Zaidi ya wachimbaji
wadogo wa dhahabu 7000 wilayani Nzega mkoani Tabora wameiomba Serikali kupitia
Wizara ya Nishati na Madini kuwapatia leseni ya uchimbaji katika mgodi mdogo wa
dhahabu wa Mwanshina, uliopo pembezoni mwa mgodi mkubwa wa dhahabu wa Resolute.
Wakizungumza na waandishi
wa habari katika mgodi huo, waliomba Serikali iwapatie leseni hiyo licha ya
kukiri kuvamia eneo hilo kutokana na kukabiliwa na shida za
kimaisha.
Walisema kuwa walivamia
eneo hilo bila kuambiwa na kiongozi yeyote kutokana na ugumu wa maisha ya
kukidhi haja zao za msing.
Mkazi wa Kijiji cha
Mwanshina, JIsena Masanja alisema walivamia eneo hilo lililopo pembezoni mwa
mgodi mkubwa ambalo halifanyiwi kazi na wawekezaji hao na kuongeza kuwa
watalinda mazingira ikiwamo kuimarisha usalama kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment