Ugua
pole! Hali ya mwanamuziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza
Stone’ ni ya kumwachia Mungu kwani bado ni tete na watu wamekuwa
wakimiminika kwa ajili ya kumuona katika Hospitali ya Mwananyamala
jijini Dar alikolazwa.
Ijumaa Wikienda lilitia maguu kwenye hospitali hiyo na kufanikiwa
kumuona Banza ambaye kwa wakati huo alikuwa amezungukwa na watu
mbalimbali, wakiwemo wanamuziki wenzake wa dansi wengi wakiwa ni wale wa
Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’.
Kila aliyekuwa akimuona mwanamuziki huyo aliyekuwa akibamba vilivyo
kila alipopanda jukwaani, alikuwa akihuzunika huku wasanii wenzake
wakiangua vilio kutokana na kutoamini alivyo Banza kwa sasa.
“Yaani inahuzunisha kwani huyu siyo yule Banza tuliyemzoea, hali yake
hii ni ya kumwachia Mungu tu kwani ndiye anayejua kila tatizo
linalomtokea binadamu litaondokaje, kikubwa ni kuendelea kumuombea tu
maana hatua aliyopo siyo nzuri, ni Mungu tu aweke mkono wake,” alisema
mmoja wa wanamuziki ambaye hakutaka jina liandikwe gazetini.
Kwa muda mrefu Banza amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa fangasi za
kichwani hali iliyomsababishia matatizo ya kutosikia na kutoona vizuri
huku akishindwa kabisa kunyanyuka kitandani.
Banza akiwa na afya yake jukwaani.
KUTOKA KWA MHARIRI
Ijumaa Wikienda linaungana na Watanzania kumuombea Banza Mungu amponye kwa neno lake kutoka kwenye Kitabu cha Yeremia 30:17 linalosema: “Kwa maana nitakurudishia afya nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana kwa sababu wamekuita mwenye kutupwa wakisema ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye.”

Chanzo: Global publishers
0 comments:
Post a Comment