Jeshi la Polisi nchini, linawashikilia watuhumiwa tisa wanaoshukiwa kumvamia, kumjeruhi na kuiba vitu mbalimbali vya Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Dkt.Sengondo Mvungi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Sa laam jana, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi,alis ema kukamatwa kwa watuhumiwa hao, kumechangiwa na ushirikiano uliotolewa na familia ya Dkt. Mvungi.
Alisema watuhumiwa hao wamekamatwa jijini Dar es Salaam kwa nyakati tofauti ambapo awali walikamatwa sita lakini majina yao yalifichwa ili kutovuruga upelelezi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova,am baye alikuwepo katika mkutano huo, waliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Msigwa Mpopela (30) ,Shabago Magozi na Hamadi Ally, jina maarufu‘Hatibu’.
Wengine ni Zakaria Raphael(dereva wa bodaboda), Mmanda Saluwa,Juma Hamisi,Longisho Semeriko(muuza ugolo), Paul Jeirosi na mwingine aliyemtaja kwa jina moja la Kilimimazoka,ambao wote ni wakazi wa Dar es Salaam
“Watuhumiwa hawa walikutwa na mapanga, kigoda ambavyo vimethibitika kuwa vilitumika katika tukio hilo, pia walikutwa na simu ya mkononi mali ya Dkt. Mvungi,”alisema.
Kamishna Kova alisema, katika mahojian o ya awali na watuhumiwa, walikiri kuhusika na tukio hilo na ushahidi umekamilika kwa asilimia 80.
“Watuhumiwa wote wamekiri kosa hivyo tunaka milisha upelelezi ili wafikishwe mahakamani mara moja,”alisema.
Dkt.Mvungi alivamiwa, kujeruhiwa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi us iku wa kuamkia Novemba 3mwaka huu , nyumbani kwake Kibamba, Dar es Salaam.
Hivi sasa,Dkt. Mvungi anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Milpark, nchini Afrika Kusini na hali yake inaendelea kuimarika .
Akizungumzia suala la kuwakamata wahamiaji haramu, Dkt.Nchimbi alisema mpango wa lio nao ni kuweka Ofisa mmoja wa Polisi kilaTarafa nchini aweze kusaidiana na Polisi Jamii pamoja na wananchi kuwabaini watu hao.

SOURCE: MAJIRA
0 comments:
Post a Comment