Mwenyekiti wa CHADEMA Ezekiel King akiteta jambo na jamaa zake mara baada ya kuhukumiwa kwenda jela miaka 7 kwa kosa la kumjeruhi mtu kilabuni |
Askari polisi wakimsindikiza Mwenyekiti wa CHADEMA baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 7 jela |
Mmoja wa jamaa waliohudhuria mahakamani akimwaga machozi baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA mtaa wa Itiji kuhukumiwa kifungo cha miaka 7 kwa kujeruhi |
MWENYEKITI
wa serikali ya Mtaa wa Itiji Jijini Mbeya mkoani Hapa anayewakilisha (CHADEMA)
Ezekiel King(52) na mwenzake Antony Simon(53) wamehukumiwa kwenda jela miaka 7
kutokana na makosa ya shambulio na kumdhuru mwili Nicholaus Mwakasinga(56) mkazi
wa Itiji mjini humo.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi wa mahakama ya Mkoa wa
Mbeya Maria Batulaine, mbele ya mwendesha mashtaka wa serikali Juliana William
alisema kuwa washitakiwa kwa pamoja walimshambulia Mwakasinga kwa kumpiga na
kumjeruhi kichwani na mkononi wakati wakiwa katika kilabu cha pombe za kienyeji
kilichopo mtaa wa Itiji.
Alisema anawatia hatiani washitakiwa hao kutoka na kuwepo
kwa mashaka juu ya ushahidi wa watu watatu upande
utetezi kugongana na hivyo kuridhika na ushahidi wa mashahidi wa upande wa
mashtaka na
hivyo kuwatia hatiani na kwamba hata hivyo wanayo fursa ya kukata rufaa iwapo
hawajaridhika na hukumu iliyotolewa.
Akitoa mifano ya kesi mbalimbali
zinazoshabihiana na kesi hiyo Hakimu Batulaine alisema kuwa makosa hayo ni
kinyume cha kifungu sheria cha
kanuni ya adhabu namba 225 sura ya 6 iliyofanyiwa marekebisho mwaka
2002.
Hakimu Batulaine alisema kuwa katika maelezo ya shahidi
namba moja Mwakasinga ambaye
ndiye mlalamikaji ni
kwamba alijeruhiwa na kuumizwa na washitakiwa alipoingia katika kilabu cha pombe
za kienyeji na kwamba
alifanyiwa hivyo baada ya kuingia ndani ya kilabu hicho na kusukumwana kuanguka
nje.
Alisema katika maelezo hayo shahidi namba moja hadi namba
tatu wa upande wa mashtaka walitoa ushahidi unaofanana lakini maelezo ya
mashahidi wa upande wa utetezi yanajichanganya na hivyo kutoa mashaka juu ya
utetezi wao.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mlalamikaji
Mwakasinga alipigwa na kujeruhiwa na washitakiwa na baadaye washitakiwa hao
walimchukua na kumpeleka kituo cha Polisi wakidai kuwa mlalamikaji Mwakasinga
alikuwa akifanya vurugu kilabuni
.
Hata hivyo mlalamikaji ambaye alilazwa katika hospitali
ya rufaa wodi namba nne ambayo hulazwa watu wenye ugonjwa wa akili ili kumpima
kama alifanya vurugu kutokana na ugonjwa wa akili alipotoka alifungua mashtaka
ya kupigwa na washitakiwa hao ambao walikamatwa na kufunguliwa kesi ya kudhuru
mwili.
Katika utetezi wake kabla ya kutolewa hukumu Mshitakiwa
King aliomba mahakama impunguzie adhabu kutokana na kuwa na watoto sita na kuwa
hakujua kama kitendo cha yeye kama kiongozi wa mtaa kuamka kwenda
kwenye tukio kingemtia hatiani.
0 comments:
Post a Comment