka
kufanya hivyo.
Wakati Rais Kikwete akiwapandisha vyeo maofisa
hao, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Samweli Ndomba kwa niaba ya
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, amewataka
kuendelea kuchapa kazi kwa bidii ili kuleta tija na maendeleo jeshi.
Pia mnadhimu huyo amewasisitizia maafisa hao
kusimamia nidhamu na uwajibikaji kwa sababu ndiyo msingi wa mafanikio
katika utendaji wa jeshi.
“Napenda kuwakumbusha suala na nidhamu ni jambo
muhimu kwani ndiyo kioo chetu katika jeshi hivyo nasisitiza kuendelea
kuzingatia jambo hilo. Lingine ambalo ningependa tuendelea kulizingatia
ni kufanya kazi kwa weledi,” alisema.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na JWTZ, maofisa
waliopandishwa vyeo ni pamoja na Kanali Denis Raphael Janga, Kanali
Jason Nestor Musikula, Kanali Jackson King Mrema, Kanali Martin Amos
Kemwaga, Kanali Joseph Cosmas Chengelela, Kanali Martin Nikubuka
Mwankanye, Kanali Harold Kidundi Mziray, Kanali Emmanuel Peter Kapesa na
Kanali Mwita Wambura Isamulyo.
Wengine ni Kanali Francis Asilia Njau, Kanali
Pendo Uledi Kamungwele, Kanali Moses Adolph Shinyambala, Kanali Ibrahim
Abdarahamani Kimario, Kanali Michael Garo Luwongo, Kanali Nelson Hosea
Msanja,Kanali Blasius Kalima Masanja, Kanali Aloyce Damian Mwanjile,
Kanali Rajabu Goma Hanti na Kanali Ignas Beatus Mubofu.
Pia wamo Kanali Dominic Basil Mrope, Kanali Hamis
Issa Majumba, Kanali Salehe Omari Semtaua, Kanali Henry Sweko Kamundo,
Kanali Sylivester Msafiri Minja, Kanali John Bangantagoka Bishoge,
Kanali Anselm Shigongo Bahati, Kanali Robinson Mboli Mwanjela na Kanali
Kaisy Philip Njelekela.
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment