LATEST POSTS

Monday, March 10, 2014

Wamama na Wadada hii inatuhusu sana. Ukivaa blauzi ya wazi, kwapa zako ziwe safi.

KATIKA maisha yetu ya kila siku hapa duniani kuna vitu vingi vinavyotuzunguka, ingawaje si vitu vyote ni vya muhimu kwa kila mtu, lakini kuna vitu kama vile chakula, malazi na mavazi, hivi ni vitu ambavyo binadamu wote tunatakiwa kuwa navyo.
Ingawa kutokana na tofauti mbalimbali kama vile za kiuchumi na kijamii, viwango vya haya mahitaji muhimu ya maisha yetu hutofautiana miongoni mwetu.
Pamoja na tofauti zilizopo lakini tunapokuja kuzungumzia suala la mavazi, ni dhahiri tunatakiwa tutambue ni wakati gani na muda gani tunatakiwa kuvaa nguo au mavazi ya aina gani, si nguo za kuongelea wewe unataka uzivae ofisini, mwingine naye nguo za kulalia yeye ndio anataka azitumie wakati wa sherehe.
Kwa ujumla ukishaonekana unavaa kinyume na malengo halisi ya aina ya hiyo nguo uliyoivaa, kwa wale wanaotambua matumizi yake lazima watakuona wewe mvaaji kuwa ni kituko mbele ya jamii husika.
Watu wengine nao pamoja na kutambua vizuri ni wapi na kwa wakati gani wavae nini na nini wasivae, lakini vituko vyao wao ni kutokuzingatia sifa za miili yao na aina ya mavazi wanayopenda kuyavaa.
Mwanadada ana kitambi mithili ya mama mjaamzito eti na yeye anataka kuvaa kitop na kimini, sasa hapo kama si kutaka kuwachekesha wasiotaka kucheka ni nini hasa unakitegemea kitatokea mbele ya hao watakao shuhudia kumuona mwanadada wa aina hiyo?
Pamoja na hao wote, lakini kilichonichosha zaidi ni pale nilipokumbana na mwanadada aliyevalia blauzi yake ya wazi ambayo kwa rangi na jinsi ilivyoonekana kutokana na maumbile yake, kwa ujumla ilimpendeza, ila tatizo hizo kwapa zake alizozianika hadharani huku zikiwa haziendani kabisa na mwonekano wake.
Inashangaza pale unapoingia ndani ya daladala na kumuona mwanadada kavalia blauzi ambayo imeshonwa katika mtindo unaoruhusu sehemu za kwapa zake kuwa wazi, lakini cha ajabu kwapa hizo zimefunikwa na nywele zisizofahamika ni za rangi gani!
Nyeusi si nyeusi wala njano si njano, lakini yeye bila wasiwasi anadiriki hata kunyanyua mikono yake juu na kushikilia bomba la daladala bila ya kujali ni kwa jinsi gani anaharibu hali ya hewa ndani ya basi hilo na kuwachefua abiria wengine.
Ingawaje niliyemshuhudia mimi alikuwa ni mwanadada tena asingeziachia kwapa zake hadharani na kuonekana kuwa ni chafu ningempa sifa zote za mwanadada mrembo, lakini wenye tabia hii ya kuziachia kwapa zao hadharani kutokana na mitindo ya nguo zao wanazozivaa huku kwapa hizo zikiwa ni chafu, si kina dada tu, hata wanaume wapo.
Kwangu inanisikitisha zaidi pale ninapomuona mwanadada ambaye kwa asili yake mara zote anatakiwa kuwa msafi au kwa lugha nyingine mtanashati, cha ajabu anatoka nyumbani kwake akiwa amekumbuka urembo mwingine wote, lakini anaziachia kwapa zake zikiwa katika hali ya uchafu kabisa na kujichanganya katika daladala kwa kushika bomba bila ya wasiwasi wowote juu ya uchafu huo ambao kwa mwanamke tena binti wa kizazi cha dot com, ni dhahiri aibu inakuwa ni mara dufu!
Hatukatai, nguo zilizoshonwa katika mitindo ya kuachia kwapa zote nje ni nzuri na zina mvuto wake kwa akinadada au akina mama, lakini kwa nini mtu kabla ya kufikia uamuzi wa kuvaa nguo ya aina hiyo asijitathmini kwanza yeye mwenyewe kama kweli yupo katika mazingira sahihi ya kuyaachia hadharani makwapa yake au la?
Kwa maana kama mvaaji wa nguo hizo akitambua hilo, bila shaka atalazimika kwanza kuzisafisha kwapa zake katika kiwango ambacho hakitawachefua watu wengine pindi itakapomtokea amenyoosha mikono yake juu huku watu wengine wakiwa karibu yake kama vile ilivyomtokea huyo mwanadada ndani ya daladala.
Uchafu ni uchafu tu, na kwa ujumla haupendezi, uwe ni kwa mwanamke au mwanamume, wote hawatakiwi kuwa wachafu. Hayo si mambo hata kidogo, utavaaje blauzi au fulana ya wazi huku kwapa zako zikiwa chafu

0 comments: