Moshi Hussein
ambaye ni mlemavu wa viungo anayeishi nyumbani kwa baba yake mzazi huko katika
kijiji cha Magiri wilaya ya Uyui mkoani Tabora,binti huyu ana umri wa miaka 13
hajawahi kupelekwa Shule kwa maana ya kupata haki kama wapatavyo watoto
wengine,Moshi amekuwa akililia hilo kwa baba yake mzazi bila mafanikio.Jambo
baya zaidi kwa mujibu wa maelezo ya Moshi baba yake anahitaji aolewe ili aweze
kupata Ng'ombe licha ya kuwa ana umri mdogo na hawezi kukabiliana na Changamoto
za ndoa kulingana na ulemavu alionao.
Moshi kwakuwa hana
uwezo wa kutembea umbali hata wa hatua kumi anawaomba wasamalia wema kumsaidia
mambo makubwa matatu,kwanza ikibidi kumuondoa nyumbani kwao ili aepukane na ndoa
ya lazima,Pili
apelekwe shuleni kwakuwa anaona kukaa kwa baba yake ni wazi kwamba atakuwa
anatafuta umasikini mwingine wa ziada ukiachana huo wa ulemavu wa viungo ambao
umekuwa kikwazo kikubwa hata cha kujihudumia masuala mengine ya kiutu wa
mwanamke.Kwa mujibu wa maelezo yake Moshi ana mshangaa baba yake kwa uamuzi wa
kutaka aolewe kwakuwa hata ndoa yenyewe haoni kama itakuwa na maana kutokana na
ulemavu alionao na pia haoni sababu ya kuwa mzigo kwa mtu mwingine katika maisha
yake.
Moshi amekuwa
akijikatia tamaa kulingana na ulemavu alionao,"Kama ningekuwa na mama labda hata ningeweza
kupelekwa shule na mimi ningekuwa msomi kama wengine,lakini kwa hali hii ni bora
hata ningekufa nimfuate mama yangu huko aliko"
0 comments:
Post a Comment