|
John Msumba(03)ameanza kupatiwa matibabu katika Hospitali
ya Rufaa Mbeya baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina na Madaktari baada ya
kupigwa kisha kunyimwa chakula na shangazi yake aliyefahamika kwa jina la
Mwanahawa Nassoro(32)mkazi wa Airport Kata ya
Iyela. |
|
Bibi Lahel Mbembela akilia kwa uchungu mara tu baada ya
kumwona mtoto John |
|
Bibi Lahel Mbembela akimkabidhi Muuguzi kiasi cha
shilingi 10,000/ kwa ajili ya kumsaidia mtoto
huyo |
|
Afisa Ustawi wa Jamii Subira Moses ambaye alisikitishwa
na kitendo kilichofanywa na Mwanahawa hivyo aliandika barua ya msamaha wa
matibabu ili atibiwe bure ambapo alilazwa Machi 13 Jioni baada ya Madaktari
kufanya uchunguzi wa kina. |
|
Joseph Mwaisango akimjulia hali mtoto John kulia ni
Msamaria mwema Grolia Kaguo ndiye aliyejitolea kumhudumia mtoto
John |
SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
kumshikilia Mwanamke mmoja, Mwanahawa Nasoro(32) Mkazi wa Airport Mkoani hapa
akituhumiwa kumtesa na kumnyanyasa mtoto wa kaka yake, Hatimaye mtoto huyo
aanza kupatiwa matibabu.
Mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la John
Msumba(03)ameanza kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya baada ya
kufanyiwa uchunguzi wa kina na Madaktari baada ya kupigwa kisha kunyimwa chakula
na shangazi yake aliyefahamika kwa jina la Mwanahawa Nassoro(32)mkazi wa Airport
Kata ya Iyela.
Baada ya mtuhumiwa kukamatwa Mtendaji wa mtaa Henry
Chaula aliomba msaada kwa wasamaria wema kumkimbiza Hospitali mtoto ili kuokoa
maisha kutokana na kuzorota kwa afya kulikotokana na kipigo na ukosefu wa
lishe.
Katika Hospitali ya Rufaa alipokelewa na Afisa Ustawi wa
Jamii Subira Moses ambaye alisikitishwa na kitendo kilichofanywa na Mwanahawa
hivyo aliandika barua ya msamaha wa matibabu ili atibiwe bure ambapo alilazwa
Machi 13 Jioni baada ya Madaktari kufanya uchunguzi wa
kina.
Hata hivyo Msamaria Mwema Groria Kaguo alijitolea
kulazwa pamoja na mtoto huyo kwa lengo la kusimamia huduma huku Madaktari na
wauguzi wakifanya jitihada kubwa kuokoa maisha ya mtoto huyo kutokana na sehemu
kubwa ya mwili wake umeathirika na majeraha yaliyotokana na
viboko.
Baadhi ya wasamaria wema Kikiwemo kituo cha Radio cha Bomba FM Mbeya, Gazeti la
Jamboleo Mbeya na Mtandao wa Mbeya Yetu wameanza kugharamia fedha za
matibabu hayo ambapo dawa alizoandikiwa hazipatikani Hospitali ya Rufaa na
kulazimu kununua kwenye duka nje ya Hospitali.
|
Mtoto Baraka Joseph(02) akiwa amelazwa katika hospitali
ya Rufaa mbeya |
|
Mtoto huyo ambaye aliokotwa na mama lishe anayefahamika
kwa jina la Subira Joseph Mwaijulu (Mama Sunche) mkazi wa Nonde Jijini
Mbeya,ambaye amekuwa akimhudumia tangu alipotelekezwa amesema kuwa baada ya
mtoto kuanza kusumbuliwa na ugonjwa huo aliamua kumpeleka Hospitali ya Rufaa kwa
ajili ya matibabu. |
|
Wakati huo huo,Mtoto mwenye umri wa miaka miwili jinsi ya
kiume ambaye alitelekezwa katika kituo kikuu cha mabasi Jijini Mbeya mwishoni
mwa mwaka jana amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kusumbuliwa
na ugonjwa wa ngiri.
Mtoto huyo ambaye aliokotwa na mama lishe anayefahamika
kwa jina la Subira Joseph Mwaijulu (Mama Sunche) mkazi wa Nonde Jijini
Mbeya,ambaye amekuwa akimhudumia tangu alipotelekezwa amesema kuwa baada ya
mtoto kuanza kusumbuliwa na ugonjwa huo aliamua kumpeleka Hospitali ya Rufaa kwa
ajili ya matibabu.
Baada ya uchunguzi wa Madaktari walibaini mtoto Baraka
Joseph(02) kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa ngiri hivyo waliamua kumfanyia
upasuaji Machi 12 mwaka huu ambapo hivi sasa anaendelea vema na amelazwa wadi 6
ya watoto katika hospitali ya Rufaa na hali yake inaendelea
vema.
Mama Sunche amemtaka mama aliyetelekeza mtoto huyo afike
kumchukua kwani uwezo wake ni mdogo kiuchumi sasa shughuli zake zimekwama
kutokana na muda mwingi kutumika kumhudumia mtoto pia kama mzazi wake aliona
kuwa tatizo la ugonjwa ndiyo kikwazo asihofu kwani sasa mtoto
ametibiwa.
Ametoa wito kwa wazazi na walezi kutowatelekeza watoto
kutokana na ugumu wa maisha au mafarakano katika ndoa bali wanandoa watatue
migogoro ya ndoa kwa hekima na uadilifu ili kupunguza wimbi la watoto wanaoishi
katika mazingira hatarishi.
Baadhi ya mahitaji yanayohitajika kwa mtoto huyo na
pamoja na nguo,chakula na mahitaji mengine madogo madogo kama sabuni na
mafuta.
Aidha amewaomba wasamaria wema kumsaidia chochote ili
aweze kujikimu kimaisha kwani hakutarajia kupata mtoto kwa muda huu na Asasi
zinazohudumia watoto kutokuwa na mwitikio wowote hivyo kuachiwa jukumu la kulea
mtoto na ametoa wito mwenye kuguswa awasiliane nae kwa namba za simu
0753732025.
Vitendo vya kutelekeza watoto na unyanyasaji wa watoto ni
miongoni mwa matukio yaliyoshika kasi hivi sasa katika mkoa wa Mbeya licha ya
kuwepo kwa Taasisi nyingi zianazopiga vita zikiwemo TAMWA na
TGNP.
Chanzo: Mbeya yetu
|
0 comments:
Post a Comment