LATEST POSTS

Monday, March 17, 2014

Mamia wadaiwa kufa baada ya kukanyagana

WATU kadhaa wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya kutokea vurumai walipokuwa wakihudhuria zoezi la serikali la kuwaajiri kazi, katika miji mbalimbali nchini Nigeria.

Maelfu ya watu waliokuwa na hamu kubwa ya kupata ajira, walijitokeza kwa wingi katika zoezi hilo kote nchini humo; waliokuwa wamejitokeza katika ofisi za wizara ya uhamiaji.
Kwa mujibu wa BBC, walioshuhudia walisema kuwa karibu watu saba wamekufa papo hapo kutokana na umati huo uliosukumana atika lango kuu la uwanja wa kitaifa wa michezo mjini Abuja.
Wengine walipoteza maisha yao katika uwanja wa michezo wa Port Harcourt na uwanja wa shule katika mji wa Minna.
Tatizo la ajira kwa vijana ni kubwa mno nchini Nigeria huku zaidi ya robo tatu ya vijana walio chini ya umri wa miaka 25 wakiishi bila kazi.

Maelfu ya watu walijitokeza kufanya mtihani wa ajira huku ikiarifiwa kuwa mkanyagano huo ulitokea wakati wakijaribu kuingia katikati ya uwanja huo wa michezo.

0 comments: