LATEST POSTS

Monday, May 5, 2014

CUF Taifa YAFUNGUAA WAZI MILANGO YA KUGOMBEA UONGOZII


Dar es Salaam. Chama cha Wananchi (CUF) kimefungua milango ya kugombea nafasi za uongozi taifa ngazi ya Mwenyekiti, Makamu na Katibu Mkuu utakaotangazwa baadaye baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa Kamati Kuu Taifa.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Profesa Ibrahim Lipumba wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza Kuu ulioanza jana kwa ajili ya kuazimia mambo mbalimbali ikiwamo kujadili, kuchuja majina ya wagombea katika nafasi ya wenyeviti wa wilaya, makamu na makatibu wakuu.
Alisema baada ya kumaliza mkutano wa Baraza Kuu kesho, utafuatiwa na Mkutano wa Kamati Kuu ambao utakutana kwa ajili ya kujadili maandalizi ya kufanya uchaguzi mkuu utakaofanyika hapo baadaye mwaka huu.
Profesa Lipumba alitoa wito kwa wanachama wenye sifa za kugombea nafasi hizo kujitokeza kuwania nafasi hizo na kuwezesha chama kupata uongozi mpya.
“Tukishamaliza uchaguzi huu wa ngazi ya wenyeviti na makatibu wa wilaya ambao utafanyika siku chache zijazo, mwezi huu katika maeneo yote nchini kwa sasa tutajadili maandalizi ya mkutano mkuu wa chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa nafasi hizo, kwa hivyo tunatoa uhuru wa kugombea nafasi hizo kwa wanachama wote wenye sifa,” alisema Profesa Lipumba.
Awali akifungua mkutano huo Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad alisema mkutano huo utafanyika kwa siku tatu ambapo moja ya maazimio ni pamoja na uchaguzi wa ngazi mbalimbali katika chama pamoja na kufanya uteuzi wa watu wanaogombea uenyekiti na ukatibu katika ngazi ya wilaya na taifa.
Akizungumzia bajeti alisema Serikali inapaswa kuwa makini katika usimamizi wa vyanzo vya mapato pamoja na kupunguza misamaha ya kodi ambayo inatia hasara taifa.
“Misamaha ya kodi ni mingi kwani kuna zaidi ya Sh1 trilioni zinapotea kutokana na misamaha ya kodi nawatu wanaokwepa kodi hali hii inatokana na kutokuwa na mfumo madhubuti wa kudhibiti tatizo hili,” alisema Profesa Lipumba. 

0 comments: