SAA chache kabla ya kuanza kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, staa wa sinema za Kibongo, Haji Adam ‘Baba Haji’ ameangusha bonge la harusi baada kufunga ndoa na mrembo aliyetajwa kwa jina la Latifa Sharji wiki moja iliyopita huku mastaa wakifanya kufuru kama kawaida yao.
Katika pati hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kibao wa Bongo Movies huku gazeti hili nalo likijipenyeza ndani, waalikwa walikula na kunywa hadi wakasaza kabla ya muda wa zawadi na kusakata muziki.Kwenye shughuli hiyo, kadiri watu walivyokuwa wakipiga ulabu ndivyo sherehe ilivyokuwa ikichangamka na mastaa kujikuta wakiserebuka muziki kwa kwenda mbele.
Baadhi ya wasanii walioongoza kutunza ni tajiri mfupi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ambaye alimwaga fedha taslimu Sh. milioni 2 akifuatiwa na Single Mtambalike ‘Richie’, Jacob Steven ‘JB’, Vincent Kigosi ‘Ray’ na wengine waliokuwa fedha za kudunduliza.
Kwa upande wa mastaa wa kike, Kajala Masanja ‘Kay’ aliongoza kwa kumwaga mkwanja akifuatiwa na Jacqueline Wolper Massawe, Wastara Juma, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ na watoto wengine wa mjini.
Hadi gazeti hili linaanua jamvi ukumbini hapo usiku mnene, baadhi ya mastaa walikuwa wakiendelea kusakata rhumba na kupiga kinywaji
0 comments:
Post a Comment