Mheshimiwa zitto Kabwe
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe,
amejibu mashambulizi kwa viongozi wa Chadema, kutokana na kile
alichosema wanazunguka na kusema maneno yasiyo ya ukweli.
Akihutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika
katika Uwanja wa Mwanga Centre, Kigoma mjini, alisema alichukua kadi ya
uanachama wa Chadema mwaka 1993 wakati huo, Katibu Mkuu wa chama hicho,
Dk Wilbrod Slaa akiwa bado yuko CCM.
“Wakati hao wenye midomo mikubwa wanaoongea sasa,
walipokuwa wamekumbatia watawala, nyinyi mlikuwa mnapigwa mabomu kutaka
mageuzi, eti leo wao wapinzani zaidi kuliko sisi na ndiyo maana hatuwezi
kuwaachia.
Hatuwezi kukubali, hatutoki, demokrasia ni
mchakato na mwenzenu nimekuwa kwenye mchakato huu. Kadi yangu ya Chadema
nimeichukulia kwenye uwanja huu, tarehe moja mwezi wa nne mwaka 1993,
nikiwa na miaka 16, wakati nachukua kadi yangu, Katibu Mkuu wa chama
changu alikuwa yuko CCM.
Akizungumza kile alichosema ni uongo unaosambazwa
na viongozi wa juu wa chama hicho, Katibu Mkuu Dk Slaa na Mwenyekiti
wake Mbowe waligawana maeneo Mbowe akaenda Kanda ya Ziwa na Dk Slaa
Kanda ya Magharibi.
Alisema kwenye mikutano hiyo, Mbowe anasema kuwa endapo mbunge huyo atarudi yeye Mbowe atajiuzulu, suala alilosema linaonyesha kuwa tayari ameshafukuzwa bila hata utetezi wake kusikilizwa.
Alisema baada ya viongozi hao kuzungumza na kusema
mambo hayo na yeye aliamua kurudi nyumbani Kigoma na baada ya kuona
hilo Dk Slaa akahoji mbunge huyo anafanya vikao hivyo kama nani.
“Mimi nimekata rufaa, wajumbe wa baraza kuu wa
Mtwara, Ruvuma wanaandika barua wanataka mkutano mkuu, Katibu Mkuu akiwa
Igunga anasema hiyo ni haramu na hao wafuasi wa Zitto watafanya Zitto
afukuzwe, si __wamwamesha nifukuza? takachokuja kunijadili, hivyo si
wameshanifukuza ?
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment