LATEST POSTS

Monday, March 10, 2014

Juhudi za kutafuta ndege ya Malaysia iliyopotea ikiwa na abiria 227 zinaendelea

 
Meli, helikopta na ndege zinashiriki katika zoezi la kuitafuta ndege ya shirika la ndege la Malaysia Airlines iliyopotea usiku wa ijumaa kuamkia jumamosi, machi 8 mwaka 2014.
Meli, helikopta na ndege zinashiriki katika zoezi la kuitafuta ndege ya shirika la ndege la Malaysia Airlines iliyopotea usiku wa ijumaa kuamkia jumamosi, machi 8 mwaka 2014.

Juhudi za kutafuta ndege aina ya Boeing 777 ya Malaysia Airlines iliopotea usiku wa ijumaa kuamkia jumamosisaa ikiwa na abiria 227 zimeendelea kushika kasi mapema leo asubuhi katika eneo la kisiwa kilichopo nchini Vietnam ambapo inashukiwa huenda mabaki ya ndege hiyo yakapatikana katika eneo hilo.

Baada ya masaa zaidi ya 48, matumaini ya kupatikana kwa ndege MH370 yameanza kukosekana.

Ndege hio ya aina ya Boeing 777, ilikua ikitokea Kuala Lumper ikielekea Beijing nchini China ikiwa na abiria 227 kutoka mataifa 14, wakiwemo 153 wa China, raia 4 wa Ufaransa na timu ya watu 12 wakiwa ni wafanyakazi wa ndani ya ndege hio.
Mamlaka ya usafiri wa anga wa Vietnam imeendesha uchunguzi jana jioni na kugundua vifaa viwili ambavyo huenda vilidondoka kutoka kwenye ndege hio kwenye umbali wa kilomita 80 katika kisiwa cha Tho Chu.
“Lakini hakuna taarifa yoyote kuhusiana na vifaa hivyo iliyotolewa”, amesema Abdul Rahman, katika mkutano na waandishi wa habari.
Meli mbili zimetumwa katika kisiwa cha Tho Chu, ili kuendelea na uchunguzi zaidi, naibu mkurugenzi wa mamlaka ya anga ya Vietnam, Ngo Van Phat, amelithibitishia shirika la habari la Ufaransa AFP.
Wakati juhudi za kutafuta mabaki ya ndege hiyo zikiendelea, utata umeibuka juu ya abiria ambao walikuwa wanatumia vitambulisho bandia.
Viongozi wa Malaysia, ambao wameanzisha uchunguzi kuhusu uwezekano wa tukio la kigaidi kufuatia kupotea kwa ndege hiyo, baada ya kugundulika kua watu wawili ambao walikua wakisafiri ndani ya ndege hio walikua na passport bandia, wameendelea kuendesha msako katika maeneo yaliyo karibu na taifa lao, kusini mwa kisiwa cha Thoi Chu.
Mkurungenzi wa idara ya Usafiri wa anga nchini Malyasia Azharuddin Abdul Rahman amesema hadi sasa hawajafaanikiwa kupata mabaki ya ndege hiyo licha ya taarifa kutoka Vietnam.
Ndege hiyo MH370 ilipotea saa moja baada ya kuondoka mjini Kuala Lumper ikielekea Beijing nchini China ambapo raia 153 wa China walisafiri ndani ya ndege hiyo.

0 comments: