Huyu ndiye Mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza Kitaifa katika Mtihani wa Kidato cha Nne kutoka shule ya Canossa Girls.Anaitwa Butogwa Charles Shija(17), akiwa mwenye furaha, nyumbani kwa wazazi wake Kipunguni Jijini la Dar es Salaam jana.Anasema kilichomsaidia kufanya vizuri ni kufanya marudio,kumwomba mungu na kujiwekea lengo la kwenda kusoma Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani.Mama yake mzazi anaitwa Angela Shija ambaye anasema binti yake tangu akiwa kidato cha kwanza aliahidi kufanya vizuri katika mtihani na amekuwa na juhudi za kujisomea kila wakati.Jina Shija ni maarufu sana kwa kabila la Kisukuma
Huyu ni Mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne Feza Girls 2015 , Mtanzania mwenye asili ya China, Congcong Wang,ameshika Nafasi ya pili Kitaifa ,amepata alama 'B' somo la Kiswahili .Alijiunga na shule hiyo mwaka 2006 akitokea China na Kulazimika kujifunza lugha tatu ambazo ni Kiswahili,Kiingereza na Kituruki ambazo hutumika katika shule hiyo ili aweze kuwasiliana na wenzake vizuri pamoja na walimu wake.
Anasema: Walinisaidia wakijua baadhi ya vitu sitaelewa,cha muhimu ni kwamba hakuna njia ya mkato zaidi ya kusoma
0 comments:
Post a Comment