Lowassa ametangaza
uamuzi huo jana katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika
Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar na kusema amekubali mwaliko wa vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Amesema
kuwa CCM haikumtendea haki katika kupitisha majina ya wagombea urais
hivyo hawezi kuendelea kubaki kwenye chama hicho ‘’ Niliwekewa mizengwe
kuhakikisha Jina langu halifiki Kamati Kuu na Halmashauri Kuu’’.
Waziri
Mkuu huyo wa zamani ameeleza kuwa nia yake ni kuleta mabadiliko hivyo
kujiunga na Chadema ni kuendeleza nia yake ya kuwatumikia Watanzania ‘’
CCM Si baba yangu wala Mama yangu, Watanzania kama wameyakosa mabadiliko
ndani ya CCM, basi watayapata nje ya CCM’’
Aidha
ameongeza kuwa hajakurupuka kufanya uamuzi huo na kuendelea kubaki
ndani ya CCM itakuwa ni unafiki ‘’ Sijakurupuka kwa uamuzi huu hivyo
basi kuanzia leo natangaza rasmi kuondoka CCM na kujiunga na UKAWA
kupitia Chadema’’ alisema Lowassa.
Hata hivyo muda
mfupi baada ya kutangaza uamuzi huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe alimkabidhi Lowassa kadi ya uwanachama.
0 comments:
Post a Comment