Haya ni madai
mazito! Pamoja na kukanusha kwa nguvu zote, bado dokta wa upasuaji wa
Hospitali ya Wilaya ya Temeke, Dar aliyetajwa kwa jina moja la Twalib,
anadaiwa kumfungia ndani baba yake mzazi, Harub Fitina akimuweka pamoja
na kuku na sungura huku akipata mateso ya kunyimwa chakula na huduma
nyingine za kibinadamu kwa miaka minne sasa, Ijumaa Wikienda limeibua
mazito.
….Akipewa chakula.
Akizungumza na gazeti hili huku
akirekodiwa, shangazi wa daktari huyo anayeishi Tegeta Masaiti, Kulwa
Pazi alisema kuwa, Twalib alimchukua baba yake kutoka nyumbani kwake,
Bagamoyo mkoani Pwani mwaka 2011 kwa ajili ya matibabu baada ya kuanguka
ghafla na kupooza upande mmoja.
Alidai kwamba, siku chache baada ya
kuhamia nyumbani hapo walishangaa kuwa kila wakienda kutaka kumuona
mgonjwa waliishia nje kwa kisingizio kuwa mgonjwa anapaswa atulie na
asisumbuliwe.
…Nyumba alimofungiwa.
Alidai kwamba, kama hiyo haitoshi, mke
wa mgonjwa ambaye walitengana siku chache baada ya mumewe kuugua, Siasa
Mloli aliyebaki Bagamoyo alidai kuwa alikosa mawasiliano na huduma ya
watoto kutoka kwa mumewe kwa kipindi hicho cha miaka minne.
Akizungumza na gazeti hili, mke wa Harub
alisema kuwa, mapema mwaka jana, mtoto wake ambaye ni mwanafunzi
aliyetajwa kwa jina la Jafar alikwenda nyumbani kwa Twalib kuomba fedha
za matumizi lakini jamaa huyo alimfukuza, kisa aligonga mlango kwa
kutumia jiwe.
Mbali na shangazi na mke wa jamaa huyo,
ndugu wengine walidai kwamba, mapema mwaka huu walisikia kutoka kwa
majirani kuwa Twalib anamtesa Harub na kumfungia kwenye banda la sungura
na kuku, lakini walipofika nyumbani hapo dokta aliwafukuza.
…Akiwa amelala kitandani.
“Baada ya hapo tulikwenda kwa mjumbe wa
mtaa na kuripoti kuhusu hali hiyo. Tukampelekea Twalib barua ya wito
lakini siku ya kikao hakutokea,” alisema Siasa.
Ijumaa Wikienda
lilipofika eneo la tukio liliwashuhudia ndugu hao wakizuiwa kuingia na
mlinzi wa nyumba hiyo licha ya kuwa na mjumbe wa serikali ya mtaa kwa
madai kuwa Twalib hakuwepo na hataki mtu yeyote aingie ndani kwake.
Ndugu hao na mjumbe walilazimika kuingia
ndani kwa nguvu ambapo walijikuta wakitokwa na machozi kwa hali
waliyomkuta nayo Harub akiwa amedhoofu.
Waandishi wetu walimshuhudia mgonjwa
huyo akiwa amelala kwenye chumba kichafu ambacho upande mmoja kilikuwa
kimetengwa kwa waya na chumba chenye kuku na sungura.
Hata hivyo, mgonjwa huyo aliangua kilio
na kutoa sauti kwa tabu huku akitumia lugha ya ishara na kusababisha
mkewe na mama yake mzazi aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwamvua naye
aangue kilio.
Mwishowe ndugu hao walimchukua Harub
hadi Kituo cha Polisi cha Wazo Hill ili kutoa taarifa na kupewa jalada
WH/RB/6116/2015, TAARIFA kisha waliondoka naye kumpeleka nyumbani kwao
Kunduchi.
Waandishi wetu walipokutana na daktari
huyo na kumbwagia tuhuma hizo, alikanusha vikali ambapo alisema
shangazi zake wanamzushia mambo mengi kwa kuwa wanataka mali za baba
yake.
0 comments:
Post a Comment