LATEST POSTS

Friday, April 5, 2013

WADAU MIEMBE YA KISASA HII HAPA

Katika mihangaiko yangu ya kikazi ya kila siku, siku moja nikiwa nimeambatana na Waheshimiwa Madiwani Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango pamoja na Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, tulitembelea kikundi kimoja ambacho kinajishughulisha na shughuli ya upandaji miti ikiwemo Miti ya Matunda. Kikundi kipo katika Kijiji cha Kasungu Kaliua. Tulipofika katika bustani hiyo,  tulishangazwa na kufurahishwa na aina ya miti ya muembe ambayo ilikuwepo katika bustani hiyo. Kiukweli kila aliyekuwepo kwenye msafara huo alishangazwa na miembe hiyo.
Kwa mujibu wa maelezo ya Wanakikundi na Wataalamu wa masuala ya kilimo ni kwamba, miembe hiyo imetokana na kuunganishwa kwa miembe miwili tofauti. Aidha, ilielezwa kuwa,teknolojia ya ubebeshaji wa mimea inapelekea upatikanaji wa miembe yenye sifa ambazo wakulima wanazihitaji mfano ladha nzuri,ukubwa wa matunda na matunda yasiyo na nyuzinyuzi.
 
Aidha, kikundi kilieleza kuwa, miembe ya kubebeshwa huchukua muda mfupi kutoa mavuno kwani mwembe unaweza kutoa matunda ndani ya miaka miwili na nusu hadi mitatu tofauti na miembe ya asili ambayo huchukua muda si chini ya miaka mitano tangu kupandwa kuanza kutoa matunda. Na kwamba, embe la mwembe uliobebeshwa lililokomaa huwa linauwezo wa kuwa na kilo moja hadi kilo moja na nusu.


 
 Wajumbe wakishangaa mwembe huo wa kubebeshwa
 Moja ya aina ya Mti ambao unapatikana katika bustani ya kikundi hiki ni huu
 
 
Kila mjumbe alitamani kupiga picha na miembe hiyo ya kisasa
 
Wadau mnaona?
 
      Mhe.Haruna Kasele Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri akipiga picha na mwembe huu

 Aliyechuchumaa ni aliyekuwa kaimu Afisa Kilimo aliyekua ameambatana na Madiwani katika ziara hiyo Bw. John Mtesigwa
Kutoka kushoto ni Mhe.Mashaka Kayanda na Mhe.Alexander Pugwi wakifurahia miembe ya kisasa

Mhe.Alexander Pugwi
 
Miembe hii huhitaji kupanda ngazi ili uchume embe. Hata mtoto anayetambaa anachuma tu kama unavyouona mti huu ulivyo

Inafurahisha sana

Diwani wa Kata ya Songambele Mhe.Elia P.Kafwenda
 


Diwani wa Kata ya Ussoke Mhe.Kandola

Theresia Chacha,
Mwandishi.

1 comments:

Anonymous said...

nimependa kilimo cha miembe mimi nahitaji kuipanda shambani kwangu nipo dar ila shamba langu lipo mkoa wa pwani nitawapataje naomba contact zao kama unazo