IDARA ya Uhamiaji imekumbwa na kashfa nyingine ya kuajiri watoto na ndugu wa vigogo wa idara hiyo.
Hayo yalibainika baada ya idara hiyo kutoa matangazo katika vyombo
mbalimbali vya habari yaliyoonyesha majina ya waliofaulu usaili wa
kutakiwa kujaza nafasi za konstebo na koplo wa Uhamiaji.
Tangazo hilo linaonyesha kuwa waliochaguliwa watatakiwa kuripoti makao makuu ya Uhamiaji Agosti 6.
Chanzo cha ndani cha habari ambacho hakikutaka jina lake litajwe,
kilieleza kuwa kati ya watu waliochaguliwa, idadi kubwa ni watoto na
ndugu wa maofisa wa Uhamiaji.
Kilieleza kuwa urasimu katika idara za serikali umeendelea ambapo
hali inaonyesha kuwa bila kuwa na ndugu ni ngumu Mtanzania wa kawaida
kupata ajira.
Chanzo hicho kilitaja majina ya walioitwa kazini na kubainisha
uhusiano wao na watendaji waliopo idarani hapo ni Abdulhaq Amin Mandemla
anayesadikiwa kuwa mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Amin Mandemla na Alphonce
E. Kishe anayedaiwa kuwa mtoto wa Ofisa Uhamiaji Aleluya Kishe.
Wengine ni Asha Burhan Idd, ndugu wa Ofisa Uhusiano Tatu Burhan Idd;
Betrice Temba, ndugu wa Ofisa Uhamiaji Joseph Kasike na Geofrey Justine
Mhagama, ndugu wa Ofsa Uhamiaji Rose Mhagama.
Aidha wamo Iginga Daniel Mgendi, mtoto wa Ofisa Uhamiaji Daniel
Mgendi; Issack Michael Makwinya, mtoto wa aliyekuwa Ofisa Uhamiaji
Makwinya; John Alfred Mungulu, mtoto wa Ofisa wa Uhamiaji Alfred Mungulu
na Joseph A. Milambo ambaye ni mtoto wa karani wa Uhamiaji, Milambo.
Wengine ni Michael J. Choma, mtoto wa Ofisa Uhamiaji John Choma;
Shimba H. Zakayo, mtoto wa Ofisa Uhamiaji Zakayo Mchele; Upendo Mgonja
ambaye ni mtoto wa Ofisa Uhamiaji Mgonja na Vaileth A. Kidesu, mtoto wa
Ofisa Uhamiaji Adam Kidesu.
Wamo pia Elizabeth Edward, ndugu wa Edward Martin; Ester Mahirane,
ndugu wa Mahirane; Basil Lucian John, ndugu wa Ofisa Uhamiaji Dismas
Lucian; Frank G. Kajura, ndugu wa Ofisa Uhamiaji Kajura na Jacob P
Ulungi ambaye ni ndugu wa Ofisa Uhamiaji Magnus Ulungi.
Wengine ni Janeth John Millinga, ndugu wa aliyekuwa Ofisa Uhamiaji
Millinga; Janeth R. Lukuwi, ndugu wa Ofisa Uhamiaji Eliza Lukuwi; Joseph
N. Yondani, mtoto wa Ofisa Uhamiaji Mary Yondani; Leila Khatib Irovya,
mtoto wa Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Naibu Kamishna, Abbas
Irovya.
Lucian F Mlula, ndugu wa Ofisa Uhamiaji Dismas Mlula; Neema Kasiano
Lukos, ndugu wa Ofisa Uhamiaji Zubeda Abbas; Pendo Daudi Gambadu, ndugu
wa Ofisa Uhamiaji Gambadu; Paschalia E. Mwenda, ndugu wa Ofisa Uhamiaji
Martin Edward Mwenda.
Wengine ni Theresia Ernest Kalunde, mtoto wa Ofisa Uhamiaji Ernest
Kalunde; Victor G. Mlay, mtoto wa aliyekuwa Ofisa Uhamiaji, Vitalis
Mlay; Catherine J. Mapunda, mtoto wa Ofisa Uhamiaji Lucy Mapunda.
Gazeti hili lilimtafuta Ofisa Uhusiano wa Uhamiaji, Tatu Burhan,
kufahamu ukweli kuhusu jambo hilo, lakini simu yake iliita bila
mafanikio na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms) hakujibu.
Tanzania Daima Jumapili, liliwasiliana na Msemaji Mkuu wa Uhamiaji,
Abbas Irovyi ambaye naye hakupatikana na simu yake haikuwa na majibu.
Naibu Msemaji wa Uhamiaji, Mbaraka Batenga, naye hakupatikana kama ilivyo kwa wenzake.
Tanzania Daima Jumapili, liliwasiliana na mmoja wa watedaji wa ofisi
ya uhusiano, Juma Dau, ambaye alisema maofisa wengi wako nje ya nchi
kikazi.
Hata hivyo, Dau, alisema yeye hana mamlaka ya kulizungumzia jambo
hilo huku akilielekeza Tanzania Daima Jumapili, liwasiliane na Kaimu
Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Batenga.
Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Idara ya Uhamiaji ilitangaza nafasi za kazi 70 kwa wahitimu wenye shahada moja na kuendelea.
Ambapo awali majina ya maombi yalikuwa zaidi ya 20,000 na uongozi wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ulipitisha majina ya waombaji 10,800
ili washindanie nafasi 70 tu katika usaili uliofanyika Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam Juni 13, mwaka huu.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment