WAANDAAJI
wa tamasha kubwa la filamu Korea Ya kusini BUSAN wametetea uamuzi wao
wa kuonesha filamu iliyoleta utata nchini humo ya Driving Bell, 'The
Truth Shall Not Sink With Sewol'
Filamu
hiyo inayoelezea maafa ya majini yaliyo ikumba nchini hiyo imeonyeshwa
kwa mara ya kwanza siku ya mwisho ya tamasha hilo kwa kuhudhuriwa na
idadi kubwa ya watu kuliko filamu zote.
Tamasha
hilo ambalo lime hitimishwa hapo jana ilionesha kwa mara ya kwanza
filamu hiyo fupi inayolezea kwa ujumla jinsi uokoaji ulivyofanyika na
kushuhudia Wananchi wa korea kusini wakihangamia katika ajali hiyo ya
majini iliyotokea nchini humo mwezi April mwaka huku ikidaiwa kupoteza
maisha ya watu zaidi 300.
Waandaji
wanasema kuwa watu wanahitaji kutoa maoni yao na sauti zao zisikike, na
kila filamu inayooneshwa katika tamasha hilo ina umuhimu kwa wananchini
na wapo tayari kuwajibika endapo lolote litatokea.
Muandaaji
Hapo
awali ilitaarifiwa kuwa waaandaji hao waliambiwa waiondoe filamu hiyo
kwenye orodha ya filamu zitakazooneshwa ikiwa ni shinikizo kutoka kwa
baadhi ya wanasiasa akiwemo meya wa jimbo la Busan.
Uamuzi
wa kuonesha filamu hiyo fupi umeiletea sifa waandaji wa filamu hiyo
baada kusifiwa na muandaaji wa filamu fupi za Marekani Joshua
Oppenheimer.
0 comments:
Post a Comment