LATEST POSTS

Friday, December 27, 2013

JACK PATRICK ADAIWA KUNASWA NA PIPI 66 ZA DAWA ZA KULEVYA ZENYE THAMANI YA MIL 215.5 CHINA


Mrembo anayedaiwa kuwa Jack Patrick (akiwa amefunikwa uso) mikononi mwa polisi nchini China baada ya kukutwa na pipi 66 za heroin tumboni.
Mwanamitindo Jack Patrick.…
Mrembo anayedaiwa kuwa Jack Patrick (akiwa amefunikwa uso) mikononi mwa polisi nchini China baada ya kukutwa na pipi 66 za heroin tumboni.
Mwanamitindo Jack Patrick.
 
Mrembo anayedaiwa kuwa Jack Patrick akipelekwa katika chumba maalum kwa ajili ya mkutano na wanahabari Jumanne Desemba 19, 2013 huko Macao China.
Polisi wakichunguza pipi zenye dawa za kulevya alizokutwa nazo mrembo anayedaiwa kuwa Jack Patrick.
Wanahabari nchini China wakichukua picha za dawa hizo za kulevya anazodaiwa kukutwa nazo Jack.
MODO maarufu Bongo, Jacqueline Patrick Cliff, anadaiwa kukamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao nchini China. Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya pipi 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720 sawa na shilingi milioni 215.5 za Kitanzania.
Inadaiwa kuwa Jack alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne ya Desemba 19, 2013. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko China.
Jack alipata jina aliposhika namba tatu kwenye Miss Ilala na kushiriki Miss Tanzania mwaka 2005/06. Pia uliuza nyago kwenye video ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marehemu Albert Magwea ‘Ngwair’ iliyokwenda kwa jina la She Got A Gwain. Kuanzia hapo jina likawa kubwa na akawa mwanamitindo maarufu Bongo.
Ni katika kipindi hicho cha umaarufu akaolewa na mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa mkongwe, Abdallah Fundikira, Abdulatif kabla ya jamaa huyo kutupwa nyuma ya nondo za mahabusu ya Keko, Dar akikabiliwa na msala wa kusafirisha mihadarati.

Kutoka Urambonews
Eeh!Mwenyezi Mungu hebu waokoe mabinti zetu maana shetani amewakamata sawasawa kupitia biashara ya madawa ya kulevya. Maana kwa utafiti wangu mdogo, idadi kubwa ya wanaokamatwa na madawa ni mabinti zetu wadogo tena warembo. Hivi kwanini hatujifunzi kupitia kwa wenzetu yarabi. Yaani mi hata sielewi. Kwanza naona hivi ninavyoandika, kuna watu wapo wanavusha madawa airport, bila hata woga.  Haya, mtu anakamatwa na madawa ya kulevya China ambapo sheria yao ni kunyongwa. Jamani hii si hasara kwa Familia na Taifa kwa ujumla. Hebu tujibiidishe kila mmoja kwa shughuli ambayo mwenyezi Mungu amemjalia. Kwa kweli inauma sana jamani.

0 comments: