LATEST POSTS

Wednesday, March 26, 2014

MICHAEL AGUSTINE LUKINDO MTANZANIA ALIYEFARIKI WISCONSIN WANATAFUTWA NDUGU ZAKE MAITI KUCHOMWA MOTO JUMAMOSI‏

 
Michael Agustine Lukindo enzi ya uhai wake.

Kuna Mtanzania mwenzetu amefariki Madison Wisconsin nchini Marekani, wanatafutwa ndugu zake. ni mtu wa Tanga Michael Agustine Lukindo. Alikuja USA miaka mingi iliyopita, inasemekana zaidi ya miaka thelathini.
Ameacha mke (African American) na watoto wanne, mkubwa alizaliwa 1989 familia yake haijui ndugu za Michael.
Mazishi yatafanyika Jumamosi March 29, 2014, ila mwili utachomwa. Kama unafununu au kujua lolote kuhusiana na ndugu yetu huyu unijulishe mimi naitwa Lugome Fautus email yangu ni.
Lengo nikuweza kuwafahamisha ndugu zake nyumbani Tanzania. Asante kwa ushirikiano wako. Tunatanguliza shukurani.
 
Michael Lukindo akiwa na mkewe na watoto wake wanne.
 
Historia yake
 
Augustino “Mike” Lukindo, 59 , departed this life on Sunday, March 16, 2014, surrounded by his immediate family. Mike was born and raised in Tanzania, Africa (Tanga) to Augustino and Josephine Lukindo. He moved to America in the early 1980’s, where he lived in Providence, Rhode Island for five years. Mike married Lillie B. in Rhode Island, and later moved to Madison where they built their family of four and confessed his life to Christ.
Mike was a family man, a funny guy with a good sense of humor. He loved to joke around. He liked comedy and he loved going to his children’s school to participate. He always had a smile and his favorite phrases were “Hey Brother-in-law , Sister-in-law, where the party at?” Mike was of true African decent, he never forgot his heritage.

Augustino “Mike” was proceeded in death by his mother, father, siblings and one sister-in-law, Irlene Person-Wilson. Mike is survived by his wife Lillie, son Augustino Franklin, three daughters Amanda, Josephine and Adrian Lukindo, all of Madison.
 
kutoka Urambonews.com
Watanzania wenzangu, hatukatai mtu kutoka kwenda katika nchi za wenzetu kujitafutia maisha. Lakini Mungu akitufungulia, ni busara sana kukumbuka nyumbani. Kule tulikotoka, kwa wazazi wetu, bibi na babu zetu hali kadhalika kuona ndugu na jamaa zetu. Hii ni aibu kubwa sana mtu kukaa ugenini kwa miaka thelathini pasipo kuwa na mawasiliano na ndugu na jamaa zake. Okay,hukutaka kurudi basi hata kuwasiliana nao na kuwaunganisha na mkeo na watoto wako napo ilikua shida? tunaonaga wengine waliokuwepo huko nchi za mbele huwa wanakuja japo kila baada ya miaka mitano na simu wanapiga. Siku hizi simu zipo kila mahali ulishindiwa nini?
Hayo maendeleo yaliyopo huko ndio yanawafanya msahau nyumbani kweli? Haya kuna raha gani unaishi maisha mazuri pasipo kujua kama baba na mama yako uliowaacha nyumbani ambao walikuhangaikia na kukufikisha hapo ulipofikia kama wanakula, wagali hai au wamekufa? Wala hushtuki?.
Haya sasa, yametokea yaliyotokea ndio mnaanza kuhangaika kutafuta ndugu zake kweli? mtawatoa wapi? Na hata ikitokea bahati wakapatikana wataweza kuja huko Marekani maskini ya Mungu pengine wameisha jizeekea na hela hawana.
Aah!Inaumiza sana jamani maana naongea kama mzazi sasa.
Jamani waandaaji filamu mi nafikiri haya ndiyo mambo ambayo inafaa tuyakemee kupitia filamu zetu badala ya kukalia kuandaa filamu za mapeeenzi tu.
Naomba nimalizie kwa kuwaambia ndugu zetu walioko katika nchi za watu kwamba hebu wawe wanakumbuka nyumbani walikotoka. Hawakukosea waliosema Go East, go West, home is best.

0 comments: