LATEST POSTS

Wednesday, April 24, 2013

WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA WILAYA YA URAMBO, WAPEWA SEMINA KUHUSIANA NA MASUALA YA UKIMWI.


Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, wapo katika semina inayohusu masuala mbalimbali yanayohusiana na UKIMWI mahali pa kazi. Semina ni ya siku mbili ambayo imeanza tarehe 24/04/2013 hadi tarehe 25/04/2013 katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.
Akifungua semina hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe.Anna Magowa aliwaeleza washiriki kuwa, semina hiyo ni muhimu sana kwao kwani itawasaidia kupata uelewa mkubwa kuhusiana na masuala mbalimbali ya UKIMWI mahala sambamba na kuwakumbusha majukumu na wajibu wao kama Wakuu wa Idara na vitengo katika kuwasaidia Watumishi ambao wanaishi na Virusi vya UKIMWI.
Aidha, alisema, ni jukumu la Wakuu hawa kushirikiana na Waratibu Ukimwi waliopo kwenye Idara na vitengo katika kuhakikisha kwamba, Idara inaweka bajeti kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali zinazohusiana na masuala ya UKIMWI katika Idara zao pamoja na Wananchi wa Wilaya ya Urambo kwa ujumla.
Katika siku hii ya kwanza, kulikuwa na ufunguzi na mada kuu iliyoongelewa ni UKIMWI na Tohara.
Katika mada hii, washiriki wameelezwa kuwa, kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa kwa wakati na Nchi tofauti (Afrika Kusini, Kenya na Uganda, matokeo yameonyesha kuwa, wanaume waliofanyiwa tohara, wanauwezekano mkubwa wa kutokupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa asilimia sitini(60%) tofauti na wanaume ambao hawajafanyiwa tohara.
Mada zingine zitaendelea kesho.
 Na hizi ni picha za matukio yaliyojiri katika siku hii ya kwanza ya semina hii.
 
Washiriki wa semina wakifuatilia kwa umakini mada kutoka kwa Mratibu wa UKIMWI Wilaya (CHAC)

Waandishi nao hawakua nyuma kuhakikisha wanachukua mambo yote muhimu


Mratibu wa UKIMWI Wilaya (CHAC) Bw. Osear Mwabusila akiwapitisha washiriki kwenye mada kwa njia ya Power point
 



 



Fundi mitambo Bw.Sabala Lukonda akiwa makini kuhakikisha mambo yanakwenda sawa
 



Kulia ni Mwandishi wa Makala hii Mwenye suti ya kijani akifuatilia mada kwa makini
 
Uandishi unaendelea


Mwenyekiti wa semina Bw.Erasto Konga akielezea jambo
 
Washiriki wapo makini kwelikweli kufuatilia mada
 
Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe.Anna Magowa akisoma hotuba ya ufunguzi wa semina hiyo

Mkurugenzi Mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Eng.Richard Ruyango akiwa makini kabisa katika semina hiyo
 
Mheshimiwa Anna Magowa akifungua rasmi Semina hiyo katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo


Urambo cable ikiwa busy kazini
 
Kaimu Mganga Mkuu Wilaya ya Urambo Dr.Kheri Kagya akitoa mada ya UKIMWI na Tohara kwa Washiriki

 

 
Washiriki wa semina wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya. Kutoka kulia walioketi ni Bw. Philbert Masaba Katibu Tawala Wilaya(DAS), Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe.Anna Magowa, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Eng.Richard Ruyango na Mwenyekiti wa semina hiyo Bw.Erasto Konga.

 
 Shukrani sana.
Theresia Chacha.
 

2 comments:

Anonymous said...

Kazi nzuri sanaa Teddy. Keep it up,

Unknown said...

Asante sana mdau