LATEST POSTS

Saturday, June 20, 2015

MAAJABU YA DUNIA!! NYOKA WAMFANYIA MTU MASAJI KWA GHARAMA YA DOLA 47

UNAPENDA kufanyiwa masaji na nyoka? Unaweza kukaza roho na usiogope kung’atwa? Kama ndio basi nenda nchini Indonesia utaipata kwa raha zako. 
Masaji hiyo inapatikana Bali Heritage Reflexology and Spa huko Jakarta, Indonesia ambako wanaweza kukuondolea uchovu wako wa siku nzima kwa massage ya nguvu inayofanywa na nyoka mkubwa.


Masaji hiyo inafanyika kwa nyoka huyo kuwekwa juu ya mwili wa mteja na mengine huachiwa yeye nyoka afanya yake. Ili kupata huduma hii mteja hutakiwa kulipa dola 47 ambazo ni zaidi ya shilingi 76,000 za Tanzania

0 comments: