Mlima Kilimanjaro.
Mtalii kutoka nchini Ujerumani anayefahamika kwa jina la Bi. Jeanne
Traska (32) akiwa na muongoza wageni Athuman Juma leo majira ya saa
mbili na nusu asubuhi wamekwama katika kilele cha Mawenzi Mlimani
Kilimanjaro kwa kamba iliyonasa na kuwafanya wasiweze kushuka chini wala
kwenda juu.
Bi. Jeanne na Athuman Juma walianza kupanda mlima kupitia Kampuni ya
Nordic Tours tarehe 18.3.2014 kwa kutumia njia ya Rongai - Kibo –Marangu
safari ambayo ingewachukua siku tano.
Hadi sasa taarifa za awali zinaonyesha kuwa Bi. Jeanne alitakiwa
kwenda kileleni Kibo lakini katika mazingira yasiyofahamika alibadili
uamuzi na kuelekea kilele cha Mawenzi ambacho huwa hakitumiwi na watalii
isipokuwa kwa kujaza fomu maalum inayoonyesha kuwa mgeni amekubali kwa
hiyari yake kupanda kilele hicho.
Shirika la Hifadhi za Taifa kwa kushirikiana na Kampuni ya Nordic
Tours wanaendelea na jitihada za uokoaji kwa kutumia askari ambao
wanaelekea eneo la tukio pamoja na helikopta itakayosaidia zoezi la
uokoaji kwa kutegemea na hali ya hewa itakavyotulia ambapo hivi sasa
kuna mawingu mazito katika eneo la mlima.
Umma utaendelea kufahamishwa maendeleo ya jitihada za uokoaji kadri zitakavyopatikana.
Imetolewa na
Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania
22.03.2014
Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania
22.03.2014
0 comments:
Post a Comment