LATEST POSTS

Saturday, April 26, 2014

SHEREHE ZA MIAKA HAMSINI YA MUUNGANO ZAFANA


Doria ya farasi wa polisi wakikatisha katika Uwanja wa Uhuru leo kuhakikisha usalama.
Magari mbalimbali kutoka idara tofauti serikalini yakiwa yamepaki katika Uwanja wa Uhuru.
Hao ni askari wa paredi …



Doria ya farasi wa polisi wakikatisha katika Uwanja wa Uhuru leo kuhakikisha usalama.
Magari mbalimbali kutoka idara tofauti serikalini yakiwa yamepaki katika Uwanja wa Uhuru.
Hao ni askari wa paredi wakiwa uwanjani huku umati mkubwa ukiwa umeketi uwanjani hapo.
Wananchi wakiwa katika majukwaa mbalimbali kama inavyoonekana.
Askari wa JWTZ kikosi cha anga wakitoka nje ya uwanja baada ya kutoa heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu.
Askari kwa kikosi cha komandoo wakiingia uwanjani kwa ajiri ya heshima kwa amiri jeshi mkuu huku wakiwa wameshikilia bunduki za AK47
komando kutoka kikosi cha Sangasanga wakiingia kwa mbwembe kumuonyesha Amiri Jeshi Mkuu jinsi wanavyojilinda wakati wakiwa wamevamiwa, kikosi ambacho kimeonesha buruduni ya hali ya juu.
Rangi hiyo ni ishara ya kuwapokea makomandoo walioko angani ikli waweze kutua sehemu gani , walioko chini ni makomando ambao wanahakikisha wenzao watafika katika hali ganiRais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Jeshi la wananchi…
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Jeshi la wananchi kwenye sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
Kikosi cha Makomandoo kikipita kwa mwendo wa aina yake wakati wa sherehe za miaka 50 ya Muungano.

Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano ambazo zimefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Kikosi cha Makomandoo kikitoa salaam kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.
Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana bila kutumia nyenzo hapa wakivunja matofali kwa kutumia kichwa na mikono.
Baadhi ya silaha zakijeshi zikipitishwa mbele ya umati kuonyesha uwezo mkubwa wa jeshi letu.
Kikosi cha Wanamaji
Ndege za kivita zikilinda Ndege ya Rais katika maonyesho ya Ndege yaliofanyika kwenye Kilele cha Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano.
Askari wa kikosi cha Mwamvuli akishuka kutoka futi 4500 kwenye uwanja wa Uhuru kwenye kilele cha miaka 50.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pongezi mmoja wa wanajeshi wa kikosi cha mwamvuli .
Maandamano ya Pikipiki.
Matembezi maalum ya kusheherekea miaka 50 ya Muungano .
Njiwa wakirushwa juu kama ishara ya miaka 50 ya Muungano ambapo watu waliorusha njiwa hao nao wametimiza miaka 50.


 

0 comments: