Aliyekuwa
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta akisaini kitabu cha wageni kabla
ya kuchukua fomu za kuwania uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania mbele ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu Mohamed Seif Khatib.
Aliyekuwa
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta akizungumza na Katibu wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu
Mohamed Seif Khatib mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya
uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aliyekuwa
mbunge wa Jimbo la Karagwe Gosbert Blandes akikabidhiwa fomu za kuwania
nafasi ya Uspika wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Katibu
wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu
Mohamed Seif Khatib.
George
Nangale akipitia fomu ya kuwania nafasi ya uspika wa bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kukabidhiwa na Katibu wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu
Mohamed Seif Khatib katika ofisi ndogo za CCM Lumumba.
Banda Sonoko akikabidhiwa fomu za
kuwania nafasi ya Uspika wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni,
Ndugu Mohamed Seif Khatib.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu
Mohamed Seif Khatib akimkabidhi fomu Ndugu Simon G.Rubugu.
Waliojitokeza mpaka sasa kuchukua fomu
Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar ni; Waziri wa
Uchukuzi, Samuel Sitta, aliyekuwa mbunge wa Karagwe, Gosbert Blandes,
Leonce Mulenda, George Nangale na Profesa Costa Mahalu, Muzamil
Kalokola, Banda Sonoko na Simon Rubugu.
0 comments:
Post a Comment