Inasikitisha!
Mrembo Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amejikuta akiangua kilio baada ya
kupewa maneno ya kejeli na aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ kufuatia kupigwa chini kwenye kura za kuwania Ubunge wa Viti
Maalum mkoani Singida kupitia Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mrembo kunako Bongo movie aliyekuwa akiwania ubunge wa viti maalum Ikungi Singida, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini kililiambia Ijumaa Wikienda
kwamba, Julai 24, mwaka huu Wema alijikuta akiangua kilio cha aina yake
kufuatia maneno ya kumshambulia kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo
Diamond muda mfupi baada ya kuangushwa katika kinyang’anyiro hicho cha
ubunge kilichofanyika katika Wilaya ya Ikugi, Singida.
Kiliendelea kunyetisha kwa sauti ya
upole kwamba, miongoni mwa vitu vilivyosababisha Wema kudondosha chozi
ni pamoja na maneno ya Diamond aliyoandika muda mfupi tu katika ukurasa
wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram huku akijua wazi kwamba
mwanadada huyo alishapoteza fedha nyingi ili apate nafasi ya kuingia
mjengoni, Dodoma.
“Ujue watu wengi hawakujua kilichomuuma
zaidi Wema ila mimi kaniambia kwamba, kilichomuuma si kukosa nafasi hiyo
ila ni maneno ya Diamond aliyoandika kwenye ukurasa wake wa Instagram
maana yamemchoma na hakutarajia kama ‘ex’ wake huyo angefikia hatua ya
kuonesha chuki zake wazi kiasi hicho.
“Wema alikuwa na matumaini makubwa ya
kuibuka mshindi kwenye mchakato huo kutokana na kujulikana kwake na
namna wajumbe walivyokuwa wanampa matumaini ila hali imekuwa ndivyo
sivyo.
“Baada ya matokeo, sisi tulimuona akiwa
kawaida tu lakini baadaye alibadilika na kuwa mnyonge hali iliyonifanya
nimuulize kisa cha kuwa vile ndipo akaniambia maneno ya kwenye mitandao
yanamchoma.
KUMBE ALITUMIA FEDHA NYINGI
“Unajua amekuwa wa mwisho kwa kupata
kura 90 hivyo ni wazi kuwa hana chake tena katika kuwania nafasi hiyo na
alitumia fedha nyingi kwenye kuomba kura kwa wanachama (haikufafanuliwa
kivipi kwa madai kwamba alitoa hongo), hawezi tena kuingia mjengoni
kwani nafasi tatu zimechukuliwa na wenzake hao, hivyo anachotakiwa
kuanzia sasa ni kujipanga ili kama itawezekana baada ya miaka mitano
ijayo agombee tena,” kilisema chanzo hicho.
WEMA ANASEMAJE?
Ijumaa Wikienda, kama
kawaida yake, baada ya kupata ‘unyunyuzi’ huo lilimtafuta Wema ili aweze
kuanika hisia zake baada ya matumaini yake kuishia njiani ambapo
alisema kwamba anaamini kila jambo limepangwa na Mungu hivyo haikuwa
bahati yake zaidi ataendelea kujipanga kwa kipindi kingine.
“Namuachia Mungu maana kila jambo
hupangwa na yeye, hakuna mtu anayeshindana akashindwa halafu awe ‘happy’
tu, nimeumia isipokuwa Mungu ndiye jibu la kila kitu,” alisema Wema na
kuongeza:
“Nilipoamua kugombea nilijua kuna kupata na kukosa. Awamu hii nimekosa lakini dunia inazunguka.
“Nawashukuru wote walionipinga kwa sababu waliniongezea ujasiri.”
Kwa upande wa Meneja wa Wema, Martin
Kadinda aliweka ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Haikuwa vile
tulivyotarajia….hongera Aysharose Mattembe.”
Maneno ambayo aliyaposti Diamond
yaliyomchoma Wema hadi kufikia hatua ya kumwaga chozi yalisomeka:
“Sitaacha kuwashukuru Wanasinginda kwa mapenzi yenu ya dhati
mliyonioneshea, Moshi tukutane Kili Home.”
Wema alikuwa ni miongoni mwa wagombea wa
Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), katika Wilaya ya Ikungi,
Singida ambapo mchakato wa kura za maoni ulifanyika Julai 24, ambapo
aliambulia kura 90 akishika nafasi ya nne huku mtu wa kwanza Aysharose
Mattembe alikipata kura 311, nafasi ya pili ikichukuliwa na Martha Mlata
aliyezoa kura 235 na ya tatu akichukua Diana Chilolo kwa kura 182.
SABABU ZA KUSHINDWA
Wikiendi iliyopita mjadala mkubwa kwenye
mitandao ya kijamii ilikuwa ni ishu ya Wema kukosa ubunge ambapo
miongoni mwa sababu hizo ni skendo mfululizo na picha zisizokuwa na
maadili zilizojaa mitandaoni na kwamba CCM kwa sasa ipo kwenye mkakati
mkali wa kusimamia maadili ya chama.
0 comments:
Post a Comment