Jeshi
la Polisi mkoani Morogoro limefanikiwa kukamata gari dogo aina ya
Toyota Spacio likiwa limebeba mwili wa mtu aliefari ambaye alitambulikwa
kwa Jila la Khalid Kitala (47) na kukutwa na kete kadhaa za Madawa ya
Kulevywa tumboni.
JESHI la Polisi mkoani Morogoro limenasa kete 24 za dawa za kulevya kwenye mwili wa marehemu Khalid Abdul Kitala (47) mkazi jijini Dar es Salaam.
Mwili wa marehemu Kitala aliyekuwa akiishi Kariakoo, Mtaa wa Kongo,
ulikuwa ukisafirishwa kutoka Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustin Shilogile,
tukio hilo lilitokea juzi usiku katika mizani ya magari makubwa iliyopo
Mikumi wilayani Kilosa.
“Baada ya taarifa za siri kutoka kwa wasamaria wema kuwa kuna gari
dogo kutoka wilayani Mbozi baadae lilitambulika kuwa ni aina ya Spacio T
887 BSW limebeba mwili wa marehemu wenye dawa za kulevya, tukaweka
mitego sehemu mbalimali na kulinasa Mikumi,” alisema Shilogile.
Alisema gari hilo lilikuwa likiendeshwa kwa kupokezana na Teddy Esco
(27), mkazi wa Mtaa wa Mwaka, Tuduma, Wilaya ya Momba mkoani Mbeya na
Lucas Atubonekisye Swila (32) wa Mtaa wa Songea wilayani Momba,
lilikuwa na abiria aliyetambulika kwa jina la Jumbe Hamad Mbano (36),
mfanyabiashara wa Kariakoo, Mtaa wa Jangwani jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Shilogile, taarifa za uchunguzi za awali baada ya
kukamatwa kwa gari hilo zilikutwa kete saba ndani ya gari zilizofanya
jumla ya kete 24 katika tukio hilo na marehemu alikuwa mfanyabiashara
katika soko la Kariakoo-Kongo jijini Dar es Salaam.
Naye Mganga Mkuu wa hospitali ya Rufaa Morogoro, Ritha Lyamuya
alisema baada ya marehemu kufanyiwa uchunguzi zilitolewa kete 17
zinazohisiwa kuwa za dawa za kulevya.
Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi
maiti katika hospitali hiyo kwa taratibu nyingine za kisheria kabla
haujaruhusiwa kuzikwa.
Chanzo: Tanzania Daima and GPL
0 comments:
Post a Comment